Pinda, Muungano, na Hatima ya Zanzibar

Wana JF Mh. Pinda ni mtu makini sana, mtegemee kuwa atakuwa rais baada ya JK.
Wazanzibar wanachotaka kufanya ni sawa na Sungura kuomba ngono kwa Tembo.

Ni kweli nakubaliana na wewe kuwa Mh pinda ni makini isipokuwa watu wake anaowaongoza ndio mbinde,hivi karibuni aliwahi kusema kuwa Rais Mstafu Ben mkapa ni mtu safi hata mie naelewa hivyo kuwa yule Mkapa ni mtu wakanisa na ni mtu safi kama alivyokwisha sema pinda sasa utakuta watu humu eti wanakejeli na kusema yeye ni mwizi kaiba cha nani ?hata Rasi wetu amesha sema achiliwe mzee mkapa apumzike sasa nyie wengine hamtaki .(wajinga ndio waliwao)
 
Tatizo lilipo ni la kihistoria, kuwa kila mtu hataki muungano umfie mikononi mwake. Hawa viongozi wa zanzibar wanaopiga kelele ni wahuni wachache wanaojitafutia umaarufu ili waendelee kushika nafasi za kudhulumu wanzanzibar wengi.

Hebu iitishwe referendum ya muungano kama walivyopendekeza kwenye muafaka na CUF. referendum isimamiwe na agency isiyokuwa na upande wowote kama UN. Na kauli za wananchi ziwe za mwisho ili tusisikie tena madai ya mchezo wa watoto kukaa kando ya barabara ili kuona ni nani wa kwanza kutamka kwa kila gari linalopita kuwa ni "langu", mwezio aking'ang'ania naye lake mnazusha ugomvi na kuumizana na "kugayana"-kuacha urafiki kwa magari ambayo hata wenyewe hamuwajui ni kina nani.

Hii kauli ya mafuta, mafuta, wakati hata kupatikana hayajapatikana ni sawa na mchezo huu wa watoto.
 
sasa naanza kumwelewa Mwalimu kwa nini miaka ya 1960 alisema kuwa angekuwa na uwezo angevisukumia mbali kabisa hivi visiwa!

kusema ukweli wakati nasoma shule ya msingi mi nilijua zanzibar na pemba ni mikoa tu kama mikoa mingine!

Sasa cha kufanya...iitishwe kura ya maoni,, na maoni ya wananchi yazingatiwe...ikionekana muungano uvunjike..basi..tutaitana tena, ule udongo nadhani unaweza kutenganishwa hata maabara....kila mtu kinamna yake....kwenda zenji kwa passport sidhani kama ni a big deal...ila wajua kuwa na waliopo bara wajiandae kurudishwa kwao na kuja huku bara ni kwa visa

ya nini kuendelea kupata chokochoko hizi kila siku wakati we feel kwamba tumewabeba vya kutosha? iweje watu takriban milioni moja wawe na HAKI zaidi ya watu milioni 39? hii mfano wake wapi jameni?
 
sasa naanza kumwelewa Mwalimu kwa nini miaka ya 1960 alisema kuwa angekuwa na uwezo angevisukumia mbali kabisa hivi visiwa!

kusema ukweli wakati nasoma shule ya msingi mi nilijua zanzibar na pemba ni mikoa tu kama mikoa mingine!

Sasa cha kufanya...iitishwe kura ya maoni,, na maoni ya wananchi yazingatiwe...ikionekana muungano uvunjike..basi..tutaitana tena, ule udongo nadhani unaweza kutenganishwa hata maabara....kila mtu kinamna yake....kwenda zenji kwa passport sidhani kama ni a big deal...ila wajua kuwa na waliopo bara wajiandae kurudishwa kwao na kuja huku bara ni kwa visa

ya nini kuendelea kupata chokochoko hizi kila siku wakati we feel kwamba tumewabeba vya kutosha? iweje watu takriban milioni moja wawe na HAKI zaidi ya watu milioni 39? hii mfano wake wapi jameni?


