Pinda, Muungano, na Hatima ya Zanzibar

Ndugu Mkandara ,haiwezekani kama kweli tunataka kujenga umoja huu ,lipekwe jeshi kwenda kuwapiga WaPemba ,tena jeshi hili sio la Zanzibar linatumia nembo ya Muungano kila unapokaribia uchaguzi inakuwa ndugu zetu wa Pemba hawana raha ,hivi kosa lao ni kitu gani hapa Tanzania ? kuikataa CCM ndio vitumike vyombo vya Muungano kuwakandamiza na kuwatesa ? watavumilia mpaka lini ? hivyo popote pale wanapoona kuwa kuna pengo la Muungano nao watajitosa na kuwa mstari wa mbele kwa maana wameshaona Muungano unawaletea mateso kila baada ya miaka mitano ,wao wameshasema kuwa CCM isitegemee kupata ushindi wa kura ,huko wasahau ,sasa sababu wanazijua wao zaidi na hili linasababishwa na vyombo hivi kuhusishwa kwenye siasa moja kwa moja. Hivyo litakalo tokea na litokee kama kufa muungano wacha ufe Pemba na Unguja watajijua wenyewe lakini isiwepo sababu ya WaTanganyika kutumiwa kwenda kuuwa Pemba hilo ni kosa lililomo ndani ya vyombo vya Muungano ,Wapemba wataungana na Waunguja kuukataa Muungano japo wenyewe wana mambo yao ,ndivyo ilivyotokea Somalia ilipovamniwa na majeshi ya kigeni ,Mmarekani na madege yake alikimbia hadi leo hataki hata kuiona.
 
Mwiba,

Hivi nani kasema ya kuwa Zanzibar kuna mafuta, mimi naona kama baraza la wawakilishi wanajadili kitu ambacho hawana uhakika nacho .

Jamani kila siku mtauliza jambo hilo hilo ,sasa wewe weka akili kichwani kwako iweje aletwe mshauri kuja kuweka rate ya mgawo wa faida na hasara ? Kaa vizuri utafute rejea kivyako uone na ujue kitu gani kimezungumzwa na kwa nini kikazungumzwa ,maana haielekei mlete mshauri muelekezi apange watu mugawane vipi ?

Mimi kusema kweli Sikumuelewa Mheshimiwa Pinda aliporuka na kusema kuwa hata dalili hakuna inakuwaje watu wavaane mwilini ? Nilizidi kumshangaa aliposema kuna mshauri muelekezi ameletwa kupanga na kujadili mgao na kurudia kusema kuwa watu wakae waupime huo mgao ,sasa wewe kwa akili yako sijui utazuka na lipi kama yapo au hayapo? Akili ni nywele unaweza kuzisuka au kuzinyoa au ukaweka rasta ili tukuone ni mvuta bangi.
 
Nakubaliana na hoja ya mafuta kama utavyoona chini kabisa ya maoni yangu. Lakini hapa katikati, nyinyi mnaojiita Wazalendo ambao mnaoniengua mimi katika listi yenu kutokana na baadhi ya vipengele vya maoni yenu, naombi mzingatie yafuatayo:

Sio kweli kwmaba Dola yetu ya Zanzibar ilivamiwa hapo usiku wa Januari 11, 1964. Bali ni Wazanzibari na Wazanzibara waafrika/weusi waliondosha "kwa bahati mbaya violently" utabaka. Utabaka uliojengwa chini ya utawala wa kisultani, waarabu, ambao kama kawaida wafanyavyo mpaka hii leo (angalia wanavyowauza kwa bei rahisi ndugu zao wa Palestine). Kiburi chao kinyume na uislamu waliwafanya makafiri (British) ndio protector wa utabaka wao. Hili la utabaka na kuwafanya makafiri protector ndio exactly Allah (SW) alilotukataza katika Qur-ani na Sunna za Mtumewe, Haramu safi.

Yaliyotokea siku ile ni haramu sio kwasababu kuwa utawala wa kitabaka wa waarabu uling'olewa, la hasha !!!. Bali ni kwasababu waislamu wa waislamu walimwaga damu, simple as that, ndio haramu. Kwanini ilifikia vile??? mtawala wa wakati ule ndio mas-uula kama nilivyooeleza hapo juu. Na kama nyinyi mnasema kuwa Wazanzibari na Wazanzibara kwasababu ni weusi/waafrika basi sio waislamu au makafiri , basi jiangalieni vizuri maana kauli au fikra za namna hii ni Allah mwenyewe ndie mjibuji na kuwaweka wahusika wanapostahili. Na kama mnasema sio wazalendo, basi mnarudi kule kulee, "kukaanga mbuyu kuwaachia wenye meno watafune". Mnatayarisha kidogo kidogo ili damu ije kumwagika tena huko mbeleni, iwe miaka mia au mia mbili ijayo lakini Mwenyezi Mungu atawafanya mas-uula kesho akhera.

