Panya road katika matukio yao ni lazima wajeruhi kila mtu?

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,964
3,895
Kwanza kabisa lazima tukubaliane kimsingi kuwa panya road ni school drop out hasa shule ya msingi na secondary, lakini wengi pia ni wale waliolelewa Kwa style ya single mothers hii nimeongea sio kukejeli lakini ni kutokana na mahojiano waliyofanya wenzao kituo Cha polisi.

Jana Tarehe 11.02.23 siku ambayo Simba ilifungwa huko Ugenini, Panya road walifanya matukio ya uvamizi na uporaji katika maeneo ya Bunju B.

Mimi najiuliza kwanini Hawa vijana wamekuwa wakatili kiasi hiki, yaani wakifanya uvamizi lazima wakuchororonge mapanga hata kama utakuwa mtiifu na kuwapa wanachotaka tofauti na majizi mengine.

Wao wakikufikia wanaanza na panga Halafu ndo wanadai Hela , simu, etc, pia wakishindwa kuchukua kitu wanakiharibu either Kwa kukipiga nyundo au kukikatakata.

Pia katika video hii hapa chini utaona Bado kuna Watanzania wachache wanakaa na hela ndani , mfano mmoja kuna mtu kakutwa na laki sita ndani, sijui ilikuwa ya matumizi ya kawaida sijui.

Pia najiuliza Hawa vijana walitumia mbinu gani kuweza kujikusanya wengi vile na kuunda timu yaani genge la wahalifu, hiyo sio kazi ndogo, huyo Kiongozi wao ana upeo fulani wa kipekee. Tunaita team building skills

Kwa jicho la ki - intelijensia nyuma ya pazia kuna uwepo wa kiongozi mkubwa katika hili. Pasi shaka, IGP atakua anafahamu who's behind the whole continuable series!
Serikali/polisi wakitaka waweze kuwakamata au kuwadhibiti hawa panya road unabidi wawakamate hawa watu wote wanaojiita matembo kwenye vituo vya daladala/mitaani, hawa ndo wanawajua vizuri. Nasema hivi kwa sababu nishakaa nao mtaani vijana hawa, hawa wanaojiita matembo ndo wanajua kila kitu kuhusu panya road
 
Wacheni lugha za Ukimbari.

Panya Road ndio nini?

Mnalazimisha misamiati ya ukimbari tu, wakati hamna mbadala zaidi ya kudhihaki, kukejeli na kudumaza.

S type
 
Kwanza kabisa lazima tukubaliane kimsingi kuwa panya road ni school drop out hasa shule ya msingi na secondary, lakini wengi pia ni wale waliolelewa Kwa style ya single mothers hii nimeongea sio kukejeli lakini ni kutokana na mahojiano waliyofanya wenzao kituo Cha polisi.

Jana Tarehe 11.02.23 siku ambayo Simba ilifungwa huko Ugenini, Panya road walifanya matukio ya uvamizi na uporaji katika maeneo ya Bunju B.

Mimi najiuliza kwanini Hawa vijana wamekuwa wakatili kiasi hiki, yaani wakifanya uvamizi lazima wakuchororonge mapanga hata kama utakuwa mtiifu na kuwapa wanachotaka tofauti na majizi mengine.

Wao wakikufikia wanaanza na panga Halafu ndo wanadai Hela , simu, etc, pia wakishindwa kuchukua kitu wanakiharibu either Kwa kukipiga nyundo au kukikatakata.

Pia katika video hii hapa chini utaona Bado kuna Watanzania wachache wanakaa na hela ndani , mfano mmoja kuna mtu kakutwa na laki sita ndani, sijui ilikuwa ya matumizi ya kawaida sijui.

Pia najiuliza Hawa vijana walitumia mbinu gani kuweza kujikusanya wengi vile na kuunda timu yaani genge la wahalifu, hiyo sio kazi ndogo, huyo Kiongozi wao ana upeo fulani wa kipekee. Tunaita team building skills

Police jamii ni muhimu kwani huwezi kuwa na police kila Kona ya nchi yetu
 
Panya road Sina namna ya kuwaelezea...

Ila kuhusu kuweka pesa ndani Tena laki sita...wala si pesa nyingi za kushangaa why mtu kaweka ndani.

Hata hivyo umeuliza why watu wanaweka pesa ndani, mkuu jibu ni jepesi Kwa makato haya makubwa na maisha yalivyo magumu ni heri kuweka ndani....hiyo pesa itayotumika kukatwa unavyotoa kihela chako unaweza nunua hata fungu la dagaa watoto wale.

Na pia huenda ni mfanyabiashara ambaye lazima awe na kiasi fulani Cha pesa wakati wote Kwa dharura.
 
Madogo nishai hao walikutana na jamaa yangu wakamuuliza unataka pilau au bokoboko akachagua pilau .Walimkata kata .Boko boko unakula bapa za kutosha.
 
Serikali inatoza kodi kila mahali lakini kutoa ulinzi wa uhakika kwa Wananchi. Aibu sana.

Jukumu la kwanza kwa Serikali ni kutoa ulinzi kwa wananchi, kuhakikisha wananchi wapo salama. Kujitetea kwa kusema Polisi ni wachache nayo ni aibu nyingine.
 
Watumie akili na ubunifu kuondoa uhalifu kwenye jamii.

Waache kufanyakazi kwa kuonea watafanikiwa sana
Unataka kudai, 'Hawatumii' akili?
Unaweza kufafanua kijana wa uswazi akakuelewa?

hawana 'Ubunifu ?' Je una suggestions zozote?

Vilevile...

Nani anayeonea hapa? manake, Mada inasimama kuwa kuna wahalifu na wanaoonea watu mitaani, Polisi wamehusika vipi na bandiko lako?
Naomba kuelewa umefikia hapo vipi na Kudai waache kuonea....je wakiacha kuonea uhalifu utapungua?
Asante mku
 
Back
Top Bottom