Polisi, Madaktari na Mahakama wanavyoshughulikia kesi za kubaka watoto ni wazi Tanzania ni 'banana republic'. Inasikitisha, inatia hasira na aibu

DidYouKnow

JF-Expert Member
Jul 28, 2019
725
1,000
Daktari alipopelekewa mtoto wa kubakwa, yeye ndiye alitakiwa kufanywa swabs za sehemu za siri za mtoto na kuzihifadhi kama sample ambazo zinaweza kufanyiwa uchunguzi wa DNA. Kumbuka kwamba hata kama mtoto aliogeshwa, ndani ya mwili wake bado angekuwa na vitu kama shahawa za mbakaji. Madaktari wanaelewa utaratibu huu, sasa huyu kwa nini hakufanya?
Nadhani kuna daktari kama daktari ambaye au ni mbobezi kwenye kitu fulani au generalist, lakini kuna forensic pathologist ambao ni wachache (na labda gynecologists). Hizo issue za swab unaweza ukazisema hapa, kwa sababu umesoma lakini je hawa madaktari wa kawaida wamepata mafunzo kwa ajili ya matukio kama hayo na namna ya kuyawasilisha pale inapobidi au wanaingia kwenye hiyo nafasi kwa kuwa forensic pathologist na au gnecologist hayupo?
 
mamylove

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
873
1,000
Hebu fikiria. Mtoto wako wa miaka sita anatoka shule. Akiwa njiani mjinga fulani mwenye akili mbaya kuliko mnyama anamkamata na kumvutia porini, kisha anambaka na kumuumiza sana. Mtoto huyu wa miaka sita analia kwa maumivu, lakini mbakazi anamziba mdomo na kumtishia kumuua ikiwa ataendelea kupiga kelele au kumtaja kwa watu.

Mtoto wako huyu anarudi nyumbani analia na ametapakaa damu kwenye suruali yake. Unamwangalia kwa uchungu na kugundua mtoto wako mdogo kipenzi, miaka sita tu, darasa la kwanza, amebakwa na kuumizwa sana. Unamuuliza nani amefanya hivi anakutajia ni fulani, kwa kuwa anamfahamu aliyembaka.

Unamchukua mtoto na kumpeleka polisi. Polisi wanafungua jarida la kesi, lakini wala hawakuulizi nguo alizobakwa nazo ziko wapi. Mnampeleka mtoto hospitali, daktari anaemtibu wala hafanyi jitihada za kuchukua sampuli ndani ya mtoto na kuzihifadhi ili waje wafanye DNA test.

Kesi inapoenda mahakamani, mbakaji anafungwa kwa ushahidi wa kutambuliwa na mtoto. Lakini baadaye, jaji mtukuka wa mahakama ya rufaa anasema mbakaji aachiliwe huru kwa kuwa wakati wa kesi ile suruali yenye damu aliyokuwa amevaa mtoto haikuletwa mahakamani kama ushahidi. Mbakaji yuko huru.

Fikiria kama huyo mtoto wa miaka sita ni wa kwako, waangalie watoto wako, au watoto wa ndugu yako wa karibu, halafu piga picha wao ndio wamefanyiwa hivyo. Unajisikiaje?

Hii sio hadithi, ni tukio la kweli. Hawa ndio polisi wetu. Hawa ndio madaktari wetu. Hawa ndio majaji wetu. Hodari na makini sana katika kufuatilia kesi za siasa na kufunga watu kwa kesi za kubambikiwa, lakini sio kesi za watoto wa miaka sita kubakwa na kuumizwa.

Sasa niambie kama nikisema nchi yetu Tanzania ni banana republic, una sababu gani za kunibishia?

Reference: Suruali yenye damu ilivyotengua hukumu
Ndio maana watu wanafanya kujichukulia sheria mkononi, unaachoamua kumfanya mtuhumiwa mpk shetani lazima akae pembeni ajifunze. Inauma asikuambie mtu

Sent from my CPH2015 using JamiiForums mobile app
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,983
2,000
Nadhani kuna daktari kama daktari, lakini kuna forensic pathologist ambao ni wachache. Hizo issue za swab unaweza ukazisema hapa, kwa sababu umesoma lakini je hawa madaktari wamepata mafunzo kwa ajili ya matukio kama hayo au wanaingia kwenye hiyo nafasi kwa forensic pathologist hayupo?
Kama daktari umepewa case ya kutibu mtoto aliyebakwa, na unajua huna uwezo wa kufanya forensic pathology, kwa nini usiwasiliane na uongozi wako kuwaeleza hilo?

