Zanzibar will remain to be part of URT kwa sababu tangu mwaka 1964 sijasikia wazanzibari wakitaka kuvunja muungano kwa kutumia njia rasmi. Wazanzibari wanaihitaji bara kuliko bara inavyoihitaji Zanzibar.
Mwisho, historia ya Tanganyika na Zanzibar inadhihirisha wazi umuhimu wa muungano huo, kwani wengi waliopo sasa hivi visiwani humo ni jamii ya wabara waliohamishwa huko miaka mingi iliyopita.
Suwala linakuja hapa kuwa Uzanzibari si kuzaliwa Zanzibar bali ni ukaazi wa sehemu hiyo. Wazanzibari hawagombanii kuiondowa Zanzibar na kuiweka mbali na Bara hilo haliwezekani. SUALA hapa ni masilahi ya Zanzibar na wakazi wake . Hivyo tunategemea mkaazi wa Zanzibar akose huduma muhimu eti kwa sababu waliobara wanaamuwa maisha yao? Si mwenye damu ya Kiarabu, Kisukuma , Kizaramo au mkiristo au muislamu awepo pahala popote atakaeacha kutetea sehemu aliyopo iwe Mwanza, Kigoma, Pemba atakaeacha kuiteteyea sehemu anayoishi. Kwani hatuoni Wabunge wakigombana na mawaziri kutetea hadhi ya sehermu zao?
Ukiangalia kwa mtazamo huu ndio utaona wenye asili zote kule Zanzibar wanapigania Zanzibar na kwa bahati mbaya Serikali ya Muungano ni double Crosser. Inahubiri Utanzania kwa faida ya upande mmoja na kujivua madaraka ya upande wa pili katika masuala ya kuiendeleza Zanzibar. Wazanzibari wanahisi basi watumie kilicho chao (mfano mafuta) kujiendeleza. JEE WAUNGWANA HILO NI BAYA?