Tuisaidie Polisi: Je, Dawati la Jinsia la Polisi linahitaji maboresho? Tujadili na kushauri

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
jzRheJV5_400x400.jpg

Nimesoma malalamiko ya wananchi wengi kulalamikia utendaji usiokidhi viwango wa Madawati ya Jinsia yaliyopo vituo vya polisi nchini.

USULI
Ujio wa Dawati la Jinsia ulishereheshwa na kukithiri kwa vitendo ukatili kwenye jamii, na ikaonekana sehemu kubwa ya ukatili umejaa kwenye mahusiano ambapo serikali kama mlinzi wa mikataba hii iliona ni vyema kukawepo na dawati la kushughulika na masuala ya kifamilia yanayosuluhikika badala ya kuwajaza magerezani wanafamilia wanaopishana. Zaidi ya hapo, dawati limekuwa linalinda haki za mtoto na kutoa elimu kila inapobidi.


Dc1UBYzW4AAYF5f.jpg

Mimi, binafsi nimewahi kupeleka dawa ya mtoto wa miaka 2 aliyekuwa anabakwa mfululizo na baba yake wa kufikia huku mama akikaa kimya bila kuchukua hatua. Dawati waligoma kumpeleka mtoto hospitali ili kupata vipimo ambapo ilibidi maafisa ustawi wa jamii waingilie kati na mtoto alipopimwa alionekana ameshaharibiwa via vyake vya uzazi. Lakini kwa kuwa mtuhumiwa ni jamaa wa polisi wa kituo kilichoshughulikia kesi hii, aliishia kupewa kesi ya ASAULT yaani shambulio na kesi haikuchukua muda akawa acquited.

Kuna, mwanamke mmoja alikuja ofisini apate msaada wa kisheria. Nilipomsikiliza nikagundua hii matrimonial case haijajijenga kwenye msingi wa kupeleka mahakamani. Nikamshauri aende dawati la jinsia polisi ambapo alichoambulia ni kuambiwa avumilie vipigo na udhalilishaji kutoka kwa mumewe na familia yake kwani hata wazee wetu walivumilia mengi.

Kuna mzazi hivi juzi nikiwa kwenye Baraza la Ardhi Wilaya kufuatilia kesi ya ndugu yangu, kuna mzee amefungua kesi akitaka mahakama ya Ardhi itoe hukumu ya kumtaka mwanae (mtu mzima) ahame kutoka nyumbani akajitegemee. Kibaya alisema wazi alilipeleka suala lake Dawati la Jinsia polisi, wakalitupilia mbali kwa kumwambia arudi akae na nduguze wambembeleze kijana akaanze maisha yake.

Leo tunasoma hapa JF malalamiko dhidi ya Madawati ya Jinsia kwenye vituo vya polisi wakiyapuuza malalamiko au masuala wanayopelekewa dawatini.

HOJA
Kwa upande wako ewe msomaji hapa JamiiForums, je una uzoefu wowote kuhusu utendaji wa Madawati ya Jinsia katika vituo vyetu vya polisi? Unaweza kutushirikisha ili kusaidia jeshi letu kujitathmini katika kuhudumia raia kama takwa la Kikatiba na Sheria linavyowaamrisha.

Mimi ninapendekeza yafuatayo;

  1. Kila askari anayeteuliwa kuhudumu kwenye Dawati la Jinsia ni budi awe na taaluma ya Ustawi wa Jamii au Jeshi lilazimike kumpeleka mafunzo akiwa kazini.
  2. Jeshi la Polisi lirekebishe kanuni zake kuhusu uendeshaji wa Madawati ya Jinsia ambapo Maaskari wanaosimamia madawati ya Jinsia wafanyekazi kwa kushirikiana na ofisi za Ustawi wa Jamii zilizopo eneo husika
  3. Jeshi la Polisi waangalie uwezekano wa kuwatumia wanasheria wa Haki za Binadamu katika kushirikiana kutatua changamoto zinazopelekwa dawatini
Tuendelee kujadili kwa minajili ya kujenga wajibikaji kwa Jeshi letu la Polisi hususani eneo la Dawati la Jinsia.

Karibu.
 
Nani kakwambia polisi wa tanzania wanashaurika? Hebu katafute hela huko kama huna mchongo njoo hapa bandarini kuna nafasi ya ukuli.

Acha kupoteza muda kushauri hao watu.
Mkuu
Hata kama hawashauriki, lakini hilo lisitilutoe kwenye kutimiza wajibu wetu kila inapobidi kufanya hivyo
 

Kuna mzazi hivi juzi nikiwa kwenye Baraza la Ardhi Wilaya kufuatilia kesi ya ndugu yangu, kuna mzee amefungua kesi akitaka mahakama ya Ardhi itoe hukumu ya kumtaka mwanae (mtu mzima) ahame kutoka nyumbani akajitegemee. Kibaya alisema wazi alilipeleka suala lake Dawati la Jinsia polisi, wakalitupilia mbali kwa kumwambia arudi akae na nduguze wambembeleze kijana akaanze maisha yake.
Hahaha, chuma kimemng'ang'ania dingi mpaka kaamua kukipeleka mahakamani Hahaha!
Kama mimi ndio dingi naezua mabati nyumba nzima kasoro ghetto kwangu tu ***** au naenda kuikopea nyumba benki, siku wakija kuipiga mnada wanamkuta huyu matako.
Huyo hana tofauti na huyu>>

View: https://youtu.be/LoD-R8hT1rw?si=HL5nPT2zCgbKFmpu
 
Back
Top Bottom