Kwa hiyo wewe ni daktari, unaletewa mtu amebakwa amejaa shahawa na damu, unaendelea tu kusafisha na kutibu bila kuelewa unapoteza ushahidi muhimu sana? Hufai hata kuitwa daktari, kwa sababu hayo ni masomo ya first year. Labda alikuwa mtu wa Rural Medical Aid sio daktari
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,983
2,000
Aisee mleta mada umeandika kwa uchungu sana. Nikajiuliza swali je iwapo huyo mtoto aliyefanyiwa unyama huo angekuwa mtoto au mjukuu wa huyo jaji je angemfunga huyo mbakaji au angemwachia huru kwanza mpaka suruali iletwe mahakamani?
Nina mtoto mdogo wa karibu umri huo Mkuu.

Katika visa vingi, huwa najiweka kwenye picha na kufikiria mhanga kama angekuwa ni bibi yangu, babu yangu, baba yangu, mama yangu, kaka yangu, dada yangu, mke wangu, mtoto wangu, mpwa wangu nk. Basi the right emotions huamshwa.

Hata ninaponunua kitu toka kwa bibi hivi, huwa siwezi ku-bargain bei kwa kuwa nafikiria, hivi imagine huyu angekuwa bibi yangu anahangaika kutafuta fedha ya kununulia mboga na unga ili mimi kama mmoja ya wajuu wake tuweze kula leo jioni? Naweza nikajikuta nanunua kitu huku machozi yananitoka. Kuna wakati nililipa mara mbili ya bei niliyopewa, na wakati mwingine kununua vitu vyote alivyokuwa mama mmoja nilipomuuliza kwani nikitaka kununua vyote hivi ili utoke kwenye hili jua urudi nyumbani, unataka shilingi ngapi?

Ndio maana wakati mwingine nina hasira sana na hawa wanaojiita viongozi wetu na wanasiasa, kwa kuwa najua hawana kabisa uchungu na masikini hawa kina mama na kina baba wanaohangaika sana na maisha. Wanasafiri na V8 zao, wananunua vitu kwa bei ya kunyanyasa wanawake na wazee, wanajisifia tumepata vitunguu Ruaha kwa bei poa. Mpumbavu wewe, je hukuona kwamba ile bei uliyolipa, na bado ukadai upunguziwe, ni ya kumkandamiza yule mama aliyekuuzia hivyo vitunguu kwa kipato ulichonacho ukijilinganisha na yeye?
 
JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
3,610
2,000
Mimi sidhani kama tutapelekana polisi, shingo ya mbakaji itakuwa halali bora nifungwe kwa mauaji.

Inaumiza sana.
Tupo pamoja,yaani kabinti kangu katendwe hivyo,namteka mbakaji,namtatua Malinda,nikishindwa haki ya nani nitakodi gari nimgonge,navunja miguu,napasua kichwa,NAMI nalala mbele,hatuwezi kuishi wote hapa duniani
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,983
2,000
Hata ingeletwa angeipima hiyo damu kwa kipimo gani kuthibitisha anayoyataka.
Ikiwa tutakutana, niko tayari kumwambia huyu jaji mbele za watu kwamba hajui sheria na hana sifa zinazomfanya astahili kuwa jaji, na kwamba ujaji wake ulipaswa kukoma siku Magufuli alipokufa
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,983
2,000
Ila waza pia kama huyo anayeitwa mbakaji akawa si mbakaji alisia itakuwaje?
Una maanisha alisingiziwa Mkuu. Ndio maana nikasema, hapa kulikuwa na ushahidi wa mtoto. Hivi kweli kwa unavyoona, nikitaka kukubambikia kesi, nitatumia mtoto wa miaka sita kama shahidi wangu mkuu?

Huhitaji kuwa na PhD ya saikolojia au hata ya kubangua korosho kama ya Magufuli kujua kwamba huyu mtoto wa miaka sita anadanganya kaambiwa cha kusema
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
5,946
2,000
Hebu fikiria. Mtoto wako wa miaka sita anatoka shule. Akiwa njiani mjinga fulani mwenye akili mbaya kuliko mnyama anamkamata na kumvutia porini, kisha anambaka na kumuumiza sana. Mtoto huyu wa miaka sita analia kwa maumivu, lakini mbakazi anamziba mdomo na kumtishia kumuua ikiwa ataendelea kupiga kelele au kumtaja kwa watu.

Mtoto wako huyu anarudi nyumbani analia na ametapakaa damu kwenye suruali yake. Unamwangalia kwa uchungu na kugundua mtoto wako mdogo kipenzi, miaka sita tu, darasa la kwanza, amebakwa na kuumizwa sana. Unamuuliza nani amefanya hivi anakutajia ni fulani, kwa kuwa anamfahamu aliyembaka.

