SoC03 Mpango wa miaka 5 ya kurekebisha vijana - Panya Road

Stories of Change - 2023 Competition

FIKRA NASAHA

Member
May 22, 2023
8
8
EXTENSIVE 5 YEARS-SW.jpg

An Extensive 5 Year Reforms Program for the Youth - Panya Road
  • Hata Wafungwa Wanaweza Kufaidika Kwenye Programu Hii.
  • Tuwatumie Panya Road, Kuimarisha Uchumi kwa Kutoa Mafunzo ya Uzalishaji, Ufundi na Kazi za Amali, Mila, Utamaduni na Uzalendo.
Haya Matukio ya Panya Road, yananikumbusha tukio moja lililotokea miaka mingi nyuma, zaidi ya miaka 40 hivi. Nakumbuka kushuhudia jamaa tukiishi naye mtaa mmoja, akikimbizwa na umati watu, wakimtuhumu kukwapua saa ya jamaa mmoja, huku wakipigia kelele za mwizi.

Yule kijana alitupita mbio tukiwa tumekaa maskani, tukizogoa na kuingia kwenye moja ya nyumba za pale mtaani, waliokuwa wakimfukuza walifika pale, wakitweta.

Kuna waliokuwa na mawe na vipande vya tofali na silaha nyingine. Vijana wote tulioko pale tunajua kuwa yule kijana alikuwa ni mwizi na miaka ile kulikuwa na vikundi vya vijana wahalifu wakisumbua sana watu kwa tabia zao za kukwapua kwapua watu na yeye alikuwa ni mmoja wao.

Kidogo niwaambia wale watu, mwizi wao kaingia kwenye moja ya zile nyumba pale mtaani. Lakini akili ikagoma, si kwa kumuogopa, ila huruma tu ilinijia nikaa kimya sawia na wale wenzangu. Binafsi sipendi waizi na pia sipendi kuona watu wakiibiwa na hata vile wakiadhibiwa kwa kupigwa mawe au kuchomwa moto si sawa yao.

Baada ya miaka isiyopungu ishrini, nilikuja kukutana na yule jamaa, mkoani Kigoma, keshakuwa mtu mzima, mwenye familia yake na uzuri zaidi ni mfanyabiashara mkubwa tu, akimiliki duka la spea za magari na boti za uvuvi.

Alinikumbuka nami nikamkumbuka, akanikaribisha nyumbani kwake, tukaongea mengi, akanambia kuwa hasingeweza kutusahau kwa sababu tuliokoa maisha yake, na tangia siku ile aliyokimbizwa ilikuwa kama ndio dawa, maana aliacha wizi, akajishughulisha na biashara na sasa anajitegemea na ana familia ya watoto wanne.

Lengo hapa si kuwahadithia tukio la kibaka mmoja aliyepata bahati ya kuokolewa miongo kadhaa nyuma, lahasha! Ila nimekuwa najiuliza hivi awa vijana tunao waita vibaka au Panya Road, ni kweli hatuna suluhisho la kudumu dhidi ya vitendo vyao vya kiuarifu?

Maana wengi wao ni vijana walio kati ya umri wa miaka 12, 20 mpaka 30 tu hivi.

MPANGO WA KUWAWEZESHA PANYA ROAD

Binafsi natamani badala ya serikali kuwafunga jela, kuwe na mipango maalum ya kuwarejesha Panya Road kutoka kwenye maisha ya uharifu wa kudhuru watu, uraibu wa dawa za kulevya na wizi na kuwageuza kuelekea kwenye maisha ya kawaida kupitia mafunzo maalum.

Kuwafundisha Panya Road kulihudumia Taifa lao na kuwatumia vijana hao katika kuwapatia mafunzo ya msingi ya stadi za maisha na kujiendeleza katika shughuli za kilimo, viwanda, uvuvi, ufundi na kazi za amali. Kuwafunza elimu ya uraia, kuwafunza na kushiriki katika shughuli za maendeleo ya kijamii na utamaduni.

Mpango huu uwe wa miaka mitano (5), huu mpango utaratibu, kusimamia na kuendesha mafunzo endelevu hivyo basi kupitia mpango huu vijana hawa watajengeka kiuzalendo, wataweza kujitegemea na kujiamini.

Nakumbuka miaka ile kuanzia 1964 mpaka katikati ya miaka ya 70, serikali ya Tanzania ilikuwa mikakati ya kuwapeleka watu kwenye vijiji vya ujamaa.

Najua kuwa kulikuwa na matatizo ya kiutendaji, ndio maana jambo lile halikufanikiwa kama lilivyotarajiwa, lakini tunaweza kuchukua lile wazo kisha tukawashirikisha wasomi na wanaharakati wakalikarabati na kuliwasilisha tena, kisasa zaidi.

