Picha na stori za Loliondo- kwa Babu

Picha na stori za Loliondo- kwa Babu

hapa si tii neno, nimeiona avatar yake jukwaa fulani!!
 
Kama wanaoenda lolyondo wote ni waathirika bac tanzania wote ni waathirika coz nusu y tanzania yote iko kule nasema hivyo coz na mimi nimeenda kupewa dawa na wala cumwi chochote.... babu kakuharibia nini sasa?
 
Atakuwa amekwenda kutibiwa ila alivyo na magonjwa mengi hata sijui atibiwe lipi kwanza!
 
Mzee wa kaya mwenyewe karipoti huko sasa wewe unasubiri nini..?
 
Nimekuwa nikiona kwenye magazeti hivi karibuni kuhusu huyu babu wa Loliondo. Hivi hii dawa ni kweli au?? Inakuwaje serikali inapeleka mpaka askali na kusimamia ugawaji wa dawa ambayo haijathibitishwa?? Je kama watu wananyweshwa sumu au wanatapeliwa serikali itasema nini?? Kwa nini serikali isiombe wataalamu wa WHO haraka ili kuifanyia utafiti hii dawa badala ya kuachia itolewe kiholele??



Vigogo wasababisha vurugu Loliondo
Send to a friend
Tuesday, 08 March 2011 21:56
0diggsdigg


loliondowagonjwa.jpg
Mgonjwa akiwa amebebwa kwenye baiskeli ya wagonjwa akipelekwa kunywa dawa kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapile katika kijiji cha Samunge, Tarafa ya Sale, Loliondo mkoani Arusha.

Nana Mollel na Mussa Juma, Arusha
WATU wanaodaiwa kuwa ni vigogo wa Serikali wamesababisha vurugu kubwa katika Kijiji cha Samunge, Tarafa Sale, Loliondo kunakotolewa tiba ya magonjwa ya sugu na Mchungaji Mstaafu, Ambilikile Mwasapile baada ya kuvuruga utaratibu wa foleni kabla ya kupata huduma hiyo.Vurugu hizo zilianza pale kundi la watu lilipobaini kuwa vyombo vya dola, askari polisi na wanamgambo waliokuwa wanalinda usalama katika eneo hilo, wanawasaidia vigogo kuwahi kunywa dawa kwa kukwepa foleni.

Hali hiyo ilisababisha wananchi kupoteza imani na ulinzi huo na kuamua kuziba barabara zilizokuwa zinakwepa foleni kwa kutumia mawe na magogo. Hata hivyo, vigogo hao waliamua kuacha magari yao na kuanza kuelekea nyumbani kwa Mchungaji huyo kwa miguu kitendo ambacho kiliwafanya wananchi kuamua kuvamia jiko linalotumika kutengeneza dawa hiyo na kuanza kuinywa bila mpangilio jambo lililosababisha utaratibu wa kutoa dawa kusitishwa kwa saa saba.
Vurugu hizo zilisababisha msongamano mkubwa na watu kutawanyika ovyo katika maeneo mbalimbali ya kijiji hicho kiasi cha kuharibu shughuli za kawaida za kila siku za wenyeji ambao nao walikerwa na hali hiyo kiasi cha kuamua kukata mabomba ya maji yanayotumika kutengeneza dawa kwa mchungaji.

Akizungumzia tukio hilo, Mchungaji Mwasapile alielezea kuchukizwa na vitendo vya watu kuvamia na kujinywea dawa bila utaratibu.Tangu kutangazwa kwa habari za Mchunguji Mwasapile kutibu magonjwa sugu, kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaomiminika kijijini hapo kutaka kupata huduma hiyo kiasi kwamba baadhi ya wagonjwa wamepoteza maisha hata kabla ya kuhudumiwa.

Uchunguzi uliofanywa umeonyesha kwamba wengi wa wagonjwa waliofariki dunia ambao wanakadiriwa kuwa kati ya sita na 14, ni wale waliotolewa wakiwa hoi katika hospitali mbalimbali nchini hasa za Kanda ya Kaskazini. Akizungumzia tukio la wagonjwa kufariki wakiwa wanasubiri huduma, Mchungaji Mwasapile aliwataka wananchi kuacha kuwahamisha wagonjwa waliolazwa hospitalini na kuwapeleka kwake.

Alisema kitendo hicho kinasababisha wengine kuzidiwa na hata kufa kwa kuwa wanaotaka huduma ni wengi kuliko uwezo wa kuwahudumia mara moja. Alisema kitendo cha wagonjwa kukaa muda mrefu katika mazingira mabaya ya kusubiri dawa kunasababisha wengi kuzidiwa na hata kufa.
Akizungumza na Mwananchi jana, mmoja wa wasaidizi wa mchungaji huyo, Paulo Dudui alisema: "Mchungaji anawaomba watu wenye wagonjwa wachukuwe tahadhari ili wagonjwa wanaowaleta waweze kufika kwa mchungaji na kupata tiba. Wajue kuna wagonjwa wengi, barabara ni mbaya na huku hakuna huduma muhimu kama chakula. Leo nimeona miili mitatu ya wagonjwa waliofariki dunia." Dudui alisema kutokana na taarifa ambazo wanazo kulikuwa na watu wengine sita ambao walifariki, akiwepo mtoto mdogo ambaye aligongwa na gari akiwa amelala.

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali alisema taarifa alizonazo hadi juzi kulikuwa na vifo vya watu sita. Hata hivyo, baadhi taarifa zilizopatikana kutoka kwa waliokuwa wanasubiri kuhudumiwa zilisema waliokufa ni 14.
Hata hivyo, mmoja wa wafiwa aliyejitambulisha kwa jina moja la Rogers, mkazi wa Kigoma alisema baada ya kufiwa na ndugu yao yeye na ndugu zake walichukua uamuzi wa kumzika ndugu yao njiani: "Tulilazimika kushuka na kumzika njiani," alisema Rogers wakati akiwa kwenye foleni ya kwenda kupata dawa akisema hata yeye ni mgonjwa.
Alisema baada ya kupata dawa itabidi arejee kwao kutoa taarifa za msiba huo ili taratibu nyingine za kifamilia zichukue mkondo wake. Baadhi ya wafanyabiashara wamevamia eneo hilo na kuanza kuuza bidhaa kwa bei ya juu. Bei ya maji ya nusu lita inayouzwa Sh500 inauzwa Sh1,000 na ya lita moja hadi moja na nusu yaliyokuwa yanauzwa Sh 1,000 yamefikia Sh 2,500.

Sahani moja ya chakula iliyokuwa inauzwa Sh1,000 kijijini hapo, sasa inauzwa Sh 2,500 hadi 4,000. Kuku aliyekuwa anauzwa Sh6,000 sasa ni Sh25,000.Wilaya nayo imekuwa ikitoza Sh2,000 kwa kila gari linalopeleka wagonjwa huko, utaratibu uliobuniwa na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro kwa ajili ya kutengeneza vyoo na huduma nyingine muhimu ambazo zinahitajika.
Tayari, wafanyabiashara kutoka mkoani Kilimanjaro wameanza kupeleka mahema na huduma za vyakula katika kijiji hicho. Dudui, alisema kuwa tayari gari moja kubwa la mahema ya kukodi lilifika jana kijijini hapo na kazi ya kuyafunga inaweza kuanza leo.
 
Toka habari za Mchungaji mstaafu wa Loliondo kuanza kuandikwa na magazeti, kummekuwa na mitazamo mingi tofauti juu ya tiba aitoayo "Babu" na uhakika wa tiba yenyewe. Kuna watu ambao wengi wao ni wataalamu wa tiba hizi za kizungu wamekuwa wakiongoza kundi linalokataa au kupinga uwezo wa dawa ya babu kutibu. Kwa upande mwingine kuna kundi la viongozi wa dini hasa wa kiislamu wengi wao wamekuwa wakipinga uponyaji wa dawa ya Babu na kufikia hatua ya kuiita tiba hiyo kuwa ni sawa na ushirikina. Wameenda mbali na kusema kuwa kama mgonjwa (mwislamu) akifa akiwa huko ni sawa na kufa "KAFILI" bi maana kuwa hana imani ya kiislamu. Kwa upande mwingine Serikali kupitia wizara ya afya hadi siu ya jana wamesema kwa sasa wao hawapingi kuwa dawa hiyo haitibu na wala hawakubali kuwa kweli inatibu hadi hapo watakapofanya utafiti vizuri.

Katika makundi yote haya mi naona yote yanafungwa na kauli moja ya kitaalamu isemayo " NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK" Badala ya kutoa kauli tofauti za kupinga uwezo wa dawa za Babu, MADAKTARI wetu walitakiwa kuitumia fursa hii iliyopo ya wagonjwa wenyewe kuwa willing kutumika kama " GUINEA PIG" bila hata ya kudai malipo. Maana kiutaratibu ili uweze fanya utafiti wa dawa kwa binadaam inabidi uwatafute watu uwashawishi tena kwa malipo wakubali ili uwatumie katika utafiti huo. Lakini hapa mungu katujaalia saana kwa kufupisha utaratibu huo maana wagonjwa wenyewe wako willing tena kwa gharama zao za kusafiri toka mbali, kinachotakiwa tu ni kwa mtafiti kuwathibitisha kuwa kweli wanaumwa maradhi hayo wanayosema kama ni HIV, Sukari, Presha nk. Baada ya hapo unaacha wapewe dawa hiyo and then unawafuatilia ili kujua kama kweli dawa inatibu au ni ujanja tu wa Babu. Na katika hili Mimi nawalaumu saana wizara ya afya imeshindwa kufanya kile inachotarajiwa kifanywe. Maana Huko Arusha na hasa hapo tu Loliondo kuna hospital ya wilaya, ambayo wao wangeitumia kama kituo cha kufanyia utafiti huo. Wangewachukua wagonjwa hapo hospital wanaosumbuliwa na maradhi hayo na kuwasafirisha hadi kwa Babu wakapewa dawa, then wakawarudisha hospital na kuwa monitor japo kwa mwezi mmoja kujua maendeleo yao ukilinganisha na hali waliyokuwa nayo kabla ya kupewa dawa. Hapo serikali ingeweza kujua ukweli juu ya dawa hii kuliko hali ilivyosasa.

Kama mimi ningekuwa na mamlaka ningefanya yafuatayo baada ya kusikia habari hii ya uwezo wa dawa ya babu:
1) Kwanza ningeongea na Babu na kumuomba kuwa zoezi la kuwapeleka pale wagonjwa wote lisimamiwe na mimi kama serikali

2) Then ningesema kuwa wagonjwa wote wanaotaka kwenda kutibiwa kwa babu wataweza kwenda huko kwa kupitia hospital za mikoa na ni wagonjwa wale tu watakaoletwa na hospital ndio watatibiwa. Hawa watasafirishwa kwa gharama za serikali kama ambavyo serikali hufanya pale mgonjwa anapopatiwa Rufaa toka hospital moja hadi nyingine.
3) Gharama zote za Babu yaani shilingi 500/= ingelipwa by cash na serikali
4) Ningepiga stop kwa wagonjwa kwenda binafsi kwa babu, na kuwa ni wale tu watakao pitia hospital ndio watapatiwa dawa

Kwa njia hii nadhani hali isingekuwa kama ilivyo sasa.
 
USHAURI: Kwanza binti anaonekana kujali afya. Mwambie nawe akupeleke ukanywe dawa ya Babu kama utaonekana una tatizo japo kwa mbaali. Kisha miezi mitatu ijayo wote mkapime hospitali kuona kama hakuna magonjwa ya kuambukiza. Kwanini hakuweka wazi safari yake-ni kutokana na kutokufahamu vizuri, ungeipokeaje vipi habari hiyo.
 
ivi huyu babu anatoa hiyo huduma masaa 24 au?? asije akafa kwa ochovu kabla wengine hatujaenda kuchukua huduma!!!!1
 
ivi huyu babu anatoa hiyo huduma masaa 24 au?? asije akafa kwa ochovu kabla wengine hatujaenda kuchukua huduma!!!!1

nasikia mwisho ni saa 12 jioni.......hivi anakula hata lunch kweli?
 
Vizuri , ila huoni hilo la kupitia hospital tena watendaji wetu hawa, rushwa ndo itaanzia hapo maskini hawataenda kumuona babu, wataambiwa njoo kesho nyingi, kwanza serikali ipi watu watapatia ulaji hapo mpaka process za kumuona zifike unaweza ukamaliza milioni, au ukaambiwa watu ni wengi sana subiri.
 
kutokana na habari hizo inaelekea hali ni mbaya serikali ichukue hatua
 
iNAWEZEKANA ALIENDA KWA MKUMBO TU KUTAKA KUMUONA BABU, NI SAWA NA KINAPOTOKEA KITU CHA AJABU KILA MTU ANATAKA KUKIONA NDICHO KILICHOTOKEA. MUULIZE AKISEMA ALIENDA KWA MKUMBO MUAMINI MAANA KWANZA KESHAPONA.
 
Baadhi ya wazee waliokula chumvi nyingi na walioona mengi wanasema muujiza huo ni kweli kwa maana hata katika vitabu vitakatifu imeelezwa. Na kwamba tukio kama hilo la muujiza na nusura inayopatikana kutokana na muujiza huo inaweza KUDUMU MIAKA KIASI MITATU na itapotea kimuujiza. Isipokuwa waliofanikiwa kunywa watakuwa wamepona kabisa. Huo ni uwezo wa Mungu. suala la kuthibitishwa na WHO na wataalamu wengine WAZEE wanasema hakuna kitu kitakachoonekana. Na hata aliyebarikiwa akitoka nje ya eneo lile kwenda kunyeshea sehemu nyingine tiba haitafanyakazi.Mambo yenyewe asili yake NDOTO utathibitisha kwa kipimo gani ?
 
Haya mambo yapo... kumbuka Yesu alipomponya yule mtu mwenye ukoma aliyekuwa ansubiri malaika atikise maji halafu awe wa kwanza kuingia. Alichofanya yesu ni kumwonesha tu kuwa yeye hana muda wala masharti ni any time ila hakupinga kuwa pale hakuna uponyaji.

Tutaendelea kumwomba mungu afunue juu ya hili na kwenda ruksa ila mtangulize Yesu kwa kila jambo ( Huenda unafanya hivyo kila wakati)
 
Tabu ni nini wote sie ni binadamu na kila atakaye ana uhuru wa kwenda kwa babu kwani vigogo sio binadamu?

Bora kuongelea mengine na sio nani kaenda nani hajaenda. Ok?
 
Kwani ukiwa kiongozi ndo huhitaji tiba? wao ni binadamu kama wengine kamera za nini?
 
now no dowan wala katiba mpya,cjui maandamano ya chadema kila m2 babu wa wa loliondo ndo tz yangu hii...
 
Back
Top Bottom