Great great! haya ndiyo mawazo yangu siku zote!

Ifike mahali tuwaulize tena wao wenyewe kama wanautaka muungano au la!

Kumbembelezana hadi lini? Homgera Pinda. Utaona hata humu jamii forum wananung'unika eti Pianda mbabe! mbona wao wamewaita vinogzi wa Bara wakolono hatukusukia mkisewasema wanzibari wababe?

Ukweli ni kwamba muungano ukivunjika watakaopoteza ni wazanzibari! HUO NDIO UKWELI KABISA!!

ZANZIBARIS ARE THE FIRST BENEFICIARIES OF MUUNGANIO BUT THEY ARE THE FIRST COMPLAINERS!!! BY MKIRA.

SOME OF US WE ARE TIRED KUBEMBELEZA OLE JIONDOENI KATIKA MUUNGANO TENA HARAKA!!
 
Nimekua nikifuatilia mjadala huu katika thread hii tangu ianze, nilichokiona ni kuwa wanaojadili wengi wao wametawaliwa na ushabiki kuliko kufikiria hali halisi ya jambo lenyewe. Mimi nafikiri wanasiasa wetu ndio chanzo cha malumbano yasiyokwisha kuhusu huu muungano wetu, sidhani kama raia wa kawaida awe kutoka Zanzibar au Tanzania Mainland ambaye ukimuuliza kuhusu muungano atakupa jibu la kutaka uvunjike kwa sababu wote wana maslahi na muungano huu. Muungano wa Bara na Visiwani haukuanza mwaka 1964 kwa kuwekwa sahihi za viongozi wa wakati ule Nyerere na Karume bali ulianza kwa karne nzima huko nyuma, wananchi wa Zanzibar na wa Tanganyika walikuwa na maelewano ya kijamii na kifamilia kabla ya hata nchi hizi kuungana na baada ya kuungana na kuwa Jamuhuru ya Muungano wananchi hawa wamezidi kuwa karibu kwa kila jambo katika maisha.
Wanasiasa wa leo ni watu hatari sana, hata muungano wa kisovieti ulivunjwa na wanasiasa, ule uliokuwa East African Community ya mwanzo pia ulivynjwa na wana siasa kwa uroho wao wa mali. Kwa hiyo hizi kelele zinapigwa na wanasiasa kwa maslahi yao yasiyo na tija kwa wananchi wote.
Tumeona kule Zanzibar wakati wa rais wa pili Aboud Jumbe, muda wake wa uongozi ulipokaribia kumalizika na alivyoona anaukosa urais wa Tanzania alitaka kuiondoa Zanzibar kwenye muungano akashtukiwa na CCM kilichofuata mnakijua, vile vile Salmin Amour naye muda wake ulipokaribia kumalizika alitaka kubadilisha katiba ya Zanzibar ili ajizatiti kwenye madaraka.
Mawaziri wa Kizanzibari kwenye Jamhuri ya Muungano kama utawauliza kuhusu muungano watakwambia kuwa wanataka udumu milele, lakini baadhi yao wakiondoka katika madaraka hao hao watakwambia muungano huu hauinufaishi Zanzibar.
Hata wapinzani ndani ya CUF kwa sababu hawana Serikali wanauponda muungano huu lakini hawana kitu mbadala ambao ukiuondoa huu wataleta nini.
Kwa hiyo tukubali kuwa wanasiasa ndio watu wa kuwaogopa kwani wao kauli zao ndizo ziinazochochea kutaka kuvuruga muungano huu kwa uchu wao wa madaraka.
Turudi kwenye usemi wa Umoja ni Nguvu utengano ni Udhaifu.
Hizi kelele za wanasiasa kwa watu wenye akili timamu haziwasumbui.
 
sasa naanza kumwelewa Mwalimu kwa nini miaka ya 1960 alisema kuwa angekuwa na uwezo angevisukumia mbali kabisa hivi visiwa!

kusema ukweli wakati nasoma shule ya msingi mi nilijua zanzibar na pemba ni mikoa tu kama mikoa mingine!

