Uwezo wa Mwenyekiti wa chipukizi wa CCM Taifa kujieleza ni mkubwa kuwashinda vijana wengi wa CHADEMA

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,280
9,719
Ndugu zangu Watanzania,

Kiukweli inafikirisha sana ,inatafakarisha sana unapomuona mtoto mdogo Qayllah Nurdin Bilal Mwenyekiti wa chipukizi wa CCM Taifa akijieleza vizuri kwa hoja ,ufasaha ,kujiamini na kwa utulivu mkubwa sana, halafu ukaja kuangalia namna vijana wengi wa CHADEMA wanavyo puyanga katika kujenga hoja na kupata shida katika kujieleza na kueleweka mbele za watu ,unabaki unasikitika sana moyoni kwa aina ya vijana waliopo ndani ya CHADEMA na namna wanavyoandaliwa kuwa viongozi wa hapo baadaye.

Embu angalia mtu kama Mdude Nyagali akiwa anaongea mbele ya camera.hivi unaweza kumuelewa anachoongea? Unaweza kutega sikio lako likapata na kuambulia chochote kutoka kwake?Unaweza kumlinganisha na huyu mtoto aliyeshinda uenyekiti wa chipukizi wa CCM Taifa? Je Mdude anaweza kuongea kwa utulivu na kujenga hoja kwa mtiririko mzuri kama yule mtoto? Mara ngapi mumeona mtu kama Mdude akiongea bila breki kama gari lililokatika usukani?

Embu angalia hata mwenyekiti wao wa Bavicha Taifa mwalimu Pambalu. Hivi anaweza kuongea kama yule mtoto wa chipukizi wa CCM? Anaweza kuongea kwa utulivu na kujiamini kama yule mtoto? Zaidi ya mihemuko na kupandisha sauti ni kipi kingine alicho nacho Pambalu kichwani mwake? Zaidi ya kuropoka na kuongea bila adabu na staha ni kipi unachoweza kusema Pambalu anakielewa na akazungumza kwa ushawishi mpaka kuwavuta vijana hapa Nchini wakamuunga mkono?

Kutokana na kukosa misingi mizuri ya kuandaa na kupika viongozi tangia wakiwa wadogo ndani ya CHADEMA ndio maana kwa sasa chama kimekosa mawazo mapya na mbadala ya kukipeleka mbele na katika mioyo ya watanzania.ndio maana chama kimegota kifikira, kimebaki kikidandia matukio na kubeba kama ndiyo ajenda za chama . kimekosa Dira na muelekeo unaoeleweka .ndio maana kimeendelea kuwa na viongozi wale wale,wenye mawazo mgando yale yale,sera zile zile,mitizamo ile ile na mbinu zile zile zisizo weza kukivusha chama wala kukipeleka popote pale wala kukipa ushindi wa aina yoyote ile katika mioyo ya watanzania.

Hii ndio sababu hata viongozi wake ni watu wasio na misimamo,ndio maana ni rahisi sana kuwayumbisha , ni rahisi sana kukikimbia chama chao.maana hawaelewi kwanini wapo CHADEMA? Wanapigania na kusimamia nini? Viongozi waliopo CHADEMA unakuta ni mkusanyiko wa wasaka tonge tu ,njaa tupu na wavizia fursa za ugombea wa ubunge na udiwani.hii ndio maana ndani ya chadema kuna ufuasi wa viongozi badala ya ufuasi wa sera,ajenda na itikadi ya chama.ndio maana hufanya kazi ya kuokoteza watu na kuwapa nafasi ya kugombea au uongozi ndani ya chama bila kujua wala kufahamu hata historia ya mhusika.ndio sababu mwisho wa siku huachwa kwenye mataa kama wajinga tu.

Ndio maana mpaka leo tangia 2004 Mbowe bado yupo kwenye kigoda chake.maana hakuna viongozi walioandaliwa,kwa kuwa chama hakina utaratibu wa kuandaa ,kulea na kukuza viongozi wake.ndio maana hata leo ukienda na kuhamia CHADEMA ukatukana sana viongozi wa CCM matusi ya kila aina kama kichaa au mwendawazimu basi kesho utaitwa kamanda uliyeiva na kupewa cheo kikubwa kabisa ndani ya chama na kushangiliwa sana na kupigiwa saluti za kichovu kama mtu aliyetoroka mafunzo ya mgambo.

Ukweli mchungu ni kuwa CCM itaendelea kuongoza Taifa hili la Tanzania bila kikomo ,itaongoza kwa kadri ya uhai wa Taifa letu,itaongoza maadamu tu Tanzania ipo basi na CCM nayo itaendelea kuwepo madarakani.hii ni kutokana na uwepo wa mfumo mzuri wa kuandaa viongozi wake wa leo,kesho na kesho kutwa. Hii ni kutokana na kuwaandaa na kuwafundisha uongozi wanachama wake tangia wakiwa wadogo,kwa kuwalea,kuwakuza na kuwafunda maadili na miiko ya uongozi na kukijuwa vyema chama chao na kuwa wazalendo kwa Taifa lao.

Waswahili wanasema Samaki mkunje angali mbichi.nyumba imara inabebwa na msingi ulio bora na imara,mti imara unategemea mizizi iliyo imara,.sasa CHADEMA haina hivyo vyote na haijajenga chama katika misingi hiyo.kimvuli kizuri cha mti kinategemea ubora wa majani ya mti husika.huwezi kupata kimvuli kizuri jangwani. CHADEMA ni jangwa katika kupata viongozi.

Sasa unaanzia wapi kuwapa nchi CHADEMA? Itabaki nchi kweli? Si watatugawa Watanzania? Si watatupeleka shimoni Watanzania? Si watatuangamiza Watanzania? Katu na kwame Watanzania hatuwezi kufanya jambo la kisaliti kwa Taifa letu hata siku moja. Hatuwezi kukabidhi Taifa letu kwa watu wasio na uchungu na maisha ya watanzania.ni CCM pekee yenye uwezo ya kuiongoza Tanzania na kuiletea maendeleo.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kiukweli inafikirisha sana ,inatafakarisha sana unapomuona mtoto mdogo Qayllah Nurdin Bilal Mwenyekiti wa chipukizi wa CCM Taifa akijieleza vizuri kwa hoja ,ufasaha ,kujiamini na kwa utulivu mkubwa sana, halafu ukaja kuangalia namna vijana

0742-676627.
Uwezo wa kujieleza mbona watu wanazidiana na hata huyo kuna wanaomzidi pia? Hii nayo kweli point inayohitaji mjadala. Kama darasani watu wanazidiana kwa nini kujieleza wasizidiane? Au ndiyo hiyo ya mwaka 2020 kwamba ni CCM tu wanajua kujaza fomu za kugombea na wagombea wa vyama vingine hawajui wakati tangu mwaka 1992 wamekuwa wakigombea?
 
Uwezo wa kujieleza mbona watu wanazidiana na hata huyo kuna wanaomzidi pia? Hii nayo kweli point inayohitaji mjadala. Kama darasani watu wanazidiana kwa nini kujieleza wasizidiane? Au ndiyo hiyo ya mwaka 2020 kwamba ni CCM tu wanajua kujaza fomu za kugombea na wagombea wa vyama vingine hawajui wakati tangu mwaka 1992 wamekuwa wakigombea?
Mchukue Mdude Nyagali na yule mtoto iwape nafasi ya kuzungumza uone namna Mdude atakavyopuyanga na kutukana matusi kama mwendawazimu au kichaa.
 
Wewe jamaa jitafakari sana.
Kuna mambo ambayo kupitia maandishi yako unatuchorea picha namna akili yako na ufahamu wako ulivyo.
Hivi ni sawa kumlinganisha MDUDE NA QAYLAH.
Mtoto anaweza akawa mzuri lakini kwa maneno yenu mnaweza mkamfanya asifike mbali.


Huna tofauti na yule anayeilinganisha google pixel na iphone kisa tu google pixel ina picha kali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom