Panya Road - Mtanzania wa hali ya chini ni mhanga mkubwa!

Tengeneza Njia

Senior Member
Jul 29, 2022
121
204
Ndugu zangu,

Baada la tukio la mauaji ya mwanafunzi kawe, nimeona leo nililete hili!

Ukiangalia matukio haya ya Panya Road sehemu ambazo huwa zinatajwa kuathirika mara kwa mara ni maeneo ambayo sisi kitanzania tunaita "uswahilini".

Huku uswahilini ndipo wanaishi wananchi wa hali za chini sana kiuchumi, gharama za maisha ni bei nafuu sana (bei zao za kodi ni cheee, chakula mama ntilie etc.) kiufupi ni jamii fulani hivi.

Kwa ambao wameshawahi kuingia vichochoro hivi vya huku kawe (mtakuwa mashahidi namna maisha huku yalivyo). Sishangai kama katika maeneo kama haya bado kuna wezi wanaoiba nguo - kwenye kamba, wanachana nyavu za madirisha kuiba simu na matukio mengine kama haya.

Kuna uhakika kabisa vijana hawa wa panya road wanaendelea kuvamia maeneo kama haya kwa sababu ya urahisi unaotokana na miundo mbinu mibovu (hakuna ulinzi, milango yao ni ya kawaida tu, nyumba sio zenye uzio, electric fence, mageti kama ilivyo kwa maeneo mengine wanayoishi watu wenye maisha mazuri).

Ni wakati sasa kuliangalia suala hili la panya road kwa sura nyingine - UMASIKINI NA HALI DUNI YA MAISHA, ni kati ya chanzo kinachofanya tatizo hili kuwa endelevu!

Hawa hawa wanaopata matatizo haya, kesho wanakuwa mstari wa mbele kupewa kanga na matishirt kupiga kura na kupewa ahadi upepo, bila kuangalia aina ya kiongozi wanomchagua.
 
Si sababu wana silaha za jadi. We ukamvamie tajiri getini na security mwenye silaha,na tajiri mwenyewe ndani ana bastola, huku wewe umeshika panga na rungu.

Hapo ndo levo zao. Hata hivyo hata matajiri pia wako hatarini sana na wanaishi kwa hofu ya kuvamiwa na majambazi makubwa yenye silaha za moto.na hayo majambazi hayawezi mvamia mtu wa hali ya chini maana sio level zao.

Kila mtu ana janga lake. Hakuna alie salama!
 
Nakumbuka miaka yetu kijijini inapigwa yowe moja vijana wote tunatoka kuwatafuta wezi au wavamizi wa kijiji usiku ule ule.

Mjini wanaogopa nini?
 
Back
Top Bottom