Sasa cha kufanya...iitishwe kura ya maoni,, na maoni ya wananchi yazingatiwe...ikionekana muungano uvunjike..basi..tutaitana tena, ule udongo nadhani unaweza kutenganishwa hata maabara....kila mtu kinamna yake....kwenda zenji kwa passport sidhani kama ni a big deal...ila wajua kuwa na waliopo bara wajiandae kurudishwa kwao na kuja huku bara ni kwa visa

ya nini kuendelea kupata chokochoko hizi kila siku wakati we feel kwamba tumewabeba vya kutosha? iweje watu takriban milioni moja wawe na HAKI zaidi ya watu milioni 39? hii mfano wake wapi jameni?

Nivizuri kumuelewa Mwalimu sasa hebu nikulize hukumuelewa mwali pale miaka ya 1970 aliposhauriwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar waweke Tv Tanzania, mwalimu akasema yeye hataki kuwepo TV Tanganyika, na sabau zake alisema kuwa watanganyika wataiga mambo ya west, lakini rais wa zanzibar yeye aliwaekea wanachi wake .sasa huoni kuwa mwalimu alijuwa kuwa nyinyi ni watu wepesi wa kuona mambo na kuiga na ndio leo pinda anapiga kelele eti watu wanacheza ngoma uchi na kutembea uchi sasa hayo ndo mambo mwalimu aliyaogopa mapema .
 
Mimi nafikiri imefika wakati wa kupima mambo.

Ningekuwa mimi Pinda na JK mwakani ningewapa waZanzibari mtihani mdogo tu, yani waendeshe uchaguzi wao wenyewe bila serikali ya muungano kuwaangilia .
 
Nivizuri kumuelewa Mwalimu sasa hebu nikulize hukumuelewa mwali pale miaka ya 1970 aliposhauriwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar waweke Tv Tanzania, mwalimu akasema yeye hataki kuwepo TV Tanganyika, na sabau zake alisema kuwa watanganyika wataiga mambo ya west, lakini rais wa zanzibar yeye aliwaekea wanachi wake .sasa huoni kuwa mwalimu alijuwa kuwa nyinyi ni watu wepesi wa kuona mambo na kuiga na ndio leo pinda anapiga kelele eti watu wanacheza ngoma uchi na kutembea uchi sasa hayo ndo mambo mwalimu aliyaogopa mapema .

Tafadhali jadili mada......hizo habari za TV na ngoma zinatoka wapi?
 
kusema ukweli wakati nasoma shule ya msingi mi nilijua zanzibar na pemba ni mikoa tu kama mikoa mingine!
usiseme zanzibar sema unguja
hivi kwa nini unguja ndiyo inajulikana kama zanzibar
uwoni kama huu ni ubaguzi kwa wapemba
ndio maana wapemba wanajiona sio sehemu ya zanzibar

hili tatizo pia lipo kwenye TZ. bara ndio inajulikana kama TZ
na hii inawafanya wa zenji wajione kama wao sio wa TZ
 
Hivi wabara mnautaka Muungano au hamuutaki ? Mbona mna makelele mengi ,tumeshasema na tutaendelea kusema kama mnatudidimiza na kutukandamiza na kutuuwa na kutudhalilisha ,sasa mkiipenda kauli hiyo msiipende kazi kwenu na tutaendelea kusema tu mpaka mmwage chozi.
 
Tafadhali jadili mada......hizo habari za TV na ngoma zinatoka wapi?

Ala hivyo ukweli unauma ehe?hutaki kulisika hilo ?ni miongoni ya kauli za Julias kambarage kama zilivyo kauli nyingine ikiwemo hiyo ya kutaka kuviangamiza visiwa vya zanzibar visikuwepo katika milki yake, kwa maana nyingine alitaka kufanya kazi ambayo ni Mmungu peke yake huifanya ,haishangazi kwa kauli yake hiyo, walikuwepo watu kama yeye na kujitangazia kuwa wao ni WAUNGU lakini ilipofika siku yao wangu hao waliaga dunia yao kama alivyoaga julias kambarage upande huu wa dunia yake.
 
