Picha ya Mwakyembe akipanda train...

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,923
mwakyembe on train.jpg
Hii picha ya Waziri Mwakyembe akipanda train imeibua mawazo mengi kichwani mwangu.Mawazo hayo yameibuliwa si kwa kitendo cha waziri huyo kupanda train, bali ni namna gani anapanda au kukwea kwenye hiyo train. Ukiitazama hiyo picha unaona kwamba anatumia nguvu nyingi kupanda hizo ngazi na kwa kushika vyuma pembezoni mwa mlango, vyuma ambavyo vimewekwa mahsusi kwa kazi hiyo.

Baada ya kuona hivyo nimeanza kuuliza, je itokeapo mtu anayepanda ni kilema, mgonjwa au mtoto, kweli ataweza kuzimudu hizo ngazi kwa urahisi? Jibu nililopata ni hapana, hataweza kamwe kupanda ngazi hizo kwa urahisi bila kupata msaada wa mtu au watu wengine.

Kuna haja ya kutengeneza miundombinu yetu ambayo inakuwa rahisi na salama kwa kila mtu kuitumia. Kama kungekuwa na sheria nzuri nchini Tanzania, itokeapo mtu akianguka kwenye hizo ngazi, angeweza kulishtaki shirika la reli na kulipwa fedha nyingi tu. Hivyo basi ni vizuri kuinua sehemu wanapokanyaga abiria, 'platform' ili kila masafiri awaye yeyote yule, aweze kupanda au kupandisha mizigo kwenye chombo hicho cha usafiri kwa urahisi. Picha hii hapa chini inaomyesha 'platform' ambapo ni rahisi kwa abiria kupanda yeye na mizigo yake:

cdg_terminal_2_rer_station.jpg

Kwa bahati nzuri siku hizi za karibuni, nimeona tangazo kwenye ITV linalotangaza kuwatilia maanani walemavu katika ujenzi wa sehemu zetu za huduma. Natumaini wahusika watapata fursa ya kusoma mada hii na kuzingatia maoni haya.
 
Wapendwa, ugonjwa kuingia ni rahisi sana sana lakini kutoka ni muda mrefu sana mpaka mtu akamilike.
Dr. Mwakyembe Mungu anampenda sana na kwa imani yeye anakiri emepona lakini kwa kuwa bado ni mapema tunasema bado anarejesha hali yake kidogo kidogo na umri wenyewe ni mkubwa kwahiyo tusishangae mwenzetu kumwona bado anapata shida kupanda kwenye Train kwa shida.....,Mungu atamkamilishia uponywaji wake
Amina
 
Wapendwa, ugonjwa kuingia ni rahisi sana sana lakini kutoka ni muda mrefu sana mpaka mtu akamilike.
Dr. Mwakyembe ((Mungu anampenda sana)) na kwa imani yeye anakiri emepona lakini kwa kuwa bado ni mapema tunasema bado anarejesha hali yake kidogo kidogo na umri wenyewe ni mkubwa kwahiyo tusishangae mwenzetu kumwona bado anapata shida kupanda kwenye Train kwa shida.....,Mungu atamkamilishia uponywaji wake
Amina[/QUOTE

hapo kwenye mabano..hii lugha si huwa inatumika kwa watu waliotutangulia kuelekea kwa baba?
 
Anaugulia maumivu.

Kwanza hakukua na sababu ya yeye kusafiri kwa treni eti kujua matatizo, labda kama anatafuta umaarufu.

Ivi ukitaka kujua mateso ya maalbino ni lazma uwe albino.
 
  • Thanks
Reactions: tz1
Wakuu, hiyo picha anapanda treni kweli? Mie nadhani hapa alikuwa anashuka, ndio maana inaonekana hivyo. Mwili umelegea kwa sababu ya kuwa he is not working against gravity.
 
point yako ni nzuri ,ila bajeti ndo zishaandikwa na waziri wa fedha ndo anasoma muda huu ya kwake!,na mwakani sijui kama tutakumbuka kuhamasisha uboreshaji wa ngazi za treni zetu!maana watanzania tunasahau tatizo haraka sana!
 
Katika suala la miundombinu bado tuna safari ndefu sana kuyakaribia mafanikio. Ee Mungu ibariki Tanzania.
 
Katika suala la miundombinu bado tuna safari ndefu sana kuyakaribia mafanikio. Ee Mungu ibariki Tanzania.

tatizo watu wanapenda sana kula, wanakula mpaka mbegu. pamoja na ubinafsi, hatufikirii vizazi vijavyo.
 
tatizo watu wanapenda sana kula, wanakula mpaka mbegu. pamoja na ubinafsi, hatufikirii vizazi vijavyo.

Ndio maana wanauza mpaka mbuga za wanyama na maeneo makubwa ya ardhi kwani hawafikirii juu ya vizazi vijavyo!!
 
Ndio maana wanauza mpaka mbuga za wanyama na maeneo makubwa ya ardhi kwani hawafikirii juu ya vizazi vijavyo!!

there you are Bulesi, mtu anakwiba mabilioni utadhani ataishi miaka elfu, yani tamaa iliyopitiliza, kinachonishangaza ni kuwa hawa viongozi wetu ndio ambao kila kukicha wako ughaibuni, hivi hawaoni wivu wa maendeleo ya wenzetu? hebu niambie kwa nini wameshindwa hata kumwaga zege la kupandia treni pale dar, yani toka alivyojenga mjerumani ndo mpaka leo. aibu kubwa sana hii.
 
Last edited by a moderator:
mwache aendelee kukwea hivyo hivyo mnafiki huyo, maana hapo hapandi anakwea (namuona kama nyani vile anavyokwea miti) angekuwa na usongo kweli angesaini ile karatasi ya zito...
 
Wakuu, hiyo picha anapanda treni kweli? Mie nadhani hapa alikuwa anashuka, ndio maana inaonekana hivyo. Mwili umelegea kwa sababu ya kuwa he is not working against gravity.

bado point yako haisaidii kumtetea, miundombinu ingekuwa mizuri asingeshuka kinyumenyume, mbona kwenye ndege hashuki hivyo bana? ashuke apande atajiju....
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom