Panapofuka moshi panaficha moto...

Panapofuka moshi panaficha moto...

Pasipo na moto hapana moshi.

Je, kuna moto unawaka chini kwa chini Tanzania? Maana moshi kila sehemu.

Cha kujiuliza ni kutafakari, huu moshi unaofuka kila sehemu ni wa mazingaombwe tu na hakuna moto au kuna moto kweli uliowaka au uliowashwa lakini zimamoto yetu haiuoni au tunaoamini kuwa ndiyo zimamoto wetu shupavu wao ndiyo wapepeaji wa huo moto?

Moto upi? Unawaka wapi? Utamuunguza nani na nini? Unaweza kuzimika? Au tunaweza kuuzima wenyewe? Au tunahitaji msaada wa kuuzima huu moto?

Wewe unauona huo moshi? Au tayari unauona moto?

Mbona sijaona moshi Tanzania, ila jana ndio niliona moshi + moto, na mlipuko mkubwa Nairobi, ktk hotel ya kifahari ya Dusit, inasemekana Al Shabab wanahusika...
 
Bibi kweli umezeeka ,huu moshi mbona wenzio tulianza kuusikia harufu yake tangu Novemba 5/2015 na sasa moshi umeongezeka.Jambo la ajabu hapo ni kwamba huu moto uanafukuta kwa miaka 3 sasa ni moto wa aiana gani!Pole sana bibi naona machozi ya kutoka kwa huu moshi
Kipindi sisi tunauona huu Moshi kwa mara ya kwanza yeye alikuwa kafunikwa na blanket la chama badala la Utaifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona sijaona moshi Tanzania, ila jana ndio niliona moshi + moto, na mlipuko mkubwa Nairobi, ktk hotel ya kifahari ya Dusit, inasemekana Al Shabab wanahusika...
Ya Kenya haifuki ni miripuko na huko moto haujajificha. Wapo vitani na Wasomali. Kazi kwao.

Kwetu hapa ndiyo kuna moshi lakini moto umejificha.
 
La CAG niliona moto uliwashwa siku aliyoteuliwa Ndalichako kuwa waziri wa elimu. Mtu ambae Waislam walimkataa kwa maandamano alipowadhulumu alipokuwa mkubwa wa mitihani.
Katika hili wanaendelea na msimamo wao. Zaidi, na inasikitisha, yeye anaendelea kwa baraka zote
 
Daahh Taratibu Pro CCM wameshaanza kupoteza muelekeo wa imani yao waliyokuwaga nayo kwa bwana banza stone ....

Angalau sasa mmeweza kubaini kwamba mlikuwa mnamshauri mtu mwenye sifa ya kuwa kama jiwe " (JIWE NI KIUMBE KISICHO HAI),Hivyo basi halifikirii halitendei " halijisogezi kutoka sehemu moja kwenda nyingine ukiona limesogea basi ujue kuna mtu/kitu kilichopelekea uwezekano wakulifikisha hapo " wala haliwezi kuwa na shauku ya kupenda maendeleo"

Sifa nyingine ya jiwe huwa linatumika kama zana ya kivita ama siraha pindi binaadamu anapokuwa ana pigana na binaadamu mwingine ....

So bado mlikuwa mnategemea kiumbe chenye hizi sifa kiweze kuwaletea mabadiliko" thubutu " hii tutakuwa sawa kama tukisema kuwa na nyinyi UBONGO wenu ulichacha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Teh teh teh huyo mtu ni Raia wa kawaida au kiongozi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Siku hizi hata anayekaa kwa shemeji yake Masaki atajifanya hazijui shida walizonazo walio wengi. Kwani hata huu wimbo wa 'mjiajiri, mjiajiri' unapoimbwa kwenye majukwaa na wanasiasa, waitikia pambio unadhani wao wamejiajiri...la hasha! Wameajiriwa kwa msaada wa shemeji na sasa wamevimbiwa kiasi hata aliyesomea uhakimu wanamuita mzembe hajajiajiri
 
Pasipo na moto hapana moshi.

Je, kuna moto unawaka chini kwa chini Tanzania? Maana moshi kila sehemu.

Cha kujiuliza ni kutafakari, huu moshi unaofuka kila sehemu ni wa mazingaombwe tu na hakuna moto au kuna moto kweli uliowaka au uliowashwa lakini zimamoto yetu haiuoni au tunaoamini kuwa ndiyo zimamoto wetu shupavu wao ndiyo wapepeaji wa huo moto?

Moto upi? Unawaka wapi? Utamuunguza nani na nini? Unaweza kuzimika? Au tunaweza kuuzima wenyewe? Au tunahitaji msaada wa kuuzima huu moto?

Wewe unauona huo moshi? Au tayari unauona moto?
Kuna chombo ni zaif!
 
Back
Top Bottom