Kama vile serikali ilivyoanzisha JKT na baadae JKU kuwa ni vyombo vya kuelimisha na kuandaa vijana wa Kitanzania kiuzalendo, kimaadili, kinidhamu na kuwafanya raia wema wanaopenda kutumikia na kulinda nchi yao. Basi kwa nia ileile na uthubutu uleule, tunaweza kuanzisha "MPANGO KINA WA MIAKA 5 YA KUREKEBISHA VIJANA - PANYA ROAD" (AN EXTENSIVE 5 YEAR REFORMS PROGRAM FOR THE YOUTH - PANYA ROAD), kiufupi MKKV-Panya Road

WIZARA ZA SERIKALI ZITOE WATAALAMU.

Mpango huu wa miaka mitano, MKKV-Panya Road, unaweza kusimamiwa na wizara kadhaa, wakiongozwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo n.k.

Kwenye hizo kambi za kudumu, vijana wapewe mafuzo ya Stadi za Maisha ya kujitegemea kinadharia na kivitendo, Kusoma, Kuandika, Kuhesabu na utoaji wa elimu ya Msingi na Sekondari kwa ujumla wake.

Programu hii ya MKKV-Panya Road, pia ijumlishe kuwaandaa awa vijana Kisaikolojia, Kuwapatia Elimu za Mafunzo ya Kilimo, Viwanda, Uvuvi, Mapishi, Elimu ya Uraia na Uzalendo, Ufugaji, Ujenzi, Ufundi wa aina mbalimbali kama vile Uashi, Useremala na Ukarabati wa magari, Elimu za Dini, Utamaduni na Michezo.

Vilevile kuwepo wataalamu wa saikolojia na ushauri nasaha watakao weza kuwashauri na kuwasaidia awa vijana katika masuala ambayo yamewafanya wawe na tabia mbaya, ili kuwasaidia kuepukana na kurejea tena kwenye maisha ya uhalifu. Na kuwabadirisha kuwa raia wema, wanaojiamini, wanaojituma, wenye uzalendo na kuipenda nchi yao.

Kwa kushiriki katika programu hii ya MKKV-Panya Road, vijana watapata fursa ya kupata ujuzi unaohitajika katika maisha yao na kuwa na ujasiri na ushindani kwa taaluma yao baada ya kuhitimu.

Mbali na ujuzi wa kujifunza ili kuwa na nguvu kitaaluma, vijana watajengeka kiuwezo na kujiamini na kuweza kuanzisha miradi yao wenyewe.

Vilevile itasaidia kuwabadirisha na kuwa raia wema, wanaojiamini, wanaojituma, wenye uzalendo na kuipenda nchi yao.

NB:

Kama kutakuwa na kesi za mauwaji kwenye uhalifu wa hao vijana, basi Sheria ichukuwe mkondo wake. Hili wazo ni kwa wale tu ambao hawana kesi za mauwaji.
 
View attachment 2640227

We hujawakuta kazini wewe!
 
We hujawakuta kazini wewe!
Nimeishi maeneo yenye wahuni, tangia wakiitwa majina tofauti kabla ya kuitwa Panya road... Kabla ya hapo wapo waliojiita "MBWA MWITU, MWENDO WA NEEMA, MASACCARA, UKITAKA UBAYA DAI CHAKO n.k."

Panya road, ni marejeo ya vikundi ambavyo vilikuwepo zamani kisha vikapotea na kuibuka vingine, nakumbuka zamani jijini Dar es Salaam, kulikuwa na vikundi kama vile Kiboko Msheli, Komando Yosso, Seven Komando, Rola Bugi, Akayesu, Nakozi Camp, Begi Bovu, Red Sonja, Siafu Family, Watoto wa Shetani, na vingine vingi tu, visivyo na majina.

Yaani ilikuwa kiza kikiingia tu kuna baadhi ya maeneo watu hawapiti kabisa na wengine inabidi kuchelewesha sala ya Asubuhi au hata kuwahi kazini kwa wale wanaofanyakazi za shifti za kuingia alfajiri kwa kuhofia vijana hawa.

Sasa wewe ukiwa kama mkaazi wa mtaani kwako au mtaa wa nduguyo au rafiki yako amekuomba kutoa suluhisho la kudumu katika suala hili, wewe kama wewe ushauri wako nini ili kufanikisha suwala la amani ya kudumu inapatikana katika jamii zetu.
Nina uhakika tukitulia na kutuliza bongo zetu, tutapata suluhisho nzuri kabisa na la kudumu.

Karibu katika mjadala.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom