Picha ya Mwakyembe akipanda train...

Anaugulia maumivu.

Kwanza hakukua na sababu ya yeye kusafiri kwa treni eti kujua matatizo, labda kama anatafuta umaarufu.

Ivi ukitaka kujua mateso ya maalbino ni lazma uwe albino.
Wee Jambazi hujafungwa tu? Kwani ukitaka baada ya maisha ya hapa duniani mtu huenda Peponi au Jehanam ni lazima ufe kwanza? Mbona tunahubiriwa kuna maisha baada ya kifo, ina maana Wahubiri hawa walishawahi kufa kwanza na kwenda kujionea ndipo wakarudi duniani kutuhubiria waliyoyaona huko? Is this the right analogy to Dr. Mwakyembe's scenario, au ni uvivu wa kufikiria tu wa huyu mhalifu?
 
mmmh!hii picha nimeikutia huku tena!

We Zamaulid wewe, umenichekesha bila kupenda wakati mie nilikuwa na masikitiko yangu ya kimaisha. Sasa mie nifanyeje jamani? Pole, hii picha imekuwa kama huyo mbuni wako. Usikubali ikufikie!
 
Last edited by a moderator:
nilisoma website ya maoni ya wwatalii waliotembelea Tanzania wengi wanasema kuwa Tanzania sio nchi ya kutembelewa an walemavu wa miguu
 
View attachment 56343
Hii picha ya Waziri Mwakyembe akipanda train imeibua mawazo mengi kichwani mwangu.Mawazo hayo yameibuliwa si kwa kitendo cha waziri huyo kupanda train, bali ni namna gani anapanda au kukwea kwenye hiyo train. Ukiitazama hiyo picha unaona kwamba anatumia nguvu nyingi kupanda hizo ngazi na kwa kushika vyuma pembezoni mwa mlango, vyuma ambavyo vimewekwa mahsusi kwa kazi hiyo.

Baada ya kuona hivyo nimeanza kuuliza, je itokeapo mtu anayepanda ni kilema, mgonjwa au mtoto, kweli ataweza kuzimudu hizo ngazi kwa urahisi? Jibu nililopata ni hapana, hataweza kamwe kupanda ngazi hizo kwa urahisi bila kupata msaada wa mtu au watu wengine.

Kuna haja ya kutengeneza miundombinu yetu ambayo inakuwa rahisi na salama kwa kila mtu kuitumia. Kama kungekuwa na sheria nzuri nchini Tanzania, itokeapo mtu akianguka kwenye hizo ngazi, angeweza kulishtaki shirika la reli na kulipwa fedha nyingi tu. Hivyo basi ni vizuri kuinua sehemu wanapokanyaga abiria, 'platform' ili kila masafiri awaye yeyote yule, aweze kupanda au kupandisha mizigo kwenye chombo hicho cha usafiri kwa urahisi. Picha hii hapa chini inaomyesha 'platform' ambapo ni rahisi kwa abiria kupanda yeye na mizigo yake:

View attachment 56347

Kwa bahati nzuri siku hizi za karibuni, nimeona tangazo kwenye ITV linalotangaza kuwatilia maanani walemavu katika ujenzi wa sehemu zetu za huduma. Natumaini wahusika watapata fursa ya kusoma mada hii na kuzingatia maoni haya.

Ungeleta na ya mwingine ili tuone kama tatizo ni platform, afya ya jamaa au creativity. Huo usafiri nilikwisha utumia sana upandaji wake sio huo, ni kupanda kama huko wima huku ukiwa kiubavu kidogo!!

Pia jamaa katumia treni labda instincts zake zimeonyesha wangeweza kum-mwakyembelize tena kama angetumia anga au barabara!!!!
 
duh mheshimiwa labda hajazoea mausafiri ya staili hii utafikiri tumbili kadandia mti??? ila safi sana ndo wajionee hali halisi ya maisha yetu sie makabwela
 
Back
Top Bottom