Mkutano wa Freeman Mbowe M/Kiti - CHADEMA Taifa (Nyehunge - Buchosa Sengerema) na Tundu Lissu Makamu Mwenyekiti kule Chato inatoa ujumbe muhimu sana!

Uzima Tele

JF-Expert Member
Jan 20, 2023
1,101
2,344
Nimefuatilia kwenye Online TVs za YouTube mikutano ya CHADEMA leo J'tano ya kuimarisha chama chao waliyoipa jina la Operesheni +255 - Katiba mpya na Okoa bandari zetu..

Leo Freeman Mbowe, Mwenyekiti Taifa (CHADEMA) amehitimishia mikutano yake mji mdogo wa Nyehunge Jimbo la Buchosa Wilaya ya Sengerema. Makamu Mwenyekiti- CHADEMA Taifa, ndugu Tundu Lissu yeye kahitimishia mikutano yake jioni hii mjini Chato, Jimbo la Chato Wilaya ya Chato Kwa hayati Rais John P. Magufuli

Kilichonifanya niposti uzi huu ni kuelezea kwa ufupi juu ya ujumbe unaotumwa kwa viongozi wa serikali hii ovu chini ya CCM na umati wa watu/wananchi wanaojitokeza kwenda kuwasikiliza viongozi wa CHADEMA..

1. MOSI, watu hawa wanakuja wenyewe kwa hiari yao kwenye mikutano hii. Hili ni moja na la muhimu sana kuliko yote..

2. MBILI, tofauti na mikutano ya viongozi wa CCM ambayo huwa na misururu mirefu ya magari ya umma, wasanii waimbaji, fedha na sound systems za kufa mtu, CHADEMA ni kinyume chake kabisa. Ukiondoa msafara wa FM ambaye anatumia helkopita, Tundu Lissu yenye msafara wake hauzidi gari nne au tano, na maeneo mengine hata sound systems ni duni sana lakini wananchi hawajali kabisa hayo. Wao wanachotaka ni kusikia CHADEMA wana ujumbe gani wa matumaini ya kesho yao kwao..

3. TATU, ukiwatazama wananchi hawa wanapokuwa kwenye mikutano hii, wanakuwa watulivu sana wakisikiliza kwa makini hatua kwa hatua kinachosemwa na viongozi. Hili ni la muhimu zaidi kuliko yote maana umakini wa mtu katika kusikiliza huleta uelewa na ufahamu ndani yake. Na mtu akielewa, anakuwa amekomboka huyo..!!

4. NNE, Ujumbe ninaoupata mimi kupitia mikutano hii ni huu...

Kwamba, lipo jambo linatokota na linaweza kulipuka wakati wowote. Pia kuna kila dalili kuwa wananchi tumechochwa na namna CCM wanavyoindesha nchi hii na watu wako tayari kufanya lolote kwa njia yoyote kufanya mabadiliko ili mradi waambiwe nini cha kufanya nje kabisa ya utaratibu wa sanduku la kura kwa mtindo na mfumo wa chaguzi za sasa..

5. TANO na mwisho, nafurahishwa sana na uwezo na ufundi wa Freeman Mbowe na Tundu Lissu wa kujenga hoja na kuwasilisha ujumbe wao kwa watu..

Kwa kweli kwa hili, kiboko yao ni Tundu Lissu. Huyu jamaa ni maridadi sana ktk kuelezea jambo gumu kwa hadhira (audience) yoyote kwa lugha rahisi na ya kueleweka kwa kila mtu hata kwa wanakijiji..

Mfano leo kule Chato na jana kule Mbogwe, alieleza kwa ufasaha usiomithilika uhusiano wa mfumo mbovu wa kisheria na kiutawala (kikatiba) na matatizo ya ukosefu wa huduma bora za kijamii kama maji, elimu, barabara nk pamoja ubovu wa mikataba mbalimbali ambayo CCM inaingia na wageni ukiwemo wa bandari unaowapa waarabu wa Dubai bandari zetu zote kupitia kampuni yao ya DP World..

Baada ya hapo akahusianisha na umuhimu wa kuandika katiba mpya bora yenye CHECKS & BALANCES OF POWERS kwa taasisi zetu za kiserikali yaani executive, parliament & judiciary..

Alipomaliza kufundisha somo hilo, na ukiangalia sura na nyuso za wananchi waliokuwa wanasikiliza, unaona wazi na bila shaka kuwa, wananchi walielewa vyema somo lile..

People are already pushed on the walls. Bila shaka maombi yetu tukiongozwa na mtumishi wa Bwana Yesu Kristo, Mch. Mbarikiwa Mwakipesile yamesikika na kumfikia Mungu kwenye kiti chake cha enzi. Amina🙏🙏🙏🙏
 
ccm wamepotezana kila wakichungulia upande wapili mikutano imejaa nyomi bila kusombwa wala kupewa pesa, wakaingiza udini ikashindikana wakasingizia wanatukanwa matusi pia wamekwama,wakiulizwa yateje hayo matusi wanashindwa waendelee kupigwa spana kila sehemu watanyosha maelezo.
 
Ukweli nikwamba CHADEMA haijawahi kukosa watu kwenye mikutano ila Bado kichapo kipo pale pale sijui shida nini!sioni mantiki ya watu kwenda kusikiliza mipasho bila ya kuchukua hatua
Katiba mpya ni jambo muhimu sana hata kama chadema wasiposhika dola katiba mpya ikipatika itaongeza uwajibikaji wa viongozi wanaotuongoza

Kinachoendelea kwa sasa rais amefanywa Mungu mtu rais ameshikilia mihimili yote mitatu leo hii mahakama kuna kesi ya wanasheria wanaopinga mkataba wa bandari lakini mpaka sasa wengi wetu hatuna uhakika kama mahakama itatenda haki
 
JamiiForums442997317_236x211.jpg
 
Ukweli nikwamba CHADEMA haijawahi kukosa watu kwenye mikutano ila Bado kichapo kipo pale pale sijui shida nini!sioni mantiki ya watu kwenda kusikiliza mipasho bila ya kuchukua hatua
Shida iko kwenye mfumo wa uchaguzi kukipendelea chama kilicho madarakani..

Ndiyo maana nikasema, wananchi wamechoshwa na hali hiyo. Kwenye mikutano kama hii wananchi tunasikiliza kwa tafakuri ya makini just in case tunaweza kuambiwa njia mbadala ya kuwatoa watesi wetu hawa..

Na option wameshatupa wenyewe hawa watawala waovu na CCM yao na kina Tundu Lissu na CHADEMA wanachokifanya ni kuitengenezea mikakati na kuifafanua kwa wananchi...

Na kusema kweli somo linaeleweka vizuri sana...
 
Umeandika ukiwa umelewa pombe mpya inaitwa Antipas mbowe ,,
Absolutely, BIG✔️✔️✔️✔️

Jamaa ananikosha sana. Namwelewa na kama ni kulewa, basi ni kweli kabisa nalewa na maarifa na ufahamu anaouachilia kwetu..

Hata wewe najua unajua kuwa jamaa ni kichwa lakini umeamua kujifanya hamnazo tu..
 
Back
Top Bottom