Picha na stori za Loliondo- kwa Babu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Picha na stori za Loliondo- kwa Babu

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Ndallo, Mar 7, 2011.

 1. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Ilikua ni majira ya saa 12:30 jioni siku ya ijumaa ambapo mimi na familia yangu tulipoamua kwenda kwa yule mchungaji anayetibu maradhi sugu kwa njia ya upako kutoka kwa Mungu kwa gharama ndogo sana ya shilingi mia tano (500) tu kwa kikombe cha dawa ya mitishamba ili upate huduma ya uponywaji kwa maradhi sugu ambayo sisi binadamu tumeshahangaika kwenda kwa waganga wa aina mbalimbali kwaajili ya kupata matibabu. Magonjwa sugu BABU anayotibu ni Pumu/Kisukari/Kansa/Ukimwi/Pepo na mengine.

  Mchungaji huyu anapatikana kule wilaya ya Ngorongoro kijiji cha Samunge mkoani Arusha, wananchi wengi kwa lugha rahisi wao wanasema ni kule Loliondo, siku nakwenda kule tuliondoka Arusha majira ya jioni saa 12 jioni tukaendesha gari letu mpaka maeneo ya kijiji cha Mto wa Mbu mkoani Manyara ni muda wa kama saa moja na nusu. tulipofika pale tukapunzika katika kambi moja ya kulaza wageni hawa wakizungu inajulikana kama Kiboko Camp tukapata chakula chetu cha jioni pale tukapunzika hadi ilipofikia majira ya saa nne na nusu za usiku ndipo tukawasha gari letu kuelekea maeneo yenyewe husika.

  Tukachukua njia moja inayojulikana kama Engaruka moja kwa moja hadi Ziwa Lake Natron kwakweli barabara ni mbaya mno na kama huna gari lenye kua na mfumo wa 4x4 wheel drive basi safari yako lazima iwe na mashaka sana, tulikutana na magari mengi mno ambayo tulikua tunafuatana nayo mengine tuliyakuta yamekwama mengine yamepinduka kutokana na uzoefu mdogo wa madereva kwenye njia hizo kwakweli barabara ni mbaya sana!

  Tulisafiri kwa mwendo wa masaa tisa na nusu usiku kucha! tuliwasili kwenye eneo lenyewe kwakweli ni porini na jamii ya wakazi wanaoishi kule ni jamii ya makabila ya Wasonjo ni wafugaji na wakulima, eneo lenyewe kwakweli halina vyoo wala maduka ya kuridhisha ni vibanda tu. Basi baada ya kuwasili pale lengo letu lilikua ni kupata huduma nakuondoka siku hiyohiyo, lakini sivyo kama tulivyofikiria. Kwanza barabara ni moja tu inamaanisha ukishafika pale inakubidi usubiri kwenye gari lako sana sana kama utatoka na kujinyoosha au kwenda kujisitiri vichakani na kurudi kwenye gari lako na kuendelea kusubiri.

  Kuhusu tiba ni kua huyu bwana ambaye ni mchungaji lakini kwajina tulilolikuta pale ambalo ni maarufu ni kwa BABU! bwana huyu wanavyosema wenyeji hawa ni kua baada ya yeye kuoteshwa na Mungu kuhusu uponyaji huu ni kua alipofika kijijini pale aliwaambia wale wenyeji kua njooni mpate dawa lakini wenyeji hawa wako waliomsikia na kumuamini lakini wengi wao walimdharau tu basi hapo mwanzo watu waliokua wanakwenda pale walikua ni wachache mno mmoja wao alikua ni baba yangu mzazi yeye aliondoka Arusha mjini saa saba za usiku akafika pale saa nne na nusu akapewa tiba na sala pia zilifanyika hususani na BABU aliwaambia historia yake na siku hiyohiyo baada ya tiba wakaondoka nakurejea Arusha na uponyaji ule umemsaidia sana ni kweli bwana huyu anatibu.

