"Sauti ya Watanzania" ni strategy dhaifu sana ya kudhoofisha upinzani. Fuatana nami, unganisha matukio, wajue na kaa nao mbali....

Uzima Tele

JF-Expert Member
Jan 20, 2023
1,101
2,344
Utangulizi

Political propaganda ni taaluma kama taaluma zingine. Inapofanyika kwa umakini huleta matokeo. Lakini inapofanyika unprofessionally kama UWT wanavyofanya hapa kwa kuwatumia hawa wanaoitwa Sauti ya Watanzania kama nitakavyoonesha hapa, inamharibia kabisa badala kumjenga anayefanyiwa propaganda hiyo iwe mtu au taasisi au chama cha siasa..

Asikudanganye mtu. Amsha amsha ya , Operesheni na mikutano ya CHADEMA ya kuelemisha wananchi iliyopewa jina la +255, KATIBA MPYA, OKOA BANDARI ZETU iliyokuwa inahudhuriwa na maelfu ya wananchi kwa hiari yao iwe jua au mvua katika mikoa ya Katavi, Kigoma, Tabora, Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara imewatia hofu CCM na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan na kuwafanya walale vitandani na viatu...

Ilikuwa ni lazima waje na plan kabambe ili ku - neutralize mambo. Fuatana nami ktk uchambuzi huu..

Sauti ya Watanzania na agenda ya katiba mpya na mkataba wa bandari. Are they real?
Mtu asipokuwa makini anaweza kudhani ni wapinzani kweli dhidi ya sera na mipango ya CCM na serikali yao na wanatetea hii kitu. Ni uongo mtupu, ni kinyume chake kabisa. Hawa ni nyoka hatari ndani ya vazi la wakosoaji na wapinzani wa CCM..

Wanatumia agenda zilezile zilizobebwa na CHADEMA yaani Katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, mkataba wa bandari kama ndoano tu ya kunasia samaki [CHADEMA] huku wakiuficha unyoka wao...

CHADEMA waliliona hili. Hawakufanya makosa kuwashitukia. Hongereni CHADEMA, mmejiokoa..

Igizo la Kukamatwa kwa Dr Wilbroad Slaa, Wakili Boniface Mwambukusi na Mdude Nyangali na kesi yao ya uhaini

Utadhani ni kweli. Lakini huo ulikuwa mwanzo na sehemu ya igizo la filamu yenyewe chini ya uratibu wa hovyo wa TISS ya CCM.

Kama kuna anayebisha, asubiri aone kama kuna kesi yoyote itaendelea na mtu asije akashangaa kwa baadhi ya wana Sauti ya Watanzania wakalamba teuzi mbalimbali iwapo watafanikiwa kuifanya kazi yao vyema..

Hizi kelele za mng'ako wa members wa kundi hili tunazozishuhudia sasa ni taharuki baada ya kuona mpango wao umeshindwa..

Just try to think. Kesi inaanza kama uhaini. Hakuna dhamana hapo. Ghafla ikabadilika na kuwa uchochezi. Watu wakatoka kifungoni. Waliowakamata wala hawakujali kinga ya kibalozi ya Dr Wilbroad Slaa. Anatoka ndo wanakumbuka kuiondoa hiyo kinga ili acheze hiyo filamu vyema na kwa uhuru usio na maswali..

Je, TISS wanahusika kwenye mkakati huu?

Absolutely Yes, 100%.!!

Ushahidi wa kimazingira unathibitisha hili. "Sauti ya Watanzania" ni strategy ya TISS kuzima nguvu ya CHADEMA. Iko mikakati mingi ya gizani na ya wazi. Huu ulikuwa wa wazi lakini ulioandaliwa kishamba sana na kumpa kazi hii Dr Wilbroad Slaa mzee wa miaka almost 77 labda wakidhani anaijua CHADEMA na viongozi wake. Na anadhani CHADEMA ya sasa ni sawa na ile ya mwaka 2015. Amekosea..!

Masikini baadhi ya vijana wa vyama vya siasa hususani toka CHADEMA na vyama vingine wameingizwa humo kwa kujua au bila wao kujua..

Na kwa ustadi wa hovyo sana and unceremoniously wakajaribu kuivuta CHADEMA yote ishiriki kwenye mkakati wao. Thank God, wameshindwa...

CHADEMA wakauona mtego huo, wamekataa. Sauti ya Watanzania wakang'aka kwamba wametengwa na CHADEMA. Wakarusha kila aina ya shutuma. Wakasema ooh, hawa CHADEMA wanajidai kupigania maslahi ya nchi kumbe wana maslahi yao..

Msimamo wa CHADEMA uliotolewa na Mwenyekiti wao Mh. Freeman Mbowe ni simple and very clear...

Lakini jamaa hawa wanajifanya kutoelewa kabisa. Bila shaka ni wajinga hawa. Haraka haraka wameigeuza vita hii kuwa ya Freeman Mbowe personally. Wanatumia kanuni ya "mpige mchungaji, kondoo watawanyike". Wenye akili wameliona hili na wanawashangaa..

Hebu take time na sikiliza kipande cha hotuba ya Mwenyekiti wa CHADEMA ndugu Freeman Mbowe kilichowakwaza hawa jamaa hapa👇👇

Hebu mtu makini aniambie, hatuba ya Mwenyekiti wa CHADEMA mpaka hapo ina shida gani hata hawa watu wakasirike kiasi hiki?

Kuhusu Dr Wilbroad Slaa kurudi CHADEMA iwapo alishatambua na kujutia kosa lake la mwaka 2015 Mwenyekiti alishamfungulia mlango siku nyingi. Msikilize👇👇

Lakini cha ajabu huyu Mzee anatumia hila kurudi kwa mlango wa nyuma na nia yake ni kumaliza kazi aliyoshindwa kuifanya vyema mwaka 2015...

Siku 30 alizotoa Mdude Nyangali zimeisha?

Ndiyo. Mpaka jana sauti ya Watanzania walikuwa Mwanza kuanza maandamano yasiyo na ukomo. Waliendelea kujifunua na kueleweka kirahisi sana...

Kilichotokea Mwanza

Hatimaye siku 30 walizompa ndugu yao Samia Suluhu Hassan serikali zinaisha. Sauti ya Watanzania wakaenda Mwanza kuanza maandamano yasiyo na ukomo...

Huko wanatoa kichekesho cha ajabu sana. Eti walikuwa wanazuiwa hata kununua maji ya kunywa madukani au kwenye vioski, kula na kulala hotelini na kunyimwa kumbi za kufanyia mikutano yao...!

Hivi mtu mwenye akili sawasawa anaweza kuamini ujinga huu? Tangu lini maandamano yasiyo na ukomo yakafanyikia ukumbini au hotelini? Na Mwanza yote ikose wanaharakati wenye mrengo na itikadi yao wenye nyumba na hoteli za kula chakula na kuwalaza?

Inashangaza sana kuwa, Sauti ya Watanzania wana Wakili Msomi Boniface Mwambukusi. Ikawaje anakubali kuwa denied haki yake na za wenzake za msingi kama kula chakula, kunywa maji, kulala hotelini na yet asichukue hatua stahiki Kwa wanaomtendea hayo?

Majibu ya maswali hayo ni rahisi tu kuwa, huu ni mchezo uliopangwa vyema na serikali hiihii Kwa kuwatumia watu hawa kuelekea kwenye lengo kuu yaani kumwangamiza Freeman Mbowe na CHADEMA....!

Poor strategy, poor planning and poor preparations. Kwa sababu hizi naweza kuelewa ni kwanini Sauti ya Watanzania mlikuwa mnawahitaji CHADEMA. Kosa lenu ni kufanya mambo kishamba na kwa pupa...!

Baada ya kila kitu kuonekana kushindikana, vijana wa Dr Wilbroad Slaa sasa wanajirekodi na kurusha shutuma hizi kwa CHADEMA akilengwa zaidi Mwenyekiti.

Msikilize huyu 👇👇👇kisha pima kama makalamiko yake yanaleta mantiki yoyote..

Yaani mwanzo mwisho ni kujichanganya tu...

Ni kana kwamba CHADEMA ndio waliwazuilia kumbi za mikutano yao kule Mwanza, au barabara za maandamano yao au hoteli za kula chakula na kulala na maduka au vioski vya kununua maji ya kunywa..

CHADEMA chini ya ya u - Wenyekiti wa mwamba Freeman Mbowe mna akili sana, mmekomaa. Mmeweza kuukwepa mtego huu..!??

Aisee hongereni
 
Utangulizi

Political propaganda ni taaluma kama taaluma zingine. Inapofanyika kwa umakini huleta matokeo. Lakini inapofanyika unprofessionally kama nitakavyoonesha hapa, inamharibia kabisa anayefanyiwa propaganda hiyo iwe mtu au taasisi au chama cha siasa..

We huna ujualo zaidi ya kumtetea Mbowe. Vitu walivyoeleza jamaa kwenye space jana vinamake sense tofauti na hizi porojo unazoleta hapa.Mbowe ndio anatumiwa na TISS kufanya CCM itawale milele na ndio maana siasa zake ni nyepesi mno dhidi ya watawala. Tumeshuhudia spana konki za akina Mwabukusi kwenda kwa watawala lakini hakuna spana zozote za maana toka upinzani hasa Chadema then Leo unasema akina Mwabukusi wanatumiwa na TISS. Mbona 2015 hukusema TISS wanamtumia Lowasa kuvuruga Chadema?Au kwakua yalikua ni maamuzi ya Mbowe?
 
Napigilia Msumari !!!!
 
Utangulizi

Political propaganda ni taaluma kama taaluma zingine. Inapofanyika kwa umakini huleta matokeo. Lakini inapofanyika unprofessionally kama UWT wanavyofanya hapa kwa kuwatumia hawa wanaoitwa Sauti ya Watanzania kama nitakavyoonesha hapa, inamharibia kabisa badala kumjenga anayefanyiwa propaganda hiyo iwe mtu au taasisi au chama cha siasa..

Asikudanganye mtu. Amsha amsha ya mikutano ya kuelemisha wananchi chini OPERESHENI +255 KATIBA MPYA, OKOA
Huyo mpuuzi anayeongea kwenye hiyo clip hapo chini ni nani?
Kwa kifupi ukifuatilia hoja zao, walipoanza hadi wanayoyaongea sasa, unaona kabisa kuna dili limesukwa na sasa limebuma wametaharuki.
 
Shida ya Chadema wanaamini Mbowe na genge lake ni kundi la malaika. Yaani hawakosei na ni wasafi. Akitokea mtu akawachallenge wanaamini anatumiwa na CCM au TISS.Kweli kwa SIASA hizi za Mbowe na genge lake mtu haoni hawa jamaa wanatumiwa na watawala kuhakikisha wanabaki madarakani milele?Watu wako kwenye hali kubwa sana ya kupinga bandari badala wao waunge mkono,wanakuja na porojo za operation 255,watu wana hasira na CCM ye anakuja na Porojo za maridhiano.Hiki chama kama sio kutumika ni nini?
 
Utangulizi

Political propaganda ni taaluma kama taaluma zingine. Inapofanyika kwa umakini huleta matokeo. Lakini inapofanyika unprofessionally kama UWT wanavyofanya hapa kwa kuwatumia hawa wanaoitwa Sauti ya Watanzania kama nitakavyoonesha hapa, inamharibia kabisa badala kumjenga anayefanyiwa propaganda hiyo iwe mtu au taasisi au chama cha siasa..

Aisee hongereni
HINGERA MBOWE NA CHADEMA KUWASHTUKIA WAJINGA HAO SAUTI YA WANANCHI
 
Lakini CHADEMA si ndo walijipendekeza kwa kina mwabukusi hadi kushiriki lile kongamano la kidini pale Temeke na kuishia kutia doa chama? Huwa ninawashauri CHADEMA acheni kurukiarukia mambo mnakuwa wabishi. Angalia sasa mmeshatolewa kwenye reli kwa sasa mnapambana na Mwabukusi.
 
Shida ya Chadema wanaamini Mbowe na genge lake ni kundi la malaika. Yaani hawakosei na ni wasafi
Hapana. Si malaika. Binafsi nawaona ni binadamu kama wewe na mimi..

Lakini tumepewa akili wa kujua zuri na baya afanyalo mtu.

Kwenye hili, hebu onesha makosa ya CHADEMA kisha tuyajadili kwa hoja na kama ni kweli tutakubalina tu bila shaka..
Akitokea mtu akawachallenge wanaamini anatumiwa na CCM au TISS.
Hawa Sauti ya Watanzania wanawa challenge CHADEMA au wanataka kuwazima kabisa?
Kweli kwa SIASA hizi za Mbowe na genge lake mtu haoni hawa jamaa wanatumiwa na watawala kuhakikisha wanabaki madarakani milele?
Tunaona Kila kitu kinachofanywa na CHADEMA. Makosa ya Freeman Mbowe na CHADEMA kama chama Cha upinzani yako wapi? Onesha tujadili na tukubaliane ili tuwashauri
Watu wako kwenye hali kubwa sana ya kupinga bandari badala wao waunge mkono,wanakuja na porojo za operation 255,watu wana hasira na CCM ye anakuja na Porojo za maridhiano.Hiki chama kama sio kutumika ni nini?
Aisee.

Kama huoioni kazi ya upambanaji wa CHADEMA kwenye ishu ya bandari, katiba mpya na changamoto za nchi zilizosabanishwa na CCM basi wewe una matatizo yako, sio bure..!
 
Lakini CHADEMA si ndo walijipendekeza kwa kina mwabukusi hadi kushiriki lile kongamano la kidini pale Temeke na kuishia kutia doa chama? Huwa ninawashauri CHADEMA acheni kurukiarukia mambo mnakuwa wabishi. Angalia sasa mmeshatolewa kwenye reli kwa sasa mnapambana na Mwabukusi.
Wakati unaanza safari ulikosea.Sawa.Hata wakati wa kurudi unakosea njia?
 
Tu - assume ni hivyo. Wamegundua kosa na ku - retreat. Kuna ubaya hapo?
 
Mbowe na genge lake hawawezi kuungana na watu wenye nia ya kweli ya kuitoa CCM madarakani. Chadema hawahawa walikua busy kupambana na kundi la Hayati Magufuli. Hili ni kundi muhimu sana kwao na ni mtaji wa kisiasa kuitoa CCM madarakani ila wao walikua busy kulipiga vita. Sio bahati mbaya, Huu ni mkakati wa CCM kuhakikisha wanatugawa ili waendelee kututawala na moja ya masharti waliyopewa Chadema ni kuwa mbali na sukuma gang na aina yoyote ya watu wenye kutishia kuitoa CCM madarakani.

Now wako busy kupambana na sauti ya watanzania, sio bahati mbaya. Hii ni mikakati ya CCM wakiwatumia akina Mbowe na genge lake. Hizi operation wanazofanya akina Mbowe hazina madhara yoyote kwa CCM na ndio maana hawapigwi pin. Kila linapotokea jambo Zito kwa CCM basi Mbowe hutumika kuzima moto kwa akili nyingi sana. Mbowe ndiye aliyetumika kuzima operation UKUTA na ni Mbowe ametumika kuzima Vuguvugu la bandari kwa kuja na operation zake Uchwara. Niulize tu toka wameanza hizo operation mmesikia utawala ukitikisika hata nywele?
 
Hapana. Si malaika. Binafsi nawaona ni binadamu kama wewe na mimi..

Lakini tumepewa akili wa kujua zuri na baya afanyalo mtu.

Kwenye hili, hebu onesha makosa ya CHADEMA kisha tuyajadili kwa hoja na kama ni kweli tutakubalina tu bila shaka..

Hawa Sauti ya Watanzania wanawa challenge CHADEMA au wanataka kuwazima kabisa?

Tunaona Kila kitu kinachofanywa na CHADEMA. Makosa ya Freeman Mbowe na CHADEMA kama chama Cha upinzani yako wapi? Onesha tujadili na tukubaliane ili tuwashauri

Aisee.

Kama huoioni kazi ya upambanaji wa CHADEMA kwenye ishu ya bandari, katiba mpya na changamoto za nchi zilizosabanishwa na CCM basi wewe una matatizo yako, sio bure..!
Ebu niambie Chadema waliandamana kupinga bandari kuuzwa kama wale vijana?
 
Mbowe na genge lake hawawezi kuungana na watu wenye nia ya kweli ya kuitoa CCM madarakani. Chadema hawahawa walikua busy kupambana na kundi la Hayati Magufuli. Hili ni kundi muhimu sana kwao na ni mtaji wa kisiasa kuitoa CCM madarakani ila wao walikua busy kulipiga vita. Sio bahati mbaya, Huu ni mkakati wa CCM kuhakikisha wanatugawa ili waendelee kututawala na moja ya masharti waliyopewa Chadema ni kuwa mbali na sukuma gang na aina yoyote ya watu wenye kutishia kuitoa CCM madarakani. Now wako busy kupambana na sauti ya watanzania, sio bahati mbaya. Hii ni mikakati ya CCM wakiwatumia akina Mbowe na genge lake. Hizi operation wanazofanya akina Mbowe hazina madhara yoyote kwa CCM na ndio maana hawapigwi pin. Kila linapotokea jambo Zito kwa CCM basi Mbowe hutumika kuzima moto kwa akili nyingi sana. Mbowe ndiye aliyetumika kuzima operation UKUTA na ni Mbowe ametumika kuzima Vuguvugu la bandari kwa kuja na operation zake Uchwara. Niulize tu toka wameanza hizo operation mmesikia utawala ukitikisika hata nywele?
Kwani hii tabia ya kuchaguliana marafiki imeanza lini?Kama hao watu wapo vizuri wanataka kuungana (wapate back-up ya ubwete)na CHADEMA kwa nini?Waende hata kwa CUF au CHAUMA!
 
Wakati unaanza safari ulikosea.Sawa.Hata wakati wa kurudi unakosea njia?
Mkuu tuko mwishoni mwa 2023 badala ya kukijenga chama mnapambana na Mwabukusi huoni ni mtego mbaya mlioingia? Au mmesahau 2024 kuna uchaguzi? Shabaha ya kila chama cha siasa ni kushika dola sasa nyie CHADEMA mseme kama shabaha yenu ni nyingine.
 
We huna ujualo zaidi ya kumtetea Mbowe. Vitu walivyoeleza jamaa kwenye space jana vinamake sense tofauti na hizi porojo unazoleta hapa.Mbowe ndio anatumiwa na TISS kufanya CCM itawale milele na ndio maana siasa zake ni nyepesi mno dhidi ya watawala. Tumeshuhudia spana konki za akina Mwabukusi kwenda kwa watawala lakini hakuna spana zozote za maana toka upinzani hasa Chadema then Leo unasema akina Mwabukusi wanatumiwa na TISS. Mbona 2015 hukusema TISS wanamtumia Lowasa kuvuruga Chadema?Au kwakua yalikua ni maamuzi ya Mbowe?
Jamaa anajichanganya, Mbowe ni mnafiki na anapiga hela ya serikali vizuri sana kupitia kujipendekeza kwa Samia na viongozi wa CHADEMA top brass ukimuondoa Lissu wote wanawaza ubunge 2025 na wanaona wakimuuzi Samia watakosa kitumbua.

CCM ikibanwa kwenye kona, Mbowe utamuona anarudi nyuma badala ya kuchochea zaidi mapambano. Wale wakina Heche, Msigwa, Mnyika et al wanaogopa kupingana na Mbowe, simply wanajua watakosa mkate. Lissu peke yake ndiyo mara nyingine anapingana na misimamo ya Mbowe hasa kwenye maridhiano na CCM!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom