Pinda, Muungano, na Hatima ya Zanzibar

Hili la 'Mafuta ya kutosha kwenye kinibu' na FIFA ni visingizio tu, suala hapa ni MUUNGANO.

CCM Zanzibar inabidi daima washukuru Serikali na CCM Tanganyika kwani kila uchaguzi wanasaidiwa kubakia madarakani. Tuhuma:
-Kumbuka kuporwa kwa masanduku ya kura?
-Kuandukishwa janjaweed, wengine kutoka Tanganyika?
-Kukataliwa kuandikishwa baadhi ya watu wa CUF Zanzibar?
-Kauli ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi anayeteuliwa na Serikali ya CCM kuwa ndio matokeo rasmi?
-Kumwagwa Polisi na Wanajeshi toka Tanganyika?
-Magari la Pilipili?

Dawa:
Ufanyike uchaguzi halali Zanzibar, tuone matokeo yake.
Maalim Seif ataingia Ikulu Zanzibar, na CCM Zanzibar watajuuuuuuta kuanzisha chokochoko. Kuanzia hapo wataisikia Ikulu kwenye bomba...

Hatima:
Inaonekana kila upande wa muungano unadhani unaonewa.
Kama vipi tutengane tu, siyo ishu.
 
Lukundo utafananisha na kila ,ila kumbukumbu mateso yanapozidi Kigoma ,mateso na shida zinapozidi Tanga uvumi huwepo kuwa ni bora wajitenge , au huko kuna Wanyarugusu ndio hamkuoni ,ila hili la Zanzibar ni lazima mulielewe ,sijui kwa nini mnakuwa wabishi ,Jamani kwa vyovyote vile iwavyo hizi ni nchi mbili ,sasa ni lazima pawepo na masikilizano na heshima ,urafiki ndipo unapokomaa na ukizidi urafiki hushinda udugu ,sasa rafiki analalamika ,wewe unajifanya kama husikii au huoni na kila siku zikienda rafiki anaona au anakuona unampuuza na kutokumheshimu sasa mnafikiri rafiki huyo ataendelea tu kuendeleza urafiki ?

Ni lazima tukubaliane katika misingi ya umoja uliosawa kabisa ili urafiki wetu uwe wa damu ,marafiki hawawezi kuwa ndugu hata siku moja ,lakini kinachosemwa urafiki ukiwa mzuri basi hushinda hata wa ndugu ,kama tunavyoona CCM Zanzibar na CCM bara unashinda udugu uliopo kati ya Unguja na Pemba.Ndivyo inavyoonekana kwamba jinsi urafiki ulivyomkubwa wanatoka watu bara kwenda kuwapiga WaPemba ,dogo hiloo ?

Sasa Zanzibar analalamika mbona urafiki wetu una matatizo ,kwamba hata serikali yangu haina njia za kupatia mapato zote umezifunga na kuzibana ,rafiki yangu wewe hutaki niendelee ,ssasa nikianza kutafuta rafiki mwengine pia hutaki ,kuna wema hapo au kuna ubaya uliojificha ? Maana inatokea marafiki wengine wakawa wabaya na japo ni rafiki lakini hataki kukuona mwenzake unapendeza ,mwenzake unavaa ,mwenzake unaneemeka ,siku zote anataka ufikwe na shida ili uende ukamuombe ni urafiki gani huo ?

Pinda anasema mbao zikigawika kuna upande utapata taabu ,sawa nakubaliana nae kuwa kuna upande utapata tabu ,(Sijui alikusudia kuwambia CCM Zanzibar) ,lakini hapa tulipo kuna matatizo yanatokea Pemba ,Pinda anajua ,Kikwete anajua na jamii ya WaTanzania karibuni wote wameshapata habari ,Tuwaulize wao kama wadau na sio wadau bali ni Serikali ya Muungano hivi wamefanya kitu gani ? Serikali ya Kikwete ilipigiwa kura Pemba japo kura moja lakini wapo wananchi ambao walimchagua , sasa matatizo yanayowakuta wananchi wa Pemba kupelekewa majeshi kwa ajili ya kuwapora haki yao ,wanayaonaje ? Au yanawafurahisha ? Ni kitu rahisi kabisa kuonekana mbali ya hayo wanayoyaita kero ,hili ni kubwa zaidi kwa sababu roho za watu zinapotea bure ,kwa ajili ya madaraka ya miaka kumi au mitano.