Damu ilimwagika 1964 na likubalike hilo, na iwe mwisho kwa damu ya waislamu kumwagika tena katika visiwa vile. Hii itakuja kwa misingi ya usawa na haki sio kwa utabaka na kukumbatia makafiri (Masultani/Waarabu) au ufisadi, kiburi na kupalilia chuki baina ya watu(viongozi wa sasa wa CCM)

Watanganyika tegeni masikio!!! Mafuta na gesi na mali ya Zanzibar na kwa waZanzibari, si vinginevyo, kama ilivyo almasi ya Mwadui ni ya Tanganyika kwa Watanganyika. Kilichobakia ni kwamba Wabara kwa kutumia Muungano(angalia chini) wanataka kuendelea kuidhulumu Zanzibar. Pinda kwa kauli zake za vitisho na Watanganyika wengine, kwanini hamjali kuwa hakuna haja ya waZanzibari kudai haki hii violently? Ni haki yao.

Nani asiyejua humu jamvini kwamba Muungano una mashaka, anyooshe mkono. !!! Lakini Wabara wanajihisi kama vile wamekamata mpini na Wazanzibari wamekamata makali. Kila siku kubwabwaja tuuuu. Kwani hamjawahi kusikia nyie mke akimtia shoka mume anaemtesa, hivi huwa makosa ya nanai hivi???. Why is this Watanganyika? Kama mimi kesho niamke ndio raisi wenu, basi siku ya pili tu, Tanzania, kwa tamko, tamko rasmi ni nchi ya serikali tatu. Na kilichobakia hapo ni utekelezaji tu ambapo natoa miezi sita kwa kila waziri anaehusika na mambo ya Muungano kukamilisha, nataka kamili, sio nusu ofisini kwangu mfumo wa serikali tatu. Kila upande una haki yake safiii na Muungano una haki yake saafi ndani ya miezi tisa tu. Maana sisi tunajua maana na faida za Muungano, lakini huu haujakaa sawa huu. Mambo mengine yanahitaji Tamko rasmi tu na utekelezaji kufuata hatua kwa hatua kwa furaha na amani.

"Hakika milki ya utajiri bora ni kinaya" sio material wealth obtained from oppression.
 
Kwa vile waliosema sio Wakiristo.Hilo linaeleweka ila ujumbe ndio huo.Kama angesema Jino au Pengo mngelisema ni maneno ya Mungu.
Samahani MKuu Mwiba, unaweza kututajia (kwa majina) hao wanaounda hilo kundi lililomjibu Pinda?
 
Mwiba,
Hapo kwa Wapemba mkuu sipo nawe.. Tuna Jeshi moja tu la Watanzania halijali kama ni Watanganyika, Wazanzibar, Wakristu au Waislaam..
Pamoja na mtazamo wangu huu tofauti bado naielewa haki ya wananchi wa Zanzibar kama nchi iliyoungana na Bara..Kuna mada moja ya Mzee mwanakijiji amezungumzia seti ndogo zinazotengeneza seti kubwa.

Sikuweza kuchangia kule kwa sababu, nimefikia wakati kuona JF imekuwa kijiwe cha Udini..Hoja zote zinazungmzia muungano (setu kubwa) kwa kudharau seti moja ndogo ambayo ni muhimu ktk ujenzi hiyo seti kubwa..
 
Hawa wazanzibara ukiamua kubishana nao utakuwa unapoteza muda, ni kuwapuuza tu maana hawaeleweki! Sera yao ni chako changu, changu changu!
 
Mr Bongolander,
Umenifurahisha kwa kusema Zanzibar haiwezi kujiunga na OIC, I'm sure kwa sababu ni organisation ya Ki-Islam tu. Lakini at the same time it's okay Tz kua na uhusiano wa kibalozi na Vatican. Nyinyi khasa wa Bara muna ugonvi gani na waislam au jumuiya zao ? Mbona wa-zenji au in general waislam in Tz hawawasumbui na makanisa yenu ?
Au most of the Post I read zinazo husisha dini ya ki-islam lazima muwa involve warabu, plse try to understand kua dini ya ki-islam ni dini ya watu wote na pia ujue kua kuna waraabu wengi tu ni wakristo, mayahudi ect. Jee Tz ilipo establish relation na Vetican iliangalia sheria ?
 
