Uongozi wa Hospitali ya Bugando chukueni hatua za haraka kurekebisha lifti zenu kabla hazijaleta madhara

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Habari wana JF wenzangu, ni kwa zaidi ya mwaka sasa nimekuwa nikifika kwenye Hospitali ya Bugando kwa ajili ya huduma za matibabu lakini nimebaini changamoto ambayo mimi kama mtu mzima siwezi kuikalia kimya.

Kwa mara kadhaa ambazo nimekuwa nikifika hapo nimekuwa nikikutana na changamoto ya 'lift', kuna wakati zimekuwa zikigoma kufunguka wakati Watu wakiwa ndani akiwemo wagonjwa wanaokuwa wamelazwa kwenye vitanda maalumu kwa ajili ya kupelekwa maeneo husika ya huduma.

Licha ya jambo hilo kuibua taharuki na hofu kwa watu wengi ambao wamekumbana na changamoto hiyo nimeshuhudi mamlaka za hospitali hiyo zikiwa zinafanya harakati za muda kufanya maboresho lakini bado hali hiyo imekuwa ikijitokeza ikiwemo kuzima kwa nguvu (mithili ya kudunda) inapofika floor ya pili au ya kwanza.

Kuna wakati nadhani kutokana na changamoto waliweka maelekezo kuwa lift zitumike kwa ajili ya wagonjwa na wahudumu lakini jambo hilo limekuwa gumu kutekelezeka licha ya kuwepo kwa lifti mbili ambazo zote zina changamoto hiyohiyo.

Jambo hilo kushindwa kutekelezeka ni umbali uliopo kutoka chini kwenda juu kwa kutumia ngazi hususani kuanzia floor ya tano hadi ya nane.

Hali hiyo imekuwa ikisababisha Wagonjwa wanaopelekwa sehemu za matibabu wodini kutofika kwa wakati kutokana na lift hizo kuwa nzito, wakati mwingine licha ya lifti hizo kuwa nzito lakini zimekuwa zikibeba watu wengi hali ambayo inafanya kama kuna mgonjwa kuchelewa kufikishwa sehemu hitajika kwa wakati.

Pia kuna wakati lifti zinapokuwa na chagamoto zaidi, wahudumu, watu wengine pamoja na wagonjwa wenye uwezo wa kutembea wamekuwa wakitumia ngazi kupanda kwenye floor za juu jambo ambalo nimelishuhudia na wengi kutofurahishwa.

Kutokana na hadhi ya hospitali hiyo ambayo ni tegemeo zaidi hususani kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa ni muhimu changamoto hiyo ikachukuliwa kwa uzito zaidi ikiwezekana kubadilisha kabisa lifti hizo ili kuondoa hofu na kuepusha athari zinazoweza kujitokeza endapo hali hiyo ikiendelea.

Majibu ya Bugando haya hapa - Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando yatoa majibu kuhusu madai ya lifi zao kuwa na changamoto
 
Mie sijawai kuziamin zile lift coz toka nakuwa napata akili naskia lift za bugando mbovu uwa Zina jizima😢we imagine hizo story za lift kuzingua ni toka uko mwaka 2000 Yani ili fika hatua tuki simama kituo cha daladala misheni ukiomba lift konda ana kujibu lifti Iko bugando 😂nenda ikakuzimikie😂
 
Back
Top Bottom