Sasa kusema Muungano hauna faida sio akina Seifu wala wafuasi wa Karume bali yale ni matakwa ya wananchi ambao manung'uniko yao yamekuwa kero kwa viongozi wa Zanzibar na hawana budi isipokuwa kuyafuata ,ili waonekane ni viongozi wanaojali maisha yao ,ndio tukaona leo hii hata CCM kule wanausema Muungano na kuutilia vizingiti kwa sababu shida zimekuwa hazifichiki tena ,Raisi hana pa kuuweka uso wake ,viongozi wanaona soo , huku mmeshikilia tu Muungano tutaulinda kwa namna yeyote ile ,Mapinduzi tutayalinda kwa hali yeyote ile ,sasa hao wenye Mapinduzi nao wamefikia kusema Muungano ndio kikwazo kinachowanyima wao kupeleka maendeleo Zanzibar ,kuna kubwa zaidi ya hilo ? Mnalinda Muungano wa kina nani ,mnalinda Mapinduzi ya wepi ? Kwa kauli ya viongozi waandamizi wa Zanzibar nyinyi ni waongo hamna mnachokilinda hata kimoja ,ni kujidanganya ,haiwezekani mnachotaka kukilinda na waliomo humo mnamolindwa wakafikia kusema kuwa kuna matatizo.

Mimi sioni kama Mheshimiwa Pinda amekosea katika kuusemea Muungano yupo sawa kabisa ,lakini usawa huo utatizamika kama wangekuwa wanafuatilia hali ya Zanzibar ,serikali ya Muungano ingekuwa mbele katika kuona kuwa serikali ya Zanzibar inaangaliwa na inapewa vipau mbele katika kuendeleza wananchi wake na pale inapokwenda usongo ,Serikali ya Muungano ingekuwa inaingilia kati kwani ndio Serikali kuu ,sasa wananchi wanapigwa risasi ,wanapigwa virungu serikali Kuu inashangilia na kuongeza nguvu ili watu wauliwe na wapigwe zaidi ,Serikali haijaonekana kupeleka majeshi kwa ajili ya kulinda sheria zisivurugwe bali inapekela kuzidisha kupindwa kwa haki , mwanzo ikisemwa ni vikosi vya SMZ lakini sare zinazoonekana kutumika ni za vikosi vya Serikali ya Muungano ,hivi watu wataufahamu vipi Muungano huu kama sio unaoleta matatizo ?

Watu wanapolalamika basi mjue kuwa wameshachoka na matatizo ambayo nyinyi Serikali kuu mnayaelewa fika ni akina nani wanaosababisha ,lakini mnafumbia macho faida yake hata wale mnaowafumbia macho mambo yakiwashinda wanawatupia mzigo Serikali kuu au wanautupa kuwa yanasababishwa na Muungano.

Sasa hii ndio sababu ya kuudharau mwiba au faida ya kumfuga Nunda. Nunda sasa anakuona hata wewe Serikali kuu inafaa kuvunjwa.
 
Kumbe muungano huu kuna watu wanadai 'unaitwa/wenye kuitwa' kwa maana ya kuwa hawaamini katika muungano

tehe tehe kumbe zenji ni koloni la Tanganyika! wanasubiri nini kwena UN kudai uhuru?
 
Click kidogo hapa na utafakari
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=9ebmlAVtHUg&feature=related"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]


Harafu umalizia na hiki hapa.
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=UsfXcyuquhA&feature=related"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]


Kisha utafakari na kubulindika hapa.

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=-xYYxFZSX54"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]
 
Last edited:
Kumbe muungano huu kuna watu wanadai 'unaitwa/wenye kuitwa' kwa maana ya kuwa hawaamini katika muungano

tehe tehe kumbe zenji ni koloni la Tanganyika! wanasubiri nini kwena UN kudai uhuru?
Mkoloni MWEUSI ,usiombe huko UN huwa hawamtambui wanamwaona bado hajawa educated na hafahamu maana ya mtu kuwa Huru ,sasa hata ukienda kudai unaambiwa jamaa hawana elimu yeyote ile tutafahamiana nao vipi ?

Ndio ukaona wakoloni WEUSI ,ona hiki kipande hapa jamaa yu maji anasema kama hana akili vizuri ,shida imemkaa na roho ,matumaini yake yote yanamezwa na wabongo ,kila anapokwenda anaona nyumbani ni nyumbani tu ,wakoloni wabongo wameivamia nchi yao.

i live in Nansio Ukerewe, Now in Dar where there is a shit load of Bongos. I swear to God I have to fight every urge to rip there monkey heads off there shoulders. Everywhere you go there standing around with that stupid look on there face, boppin around to there rap and talking all that Bongo shit. And to all you Zanzibarians who loves Bongo, you are a disgusting disrespect to our NATION. The biggest problem with all the Bongos today is that they truly believe all their rap and shit is the way of the futer. Bongo celeberties are all over the TV, movies, and music. They think they are really comming up. Bongo people have nothing but hate for Zanzibarians. And the more self-empowered they feel the worse it is going to get. Zanzibarians people need to unite, and stop this bullshit. This is Zanzibar, Bongoz came here as slaves, now there up on TV! this is the Zanzibarians mans land, no bongo are going to ever take that. Its time to put a stop to all this Bongo shit.