Unamchukua mtoto na kumpeleka polisi. Polisi wanafungua jarida la kesi, lakini wala hawakuulizi nguo alizobakwa nazo ziko wapi. Mnampeleka mtoto hospitali, daktari anaemtibu wala hafanyi jitihada za kuchukua sampuli ndani ya mtoto na kuzihifadhi ili waje wafanye DNA test.

Kesi inapoenda mahakamani, mbakaji anafungwa kwa ushahidi wa kutambuliwa na mtoto. Lakini baadaye, jaji mtukuka wa mahakama ya rufaa anasema mbakaji aachiliwe huru kwa kuwa wakati wa kesi ile suruali yenye damu aliyokuwa amevaa mtoto haikuletwa mahakamani kama ushahidi. Mbakaji yuko huru.

Fikiria kama huyo mtoto wa miaka sita ni wa kwako, waangalie watoto wako, au watoto wa ndugu yako wa karibu, halafu piga picha wao ndio wamefanyiwa hivyo. Unajisikiaje?

Hii sio hadithi, ni tukio la kweli. Hawa ndio polisi wetu. Hawa ndio madaktari wetu. Hawa ndio majaji wetu. Hodari na makini sana katika kufuatilia kesi za siasa na kufunga watu kwa kesi za kubambikiwa, lakini sio kesi za watoto wa miaka sita kubakwa na kuumizwa.

Sasa niambie kama nikisema nchi yetu Tanzania ni banana republic, una sababu gani za kunibishia?

Reference: Suruali yenye damu ilivyotengua hukumu
Ni kweli ni mambo yanayoumiza sana, lakini kesi ina jengwa toka polisi, ushahidi ukishaharibiwa tu, basi na mala nyingi mahakama za chini hata huwa sielewi maamuzi mengine huwa wanayafikia vipi, na yakifika kwa majaji, mengi huwa yanatupiliwa mbali!!sasa kweli ushahidi wa suruali nao ulikuwa mgumu kuwa nao?mambo ya sheria ndugu ni magumu usichukulie tu kwa kuwa ni mtoto kasema basi ni ushahidi tosha!kuna kesi ngapi ambazo watu wamewatumia watoto kuwabambikizia kesi maadui zao, na baada ya muda watoto hao walipokuja kuwa wakubwa wakakiri kuwa haikuwa kweli?!!wakati mtu ameshachezea miaka kibao tu jela?Nadhani ushahidi wa kesi nyingi za ubakaji /ulawiti zinaharibiwa toka mwanzo kabisa, ngazi ya familia, hospitalini na polisi.
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
14,755
2,000
Mkuu, unajua uzito wa ushahidi wa mtoto katika kesi? Katika kesi hii inawezekana kusiwe na collaborating evidence, lakini haiondoi uzito wa ushahidi wa mtoto. Hivyo jaji alitakiwa aangalie sana upande huu.

Mtoto wa miaka sita ukimwambia akadanganye ni fulani kambaka, ukimfanyia cross examination ya juu kutumia mtaalamu wa saikolojia, ataishia kusema baba alisema nimtaje fulani. Jaji anajua kabisa kwamba kama mtoto alisema ni fulani kanibaka uwezekano wa kuwa si kweli ni o.o1%, kwa hiyo hakupaswa kusimamia rufaa kwenye suruali, bali alipaswa kusimamia kwenye ukweli wa aliyosema mtoto.

Kama rufaa ingejenga shaka juu ya ushahidi wa mtoto hapo ningekubaliana na jaji. La sivyo huyu lazima ni jaji kihiyo tu, wale majaji wa Magufuli labda.

Jamhuri inatakiwa kukata rufaa ili hukumu ya huyu jaji mpuuzi itupiliwe mbali.
Una point nzuri sana. Ila sisi kutoa judgement kwa kusoma tu kilichoandikwa kwenye gazeti nadhani tunaweza tusitende haki kwa jaji aliyesikiliza. Bila kusoma hukumu yote na jinsi cross examination ilivyokwenda tunaweza tusijue kama mtoto alionekana kusema ukweli au uongo. Lawama nyingi ziwaendee polisi walioshughulikia hii case. Hata kama huna vifaa vya utambuzi kwa wakati ule lakini kitu kama hiyo suruali na mabaki ya manii kama yalikuwepo ilikuwa ni muhimu kabisa kabisa vichukuliwe na kuhifadhiwa. Ulaya sasa hivi kuna cases za miaka ya nyuma kabisa wakatika DNA haijagundulika zinateguliwa kwa sababu waliweka exbit za matukio. Polisi waliohusika wote inabidi waondolewe kazini kwa uzembe.
 
