Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,923
Hii picha ya Waziri Mwakyembe akipanda train imeibua mawazo mengi kichwani mwangu.Mawazo hayo yameibuliwa si kwa kitendo cha waziri huyo kupanda train, bali ni namna gani anapanda au kukwea kwenye hiyo train. Ukiitazama hiyo picha unaona kwamba anatumia nguvu nyingi kupanda hizo ngazi na kwa kushika vyuma pembezoni mwa mlango, vyuma ambavyo vimewekwa mahsusi kwa kazi hiyo.
Baada ya kuona hivyo nimeanza kuuliza, je itokeapo mtu anayepanda ni kilema, mgonjwa au mtoto, kweli ataweza kuzimudu hizo ngazi kwa urahisi? Jibu nililopata ni hapana, hataweza kamwe kupanda ngazi hizo kwa urahisi bila kupata msaada wa mtu au watu wengine.
Kuna haja ya kutengeneza miundombinu yetu ambayo inakuwa rahisi na salama kwa kila mtu kuitumia. Kama kungekuwa na sheria nzuri nchini Tanzania, itokeapo mtu akianguka kwenye hizo ngazi, angeweza kulishtaki shirika la reli na kulipwa fedha nyingi tu. Hivyo basi ni vizuri kuinua sehemu wanapokanyaga abiria, 'platform' ili kila masafiri awaye yeyote yule, aweze kupanda au kupandisha mizigo kwenye chombo hicho cha usafiri kwa urahisi. Picha hii hapa chini inaomyesha 'platform' ambapo ni rahisi kwa abiria kupanda yeye na mizigo yake:
Kwa bahati nzuri siku hizi za karibuni, nimeona tangazo kwenye ITV linalotangaza kuwatilia maanani walemavu katika ujenzi wa sehemu zetu za huduma. Natumaini wahusika watapata fursa ya kusoma mada hii na kuzingatia maoni haya.