UMOJA, UHURU, UADILIFU

Qauli ya Umoja wa Wazalendo
Kukhusu Maelezo ya Mhishimiwa Waziri Mkuu
Bwana Pinda juu ya huu wenyekuitwa muungano

Kwa hishima tunaleta hapa yale yalioandikwa kwenye gazeti la “MWANANCHI” la Ijumaa, taarikh 24 July, 2009 kukhusu maelezo ya Mhishimiwa Waziri Mkuu, Bwana Mizengo Pinda juu ya huu wenyekuitwa muungano. Maelezo yetu, sisi Umoja wa Wazalendo; tumeyabainisha kwa khati za italic.

Pinda: Vunjeni tu Muungano muone

ASEMA UKIVUNJIKA UPANDE MMOJA UTASAGA MENO

Habel Chidawali, Dodoma

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameonya uwezekano wa Muungano kati ya Tanzania Bara na Zanzibar kuvunjika endapo malumbano kuhusu gesi asilia na mafuta yalioanza sasa yataendelea na kuonya kwamba baada ya hatua hiyo upande mmoja utapata shida. Wazee wetu wanasema: “Aliezama hachelei kutota”. Sisi Wazanzibari kwa hivi kuvamiwa Dola yetu ya Zanzibar siku ile ya Januari 11, 1964 na kutiwa chini ya ukoloni wa Tanganyika; siku ile ya April 24, 1964 ni kupotezewa kila chetu, ndipo tulipozamishwa; kwahivyobasi sisi Wazanzibari si wenye kuchelea kutota, madhali tushazama.

Pinda alitoa onyo hilo bungeni jana, wakati tayari viongozi wawili wa ngazi ya juu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) walishatoa msimamo rasmi wa kutaka suala la mafuta na gesi asilia liondolewe katika orodha ya mambo ya Muungano. Si suala la kutaka lifanywe, ni suala lenye kutekelezwa.

Viongozi hao ni Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansour Yusuf Himid ambaye alitoa msimamo wake wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2009/2010 katika Baraza la Wawakilishi Mjini Zanzibar. Inapasa ifahamike kwamba huu si msimamo wa Mhishimiwa Mansor binafasi yake, huu ni msimamo rasmi wa Sirikali ya Zanzibar uliokubaliwa na Baraza la Wawakilishi na Baraza la Mawaziri na kutolewa na yeye Mhishimiwa Mansour kwa vile hili suala linakhusiana na wizara yake. Wazanzibari kwa khatuwa ya kuthibitisha huu msimamo wa Sirikali ya Zanzibar, na msimamo wa Wazanzibari wote kwa jumla ndio ikapangwa kufanywa maandamano kuungamkono suala hili. Maandamano haya yalikuwa yahudhuriwe na Wazanzibari kutoka kila pembe, mashamba na mjini. Inaaminika na wengi kwamba ni amri ya Bara ndio kuzuiliwa maandamano haya, wakikhofia kudhihiri mshikamano wa Wazanzibari katika kuhami haki na milki zao.

Naye Naib Waziri Kiongozi Zanzibar, Ali Shamhuna, amewahi kutoa kauli kama hiyo akidai kuwa suala la mafuta ni la Zanzibar peke yake, Bara hawahusiki nalo. Hapana shaka mali ya Zanzibar ni kwa Wazanzibari.

Pinda alitaka Watanzania kuangalia jambo hili ili kujua nani ataathirika zaidi endapo jambo hilo litafanyika. Wazanzibari kimsingi hawaoni kuwepo nguvu za hoja katika kulizingatia suala hili katika hoja ya kuathirika kwa kuvunjika huu wenyekuitwa muungano. Hoja yetu ni kama tulivyoeleza hapo juu, yaani; “aliezama hachelei kutota”. Kurejea Dola Huru ya Zanzibar ni haki ya maumbile.

