Pinda, Muungano, na Hatima ya Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda, Muungano, na Hatima ya Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Babylon, Jul 23, 2009.

 1. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Pinda kwa mara nyinge amejitokeza na kuwadhihirisha wazanzibari nini kina ajiria katika akili yake,kwani siku zote inapofika wazanzibar kupigania haki yao anakuwa hafurahi ni zahiri shahiri haya yote hutokea pale tu wazanzibari wanapodai haki zao kwa mfano mambo kujiunga na mashirika ya kisilamu ,michezo mengineno ,binafsi nakushukuru kwa kauli yako kwani ndizo zinazo waamsha waliolala, kwa mara nyinge tena nasema asanta mzee pinda (lakuvunda halina Ubani) endelea kuwafokea,na vitisho vya hapa napale.


  Pinda awapasha wazanzibari

  Imeandikwa na Mgaya Kingoba;
  Tarehe: 23rd July 2009


  Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewatolea uvivu Wazanzibari kwa kuwaeleza kuwa, wanaotaka kuvunja Muungano au kutaka kujiunga na jumuiya za kimataifa nje kama nchi wajaribu na wataona matokeo yake.

  Pinda leo ametoa majibu yanayoashiria kuwa haridhishwi na namna baadhi ya watu wakiwamo wabunge na viongozi wa Zanzibar wanavyojaribu kutaka kupata uwakilishi wa kimataifa nje bila kuihusisha Tanzania.

  Kwa namna alivyojibu bungeni,wanaochokonoa Muungano kwa visingizio mbalimbali vikiwamo vya mgawanyo wa rasilimali pia wanamuudhi.

  Ametoa msimamo huo wakati anajibu swali la papo kwa hapo la Mbunge wa Chwaka, Yahya Kassim Issa ikiwa ni utaratibu wa Bunge kila Alhamisi kabla ya kipindi cha maswali na majibu.

  "Si mjaribu basi huko mnakotaka kwenda, kisha tujajua kama mmepata au la” amesema Waziri Mkuu.

  Wakati anauliza swali hilo, Mbunge huyo alieleza kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inazungumzia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kama mwakilishi wa masuala ya nje, lakini vipi Zanzibar isiwe na uwakilishi wake?

  Waziri Mkuu amesema, “sijui Mheshimiwa Yahya anataka nini kwa swali hili? Kama ni nje tunawakilishwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Wizara hii ni kiungo cha nchi yetu na mataifa mengine.”

  Mbunge wa Nzega, Lucas Selelii (CCM), alisema kazi ya Mbunge ni kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na hivi karibuni kumekuwa na kauli zinazoashiria uchochezi wa kuvunja

  Muungano kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar na hakuna kiongozi ye yote mwandamizi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Rais wala Waziri Kiongozi aliyetoa kauli, hivyo alitaka kupata kauli ya Waziri Mkuu, Pinda.

  Pinda alisema, “nilikuwa nikisubiri sana swali hili, nilijua litakuja kutoka kwa akina Mnyaa (Mohamed Habib, Mbunge Mkanyageni), lakini wamekaa kimya kama wameshabikia yale yaliyotokea.”

  Waziri Mkuu alisema msingi wote wa mjadala huo wa wabunge wa Baraza la Wawakilishi ni suala la mafuta na gesi, ambalo aliongeza kuwa Rais Jakaya Kikwete alishalitolea kauli katika hotuba yake ya miezi michache iliyopita kwa Taifa.

  Waziri Mkuu alisema suala la mafuta na gesi limekuwapo katika mambo ya Muungano tangu mwaka 1968, lakini kutokana na kauli ya Rais, suala hilo halipaswi kuwagawa Watanzania kwa sababu mafuta yenyewe hayajagundulika; hivyo hakuna sababu ya kutupiana maneno makali.

  “Pia suala hili halina tatizo, ni moja ya mambo yaliyoonekana yazungumzwe kwenye Kamati ya Pamoja chini ya Makamu wa Rais. Tukateua Mshauri Mwelekezi ambaye Juni 27 mwaka huu, alikabidhi ripoti yake kwa pande mbili… ingekuwa vyema kupitia hiyo taarifa na kuona jinsi ya kushughulikia suala hili katika Muungano,” amesema Waziri Mkuu.

  Alimshukuru kwa dhati Selelii kuuliza swali hilo, akisema ametiwa simanzi na kauli za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliotoa kauli kama “Wakoloni” na “wezi wa mchana” ambazo Waziri Mkuu alieleza kuwa zimemshangaza.

  “Ni mawazo yangu kuwa Muungano ni mzuri…ipo siku tutafarakana… otherwise(vinginevyo) muwe tayari kujua ni upande gani utaathirika zaidi,” amesema Waziri Mkuu akihitimisha kujibu swali la Selelii.

  Hivi karibuni, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walitangaza kuwa suala la mafuta na gesi linaondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano na Zanzibar itasimamia yenyewe masuala hayo
   
  Last edited by a moderator: Aug 1, 2009
 2. M

  Maquiseone Member

  #2
  Jul 23, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nadhani Mh. Pinda kawapa sawasawa kabisa, kwani kuna baadhi ya wabunge na wajumbe wa wawakilishi wanakuwa kama hawana vision ya mbali juu ya Muungano. Maana mataifa makubwa yanajaribu kutafiuta mbinu ya kuweka nguvu pamoja but huku watu wanatafuta kuvunja hata kadogo kalikopo.
  Issue ni kutafuta jinsi ya kuboresha na pia sometime ni vema kufanya majaribio hasa kwani hebu uvunjike then tuoine nani hasa wataumia kwa tendo hilo.
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hapa ndipo utakapoona kwamba Nahodha, pamoja na shutuma zote alizopewa kwa kukataa maswali ya hapo kwa papo na swala lililo wazi kwamba ni mtu asiyeweza kujibu maswali hapo kwa papo, angalau alikuwa na busara ya kulikubali hili na kukataa kujibu maswali haya.

  Huyu Pinda ameonyesha kukosa diplomasia kwa hali ya juu, kutumia lugha iliyozidi ubabe isivyotakika, kuchocheza moto zaidi badala ya kuzima moto na umangimeza wenye kuhodhi rungu la dola na kulitumia kwa kitisho.

  Jigga alisema "everytime I tried to get out, they pull me right back in".Kila mara Pinda anapotaka kuji-redeem anajivuta mwenyewe right back in the midst of mediocrity.
   
  Last edited: Jul 23, 2009
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Jul 23, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,751
  Likes Received: 4,969
  Trophy Points: 280
  ..aah mwacheni abwatuke.

  ..kwani hamkusikia matusi aliyovurumisha yule waziri Himid wa Zenj.

  ..yaani kila siku waZenj waruhusiwe kutoa madukuduku yao sisi Watanganyika tukae kimya.

  ..Pinda kawaambia ukweli kwamba kama wanataka kujiunga na OIC,FIFA etc wajaribu. Pinda anajua vyombo hivyo vinaitambua Tanzania na siyo Zenj.
   
 5. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Bwatu!

  Atakuja kulia tena...teheteheee 'kayaanza/endelea kupinda':eek:
   
 6. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Pinda kaishiwa hana moja alilowapasha, Wazanzibar weshatowa msimamo wao na alichokionyesha ni kwao ni kuwa yeye Pinda amesikia na yamemuuma na hata bado ataumia sana tu, maana tunajuwa mbinu zake na waziri wake Masha za kuleta machafuko visiwani, tunampa pole Pinda na ajuwe wazanzibar sio wapumbavu tena, watadai haki zao na kila kilichokuwa chao na apwage mpaka achoke. Hatuwezi kuishi kwenye muungano wa dhuluma na kifisadi wa wachache tu kufaidika na wananchi wetu wafe masikini! Wazanzibar tupo tayari kwa lolote.
   
 7. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Chonde chonde usije geuka kuwa wa kidini tena!
   
 8. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Huu mkoa wa zanzibar shida kweli. Ni mkoa umepewa kila kitu na unahitaji kila kitu!
   
 9. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Nani rais wa Kagera..aaaah..... sijuwi Bukoba....????
   
 10. W

  Wandugu Masanja JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2009
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 1,535
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Zanzibar tatizo ni kero za maisha sio za muungano, wanashindwa kugundua baina ya tatizo la muungano na tatizo la maisha, iwapo watapata ufumbuzi wa kero za maisha hakuna kero za muungano, SMT wajaribu kusaidia kutatua kero za maisha kule Zanzibar hatutosikia tena kero za muungano
   
 11. Yombayomba

  Yombayomba JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2009
  Joined: Aug 23, 2006
  Messages: 818
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Pinda, ana haki kabisa kufikia aliposema kwani ni dhahiri hata kwa mtu asiyejua mambo ya kiutawala kuwa SMZ na Karume wanatafuta upenyo kuvunja muungano. Lakini wanashindwa kusema waziwazi, itakuwaje SMZ itoe uamuzi katika baraza la uwakilishi na kama si tamko la serikali basi Karume alitakiwa aelelze umma. Hata kukosa sherehe za Muungano alifanya makusudi na wote wanajua. Kinachotakiwa sasa ni SMZ waseme wanataka nini, hamlazimishwi muungano. Kama swala ni la kikatiba kwa nini SMZ wasilipeleke lijadiliwe na uamuzi ungetangazwa na raisi wa jamhuri ya muungano. Sasa tunataka kusikia majibu ya baraza la wakilishi na wabunge wa zanzibar, kama wana ubavu wabunge wa Zanzibar si wafunge virago waondoke Dodoma warudi Unguja kujadiriana na Karume.
   
 12. A

  August JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna hili suala lingine la mapato ambayo wanaona 4% wanayopewa ni ndogo, je kwanini serikali isiwaachie wakusanye mapato yao kutokana na uvuvi, tcra, kodi pale bandarini angalau kwa miezi sita na wao walipie gharama za ulinzi umeme etc kama nchi iliyo inje ya muungano waone zuri ni lipi.
   
 13. Sekenke

  Sekenke Senior Member

  #13
  Jul 23, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 132
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Muungano ukivunjika, Karume ataweza kujiongezea muda wa kutawala. Hivyo chokonoa chokonoa hiyo ndiyo tuelekeako. Tuliyaona kwa Salmin, hayo yanajirudia.
   
 14. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Jamani shule shule shule .Hawa jamaa wana endekeza u mimi na udini na shule hawana .Wanadhani hata wao watalii wanao jazana kwao ni kwa kuwa ni Zanzibar ama ni Tanzania ? Jamaa hawa wana ndamu za kiarabu na akili za kitumwa they think no far from where they in their cage .
  Leo Muungano ukifa hakuna sifa ya Zanzibar .Jamaa hawa wana matatizo sana .Ni wakati sasa wa Amiri jeshi Mkuu JK kusema ujinga mwisho na Karume fuata tunayo yasema .Yes we can do that .Sasa nimeona why CUF haitakaa itawale Zanzibar .

  Hawa ni sehemu tu na ni mkoa waache wapike kelele .Pinda sema bwana labda JK mtu wa pwani mwenzao anawaonea haya .Mwaka Mkuu wa Majeshi yuko bara na anakohoa hadi kule ushenzini kwa wavivu wa kufikiri .
  Tumechoshwa na vijitabia vya watu wavivu wa kazi hadi kufikiri .
  Hakuna OIC , Kadhi undeni wenyewe na Muungano upo .Mkitaka tuone mko serious kuuvunja Wabunge wa Zanzibar wasije Dodoma wakae kule kwao waendelee na misimamo .Mnafanya nini huku ? Si mbakie kwenu muendelee kudai mnayo yataka ?
   
 15. b

  bnhai JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Sorry to say, huyu bwana huwa hana point kabisa. Anajitahidi kuchangia lakini mh, uwezo wa kuanalyse mambo ni mdogo. Kashambulia Wazanzibar, Waislam na matusi kibao. Changia hoja sio kushambulia watu. Na kama huna cha kuchangia tulia subiri watu watu waandike
   
 16. A

  August JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Hawa wanataka kuwa kama Somalia, miaka mingapi sasa hakuna serikali ni kuchinjana kwa zamu tu , na kujitenga Somali Land na Somali ya kusini yenye mapigano mpaka leo au waangalie yalitokea Comoro na hivyo visiwa vitatu Anjoun, Great Comoro sijui nani mpaka majeshi yetu yalienda ku-restore order.
  Leo hii ukiwaambia hao wavisiwani ondokeni Namanga, Buguruni, etc etc utasikia kilio chao, kama wanaona Zanzibar kuna rasilimali au utajiri wanao upigia kelele, why invest Bara?
  Lazima waju kitamu pia kina uchungu, kama wanataka hiyo faida bara ya kuishi kwa amani, kufanya biasha, kujenga nyumba, basi ni lazima na machungu yake wayakubali.
   
 17. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  pole sana kaka wenzio hatujui siasa wala kupangilia tunasema yalivyo naona yame kuingia meza tu hivyo we are tired of you guys badilikeni au mtaendelea kulia lia .
   
 18. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  lakini nadhani hawa jamaa hatuna haja ya kuwalaumu kwani wabongo tunalala sana na huu ufisadi wao japo wanaweza kupiga kelele sie kelele zetu ni kama za maiti kwani hazifiki popote wao wanalalamika waziwazi,siwaungi mkono na uzanzibari wao but linapokuja swala la haki wanajua kuipigania si sawa na sisi ambao utafananisha na dua la kuku..........?
   
 19. b

  bnhai JF-Expert Member

  #19
  Jul 23, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Wewe Vinyungu, nadhani unachanganya vitu hapa. Well suala la kubadilika ki mtazamo ni kila mmoja katika jamii. For yr info wazazi wangu wana dini zote mbili. Mie nimebakia kubakia kama nilivyo. Lakini michango yako humu JF ni hakuna kitu kabisa. haijengi yaani ni mvurugaji. I am sure uwezo wako ni wa kibababishaji pamoja na ufanisi wako pia
   
 20. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #20
  Jul 23, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi Nyerere hakuweza kusema maneno kama anayosema Mzee Pinda. Eti anatisha ni nani wa kuathirika kama Muungano unavunjika ? Pinda ni pinda kweli (kumradhi hapo). Ni Mtu wa jazba . Busara iko wapi kwa huyo Mzee? Anakuwa sawa na wale wabunge wa upande ule?
   
Loading...