Panya road ni hatari ila kauli za viongozi juu ya panya road ni hatari zaidi

P Didy Wa Tanzania

JF-Expert Member
May 6, 2022
2,376
3,891
Hivi karibuni kumekuwa na matukio mengi sana ya uhalifu yakihusiana na makundi ya vijana jiji Dar Es Salaam . makundi ayo maarufu kwa jina la PANYA ROAD .

Matukio yamezidi kuwa mengi na athari ya matukio hayo ya uhalifu yamepelekea mpaka wanajamii kupata ulemavu , kubakia na majeraha na wengine vifo kabisa.

Hivi sasa ukisikia jina la PANYA ROAD wanakuja nadhani ushaelewa unatakiwa ufanye nini ili kuokoa maisha yako ila kila mtu sasa hivi anaitegemea serikali kwa kushirikiana na jeshi la polisi kuondoa panya road. lakini kauli za viongozi kuhusu panya road zinatisha zaidi kuliko hata PANYA ROAD wenyewe nadhani

• Viongozi wameshindwa kujua chanzo cha tatizo ni nini 🤔🤔🤔

Mkubwa anaposema mdogo utekeleza

Lakini je tukisha wakamata vijana na kuwapeleka polisi ndio tutakuwa tushamaliza tatizo la panya road ?

JIBU NI HAPANA

Kukamata vijana tu ambao ni panya road sio dawa ya kuondoa uhalifu kwanza tunatakiwa kujiuliza

CHANZO CHA PANYA ROAD NI NINI ?

PANYA ROAD NI WAKINA NANI ?

WANATOKEA WAPI ?

NA WANATAKA NINI ?

Tukipata majibu ya ayo maswali manne basi tunaweza kulimaliza tatizo la PANYA ROAD

Kiupande wangu ukiniuliza chanzo cha panya road ni nini nitakujibu

• NI UKOSEFU WA ELIMU , UMASIKINI , MAKUNDI NA UPOROMOKAJI WA MAADILI

Lakini sio swala la ukosefu wa ajira kama wanavyosema watu wengi. kuwa panya road chanzo chao ni UKOSEFU WA AJIRA.

Kwa sababu ukitazama ao panya road ni vijana wadogo sana ambao umri wao ni kati ya miaka 10 hadi 17

Sasa unamuajiri vipi mtoto mwenye miaka chini ya 🔞 ni watoto ambao hawatakiwi kuajiriwa. Wakiajiriwa basi ni ajira za utotoni ambalo ni kosa pia.

Umri huu chini ya miaka 🔞 alitakiwa sasa hivi awepo shule anasoma lakini unakuta sasa hivi yupo mtaani anapora watu.

Njia ya kutatua tatizo la panya road ni


i. Vijana wapewe elimu ; hapa kwenye siala la elimu ni eneo pana kidogo lakini vijana wa makundi ya panya road wamekosa elimu kwanza ile ya SHULE na ELIMU YA KUJITAMBUA hii ambayo inapatikana nyumbani / Jamii. hawa vijana ambao wapo chini ya 🔞 na ambao hawana ajira lakini washaiitimu wapo mitaani tu wapewe elimu mbadala.

Maana hao vijana wote ni wale waliokosa kazi za kujiingizia vipato hivo wanaona Bora wapore.

ii. Kuondolewa kwa makundi na kutengeneza maadili kwa vijana;

Suala la mmomonyoko wa maadili ni pana sana .

Na ili ulielewe vizuri nilazima uangalie chanzo na chanzo ni WAZAZI NA JAMII

Wazazi siku hizi wazazi walio wengi wanawapenda sana watoto wao to the point wanapokosea hawataki kuwaadhibu kwa kuhofia watawaumiza.

Pia mzazi anakuwa mkali mwanae kuadhibiwa au kukalipiwa na mtu baki pale anapokea utafsiri kama anamuonea sana mwanae.

Lakini tukiachana na wazazi kuna upande wa pili walezi upande huu sasa ndo unakutana na jamii.

"Vijana ni wanafunzi wa wazee na vijana wanafaa kuwa watiifu ndio wapate elimu ya maadili kutoka kwa wazee."

Kwa upande mwingine na maisha tuliyonayo siku hizi vinywa vya wazee vimekuwa si daraja salama la kutangaza hekima na maadili kwa vijana wazee.

Siku ya siku tunatengeneza kizazi cha ovyo... hatua zichukuliwe mapema kuleta mabadiliko.




iii. Kutengeneza mazingira rafiki kwa mjasiliamali / machinga ;

Ukiachana na kundi la vijana chini ya 🔞. kuna kundi la vijana ambalo lipo juu ya miaka 18 na ili ndio tegemezi zaidi kwenye jamii. na kundi ili asilimia kubwa sana linategemea katika kujiajiri maana nafasi za kuajiliwa ni chache. na mitaji yao ni midogo sana wanachoweza kujiendeleza nacho ni kufanya biashara ndogo ndogo maarufu kama machinga

Sasa baada ya kuwaondoa barabarani nakupola vitu vyao wamekosa mwelekeo wamekosa muelekeo. hali ya maisha imekuwa ngumu wanawindwa huko mabarabarani wengine washapoteza biashara zao.

Kwa muda huu hasira zao wanazimalizia huku mitaani .

Tunaishauri serikali kutengeneza mazingira rafiki kwa machinga ili kupunguze idadi ya vijana wasiokuwa na kazi mitaani. hawa vijana ndio wanategemewa na familia zao.