Alisema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Nzega, Lukas Selelii aliyetaka kujua sababu za viongozi wa juu akiwamo Rais Jakaya Kikwete kuwa kimya kuhusu jambo hilo ambalo linaonekana kuuweka Muungano katika hali tete. Akijibu swali hilo, Pinda wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo bungeni jana, alieleza wasiwasi wake kuhusu jambo hilo akisema kuwa likitokea lazima kuna upande ambao utaathirika, bila ya kutaja ni upande gani. “Kama kuna uwezekano jambo la mafuta na gesi asilia kuondolewa katika Katiba ya Muungano ambako liliingizwa mwaka 1968 itakuwa ni jambo la heri, lakini sio kuvunja Muungano,” alisema Inapasa ifahamike kwamba kulingana na misingi ya Umoja wa Wazalendo, suala la mafuta na jengine lolote lile lenye kukhusiana na huu wenyekuitwa muungano ni matawi ya mti uliooza, kwahivyobasi; madhali mti umeoza haitarajiwi matawi kuwa na uhai. Vilevile, ni imani ya Umoja wa Wazalendo kwamba linalojengeka juu ya haramu ni haramu, hivi ni kwamba huu wenyekuitwa muungano umejengeka juu ya haramu – haramu ya kuvamiwa Dola huru ya Zanzibar – kwahivyobasi; kila lenye kujengeka juu ya huu wenyekuitwa muungano ni haramu. na kuongeza: “Tumekuwa tukipata tabu sana na kusumbuliwa na kauli zinazotolewa na baadhi ya wenzetu. Mara tunaambiwa kuwa ni wezi wa mchana, wakati mwingine tunaambiwa kuwa ni wakoloni…. Suala la kuambiwa Tanganyika ni wakoloni wa Zanzibar hilo halina shaka, ni ndivyo kabisa. Si tu ni wakoloni, bali ni wavamizi wa Dola huru ya Zanzibar, ni wakoloni kuliko wakoloni Waingereza walioondoka. Wakati wa wakoloni Waingereza Zanzibar iliendelea kuwa Dola Kaamili, lakini kwa ukoloni wa Tanganyika imepotezwa Dola ya Zanzibar kwa huu wenyekuitwa muungano. Kheri ya mkoloni Muingereza kuliko mkoloni Tanganyika. Ahaa jambo hili linanisikitisha sana…., ipo siku muungano utavunjika na ikifika hatua hiyo, nina hakika upande mmoja wa muungano utaathirika.” Ilipovimiwa Dola ya Zanzibar, ilikuwa na kila uwezo na nguvu kamili za kidola; haikuwa masikini au faqiri wa lolote lile. Zanzibar juu ya kuwa imedhiliwa na kufukarishwa katika hiki kipindi cha miaka arubaini na tano ya utawala wa Tanganyika, mpaka leo Zanzibar inao uwezo kaamili wa kujiendesha katika hali ya salama, amani na kila mafanikio na maendeleo, muhimu ni kutoka chini ya huu ukoloni wa Tanganyika na kurejea kuwa Dola Huru Kaamili kama ilivyokuwa kabla ya huu wenyekuitwa muungano.

Katika swali lake Selelii alimtaka Waziri Mkuu aeleze ukimya wa viongozi wa juu akiwemo Rais wa Jamhuri pamoja na Rais wa Zanzibar kuhusu jambo la mafuta ambalo linaonekana kuuweka Muungano katika hali tete. Zanzibar, wananchi na Sirikali yao, suala hili la mafuta wamelibainisha wazi kabisa kama vile ilivyoelezwa na Mhishimiwa Mansour katika Baraza la Wawakilishi (Bunge la Zanzibar). “Mheshimiwa Waziri Mkuu, kumekuwa na maneno ambayo yanaonekana kuuchokonoa Muungano kutoka kwa baadhi ya wabunge pamoja na Baraza la Mapinduzi Zanzibar ambapo sote tuliapa kuulinda na Katiba yake; lakini viongozi wa juu mmekuwa kimya sana, hamuoni kuwa hivi ni viashiria vya kuvunja Muungano?”alihoji Selelii. Kama tulivyosema hapo juu, na tunavyosema daima; kwamba lenye kujengeka juu ya haramu ni haramu, kwahivyobasi, kuapa kulinda haramu ni haramu; kwahivyobasi, kiapo hiki ni haramu.

Akijibu swali hilo, Pinda alitumia baadhi ya maneno ambayo yalitolewa katika hotuba ya Rais Jakaya Kikwete Juni 26, mwaka huu akisema: “Hata rais alishasema na kukemea juu ya jambo hilo”. Pinda aliongeza: “Rais alishasema kuwa mafuta hayajapatikana na huenda yasipatikane kabisa. Ikiwa hii ndio hali, basi kwa nini mayowe yote haya? Kiongozi wa nchi alionya juu ya malumbano hayo na kuagiza kuwa yaachwe mara moja”. Alifafanua kuwa ilishaundwa tume ya wataalamu kutoka nje ili kuangalia uwezekano wa namna bora ya kuzishauri serikali mbili juu ya kugawana pato litakalotokana na mafuta na kwamba, tume ilishawasilisha taarifa yake ndani ya serikali tangu Juni 23 mwaka huu. Alisema tume iliyoundwa ambayo iko chini ya ofisi ya Makamu wa Rais inafanya utaratibu mzuri wa kuangalia masilahi kwa pande zote mbili ndani ya Muungano ili kutoa nafasi sawa. Imeshaundwa tume ya wataalamu kuzishauri sirikali mbili juu ya kugawana pato litakalotokana na mafuta. Maelezo haya ni kinyume kabisa na maelezo hayo hapo juu kuwa “mafuta huenda yasipatikane kabisa”.

Hata hivyo, akijibu swali lingine lililohusu Muungano, Waziri Mkuu alionekana kuwa na hasira baada ya kujibu swali lililohusu Katiba ya Muungano ambalo alilijibu kwa mkato tena kwa hasira. Mhishimiwa Waziri Mkuu, hasira hizi ni za nini? Kwa nini kuwacha nguvu za hoja na kuingia kwenye hoja za nguvu, yaani vitisho na hasira? Swali hilo liliulizwa na Yahya Issa mbunge wa Chwaka (CCM) aliyetakakujua juu ya Zanzibar kuingizwa katika ushirikiano wa Kimataifa. Issa alisema kuwa kutokuingizwa Zanzibar katika ushirikiano wa Kimataifa ni njia moja wapo ya kuinyanyasa Zanzibar kwa kuwa jambo hilo halipo ndani ya Katiba, hivyo upande huo wa pili wa nchi ni kama unakandamizwa. Akijibu swali hilo, Pinda alisema Katiba ya Muungano ndio mwakilishi wa nchi ya Zanzibar pia, hivyo upande huo wa pili wa Zanzibar utaendelea kuwakilishwa na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa siku zote. “Mkitaka mjaribu muone kama kuna urahisi katika jambo hilo,”alijibu Pinda kwa mkato. Mhishimiwa Waziri Mkuu, hapana shaka ni vyema kutumia busara katika utekelezaji wa dhamana; inatarajiwa mfano mwema.

