Pendekezo: Prof. Abdallah Safari awe Mwenyekiti CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pendekezo: Prof. Abdallah Safari awe Mwenyekiti CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by promi demana, Oct 9, 2012.

 1. p

  promi demana JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2012
  Joined: Oct 9, 2012
  Messages: 309
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari wakuu!

  Katika tafakuri zangu nimeona ni vyema Prof. Abdallah Safari agombee kiti cha uenyekiti CHADEMA ktk kuelekea 2015, kupitia fursa hii itawezesha chama ku-overcome propaganda chafu za udini ambazo zimekuwa zikienezwa na mpinzani wa CHADEMA (CCM), kwani hoja nyingi za CCM kuhusu udini zimekuwa ziki-base ktk kunyoshea kidole structure ya uongozi wa juu wa chama kwamba upo kiparokia zaidi.

  Pia tukubali tukatae ni kwamba CCM bado inanufaika sana na hii cheap propaganda ya udini na kama CHADEMA haitokubali kuneutralize structure ya uongozi CDM basi tujue kuwa out appearance ni 1 ya fact muhimu sana ktk siasa za nchi yetu.

  Kwa CHADEMA: Tusibakie tu na utetezi wa kila siku bali tunatakiwa pia tusiwe conservative kama CUF bali tuendane na hali halisi ya siasa za Tz japokuwa somehow itatucost but ni vyema kwa mustakabali wa chama na ukombozi wa taifa letu.

  CHADEMA NI CHAMA CHA KITAIFA

  Peoples power!
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mbona poa tu; kada yule!!!
   
 3. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hatuchagui viongozi ku-overcome Propaganda! After all unajua maana ya Propaganda? Maana yake ni Uongo, Fix, Uzandiki nk? Jenga vizuri hoja yako, tunaweza kukuunga mkono lakini kwa mtindo huu hatupo pamoja kamanda.

  TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),
  tumbiri@jamiiforums.com
   
 4. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Profesa Safari ni msomi! hana papara kama Mzito kabwela! ila ana haki ya kugombea.
   
 5. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Prof safari ni mtendaji zaidi si mwanasiasa wa kulishambulia jukwaa.CDM haiendeshwi kwa woga wa propaganda za ccm a,b,c etc.Prof agombee umakamu mwenyekt hafu 2015 agombee urais au umakamo
   
 6. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  mkuu Tumbiri nakuunga mkono 100% kwa statement yako.
   
 7. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  yaani mtu apewe uwenyekiti kwa sababu ni muislam, hapo sa si tayari tumemchagua mtu kwa sababu ya udini...udini utabaki kua pale pale...ur talkin nonsense
   
 8. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mkuu aliwezekani kabisa.
   
 9. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #9
  Oct 9, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  alishindwa hata na Lipumba huyo.... Sio kila mtu ana kaliba ya kuwa kiongozi, wengine wabaki kama strategists tu
   
 10. p

  promi demana JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2012
  Joined: Oct 9, 2012
  Messages: 309
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mkuu kama utakuwa umesoma angalau vitabu ya political science basi hutopata shida kujua my content,
  pia kama hyjui prof.Safari ni mtu mwenye uwezo mkubwa na kama bado unatailia mashaka haya basi nenda kamuulize kilichomkuta Lipumba pale ambapo prof.Safari alipotaka kugombea uonyekiti wa CUF that time.

  CHADEMA NI CHAMA CHA KITAIFA.
   
 11. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Promidemana kwani amekutuma? Kama unamuona anafaa sana anzisha chama chako umpe uenyekiti na kama huna chama basi muite awe mwenyekiti wa familia yenu. Mawazo mwengi ni mfu ingawa wanaoyatoa wako hai. We umeona Safari ndiyo muarobaini wa siasa? Mbona mwenyekiti wa Chama anachaguliwa na wanachama na si kutokana na upuuzi kama huu wako. Shame on you!
   
 12. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,199
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mbona hata mwenyekiti wetu Bob Makani (RIP) alikuwa muislam na wala haikuwa tatizo tusimfananishe prof safari na Yule sultan Lipumba
   
 13. p

  promi demana JF-Expert Member

  #13
  Oct 9, 2012
  Joined: Oct 9, 2012
  Messages: 309
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  uliza watu historia ya prof.safari na kisa kilichomkuta baada ya kugombea uenyekiti CUF.
   
 14. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #14
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Kutenda kwa kuogopa maneno ya watu ni tatizo kubwa katika utekelezaji wa maazimio. Anaweza akagombea na hata kuteuliwa ikiwa chama kitaona anafaa. Lakini kuteuliwa kwa vile yeye ni "Muislamu ili kuepuka propaganda mfu za thithimwewe" wala suala hili siwezi kuafikiana nalo kwa vile ni kinyume cha Good Management System!!!!!
   
 15. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #15
  Oct 9, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Nilishuliza.....
   
 16. p

  promi demana JF-Expert Member

  #16
  Oct 9, 2012
  Joined: Oct 9, 2012
  Messages: 309
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  bila historia mbele ni kiza- Malcom X stated.

  Elewa vizuri my content.
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Oct 9, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Naogopa kusema yaliyo moyoni mwangu lakini maadam mada hii imegusia uongozi wa Chadema basi sina budi kuchangia maana inatuhusu sote. Kwanza kabisa binafsi yangu sio swala la Uongozi wa chama kuwa sababu ya mwelekeo wa chama. Hizi Fikra za kugawana vyeo sawa baina ya Waislaam na Wakristu ndizo zinazotuponza sana nchini na ndizo zinazochochea Udini zaidi.

  Kinachotakiwa ni Chadema kama chama kuonyesha wazi sera zake ikiwa ni pamoja na mikakati ya kuondosha UDINI nchini. Na haitajalisha kiongozi ni Mbowe au Professoer Safari au Kamuhanda. Udini sio hesabu ya watu kila upande isipokuwa UDINI ni kitendo cha kuwadhalilisha, kuwagawa na hata kuwanyima haki ya kuabudu, kushiriki waumini wa dini nyingine. Chadema hakuna mtu anayebaguliwa na wala sidhani inatokea CCM au vyama vinginevyo.

  Hivyo maadam ndani ya chama watu wenye imani tofauti wanakaribishwa na wanapewa nafasi za kugombea uongozi hakuna sababu wala haja ya kuendeleza hizi habari za uuwiano..Kinachotokea ni kwamba vyama vya siasa vimeshindwa kusimamia haki za waumini wa Kiislaam iwe Chadema au CCM wote wanaogopa kugusa mabo ya kiimani isipokuwa kufuata mfumo uliopo japokuwa wanayaona mapungufu.

  Mabaya ya Uuwiano ndiyo yanatukuta ktk Muungano wetu na Zanzibar, hakuna jingine isipokuwa Wazanzibar wanatazama nafasi zao ktk uongozi wa juu nchini badala ya kupima serikali ya Muungano inawafanyia nini Wazinzibar. Kuna sheria na haki zipi ambazo wanazikosa kama Watanzania. Haya ya uuwiano ndiyo yamepeleka Wabunge wa viti maalum bungeni wakati wabunge hawa hawawakilishi maslahi ya wanawake nchini. Ni bora Jumuiya za Wanawake wapewe nafasi ya viti maalum bungeni badala ya jinsia zao kuwa kigezo cha uwakilishi. Bado tutakuwa tumefikia mwisho ule ule wa kuona wanawake wengi bungeni lakini at least hapa watakuwa wawakilisha wa hoja za wanawake nchini.

  tatizo liko wapi?...Kuna maswala muhimu sana ambayo waislaam wamekuwa wakiyazungumzia sana, lakini chama na wananchi hasa wanaChadema wamekuwa wapinzani wakubwa ktk maswala hayo. Na kinachowafanya Waislaam kuweka mashaka ktk uongozi wa Chadema ni pale hoja ya Waislaam kwa serikali ya CCM inapojibiwa na watu wa Chadema wakati hawakuulizwa wao. Chadema imekuwa mstari wa mbele kupinga Mahakama ya Kadhi, Kupinga OIC na hata kupinga madai kuhusu NECTA pasipo kufanya uchunguzi wa kina juu ya tuhuma hizi. sasa ikiwa hoja sio yao kwa nini wanaibebea mbeleko?.. hapa ndipo utata na hutuma zinapoanzia.

  Binafsi yangu nilitegemea sana kabla ya Chadema ama wanachama wake kujibu lolote wangeliacha swala hili liwe la CCM ama wafanye uchunguzi kujua kwa uhakika faida na athari za hoja hizi badala ya kutoa majibu ya dharau na kejeri yanayoichimba dini. Kwa kila hoja inayotolewa na kingozi yeyote wa dini imekuwa matusi kwa imani nzima ya kiislaam kutokana tu na propaganda za chuki dhidi ya Uislaam. Na kikubwa zaidi chuki hizi zimepandikizwa na nchi za Magharibi ambao malengo yao ni kuzitawala nchi za Kiarabu kiuchumi hivyo Uislaam umekuwa mwiba kwao na hivyo unapigwa vita imefkia kwamba leo hii wana Mapinduzi huitwa Magaidi..

  Kuna ukweli mkubwa sana ktk historia ya Uislaam kupingana na watu Kutawaliwa Kiuchumi. Na zipo hadithi nyingi zinazohalalisha vita kupigania haki yako hasa pale inapopokonywa na mgeni na kutokana na nadharia hiyo kulitokea hii kitu Revolution - Mapinduzi ambayo kwao wakoloni hawakutegemea kuwa Uzalendo na sifa ya Uraia isipokuwa huu ni Uislaam. Mahatma Gandhi aliusifia Uislaam na pengine hata kurudi India kupigania Uhuru wake ilitokana na imani hii ya kutotawaliwa..
   
 18. p

  promi demana JF-Expert Member

  #18
  Oct 9, 2012
  Joined: Oct 9, 2012
  Messages: 309
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sjasema ateuliwe bali nimesema agombee ili awe chairman.
   
 19. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #19
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,519
  Likes Received: 5,656
  Trophy Points: 280
  Lolote Chadema watakalofanya ili kuondoa propaganda za udini na ukanda itahalalisha kuwa Chadema kuna Udini na Ukanda! Hivi Chadema pamoja na hizo propaganda umaarufu unapungua au unazidi?
   
 20. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #20
  Oct 9, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,839
  Trophy Points: 280
  Si vyema kumchagua mtu kwa sababu ya dini yake ni vyema kumchagua mtu kwa kuwa anaweza kuchapa kazi na kukiendeleza chama.

  Sina tatizo na huwezo wa prof safari lakini kigezo cha kumpendekeza kwa sababu ya dini yake ni kukubaliana na propaganda za udini kutoka kwa sisimweli.
   
Loading...