Mkuu wangu unajua mnachekesha sana.. Unaposema hakuna mtu anayepinga mahakama ya Kadhi una maana gani ikiwa unatoa masharti? Mbona chombo cha kikristu kama CSSC inaongoza shughuli za ELIMU na AFYA nchini kwa fedha za serikali na siwaoni mkilipinga hilo..Au kwa sababu ni chombo cha kikristu? Hivi kweli ingekuwa chombo hicho ni Bakwata mngekuwa na maamuzi hayo hayo..Swala la NECTA unasema hudhani kama lina Ukweli? halafu unakuja na mahesabu yako wewe. Je, umefanya uchunguzi (utafiti) au unasema tu kwa sababu wanaoweka madai haya hukubalinani nao. Na kwa nini mnaona taabu sana kubadilisha mfumo wa chombo hiki, Je, ktk utetezi huu huoni kama ndio mnazidisha mashaka?.Sidhani kama kuna mtu anapinga Mahakama ya Kadhi,ila tunachopinga ni nani aigharamie Mahakama hiyo?Je ni halali kwa serikali kuigharamia ilhali walipa kodi ni wakristu na waislamu? Je kama Mkristu Mahakama hiyo inamsaidiaje?Kama waislamu wenyewe wanauwezo wa kuigharamia mahakama hiyo wamepewa ruhusa ya kuifungua na kuitumia.
Swala la NECTA sidhani kama linaukweli kwani kuna watoto wakiislamu waliosoma shule za Wakatoliki au Wakristu na wamefaulu vizuri kuliko hata wakristu wenyewe,tatizo ni bidii za watoto wetu kujifunza na kutilia maanani masomo na shule.Makosa mdogomadogo yasifanye tatizo kuwa kubwa sana.Nina historia na kusoma na mabinti kutoka Handeni miaka ya themanini ,mabinti wale walikuwa shule hawaithamini kabisa na wengi walifeli karibu asilimia tisini na tano ya wasichana toka Handeni walifeli,je utawalaumu walimu au NECTA?
Tuwafundishe watoto wetu kujali masomo bila kuangalia udini wao,kwani taifa letu limejengwa na watu waimani tofauti (wakristu,waislamu,wapagani wahindu N.k)
Hata huyo mtoto mkristu leo kesho anaweza akabadili kuwa muislamu na muislamu kuwa Mkiristu,tusiwabague watoto wetu.
Ifike mahala Chadema wawe wawazi. Binafsi yangu nimeshawaonyesha mwanga mkubwa sana juu ya mahakama ya Kadhi, OIC, NECTA na MoU humu JF ili wapate hata kutumia baadhi ya hoja na majibu yangu ktk kujitambulisha kwa wananchi na hasa waislaam lakini Chadema wamekuwa wakimya sana. Rejea Hotuba ya Dr.Slaa kule Kilombero ktk uchaguzi wa mwaka 2010 kuna maneno aliyazungumza kule na ndio yakaleta utata mkubwa sana. Hivyo ni muhimu sana kwa Chadema pamoja na umaarufu huu wa Muda wawe WAZI kuhusu maswala muhimu kwa jamii zetu.
Wanawake wamekuwa wakilalamika sana kuhusu huduma ya AFYA, tokea maswala ya mimba, uzazi, watoto, magonjwa ya kike, vitanda, dawa na kadhalika lakini serikali yetu imekuwa ikiwapuuza kwa miaka yote.. Ati majuzi JK amekwenda Marekani na kupewa msaada na chombo cha mtu binafsi anayeghulika na NGOs badala ya serikali yetu wenyewe kuwa na SERA zinazopambana na sheria dume ktk kuwakandamiza wanawake na watoto. Hizi ndizo sehemu Chadema inatakiwa kuzipa kipaumbele ktk utambulisho wa sera zake maana hawa ndio wapiga kura wenyewe..
Chadema kama chama kinatakiwa kuweka sera zake hasa ktk kupambana na adha hizi toka swala la Muungano, Waislaam na wanawake maana huwezi kuijenga jamii yetu pasipo kuondosha Ubinafsi ulokwisha jengeka chini ya CCM kwa kutugawa katika makundi kufikia maendeleo.