kamili
JF-Expert Member
- Feb 10, 2011
- 1,213
- 849
Mheshimiwa nina taarifa mbili kama ifuatavyo:
Tarehe 24/10/2023 kati ya saa tatu na saa nne nilipita Moshi na gari binafsi nikitokea Arusha. Safari yangu hiyo ilikuwa ni safari ndefu iliyoanzia Tanga, Dar, Morogoro, Dodoma, Manyara, Arusha na siku hiyo nilipita Moshi katika safari ya Kurudi Dar. Taafira yangu ni kuwa siku hiyo kati ya Moshi mjini na njia panda nilipigwa faini mara tatu kwa madai ya mwendo kasi! Pamoja na kwamba nililipa faini kupitia mtandao lakini nina mashaka makubwa sana na utendaji wa polisi wetu maeneo haya kwa sababu zifuatazo:
1. Nillipata leseni mwaka 2016 mkoani Mbeya na nimetembea mikoa mingi ya Tanzania lakini hii ni faini ya nne kupigwa nikiwa kati ya Moshi na njia panda na sijawahi kupigwa faini sehemu yoyote Tanzania nje ya Mkoa wa Moshi inayohusiana na mwendo kasi sehemu ya spidi 50!
Picha zote tatu zinazodaiwa zilipigwa maeneo tofauti yenye spidi 50 zinaufanano wa mashaka ufuatao:
(a.) picha zote zilipigwa, mpiga picha akiwa upande wa kulia wa dereve (b) mpiga picha alikuwa nyuzi 45 na uelekeo wa gari (c) gari inaonesha dirisha la dereva lilikuwa limefungwa licha ya kwamba dirisha la gari yangu halikuwa limefungwa tangu tumetoka Arusha. (d) picha zote tatu zilionesha nilikuwa spidi 59!!!. Hizi sababu zinanitia mashaka sana huenda kuna ujanja wa kuedit picha Mkoani Moshi, nasema hivyo kwa sababu sijawahi pigwa faini mahali popote nje ya Moshi na mwendo wangu ni wa kutii sheria bila shuruti. Na tarehe hiyo nilitii sheria vyema ndio maana hata mikoa mingine nilipita salama.
2. kilometa moja au mbili kabla ya kufika Mwanga ukiwa unatokea Korogwe kuna kibanda cha polisi mkono wa kulia. Hapa napo sijawahi pita salama nikiwa natokea upande wa Korogwe kuelekea uelekewo wa Moshi. Hapa nimelipa faini mara sita kati ya 2020 na 2022!!!!. Kimsingi zilikuwa sita, hiyo ya sita ilikuwa June 2022 ambapo walidai kuna daraja nilipita na spidi 65!!! Nilipowauliza hilo daraja lipo wapi walisema lipo nyuma umbali wa KM 15! Baada ya maongezi ya muda mrefu ikiwa ni pamoja na kuwaonesha kitambulisho changu cha kazi ya serikali walinisamehe!
Hii safari yangu ya mwisho ya tarehe 24/10/2023 nikiwa natokea Moshi sikukuta askari hapo nilitamani kupiga picha hicho kibanda but Tanzania imebadilika sana, kuweka picha hapa chochote kinaweza tokea (eg. kukamatwa!, kushtakiwa! kubambikiwa kesi nk) sina hakika ni sheria zimebadilika au utendaji umebadilika.
Kati ya 2016 na Octoba 2023 nimeshapigwa faini mara 10. moja ni ya Tanga sehemu inayoitwa Amboni mwaka 2019 ambapo Bima ya gari ilikuwa ilikuwa imeisha kwa kiasi cha siku 11. Nne ni za kati ya Moshi kuelekea njia panda. Tano ni za Mwanga. Mikoa mingine yote pamoja na Dsm sina faini!
Ombi langu kwako ni kwamba naomba idara yako ijiridhishe juu ya uadilifu wa hawa askari wetu wa Mkoa wa Moshi, na ubora wa vitendea kazi vyao. Binafsi nitaendelea kulipa faini hata kama ni za kubambika kwa sababu kinyume na hapo askari wanasema niende mahakaman kama sijaridhika. But mfumo wa mahakama utachukua miaka kutoa haki, huko ni kupoteza muda na fedha nyingi.