Wakati huo huo, Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohamed amepinga majibu ya Pinda, akidai kuwa chokochoko za Muungano zilianza tangu wakati wa hayati Karume na Mwalimu Nyerere. Kwa hakika si chokochoko, bali ni madai ya Wazanzibari ya kutaka kurejea Dola Huru Kaamili ya Zanzibar na kutokana na ukoloni wa Tanganyika. Alisema katiba ya Muungano ndiyo kikwazo kikubwa kwa kuwa iliongezwa vipengele ambavyo havikuwepo awali. Mzizi wa ukoloni huu wa Tanganyika juu ya Zanzibar ni zile “Articles of Union, 1964”, ambazo zimeipoteza Dola Huru ya Zanzibar kwa kisingizio cha huu wenyekuitwa muungano. “Kuongezwa kwa vipengele hivyo kulitokana na Katiba ya muda ambayo ilikuwa imepanga kuwa kabla ya mwaka kumalizika, baada ya muungano, kuwe na katiba ya kudumu, lakini haikutekelezwa badala yake ikakamilishwa baada ya miaka saba,” alisema Rashidi. Aliyataja mambo yaliyoongezwa katika kipindi hicho kuwa ni pamoja na suala la mafuta ambalo mwanzo halikuwepo.

Aliongeza kuwa jambo lingine linaloyumbisha Muungano ni pamoja na kuondolewa kwa wadhifa wa Rais wa Zanzibar katika nafasi ya makamu wa rais wa Muungano. Alisema hakuna usawa wa kimasilahi kwa nchi hizo mbili kutokana na upande mmoja kupata masilahi zaidi ya upande wa pili.

Sio kupata maslahi zaidi, bali ni kujipa maslahi zaidi. Umoja wa Wazalendo unasisitiza juu ya msingi wa imani yake, kwamba kilichojengeka juu ya haramu ni haramu. Katika msingi hii, na kupotezwa Dola ya Zanzibar ndio Umoja wa Wazalendo kuendelea kuwania kwa kila njia na hali za amani kurejea Dola Huru Kaamili ya Zanzibar kama ilivyokuwa kabla ya huu wenyekuitwa muungano.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, Subhaanahu wa Taáala atujaalie kila kheri na atuepushe na kila shari, Aamyn.

Wa Billahi Tawfiiq

Umoja wa Wazalendo

Zanzibar
July 24, 2009
 
Si mjitoe tu huo muungano nyie Wazanzibari halafu muwe koloni la Waarabu,lakini msisahau muda si mrefu Sharia itapiga hodi ikifuatiwa na Al Qaeda kwanza mimi nashangaaaa sana tunawabembeleza hao wazanzibari sijui kwa kitu gani jamani waacheni wajiunge na hao waarabu wao wa Omani then kwa wao wanaovyoona ndio wataendelea,nawakumbusha tu baadaye nao wapemba watataka kujitenga baadaye watumbatu then wangazija na tena wamakunduchi eh orodha ni ndefu .Hata kwenye ndoa mkeo akianza kulalama jua kuna mtu anamchombeza kwa pembeni,haa ndugu zangu Wazanzibar ama kwa hakika hamna shukrani,hayo mafuta imekuwa nongwa ,mangapi mnafaidi katika huu muungano ilihali hao watanganyika wenyewe wa huko geita hawapati.
 
Hakika porojo tu, hakuna hoja ya maana katika hayo waliosema hao wajiitao umoja wa wazalendo


Ni Porojo au ni ukweli. Kwani si Wazanzibari wanadai kilicho Zanzibar? Akili ya kawaida inasema " Sitaki mwenziwe BASI"
 
Stori hii ya muungano inafanana sana na maisha ya ndoa zetu za kiafrika. Utasikia mkitofautiana na mwanake, anasema, nipe taraka, nirudi kwetu, ulitoak kwetu, nakula nashiba, hapakuwa na tatizo kwetu. Basi unamuuliza, kwani lazima nikutimue, nauli si unayo, sasa si uondoke tu, kwani lazima hadi niseme? Sasa hawa jamaa zetu wazenj, kwa nini wasijichomoe wenyewe, kwani hadi bara tuseme ndo waondoke. Kama mtume alivyoonya mwanamke anayemsema sana mumewe hadharani, ndivyo zanzibar inavyoonywa kupiga lele ovyo. Shauri lenu, mtajaangukia pua!!!!
 
Back
Top Bottom