Mkandara,
For your information kuna jeshi znz linaitwa KMKM and it has nothing to do with Tz, kwa nini ikifika siku za uchaguzi halipelekwi hilo tu?. Infact wanapelekwa mpaka majeshi wa zimbabwe na trick zote za kuiba matokeo ya uchaguzi ni the same na yale ya zimbabwe. Mimi naona hii multi party system ni fitna aliotuachia Nyerere kwani miaka yote aliotawala yeye mbona hakufanya multi party ? I think we are not ready for the real democracy, kwani ukienda huko zenji wanakwambia " Ehh bwana ati serikali tumepindua kwa mapanga hatuwezi kuitoa kwa vikaratasi " Tujifundisheni kutambaa kabla ya kutembea. Tushukuruni sasa tuna Internet , saterlite dish anterna na uwezo wa kutembelea dunia nzima kwa hivyo tu-import mazuri ya wenzetu waliotutangulia sio tunarudi na vidani na marasta na kuona huo ndio ustarabu. Wake up my beloved Tz.
 
Jamani waende tu wachimbe mafuta yao, hatuwahitaji
Great, great, ndoa inapofungwa na wawili inaweza kuvunjwa na mmoja.

Kama zanzibar wanaona wanaonewa wajiondoe mapema wasitubabaishe hata kidogo. KWA VILE WAO NI FIRST BENEFICIARIES AND FIRST COMPLAINERS! NDIYO MAANA WANAJUA NA HAWAJIONDOI NG'oooooooooooo!!

ONDOKENI MWAMBIE KARUME ATANGAZE KUJUIONDOA ILI KAMA TANNANYIKA ITANG'ANG'ANIA BASI uN IIINGILIE KATI ILI MUACHIWE MWENDE KWA WAARABU WENU.

MSITUBABABISHE JIONDOE HARAKA SANA
 
..aah mwacheni abwatuke.

..kwani hamkusikia matusi aliyovurumisha yule waziri Himid wa Zenj.

..yaani kila siku waZenj waruhusiwe kutoa madukuduku yao sisi Watanganyika tukae kimya.

..Pinda kawaambia ukweli kwamba kama wanataka kujiunga na OIC,FIFA etc wajaribu. Pinda anajua vyombo hivyo vinaitambua Tanzania na siyo Zenj.
Kwani umesahau matusi ya DR Idrisa juu ya umeme? Hivyo si nyie mlioshangiria eti hawalipi umeme mnaodai kuwa ni wenu ? Sasa kwa chao mnaona kuwa ni matusi? Ama kweli mbabe ndie mwenye haki ya kuoneya.
 
Pinda, ana haki kabisa kufikia aliposema kwani ni dhahiri hata kwa mtu asiyejua mambo ya kiutawala kuwa SMZ na Karume wanatafuta upenyo kuvunja muungano. Lakini wanashindwa kusema waziwazi, itakuwaje SMZ itoe uamuzi katika baraza la uwakilishi na kama si tamko la serikali basi Karume alitakiwa aelelze umma. Hata kukosa sherehe za Muungano alifanya makusudi na wote wanajua. Kinachotakiwa sasa ni SMZ waseme wanataka nini, hamlazimishwi muungano. Kama swala ni la kikatiba kwa nini SMZ wasilipeleke lijadiliwe na uamuzi ungetangazwa na raisi wa jamhuri ya muungano. Sasa tunataka kusikia majibu ya baraza la wakilishi na wabunge wa zanzibar, kama wana ubavu wabunge wa Zanzibar si wafunge virago waondoke Dodoma warudi Unguja kujadiriana na Karume.
Hivyo Muungano ni Mafuta tu? Hivyo Zanzibar wakiachiwa mafuta yao kama ilivyo kwa madini yenu ndio Muungano utakuwa basi? Hivyo mlitaka Muungano kwa ajili ya kupata kitu kutoka Zanzibar na kukisoma basi hakuna haja ya Muungano? Niaminivyo mimi Muungano ni zaidi ya upande mmoja kutaka kuhodhi cha upande mwengine. Kama dhana ya Muungano kwenu ni hiyo basi inabidi muelewe kuwa hakuna alietayari kukigawa chake huku mwengine anatumia chake kwa anavyopenda.
 
Great, great, ndoa inapofungwa na wawili inaweza kuvunjwa na mmoja.

Kama zanzibar wanaona wanaonewa wajiondoe mapema wasitubabaishe hata kidogo. KWA VILE WAO NI FIRST BENEFICIARIES AND FIRST COMPLAINERS! NDIYO MAANA WANAJUA NA HAWAJIONDOI NG'oooooooooooo!!

ONDOKENI MWAMBIE KARUME ATANGAZE KUJUIONDOA ILI KAMA TANNANYIKA ITANG'ANG'ANIA BASI uN IIINGILIE KATI ILI MUACHIWE MWENDE KWA WAARABU WENU.

MSITUBABABISHE JIONDOE HARAKA SANA


Mkira mie nadhani hawa twende nao kama Israel na palestina hadi wakiamua kuvaa mabovu basi na Urais wa mwenyekiti baraza na kupindua unafutwa inakuwa completely kuliko hivi sasa .

Watu bwana .KMKM ni jeshi kweli ama msemaji wa hili hajua tofauti ya jeshi na KMKM ?
 
Jamani shule shule shule .Hawa jamaa wana endekeza u mimi na udini na shule hawana .Wanadhani hata wao watalii wanao jazana kwao ni kwa kuwa ni Zanzibar ama ni Tanzania ? Jamaa hawa wana ndamu za kiarabu na akili za kitumwa they think no far from where they in their cage .
Leo Muungano ukifa hakuna sifa ya Zanzibar .Jamaa hawa wana matatizo sana .Ni wakati sasa wa Amiri jeshi Mkuu JK kusema ujinga mwisho na Karume fuata tunayo yasema .Yes we can do that .Sasa nimeona why CUF haitakaa itawale Zanzibar .

Hawa ni sehemu tu na ni mkoa waache wapike kelele .Pinda sema bwana labda JK mtu wa pwani mwenzao anawaonea haya .Mwaka Mkuu wa Majeshi yuko bara na anakohoa hadi kule ushenzini kwa wavivu wa kufikiri .
Tumechoshwa na vijitabia vya watu wavivu wa kazi hadi kufikiri .
Hakuna OIC , Kadhi undeni wenyewe na Muungano upo .Mkitaka tuone mko serious kuuvunja Wabunge wa Zanzibar wasije Dodoma wakae kule kwao waendelee na misimamo .Mnafanya nini huku ? Si mbakie kwenu muendelee kudai mnayo yataka ?

Kama shule za huko zimeendwa na watu kama nyinyi sishangai kuwa mbali ya majilabu yenu bado hamna na maana la kuonyesha kwa hiyo elimu unatoiita.
Hivyo unaikiri Zanzibar inahusishwa na Tanzania huko nje ya nchi? Nikupe mfano mmoja. Niliwahi kujieleza kuwa mimi ni Mtanzania na nilpoeleza kuwa natoka Zanzibar Msomi mmoja alinishangaa na kusema anashangaa kua nimetanguliza Utanzania kabla ya ya Uzanzibari.
Kuhusu damu ya Wazanzibari hilo lisikupe tatizo wanachotaka Wazanzibari ni kujiendeleza na mfumo wa Muungano wa sasa hautowi nafasi hiyo. Zanzibar ndani ya Muungano ikimiliki chake nini tatizo after all ni nyie mliotufunza hilo kwa kungangania madini yenu.
Isitoshe unachonesha wewe si chengine bali nichoyo na chuki kwani kama Zanzibar itaachiwa ijiamulie mambo yake mambo yatarudi kama hapo mwanzo.
 
Hawa wanataka kuwa kama Somalia, miaka mingapi sasa hakuna serikali ni kuchinjana kwa zamu tu , na kujitenga Somali Land na Somali ya kusini yenye mapigano mpaka leo au waangalie yalitokea Comoro na hivyo visiwa vitatu Anjoun, Great Comoro sijui nani mpaka majeshi yetu yalienda ku-restore order.
Leo hii ukiwaambia hao wavisiwani ondokeni Namanga, Buguruni, etc etc utasikia kilio chao, kama wanaona Zanzibar kuna rasilimali au utajiri wanao upigia kelele, why invest Bara?
Lazima waju kitamu pia kina uchungu, kama wanataka hiyo faida bara ya kuishi kwa amani, kufanya biasha, kujenga nyumba, basi ni lazima na machungu yake wayakubali.

Hayo ni matusi kwa upande mwengine na sio Zanziar. Nafikiri umepumbazwa na chuki au si mwelewa. Hivyo umeona Zanzibar kuna kanda maalum za kipolisi? Kama huna hoja basi bora ubaki kimya.
 
The Zanzibari want to go seprate ways. Honestly, I don't see how Tanganyika loses by letting them go. This Union thing and the discussion has been going in circles. Slowly everyone is losing their cool. Pinda, and Seleli for asking that question, have started taking the bull by its horns: the road towards separation... which, to my opinion, will be better for both, remember the majority were not invloved to begin with.

Are Oil and gas everything in this Tanzania Union? If so this Union is useless and has no value to each sides because our President has since assured us that there is no oil in Zanzibar. My regret is the cost and time one side has used to wait for that oil.
If the picture is contrary to what I have guessed above I think we have to listen to each other demands through negotiation and not threat more from the stronger side.
 
Back
Top Bottom