  Tofauti ya siku za nyuma na sasa kuhusu kwenda na kurudi siku inayofuata sasa hivi imekua ni kitendawili kama sisi tulivyokua tunajua kutokana na baba yangu kurudi siku inayofuata, makundi tuliyoyakuta pale kuna watu niliokua nawafahamu waliniuliza mimi nimefika pale siku gani nikawaambia ndio nimefika na ninataka kupata dawa halafu nirejee nyumbani ili niweze kuingia kazini siku ya jumatatu, kwakua siku naondoka Arusha ilikua ni siku ya ijumaa kwahiyo tulifika pale siku ya jumamosi asubuhi. Basi kwa mtizamo wangu nikua nipate tiba siku ya jumamosi halafu usiku tuondoke ili nifike Arusha siku ya jumapili, wale jamaa zangu walinishangaa sana wakaniambia kua wao wana siku tano na huduma bado hawajapata na bado wataendelea kusubiri mpaka kieleweke! Nilivunjika moyo sana kusikia vile na ukitegemea sisi wenyewe tulikwenda kwa madhumuni ya kurudi mapema kutokana na kazi zetu hizi za kuajiriwa na hatupendi kupoteza kazi.

  Nilifikiri kwa kina sana tukaamua tutoke ndani ya gari letu halafu tutembee kwa miguu kwa umbali wa kama kilometa 28 tukawacha gari letu tuone kama tutafanikiwa kupata dawa halafu tukishapata dawa turejee kwenye gari letu halafu tufunge safari yakurejea nyumbani, Loh tulipofika pale watu ni wengi sana hususani wale jamii ya Wasonjo wanajaribu kuleta fujo ili wapate dawa, narejea tena kama nilivyosema kua jamii hii BABU alishawaambia kua njooni mpate dawa wao wakaghairi sasa baada ya kuwaona watu ni wengi na nimatajiri sasa wao wanafanya fujo ili wao wawe wa kwanza kupata dawa kweli moyo wangu ulizidi kuvunjika kwa kutokua na matumaini ya kurudi nyumbani hii siku. Tulikuta askari pamoja na wanamgambo wanaojaribu kuwazuia wasiendele kufanya fujo jamaa walishawahi kufanya fujo hadi wakamwaga dawa hii ya BABU ambapo ilibidi BABU asitishe utoaji huu wa dawa na akenda zake ndani nakujifungia hadi pale wale wanamgambowalipowatuliza Wasonjo hawa na wakarejea kwenye hali ya utulivu lakini bado jamaa hawa sio wasikivu na halafu BABU hapendi Mgambo na askari wapige watu BABU alishakataa akawaambia msipie mtu hata mmoja hapa kwakua kila mtu hapa ni mgonjwa kwahiyo askari na magambo wanachofanya nikutishia tu watu na wala si kuwapigaa kama BABU alivyowaambia.

  BaBU baada ya kuona utaratibu huu hauwezekani ikabidi atafute njia mbadala wa watu wote waliokuja na magari wakae kwenye magari yao watapata huduma kwa njia ya gari moja likifuatia na gari lingine, sasa wewe ndugu yangu unayetaka kupata huduma ya leo kesho uondoke kama mimi kweli hiyo sahau fikiria gari letu lilikuani gari la 1350 ili tupate tiba ni kua gari la namba moja hadi sisi tufikie pale je naweza kurudi siku kama tulivyokua tumepanga? Basi tukatafuta suluhishi ni nini tufanye, basi tukawa tunasikia kutoka kwa watu kua kipindi hiki cha wakristo wanafunga KWARESMA BABU hatatoa huduma mpaka siku 40 za mfungo wa wakristo ziishe, bado naendelea kusononeka! baada ya muda tukamsikia BABU kutoka kwenye kipaza sauti akisema wanaosema kua hataponya watu kwa kipindi hicho cha kwaresma sio kweli akasema yeye ametumwa kutibu watu kwahiyo ataendelea kufanya kazi aliyotumwa na Mungu! kweli nilirukaruka kwa furaha sana. Basi tukaa chini na familia yangu na hata watu wengine walikua na mtazamo kama wangu kua kwakua BABU kashasema kua ataendelea kutoa huduma basi wacha tuondoke halafu tukajipange ili turudu siku nyingine ambayo itatubidi tuchukue likizo ya kama wiki moja ili kukabiliana na hali halisi tuliyoiona kule.

  Ilipofika saa tatu na nusu usiku tukawa tumeshapata jibu nini cha kufanya tukiangalia kwa haraka haraka tu ni lazima tuondoke! Kwanza hatuna chakula/maji/nguo za kubadilisha/hatujaomba ruhusa kazini ya kukaa zaidi ya ijumaa hadi jumapili ili jumatatu turejee kazini! basi safari yetu ya kurudu nyumbai Arusha ikaanza tena bila ya kupata dawa toka kwa BABU ilituchua tena kama masaa tisa usiku kucha kuendesha gari kwenye pori nene na barabara ni mbovu mno, tulipishana na magari kwa hesabu zangu za harakaharaka kwakua mimi ndio nilikua dereva nilipishana na mabasi kama 8 yakitokea mikoni pamoja na magari ya Land Rover na Toyota Land Cruiser yakiwa yanaelekea kwa BABU huku mimi najiuliza je hawa watarudi lini? Hii ndio ilikua ndio safari yangu ya kihistoria kwenda kwa BABU na bado sikufanikiwa kutokana na kua na muda finyu lakini nitarudi tena tu mpaka kieleweke.

  Ushauri wangu kwa wale wenyekutaka kwenda kupata dawa kwa BABU naomba chukua tahadhari hii!

  1. Uwe na muda wa kama wiki moja na zaidi kwakua hujui utapata dawa lini
  2. Uwe na chakula cha kutosha kwakua hakuna hoteli wala duka
  3. Chukua maji ya kutosha, maji yapo ya bomba na ni masafi lakini maji haya yana magadi
  4. Kuna maji ya kuuzwa ambayo kwa sisi waTZ sasa hivi utauziwa chupa ndogo ya maji ya Kilimanjaro ni shilingi 2500 na bei hii inaweza kua imeshapanda
  5. Chukua mahema pamoja na magodoro/mashuka vyoote vinanvyohusiana na maisha ya kilasiku ya binaadamu
  6. Ukiwa na usafiri binafsi au wa kukodi utakua huru sana.

  Hii ndio safari yangu ya Loliondo ambayo niliondoka siku ya Ijumaa saa 12:00 jioni na kurudi siku ya jumapili saa 2:30 asubuhi.
   
 2. d

  dropingcoco Senior Member

  #2
  Mar 7, 2011
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu Ndallo, nina hakika hii safari yako ya Loliondo itakuwa inavutia kusoma, lakini ungeongeza ukubwa wa maandishi kidogo ungetusaidia zaidi
   
 3. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pole na ahsante sana kwa maelezo mazuri, yametupa mwanga nini kinatokea huko.

  Mungu akusaidie ukirudi tena upate hiyo tiba.

  Serikali ingeingilia kati na kujaribu kusaidia ili pawepo na utaratibu mzuri wa watu kupata huduma hii.

  Red Cross na NGOs kwa ujumla haziwezi kutoa msaada wa huduma muhimu kama vyoo, maji ya kunywa, mahema ya kupumzikia wagonjwa nk?
   
 4. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #4
  Mar 7, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Ndallo font plz natamani kuendelea ila ndefu mnoa na font ni ndog jaribu kuedit kidogo basi ni ombi tu lakini si amri wala lazima
   
 5. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #5
  Mar 7, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Je, mawasiliano ya simu yapo. Namaanisha kuna mtandao wa simu unaotoa huduma huko kwa babu?
   
 6. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ndallo asante kwa info
   
 8. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #8
  Mar 7, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Yule msemaji wa nchi ya Tanzania na anayedhani ni mjuaji wa kila kitu kinachoihusu Tanzania na watu wake, ameonekana kwenye foleni ya Loliondo. Haijajulikana mara moja ameenda kufanya nini. Mwenye tetesi kamili atujuze. Nafuatilia picha, nitaziweka soon.
   
 9. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #9
  Mar 7, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ilikua ni majira ya saa 12:30 jioni siku ya ijumaa ambapo mimi na familia yangu tulipoamua kwenda kwa yule mchungaji anayetibu maradhi sugu kwa njia ya upako kutoka kwa Mungu kwa gharama ndogo sana ya shilingi mia tano (500) tu kwa kikombe cha dawa ya mitishamba ili upate huduma ya uponywaji kwa maradhi sugu ambayo sisi binadamu tumeshahangaika kwenda kwa waganga wa aina mbalimbali kwaajili ya kupata matibabu. Magonjwa sugu BABU anayotibu ni Pumu/Kisukari/Kansa/Ukimwi/Pepo na mengine.

  Mchungaji huyu anapatikana kule wilaya ya Ngorongoro kijiji cha Samunge mkoani Arusha, wananchi wengi kwa lugha rahisi wao wanasema ni kule Loliondo, siku nakwenda kule tuliondoka Arusha majira ya jioni saa 12 jioni tukaendesha gari letu mpaka maeneo ya kijiji cha Mto wa Mbu mkoani Manyara ni muda wa kama saa moja na nusu. tulipofika pale tukapunzika katika kambi moja ya kulaza wageni hawa wakizungu inajulikana kama Kiboko Camp tukapata chakula chetu cha jioni pale tukapunzika hadi ilipofikia majira ya saa nne na nusu za usiku ndipo tukawasha gari letu kuelekea maeneo yenyewe husika.

  Tukachukua njia moja inayojulikana kama Engaruka moja kwa moja hadi Ziwa Lake Natron kwakweli barabara ni mbaya mno na kama huna gari lenye kua na mfumo wa 4x4 wheel drive basi safari yako lazima iwe na mashaka sana, tulikutana na magari mengi mno ambayo tulikua tunafuatana nayo mengine tuliyakuta yamekwama mengine yamepinduka kutokana na uzoefu mdogo wa madereva kwenye njia hizo kwakweli barabara ni mbaya sana!

  Tulisafiri kwa mwendo wa masaa tisa na nusu usiku kucha! tuliwasili kwenye eneo lenyewe kwakweli ni porini na jamii ya wakazi wanaoishi kule ni jamii ya makabila ya Wasonjo ni wafugaji na wakulima, eneo lenyewe kwakweli halina vyoo wala maduka ya kuridhisha ni vibanda tu. Basi baada ya kuwasili pale lengo letu lilikua ni kupata huduma nakuondoka siku hiyohiyo, lakini sivyo kama tulivyofikiria. Kwanza barabara ni moja tu inamaanisha ukishafika pale inakubidi usubiri kwenye gari lako sana sana kama utatoka na kujinyoosha au kwenda kujisitiri vichakani na kurudi kwenye gari lako na kuendelea kusubiri.

  Kuhusu tiba ni kua huyu bwana ambaye ni mchungaji lakini kwajina tulilolikuta pale ambalo ni maarufu ni kwa BABU! bwana huyu wanavyosema wenyeji hawa ni kua baada ya yeye kuoteshwa na Mungu kuhusu uponyaji huu ni kua alipofika kijijini pale aliwaambia wale wenyeji kua njooni mpate dawa lakini wenyeji hawa wako waliomsikia na kumuamini lakini wengi wao walimdharau tu basi hapo mwanzo watu waliokua wanakwenda pale walikua ni wachache mno mmoja wao alikua ni baba yangu mzazi yeye aliondoka Arusha mjini saa saba za usiku akafika pale saa nne na nusu akapewa tiba na sala pia zilifanyika hususani na BABU aliwaambia historia yake na siku hiyohiyo baada ya tiba wakaondoka nakurejea Arusha na uponyaji ule umemsaidia sana ni kweli bwana huyu anatibu.

  Tofauti ya siku za nyuma na sasa kuhusu kwenda na kurudi siku inayofuata sasa hivi imekua ni kitendawili kama sisi tulivyokua tunajua kutokana na baba yangu kurudi siku inayofuata, makundi tuliyoyakuta pale kuna watu niliokua nawafahamu waliniuliza mimi nimefika pale siku gani nikawaambia ndio nimefika na ninataka kupata dawa halafu nirejee nyumbani ili niweze kuingia kazini siku ya jumatatu, kwakua siku naondoka Arusha ilikua ni siku ya ijumaa kwahiyo tulifika pale siku ya jumamosi asubuhi. Basi kwa mtizamo wangu nikua nipate tiba siku ya jumamosi halafu usiku tuondoke ili nifike Arusha siku ya jumapili, wale jamaa zangu walinishangaa sana wakaniambia kua wao wana siku tano na huduma bado hawajapata na bado wataendelea kusubiri mpaka kieleweke! Nilivunjika moyo sana kusikia vile na ukitegemea sisi wenyewe tulikwenda kwa madhumuni ya kurudi mapema kutokana na kazi zetu hizi za kuajiriwa na hatupendi kupoteza kazi.

  Nilifikiri kwa kina sana tukaamua tutoke ndani ya gari letu halafu tutembee kwa miguu kwa umbali wa kama kilometa 28 tukawacha gari letu tuone kama tutafanikiwa kupata dawa halafu tukishapata dawa turejee kwenye gari letu halafu tufunge safari yakurejea nyumbani, Loh tulipofika pale watu ni wengi sana hususani wale jamii ya Wasonjo wanajaribu kuleta fujo ili wapate dawa, narejea tena kama nilivyosema kua jamii hii BABU alishawaambia kua njooni mpate dawa wao wakaghairi sasa baada ya kuwaona watu ni wengi na nimatajiri sasa wao wanafanya fujo ili wao wawe wa kwanza kupata dawa kweli moyo wangu ulizidi kuvunjika kwa kutokua na matumaini ya kurudi nyumbani hii siku. Tulikuta askari pamoja na wanamgambo wanaojaribu kuwazuia wasiendele kufanya fujo jamaa walishawahi kufanya fujo hadi wakamwaga dawa hii ya BABU ambapo ilibidi BABU asitishe utoaji huu wa dawa na akenda zake ndani nakujifungia hadi pale wale wanamgambowalipowatuliza Wasonjo hawa na wakarejea kwenye hali ya utulivu lakini bado jamaa hawa sio wasikivu na halafu BABU hapendi Mgambo na askari wapige watu BABU alishakataa akawaambia msipie mtu hata mmoja hapa kwakua kila mtu hapa ni mgonjwa kwahiyo askari na magambo wanachofanya nikutishia tu watu na wala si kuwapigaa kama BABU alivyowaambia.

  BaBU baada ya kuona utaratibu huu hauwezekani ikabidi atafute njia mbadala wa watu wote waliokuja na magari wakae kwenye magari yao watapata huduma kwa njia ya gari moja likifuatia na gari lingine, sasa wewe ndugu yangu unayetaka kupata huduma ya leo kesho uondoke kama mimi kweli hiyo sahau fikiria gari letu lilikuani gari la 1350 ili tupate tiba ni kua gari la namba moja hadi sisi tufikie pale je naweza kurudi siku kama tulivyokua tumepanga? Basi tukatafuta suluhishi ni nini tufanye, basi tukawa tunasikia kutoka kwa watu kua kipindi hiki cha wakristo wanafunga KWARESMA BABU hatatoa huduma mpaka siku 40 za mfungo wa wakristo ziishe, bado naendelea kusononeka! baada ya muda tukamsikia BABU kutoka kwenye kipaza sauti akisema wanaosema kua hataponya watu kwa kipindi hicho cha kwaresma sio kweli akasema yeye ametumwa kutibu watu kwahiyo ataendelea kufanya kazi aliyotumwa na Mungu! kweli nilirukaruka kwa furaha sana. Basi tukaa chini na familia yangu na hata watu wengine walikua na mtazamo kama wangu kua kwakua BABU kashasema kua ataendelea kutoa huduma basi wacha tuondoke halafu tukajipange ili turudu siku nyingine ambayo itatubidi tuchukue likizo ya kama wiki moja ili kukabiliana na hali halisi tuliyoiona kule.

  Ilipofika saa tatu na nusu usiku tukawa tumeshapata jibu nini cha kufanya tukiangalia kwa haraka haraka tu ni lazima tuondoke! Kwanza hatuna chakula/maji/nguo za kubadilisha/hatujaomba ruhusa kazini ya kukaa zaidi ya ijumaa hadi jumapili ili jumatatu turejee kazini! basi safari yetu ya kurudu nyumbai Arusha ikaanza tena bila ya kupata dawa toka kwa BABU ilituchua tena kama masaa tisa usiku kucha kuendesha gari kwenye pori nene na barabara ni mbovu mno, tulipishana na magari kwa hesabu zangu za harakaharaka kwakua mimi ndio nilikua dereva nilipishana na mabasi kama 8 yakitokea mikoni pamoja na magari ya Land Rover na Toyota Land Cruiser yakiwa yanaelekea kwa BABU huku mimi najiuliza je hawa watarudi lini? Hii ndio ilikua ndio safari yangu ya kihistoria kwenda kwa BABU na bado sikufanikiwa kutokana na kua na muda finyu lakini nitarudi tena tu mpaka kieleweke.

  Ushauri wangu kwa wale wenyekutaka kwenda kupata dawa kwa BABU naomba chukua tahadhari hii!

  1. Uwe na muda wa kama wiki moja na zaidi kwakua hujui utapata dawa lini
  2. Uwe na chakula cha kutosha kwakua hakuna hoteli wala duka
  3. Chukua maji ya kutosha, maji yapo ya bomba na ni masafi lakini maji haya yana magadi
  4. Kuna maji ya kuuzwa ambayo kwa sisi waTZ sasa hivi utauziwa chupa ndogo ya maji ya Kilimanjaro ni shilingi 2500 na bei hii inaweza kua imeshapanda
  5. Chukua mahema pamoja na magodoro/mashuka vyoote vinanvyohusiana na maisha ya kilasiku ya binaadamu
  6. Ukiwa na usafiri binafsi au wa kukodi utakua huru sana.

  Hii ndio safari yangu ya Loliondo ambayo niliondoka siku ya Ijumaa saa 12:00 jioni na kurudi siku ya jumapili saa 2:30 asubuhi.

  By Ndallo.
   
 10. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #10
  Mar 7, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Mkuu asante kwa tahadhari yako nzuri, na maelezo yako ya kina.
   
 11. d

  dropingcoco Senior Member

  #11
  Mar 7, 2011
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 12. c

  carefree JF-Expert Member

  #12
  Mar 7, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Pole hawa wasonjo wanafanya vurugu za nini na walishindwa kutumia fursa waliyopewa sasa wanaona watu ndiyo wanaleta style za wazawa kwanza . Ila kwa style hiyo ya kutoa dawa kufuatia mpangilio wa magari ndiyo wamefutwa kwani wao nadhani hawana usafiri .
  Pole next time watu wanaweza pungua na wewe uponyeke
   
 13. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #13
  Mar 7, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Mhh! Kazi ipo!
   
 14. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #14
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Bora akatibiwe ugonjwa wa kichwa na ubongo uanze kufanya kazi!
   
 15. birungi

  birungi JF-Expert Member

  #15
  Mar 7, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  utaambiwa ameenda kuripoti habari,kipindi cha JE WAJUA?
   
 16. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Na ngoma pia
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Mar 7, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,588
  Likes Received: 18,570
  Trophy Points: 280
  Wajameni, pamoja na maroroso yake yote, Kibonde pia ni human being kama mimi na wewe, anayestahili heshima ya utu wake, 'dignity' na right to privacy!. Hata mimi binafsi nasubiri foleni zipungue, nitie timu Loliondo!.
   
 18. d

  dropingcoco Senior Member

  #18
  Mar 7, 2011
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 124
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukisikia umbea ndio huu, kwani yeye si binadamu?
   
 19. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #19
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  So what? Nawewe unamatatizo ya kichwa kama kibonde?
   
 20. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #20
  Mar 7, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni binadamu anayependa kuchonga sana juu ya watu wengine!
   
Loading...