------------

Sasa mnaona hilo ndilo ambalo hamtaki kulisikia ,haendi mtu UN isipokuwa WaPemba tu wao wana matatizo yao mengine kabisa maana wamewachanganya wote WaTanganyika na Rafiki zao wa Unguja.
 
Kwa mwananchi wa kawaida huu Muungano hauna maana yoyote, hasa ikichukuliwa kuwa kila upande (Tanganyika na Zanzibar) unaona kama vile mwenzake ndiye anafaidi matunda ya Muungano, na yeye ananyonywa.

Muungano unalindwa na viongozi hasa wa juu wa CCM-Tanganyika na CCM-Zanzibar.
Kikwete alisaidiwa kuchaguliwa mgombea wa CCM kutokana na kura za wajumbe wa CCM-Zanzibar.
Karume alishindwa na wengi tu Znz, huku Dk. Bilali akiibuka kidedea kule CCM-Zanzibar, ila alikuja kuokolewa na wajumbe wa CCM-Tanganyika Dk. Bilali akapigwa chini.
Hivyo viongozi wa CCM pande zote wanategemeana. Na hao ndio wameshika dola, walau kwa sasa.

Chama cha Upinzani kikishika Dola (Madaraka) kwenye upande mmoja wa Muungano ndio itakuwa mwisho wa CCM kuwa Chama-Dola. Hiyo itasaidia, na inaweza ikawa ni Mwanzo wa Mwisho wa Muungano. Itakuwa ni poa tu kwani kila upande naamini utafurahi, Tanganyika kuacha kuibeba Zenji, na Zenji kuwa nchi na Taifa. Zitabaki nchi mbili jirani.
Itakuwa poa.

Angalizo:
Kwa uchaguzi huru na haki kwa 100%, matokeo yanaweza kuwa vipi ikiwa:

-Hakuna kupora masanduku ya kura?
-Hakuna kupenyeza janjaweed? wengine kutoka Tanganyika?
-Hakuna kutangaza matokeo yasiyo ya kweli? ( ila yatangazwe ya haki?)
-Hakuna kukataa kuandikisha wafuasi wengi wa CUF?
-Hakuna kujaza Polisi na Wanajeshi kutoka Tanganyika?
-Hakuna magari ya Pilipili?

CCM-Zanzibar itakuwa hoi.
Itapendeza CCM kuwa Chama cha Upinzani...
Rais Hamad...
Waziri Kiongozi Duni...
 
Mwiba,
Mimi nilifikiri unatuletea habari kwamba baraza la mapinduzi, balaza la wawakilishi, wabunge wa zanzibar na mawaziri wa SMZ wamefanya kikao cha pamoja na kutafuta mwanasheria awasaidie kutazama jinhsi ya kuvunja muungano.
 
AHSANTE Mkuu MWIBA
Ujumbe wetu umefika,mkakati wetu uliobaki ni kuirejesha CCM huko huko ilikotoka,Butiama sijuwi Dodoma,badala ya hapo,mapambazuko ya uhuru kamili yatatimia, we are tired of this so called union.
 
Mwiba,
Mimi nilifikiri unatuletea habari kwamba baraza la mapinduzi, balaza la wawakilishi, wabunge wa zanzibar na mawaziri wa SMZ wamefanya kikao cha pamoja na kutafuta mwanasheria awasaidie kutazama jinhsi ya kuvunja muungano.

Wewe wacha kucheza na siasa ,mi nipo hapa kustawisha barza tu ,haya ya siasa wala sina habari nayo ,huwa napiga debe tu , maana wote hao siku ya pili utawaona wanatoka kanisani au msikitini kula pilau au alua ,huku wamekenua na kucheka , sasa mimi sifaidiki na chochote kile ,zaidi ya kupoteza hela yangu kuwepo hapa mtandaoni ,sema hapa ni mfanyakazi wa Ngurdoto huwa napata kukong'oli bure.

Wale watu na kazi zao ,Pinda yupo kazini akitetea mlo wake na wale waZanzibar nao wako kazini wakilinda tonge zao ,mimi nipate ziki yanini ?

Nawashangaa sana hapa watu wanaopanda jazba ,mi nipo kuul tu ,naandika na kusoma ,na kuzusha ya kuzusha ni uandishi tu ,nimeokota kipande huko na kukifanyia usanii.

Ila najua kitawagusa tu.maana ni ukweli na ukweli huwaga unauma. Ngoja kesho kutwa ramazani utawaona wanatoka kula futari ikulu.
 
Mkoloni MWEUSI ,usiombe huko UN huwa hawamtambui wanamwaona bado hajawa educated na hafahamu maana ya mtu kuwa Huru ,sasa hata ukienda kudai unaambiwa jamaa hawana elimu yeyote ile tutafahamiana nao vipi ?


