Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,744
Ndugu Mkandara ,haiwezekani kama kweli tunataka kujenga umoja huu ,lipekwe jeshi kwenda kuwapiga WaPemba ,tena jeshi hili sio la Zanzibar linatumia nembo ya Muungano kila unapokaribia uchaguzi inakuwa ndugu zetu wa Pemba hawana raha ,hivi kosa lao ni kitu gani hapa Tanzania ? kuikataa CCM ndio vitumike vyombo vya Muungano kuwakandamiza na kuwatesa ? watavumilia mpaka lini ? hivyo popote pale wanapoona kuwa kuna pengo la Muungano nao watajitosa na kuwa mstari wa mbele kwa maana wameshaona Muungano unawaletea mateso kila baada ya miaka mitano ,wao wameshasema kuwa CCM isitegemee kupata ushindi wa kura ,huko wasahau ,sasa sababu wanazijua wao zaidi na hili linasababishwa na vyombo hivi kuhusishwa kwenye siasa moja kwa moja. Hivyo litakalo tokea na litokee kama kufa muungano wacha ufe Pemba na Unguja watajijua wenyewe lakini isiwepo sababu ya WaTanganyika kutumiwa kwenda kuuwa Pemba hilo ni kosa lililomo ndani ya vyombo vya Muungano ,Wapemba wataungana na Waunguja kuukataa Muungano japo wenyewe wana mambo yao ,ndivyo ilivyotokea Somalia ilipovamniwa na majeshi ya kigeni ,Mmarekani na madege yake alikimbia hadi leo hataki hata kuiona.