Watengenezeeni mazingira nyie mutapata kodi kwa wingi ( Bidhaa zinauzika sana kwa mda mfupi) na wao watapata riziki zao za halali kwa utulivu kabisa.



iv. Ushirikiano baina ya jeshi la polisi na wananchi;

Ni ukweli uliowazi kabisa polisi hawana ushirikiano mzuri na jamii. wananchi anaweza kupeleka taarifa akawa mhanga mwenyewe au akanza kusumbuliwa na kuacha kazi zake na Wakati mwingine kamata kamata haifanyiki kwa weredi , kuna watu wataonewa pasina kushiriki au kujihusisha na ualifu huo.

Jamii pia : Panya Road wanafichwa na jamii ikiwemo wazazi wao.
Huwa mara baada ya kufanya matukio ya kiuba wanawapelekea wazazi wao hela.

Wazazi wengi wanaoishi na hao vijana hata hawahoji wanapataje pesa. Ili mradi wapokee tu,n a kuna mda wazazi au walezi huwasafirisha mbali watoto hao ili wasikamatwe na polisi. Baada siku kadhaa kupitia, wanarudi uraiani.

Muda ni sasa wa kufanya mabadiliko tusipochukua mabadiliko sasa baada ya mda mfupi hatari itakuwa kubwa mno inaweza kupelekea vifo vya watu wengi au visasi vya wenyewe kwa wenyewe ( mtu fulani alimuua ndugu yangu na mimi namuua na wengne niliyemuulia ndugu yake atakuja kuniua mimi na kuna ndugu yangu nae atakuja kumuua aliyeniua mimi).

Asanteni sana nawasilisha.
IMG_20220916_152216.jpg
 

Safi sana mkuu, uzi makini.

Sasa usubiri siku wakishavamia nyumbani kwako na mapanga na nondo ndio ukae nao chini uanze kuwapa elimu ya ujasiriamali na jinsi ya kuondokana na makundi.

Nondo ulizojaza kwenye huu uzi wako makini sana zitawafanya waweke mapanga yao chini na wakaanze kuchakarika na kufanya biashara.
 
Hawa panya road tusipoangalia watakua magaidi wakubwa sana kama boko harama,Alshabab,Al qaeda na Taliban
Nawashangaa sana watu wanaoleta tantalila za haki za binadamu na mambo ya huruma huruma kwa watu kama hao vijana.

Tumezoea majambazi wakivamia eneo, wakipewa pesa hawadhuru mtu,wanaiba na kuondoka ila hao vijana, hata ukitoa ushirikiano ni lazima watakukatakata hawajali wanakata wapi, hao wameshavuka hatua ya ubinadamu, ni wanyama na hata njia za kupambana nao inabidi ziwe hivyo pia.


 

Safi sana mkuu, uzi makini.

Sasa usubiri siku wakishavamia nyumbani kwako na mapanga na nondo ndio ukae nao chini uanze kuwapa elimu ya ujasiriamali na jinsi ya kuondokana na makundi.

Nondo ulizojaza kwenye huu uzi wako makini sana zitawafanya waweke mapanga yao chini na wakaanze kuchakarika na kufanya biashara.
boss tunatafuna mbinu ya kutoa tatizo au kuliendeleza tatizo
 
Nawashangaa sana watu wanaoleta tantalila za haki za binadamu na mambo ya huruma huruma kwa watu kama hao vijana.

Tumezoea majambazi wakivamia eneo, wakipewa pesa hawadhuru mtu,wanaiba na kuondoka ila hao vijana, hata ukitoa ushirikiano ni lazima watakukatakata hawajali wanakata wapi, hao wameshavuka hatua ya ubinadamu, ni wanyama na hata njia za kupambana nao inabidi ziwe hivyo pia.


haina haja ya kushangaa ili tatizo lipo kwenye nyumba zetu.... now mpaka wasiohusika wanakamtwa mitaani.
 
boss tunatafuna mbinu ya kutoa tatizo au kuliendeleza tatizo
Mbinu zako ni sahihi,lakini sio sahihi kwa wakati huu mkuu.
Tunatakiwa kwanza kupambana nao hawa waliokwisha haribika, hawa ambao wanaona wanaweza kuishi kwa kuvamia,kupora na hata kuua watu wasio na hatia, na njia za kupambana nao hao haziwezi kuwa hizo ulizotaja.
 
Uovu uko kokote hata Kwenye kwenye Neema vibaka na maharamia wapo

Hawa madogo washikishwe Adabu kama walivyoshikishwa wale wa kibiti

Msisingizie ajira vijana wangapi hawana ajira Lakin sio panya road Hawa wasichekewe hata kidogo huko wanakoenda Kufanya Fujo uswahilini wao wenyewe Wana Maisha magumu kama wao bado wanawapiga mapanga juzi wameua mwanafunzi yeye anafanya kazi hazina yule???

PANYA ROAD WAULIWE TUUUU
 
Uovu uko kokote hata Kwenye kwenye Neema vibaka na maharamia wapo

Hawa madogo washikishwe Adabu kama walivyoshikishwa wale wa kibiti

Msisingizie ajira vijana wangapi hawana ajira Lakin sio panya road Hawa wasichekewe hata kidogo huko wanakoenda Kufanya Fujo uswahilini wao wenyewe Wana Maisha magumu kama wao bado wanawapiga mapanga juzi wameua mwanafunzi yeye anafanya kazi hazina yule???

PANYA ROAD WAULIWE TUUUU
kwahiy mkuu kuua ndo solution
 
Back
Top Bottom