Picha na stori za Loliondo- kwa Babu

Picha na stori za Loliondo- kwa Babu

Kama huyu mganga ni Kweli basi Serikali MARA MOJA impeleke pale Muhimbili akasaidie kutoa huduma.

title haiendani na content ,pia tambua kuwa yule si mganga ,ni mchungaji aliyestaafu pia anatoa dawa LOLIONDO ikiwa na mana kwamba kwa uwepo wa dawa kule then juhudi za lazima zitachukuliwa ili kupaendeleza maeneo yale yaliyosahaulika ,pia akitoa dawa mbali na hapo eneo ilipogunduliwa then inakuwa haina nguvu. source:mgunduzi
 
Nimeona kama Rostam yupo hapo kwenye picha namba 4.
Lini TRA watajichoma pale kudai ushuru?
 
Wakati wengine wanasubiri , kwanini wasijaribu kuchemsha huo mti na kujaribu kunywa maji yake au mpaka babu mwenyewe afanye?
 
je hakuna aliegundua dawa ya kuitoa ccm jamani sio kuumwa tu ki mwili je umasikini sio homa
Conquest-umasikini si homa bali ujinga:A S 13:
 
Usituzuge kama umeshakula mzigo na wewe nenda Loliondo kamuone mzee Ambilikile
 
CAMERA YETU BADO INASUBIRI KUPHOTOA VI GOGO KWA BABU AU KWA MASIKINI NDIO WAENDE HUKO HUKO WAO WANAPELEKEWA KWAO MAANA WAGONJWA TZ NI WENGI ZAIDI YA PESA
JUST ON DA WAY TO BABU WITH MY HIDDEN CAMERA
cONQUEST- SOTE TUNAUMWA BALI JUST TIME WILL TELL:rain:
 
mawazo mabaya huleta ujumbe potofu/mbaya nje ya vinywa vetu yawezekana alipeleka ndugu au kafuata mkumbo sasa unapata wasiwasi wa nini kwa jambo usilokuwa na uhakika nalo.
 
Wakuu huyo tayari kamega lakini hataki kusema ingekuwa hujamega usingekuwa na hofu mpaka ufikekuchunguza mzigoni kwao kaondokaje
 
Ah! Babu anakula vichwa kama kinyozi vile. Kamua kamua babu!
 
Ah! Babu anakula vichwa kama kinyozi vile. Kamua kamua babu!
 
nimeskia kuna Mkulu alifika kwa babu usiku apewe dawa,babu amekataa amesema Dawa anatoa mchana tu,so asubiri mpaka asubuhi ,mkulu kaona noma akarudi alikotoka by Air
Nimecheka sana baada ya kusikia kisa hiki leo
 
Wapendwa wana Jf na Watanzania kwa ujumla.
Napenda kuchukua fursa hii kushauri serikali yetu km kweli ina nia njema na watu wake ifuate ushauri huu ili kumsaidia babu wetu wa Loliondo ambaye anaokoa maisha ya watu.

Nimeona nitoe ushauri huu baada ya kuona vyombo vya habari na baadhi ya watendaji serikalini wameanza kuropoka ropoka bila kutoa mwelekeo wa kusaidia watu waendelee na matibabu kwa utaratibu mzuri. Mfano, kusema eti unaenda kuchukua sample ufanyie majaribio na ikibainika siyo kweli uzuie hii sio kauli sahihi, kwani suala hili linaendana kiimani zaidi kuliko kisayansi.


USHAURI WANGU NI HUU:

1. Kuanzishwe vituo maalum katika Mkoa wa Arusha, mji wa Moshi na Mji wa Loliondo na Kuundwe Kikosi kazi kwa ajili ya kuwaratibu wale wote wanaotaka matibabu. Yaani watu wajiandikishe bila vitambulisho katika vituo hivi na kisha serikali ipange utaratibu wa kupekela idadi maalum ya wagonjwa kwa babu kila siku. mfano km babu anaweza tibu watu 1000 kwa siku na tuna vituo 3, basi kila kituo kinapeleka watu takribani 330 kwa siku. Kila anayejiandikisha mwanzo ndio aanze kupata matibabu.