Sasa mnaona hilo ndilo ambalo hamtaki kulisikia ,haendi mtu UN isipokuwa WaPemba tu wao wana matatizo yao mengine kabisa maana wamewachanganya wote WaTanganyika na Rafiki zao wa Unguja.


AHSANTE Mkuu MWIBA
Ujumbe wetu umefika,mkakati wetu uliobaki ni kuirejesha CCM huko huko ilikotoka,Butiama sijuwi Dodoma,badala ya hapo,mapambazuko ya uhuru kamili yatatimia, we are tired of this so called union.

tehe tehe tehe.,..kumbe baada ya kuuvunja huu muungano, itafuata kuidai pemba kutoka unguja

next steps?
 
kwanza wanafaidika na soko la watanganyika.hao watu 1mil. ni soko gani.China wanajivunia soko lao kubwa la ndani. wanabemberezwa na ulaya maake ukipatasoko hapa umewin. Tuawaache tuone wanazalisha nini na wanauza wapi.
 
kwanza wanafaidika na soko la watanganyika.hao watu 1mil. ni soko gani.China wanajivunia soko lao kubwa la ndani. wanabemberezwa na ulaya maake ukipatasoko hapa umewin. Tuawaache tuone wanazalisha nini na wanauza wapi.
Wewe inabidi urudi zhule ukazomeshwe vizuri ,hivi unasikia yanayotokea huko China au bado umo usingizini ? Soko la ndani lipi hilo ndugu yangu ? Yaani ukisikia watu wanadandia treni kwa mbele ndio wewe, unajua ni viwanda vingapi vimefungwa China ? Unajua ni watu wangapi wametolewa makazini huko China ?Unajua ni meli ngapi zimekosa mzigo wa kusafirisha na sasa zimeanza kuoza huko katika bandari zao ? Sasa wewe hushangai kuwa wamevamia kariakoo wanauza karanga ? Na nia sio kuuza karanga ni kupata uenyeji na kuwaondoa wazalendo wote hapo ,watanunua na kukodi milango ya maduka kwa bei mtakayowambia ? Kwa maana huko kwao hakuna kinachouzika ,hakuna wanunuzi ,watu awana ela kaka .Ndio wanakuja kuzitafuta hata hizi za madafu.Halafu wanakuuzieni kwa bei ya chini kabisa ,mzalendo wa kariakoo baada ya miaka mitano akatafute jembe akalime. Ndio maana ya utandawazi ,umemsikia waziri akipiga makelele kuwa anawashangaa wachina kuuza njugu kariakoo. Basi rudi zhule mwanangu.
 
Mwiba,

Hivi nani kasema ya kuwa Zanzibar kuna mafuta, mimi naona kama baraza la wawakilishi wanajadili kitu ambacho hawana uhakika nacho .
 
Jamani wakuu zangu hizi habari za Ubabe hazina hata radha hata kidogo..
Viongozi wetu inabidi wajifunze ktk maswala haya hasa pale tunapounganishwa sehemu mbili kuunda Jumuiya moja..
Matatizo makubwa ya Tanzania leo hii ni UDINI na huo MUUNGANO, jambo ambalo linachukiza kusoma wala kusikiliza..
Navyojua mimi hakuna nchi hata moja duniani iliyounda Muungano wa jamii mbili au Tatu tofauti wakaweka masharti magumu kama yetu kwa seti moja..
Ukitazama Muungano wa Canada, Majimbo yote yalikuwa chini ya Muingereza isipokuwa moja la Quebec..lakini hawa wameruhusiwa kujiunga na Jumuiya ya Kifaransa. Nchi kama Switzekand majimbo yake yamegawanyika ktk Swiss - Germany, Swiss -France na Swiss Italia na wote wamejiunga na jumuiya za makabila hayo tena basi hata lugha wanazungumza lugha zao, hadi sign za barabarani wanatumia lugha zao..Muungano upo palepale kwa kutambua tofauti zao..

Sisi inapofikia swala la Muungano na dini basi tunataka kulazimisha wengine wafuate nchi moja au dini moja kwa kuweka masharti, jambo ambalo halijengi.. Inakuwa kama mila ya mwafrika kuwa mume ndiye mwenye amri afanye analotaka, anatoka na kurudi atakavyo lakini kwa mke ni lazima apate ruksa ya bwana..
 
Mwiba,

Hivi nani kasema ya kuwa Zanzibar kuna mafuta, mimi naona kama baraza la wawakilishi wanajadili kitu ambacho hawana uhakika nacho .


Mkuu na wewe wacha Mashauo juzi hapa bungelini waziri alisema kuwa uwezekano wa kupatikana mafuta upo Tanganyika na hapa zanzibar sasa wewe unachokesema kama vile mtu anajishauwa jambo fulani.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom