Picha na stori za Loliondo- kwa Babu

Picha na stori za Loliondo- kwa Babu

Itakuwa ngumu kwa serikali kulifanyia kazi hilo suala kwa sabau serikali bado iko kwenye mchakaato wa kuchunguza ile dawa ya babu.
pia ikifanikiwa kupita ndo hapo sasa itaanda utaratibu wa kwenda kwa babu...kupitia hosp ni ngumu kwa sababu serikali itakuwa inatibu kwa miti shamba na sio tena dawa zilizothibitishwa...kuna chombo kama WHO kitapinga pia.
Tusubirie tujue werikali kupitia NIMR watasemaje kuhusu hilo......ndo mawazo yangu!

Watu wanaumwa Dowans saa ngapi tena? tutakuja kuibana Dowans tukiwa na afya wacha kwanza watu wapige vikombe ha ha ha ha ha

Unajua hata wakifanya utafiti hawawezi kupata kitu, kwani kinachoponya pale ni nguvu ya Mungu kupitia ile dawa. Kikombe anachopewa mgonjwa ni kupima tu imani yake.

wa ngumu kwa serikali kulifanyia kazi hilo suala kwa sabau serikali bado iko kwenye mchakaato wa kuchunguza ile dawa ya babu.
pia ikifanikiwa kupita ndo hapo sasa itaanda utaratibu wa kwenda kwa babu...kupitia hosp ni ngumu kwa sababu serikali itakuwa inatibu kwa miti shamba na sio tena dawa zilizothibitishwa...kuna chombo kama WHO kitapinga pia.
Tusubirie tujue werikali kupitia NIMR watasemaje kuhusu hilo......ndo mawazo yangu![/QUOTE]
Na hapo ndio penye tatizo kwa nchi zetu hizi. Tunategemea saana maamuzi yetu yafanywe na wazungu. Nafikiri kama nchi inabidi tufikie sehemu tuwe na maamuzi yetu wenyewe. Hizo dawa za WHO zinaanzia na miti shamba, sasa sioni ajabu iwapo sisi tutajulikana kuwa tunatumia dawa hizi. China na India wako juu saana duniani kwa matumizi ya dawa hizi. Tuachane na hao wazungu

Kama huyu mganga ni Kweli basi Serikali MARA MOJA impeleke pale Muhimbili akasaidie kutoa huduma.

Huyo sio mganga ni mtumishi wa Mungu ambaye ametumwa kwa makusudi maalumu. Uwepo wake hapo Loliondo ni mpango wa mungu ndiyo maana yeye ni mwenyeji wa Mbeya lakini huduma yake aliyoitiwa ipo Loliondo. Msifanye utani na Mungu jamani.

Huyo sio mganga ni mtumishi wa Mungu ambaye ametumwa na kwa makusudi maalumu. Uwepo wake hapo Loliondo ni mpango wa mungu ndiyo maana yeye mwenyeji wa Mbeya lakini huduma yake aliyoitiwa ipo Loliondo. Msifanye utani Mungu.

Jamani msimuingize mungu kwenye haya mambo ya huyu mganga wa kienyeji,wapi katika biblia mungu alifanya hivyo anavyofanya huyu ex-mchungaji? Jamani tuwe waangalifu sana hizi siku za mwisho. Huyu anatumika tu na ibilisi wala siyo mungu!

Jamani msimuingize mungu kwenye haya mambo ya huyu mganga wa kienyeji,wapi katika biblia mungu alifanya hivyo anavyofanya huyu ex-mchungaji? Jamani tuwe waangalifu sana hizi siku za mwisho. Huyu anatumika tu na ibilisi wala siyo mungu!

anatumia tunguli?

Jamani msimuingize mungu kwenye haya mambo ya huyu mganga wa kienyeji,wapi katika biblia mungu alifanya hivyo anavyofanya huyu ex-mchungaji? Jamani tuwe waangalifu sana hizi siku za mwisho. Huyu anatumika tu na ibilisi wala siyo mungu!
Una ushahidi kuwa anatumika na shetani??

Wametangaza asubuhi wakati wa magazeti kwenye habari picha Radio one nimesahau gazeti, picha inamuonyesha Mwenyekiti wa CCM Kilimanjaro Vick Nsilo Swai akiwekewa dawa na babu

Heri yake yeye aliyekubali na kutii atakula mema ya nchi...wewe baki na ushabiki wako wakuhesabu wenzio as if death is excluded from you!

Kama wanatafuta tiba wapone ni vizuri tu!!
Tunawaombeaga watu afya njema!!

Hakuna mtu yeyote anayependa kuwa mgonjwa, ugonjwa ni adha ni mahangaiko, hivyo tujaribu kuwasitiri ndugu zetu wanaokwenda kujaribu kupata uponyaji sio vizuri kuwa tangaza na kuwaumbua sio uungwana, uzima ulio nao usikufanye uone wanaougua wamestahili. Nimesema hivi kwani naona kuna watu wengi wanahamu ya kujua nani na nani anakwenda huko nafikiri la msingi ni kuwatia moyo wale wote wenye matatizo ili waondokane na shida wapate uponyaji sio busara wala uungwana kutafuta picha zao na majina ili kuwaumbua.

Siku zote kile kimjazacho mtu ndicho kimtokacho.kama mtu amezoea kunena maneno ya busara ana busara, kama ni matusi hana busara hali kadhalika wale wanaokua wepesi sana kusema kua babu ni mganga wao ni wa kundi hilo pia.na wale wanasema kua babu ni mchungaji na kuamini amepewa maono pia ni hukohuko

Sasa hapo issue ni nini?? Kama wako Loliondo so what, ina maana wewe LD huna ugonjwa wowote. Achana na maisha binafsi ya watu. kama wako huko well and good wanaonyesha wanajali afya zao.

Binafsi sijaenda Loliondo ,lakini haijaninyima kutafuta shuhuda za watu mbalimbali ili kujua nini kinaendelea . Mchungaji Mwasapile amepata ufunuo na kuoteshwa katika ndoto,akakabidhiwa kikombe ambacho atawapatia watu dawa nao watapona magonjwa mbalimbali yakiwamo ya kisukari,pumu,presha na hata ukimwi na magonjwa mengine sugu .kama una virusi ukishapatiwa
dawa hiyo baada ya siku saba utaitajika kwenda kupima ili ukiri mwenyewe muujiza wako .

Kwangu sio tiba ya kisayansi na napinga wale wote wanaotaka kuingiza ubinadamu na hata usayansi wao katika hili . katika mambo haya ya kiroho hatua zozote za kibinadamu zitashindwa kabisa . kakobe kumpinga mchungaji huyu ilhali wapo mashuhuda wa miujiza hii ni anaonekana jinsi alivyo pindi anapokosa la kusema . Kama kakobe ataongea katika mlengo wa ushindani wa kibiashara katika huduma ya kiroho analipeleka wapi kanisa lake . Ina maana kama ni kweli yeye ( kakobe ) ana ufunuo wake ina maana hakuna mtu mwingine yeyote anaeweza kupata ufunuo kama wake na hata kumzidi .maneno yake dhidi ya mchungaji mwasapile hayana tija,hayafai kusikilizwa na anajivunjia heshima yake.

Jumapili katika vijiwe vyetu vya weekend tumepata watu wakishuhudia miujiza yao . Kuna mzee mmoja alikuwa na presha mbaya kabisa leo hii presha yake ipo normal .Sijapata shuhuda wa HIV lakini wapo na nimesoma kwenye vyombo vya habari . Jana tarehe saba nimekutana na mzee mmoja / mfanyabiashara katika maongezi yake amesema sukari yake kwa sasa ipo normal . Alikuwa dhaifu sana mwanzoni na katika safari yake ya kurudi kutoka Loliondo alipofika mto wa mbu alikula Chips mayai kitu ambacho ni nadra sana kwa watu wenye kisukari.

Katika maelezo haya tunapaswa kuelewa kwamba uwepo wa mungu ni dhahiri,hasa kwa wale wanaomtumaini . Waliokuwa na mizigo yao ya maradhi hatimaye mungu amekuja kiuhalisia kumtumia mtumishi wake Mwasapile ili kuponya .

Wagonjwa wote wenye matatizo sugu waanze kuelekea loliondo . Zipo Changamoto kadhaa hasa za usafiri na wingi wa watu . Wajasiriamali wameshatumia mwanya huu na nauli kwenda na kurudi Lolionda kutokea Arusha ni Sh 100,000 kwa sasa . Usisahau 500 ya mzee yeye hana makuu kwani ana roho mtakatifu na sio roho mtaka vitu .Katika 500 hiyo 200 ni kwa ajili ya wamama wanaochemsha dawa,200 ni kwa ajili ya kanisa na mia ndio ya kwake.

Leo asubui nimemsikia naibu waziri wa afya akiongea na waandishi wa habari anasema wizara haiwezi kutoa tamko juu ya tiba hiyo lakini wanafuatilia ubora wa tiba hiyo na mazingira inapotolewa. Hapa namshauri mheshimiwa waziri abadili mawazo yako ,aondoe huo uchunguzi wake. Atakuta anachunguza matendo ya mungu ambapo ni dhambi kubwa . Hakuna chembe ya ubinadamu katika hili . Dawa hiyo hiyo inaponyesha ukimwi,kisukari na hata presha .hashangai ! Asije akatuma na/au akaunda tume katika hili kwani atashindwa.

Natumaini Mmenisoma

This is well spoken mushynoe...As forme "imekaa vyema"!!! Thanx!

Kuna tatizo gani? Hawa ni wana jamii wenzetu kama wameafuta tiba sawa tu wala siyo issue.Na wewe umejuaje au mko pamoja?

Back
Top Bottom