Hii itamsaidia pia babu kupata muda wa kupumzika maana kwa utaratibu wa sasa wa kila mtu kufunga safari kivyake babu anachoka sana.

2. Utaratibu wa kusafirisha wagonjwa ufanywe kwa utaratibu maalum na bei ishuke. Kwa bei ya sasa ya Tsh 100,000 au hata zaidi inawawia vigumu wasio na kipato cha kutosha kufuata matibabu hayo.

3. Serikali au watu wenye uwezo ambao wameshatibiwa watoe msaada wa kujenga miundombinu, km kurekebisha barabara, kujenga vyoo, kuweka sim tanks za maji nk. Maana wengine wanataka kumpa mamilioni babu, sasa babu anataka 500 tu, hivyo hizo pesa zao watoe sadaka kwa kusaidia kujenga miundombinu na kuweka mazingira ktk hali nzuri. wanaweza hata kujenga mahema ya muda na kununua viti vya plastick. Pia wanaweza mnunulia babu hata gas cooker na mitungi ya gas akaachana na kutumia kuni kuchemsha dawa.

4. babu apate japo siku moja ya kupumzika mfano, jumapili kusiwe na pilika pilika zozote, au basi siku hiyo ahudumie walio mahututi tu.

5. Vituo vya uandikishaji visitoze pesa wananchi na wala kuchakachua kwa kuwatanguliza mbele ya foleni wale watakaokuja na pesa zao, wakifanya hivyo wajue dawa haitafanya kazi. Hii imejitokeza kwa babu na ni kweli kabisa, kuna watu waliwavuka wenzao na kujipeleka mbele ya foleni, walipofika kwa kunywa dawa, babu bila hata ya kuambiwa na mtu aliwaambia warudi katika foleni zao. watu walistaajabu sana mijuziza ya bau kugundua hilo bila kuambiwa.

6. Kuna watu wanataka kujitajirisha kwa mgongo wa babu, mfano kuuza vyakula kwa bei ya kilimanjaro hotel, kutoza nauli ya kufa mtu n.k. Watu hawa na hakika km watakuwa nao ni wagonjwa sidhani km wakienda kwa babu watapona maana Mungu anawaona. Hili serikali ndio inatakiwa kuliingilia na siyo kumwingilia babu katika kazi zake au kuingiza sayansi ambayo na hakika haitatoa majibu sahihi.\

naona niishie hapa na mtu mwingine mwenye maoni na ushauri zaidi anaweza kuendeleza.

haya ni mawazo yangu na wewe unaweza toa ya kwako au kuboresha haya lakini siyo kunishambulia.
Ahsanteni nawasilisha kwa manufaa ya wote.
 
mbona hawachukui sample za kina pedeshee dr. ndodi au sample za upako na kina majimarefu na wengine wengi..... ?

mama yangu mzazi amerudi jana ... 15yrs in critical struggles over diabate and high blood pressure as of today the two are in normal

thanks god and babu ..... i wish babu a gracious life
 
so umeharibiwa kitu gani hapo na babu???
 
Wametangaza asubuhi wakati wa magazeti kwenye habari picha Radio one nimesahau gazeti, picha inamuonyesha Mwenyekiti wa CCM Kilimanjaro Vick Nsilo Swai akiwekewa dawa na babu
 
Kama huyu mganga ni Kweli basi Serikali MARA MOJA impeleke pale Muhimbili akasaidie kutoa huduma.

We vipi? kwa sababu Muhimbili tu ndo kuna wagonjwa, kwa nini usiseme Mount Meru au hospital ya wilaya ya Ngorongoro, usiharibu maono ya babu, anafuata maelekezo
 
maono alopewa ni pale pale na naniajuaje pori linaweza kuwa mji ni vile hii serikali yakifisadi vinginevyo saa hizi kwa babu pangekuwa ulaya
 
Back
Top Bottom