drilling

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
2,642
2,000
mimi nimezulumiwa pesa na kampuni ya universty abroad dolla 2000 na ushahidi ninao lakini nashindwa kwenda polisi kwa kujua sintofanikiwa
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,983
2,000
Una point nzuri sana. Ila sisi kutoa judgement kwa kusoma tu kilichoandikwa kwenye gazeti nadhani tunaweza tusitende haki kwa jaji aliyesikiliza. Bila kusoma hukumu yote na jinsi cross examination ilivyokwenda tunaweza tusijue kama mtoto alionekana kusema ukweli au uongo. Lawama nyingi ziwaendee polisi walioshughulikia hii case. Hata kama huna vifaa vya utambuzi kwa wakati ule lakini kitu kama hiyo suruali na mabaki ya manii kama yalikuwepo ilikuwa ni muhimu kabisa kabisa vichukuliwe na kuhifadhiwa. Ulaya sasa hivi kuna cases za miaka ya nyuma kabisa wakatika DNA haijagundulika zinateguliwa kwa sababu waliweka exbit za matukio. Polisi waliohusika wote inabidi waondolewe kazini kwa uzembe.
Mkuu, kama judgement ya rufaa ingetokana na ushahidi wa mtoto, kwa nini gazeti liandike imetokana na suruali? Hapo unalaumu tunatoa judgement, lakini wewe ndio unatoa judgement kwa kitu ambacho hakipo kwenye taarifa ya gazeti.

1626362851246.png
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
14,755
2,000
Mkuu, kama judgement ya rufaa ingetokana na ushahidi wa mtoto, kwa nini gazeti liandike imetokana na suruali? Hapo unalaumu tunatoa judgement, lakini wewe ndio unatoa judgement kwa kitu ambacho hakipo kwenye taarifa ya gazeti.

View attachment 1855026
Hoja yangu ni kuwa ili uweze kujua kama jaji alipotoka, ni lazima upitie kesi nzima. Usome mashahidi wote walivyowasilisha ushahidi wao, walivykuwa cross examined nk. Uandishi wa Tanzania mimi najua, na pengine hata wewe unaujua. Hapa inawezekana jaji alitilia maanani vipengele vingine pamoja na cha hiyo suruali. Mimi skutoa judgement yoyote ila nimetoa tahadhari kuwa inatakiwa tujue mwendendo mzima wa kesi. Kitu ambacho mimi naona kipo wazi hapa ni uzembe wa polisi katika kuchukua vielelezo. Au pengine inaweza isiwe ni uzembe bali ni makusudi baada ya mshukiwa kuwashikisha kitu kidogo. Otherwise inauma sana sana kwa kitendo alichofanyiwa huyo mtoto na zinatakiwa hatua zaidi zichukuliwe ili kama yeye ndiye mhusika basi apate haki yake.
 
Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
4,704
2,000
Una maanisha alisingiziwa Mkuu. Ndio maana nikasema, hapa kulikuwa na ushahidi wa mtoto. Hivi kweli kwa unavyoona, nikitaka kukubambikia kesi, nitatumia mtoto wa miaka sita kama shahidi wangu mkuu?

Huhitaji kuwa na PhD ya saikolojia au hata ya kubangua korosho kama ya Magufuli kujua kwamba huyu mtoto wa miaka sita anadanganya kaambiwa cha kusema
Mkuu yote yanawezekana na ndio maana Mahakama haina desturi ya kutumia hisia kutia hukumu na wengi wanaotumia hisia huwa wanafeli.

Kuna msemo Mahakamani, "Ni bora kumuachia mkosaji huru kuliko kumfunga asiye na hatia" huu unajibu kila jambo hapo juu Mkuu.
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,983
2,000
Mkuu yote yanawezekana na ndio maana Mahakama haina desturi ya kutumia hisia kutia hukumu na wengi wanaotumia hisia huwa wanafeli.

Kuna msemo Mahakamani, "Ni bora kumuachia mkosaji huru kuliko kumfunga asiye na hatia" huu unajibu kila jambo hapo juu Mkuu.
Point unazotoa huna tofauti na huyu jaji. Mie ninasema, kesi hiiinapaswa kusimamia kwenye ushahidi wa mtoto, wewe unachomaanisha i kuwa mtoto anaweza kudanganya. Ngoja mwanao wa miaka sita siku aje anavuja damu na kukuambia amebakwa na jirani ndio umtilie shaka kuwa anadanganya
 
Mwambwaro

JF-Expert Member
Jan 26, 2018
1,621
2,000
Hii jamii nayo imeharibikiwa unakuta jitu zima linatongoza katoto kadogo tena bila uwoga alafu Watu wanamuacha tu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom