Ulinzi shirikishi pia ni chanzo cha kuongezeka kama matukio ya wizi “panya road”

Tajiri Kichwa

JF-Expert Member
Apr 2, 2017
9,019
21,909
Ulinzi shirikishi naweza sema ni moja ya chanzo cha panya road. Wengi wanakua watu waliojikatia tamaa na maisha, wahuni wahuni wanalipwa ujira kuzurura usiku. Hii ni fursa kwao wanachora ramani ya mtaa kwa ajili ya matukio kupitia wenzao.

Ulinzi shirikishi ni chanzo maana mtu unaweza kutana na kundi la vijana usiku ukahisi ni ulinzi shirikishi kumbe ndio hao hao vijana wako kwa kipindi chao cha kufanya tukio mtaa huo. Maana ulinzi shiriki wengi wao wanatembea kama kikundi na silaha za jadi.

Kama umewai kutana usiku na ulinzi shirikishi unaweza kuwa shahidi jinsi wanavyotisha na kuogopesha na wengi wao wametanguliza pesa, na kujeruhi mbele.

Suluhu ya ili jambo moja ni tuanze kwa kuzuia ulinzi shiriki. Popote mtu atakapo onekana na silaha usiku huyo ni mwalifu yuko kufanya matukio.

Polisi waongeze doria hasa maeneo yenye muuingiliano mkubwa wa watu. Watumie piki piki sehemu gari zisipo fika. Ikiwezekana wapandikize mamluki wao wapange kwenye mitaa mbali mbali kama wakazi ili wasaidie kutoa taarifa.

Nayeyuka
 
Ni ngumu sana kuwagundua wahalifu waliovaa kiraia kama hujawakuta kwenye tukio.

Tunahitaji utafiti mkubwa sana kwa kuwashirikisha mabalozi na wenyeviti wa serikali za mitaa. Hawa ndio wanawajua vijana kutoka ngazi ya chini kabisa ya uongozi.

Naamini uhalifu mdogo mdogo huu utamalizwa kwa njia hii.
 
Hili lina ukweli mkuu, hao vijana wenyewe wanaopewa majukumu ya kulinda mitaani kwa kuchangiwa kama ulinzi shirikishi sidhani kama uadilifu wao unaeleweka. Ni bora zitafutwe njia za kufaa zaidi kuimarisha ulinzi maeneo ya makazi ya watu kuliko kuwatumia vijana ambao hawaeleweki hata uadilifu wao kuwa walinzi wa mitaa.​
 
Back
Top Bottom