Orodha ya Watumishi wenye vyeti vya Kughushi...

Orodha ya Watumishi wenye vyeti vya Kughushi...

Kweli tuna watu wenye Vyeti feki wapo wengi nakupongeza kuwatoa kwenye utumishi wa umma ila moyo wangu Bado una wasiwasi mkubwa juu ya kuwatumbua wenye Vyeti Feki kwa sababu kuu moja mwaka Jana mliajiri vijana 300 kanda ya mahakama na kuwasainisha mikataba na kuwapa posho za kujikimu walifanya kazi mwezi mmoja na baadae mliwasimamisha kazi kwa mda usiojulikana Leo hii wapo nyumbani hawajui hatima yao serikali ipo Kimya.

Wasiwasi wangu zoezi la kufukuza kazi jana limewakumba hata wenye Vyeti original ninaamini Kama mliwasimamisha kazi Hawa bila utaratibu mnashindwaje? Kuwaonea wengine kwa maslahi binafsi?? Naamini kuna watu wameonewa wengi tu
Mmh [emoji12]
 
Asilimia 99% ya majina ni wakike duuh
Kuna mtumishi mwenzangu ni nesi jina lake limo ila ni kwa ujinga wake tu, story ipo hivi:
Aliolewa na njemba mmoja muhaya, tabia za wahaya jina la bwana lazima liwe la pili( kama la mzazi) kwahiyo vyeti vya sekondari vinaonyesha mf: Hidaya Makwaya Majige na huku kwenye pay slip ameandika Hidaya Kabyemela Mutungi, ili kudumisha mila ( kuna kipindi sikumbuki ni lini ulitoka mwongozo serikalini wa watu wanaotaka kubadiri majina yao ya utumishi.....nadhani hapo ndio walimu na manesi wengi wa kike walipobadirisha majina ya baba na kuweka ya waume zao! Nina imani hawa watu watarudi kazini tu!
 
Mbona waligunduliwa wengi kabla lakin jamaa wakaona kuwafukuza jeshi waliokwisha pata mafunzo na wapo kazin kitambo nchi itayumba wamewaacha tu wapige kaz
Basi asijiite mtu wa Mungu labda wa mungu, hakuna Mungu anayependelea.
 
Tanzania kila kitu ni feki inawezekana hata list hii ya vyeti feki nayo ni feki.
Kule jimbo la hai wananchi wameomba msamaha feki kwa magufuli Nchi hii kuna vioja hakuna mfano Duniani.
 
NImeona jina la dada mmoja alikuwa Nesi kituo cha Afya MELELA,kipo MVOMERO,alikuwa muuguzi mzuri sana,alifanya kazi yake kwa moyo kiasi kwamba wananchi wengi walimpenda sana,ila ndo hivyo tena kumbe alikuwa na cheti feki,Daah,pole sana dada BELADONA!!!!
 
Ila bado hawajamaliza kuna nurse yuko hospitair ya rufaa mbeya cheti sio chake na mwingine ni mwalimu tukuyu mbeya namjua cheti sio chake lakin hawapo kwenye orodha inamaana bado kuna watu wameachwa
Waliokaguliwa na mtambo ni wale wenye vyeti ambavyo havikutolewa na baraza , vyeti vilivyonunuliwa mitaani tu. Hao unaosema ni vyeti halali vilivyotolewa na baraza yaani mmoja anakaa na copy na mwingine anakaa na original . original kinahama tu kutegemeana uhitaji wa mhusika. Hao pia ni wengi sana hawajaguswa na dhahama hii. na ili kuwapata inabidi uhakiki ufanyike kwa pamoja sehemu zote vinginevyo mtu akakuchomee.
 
Salaam.

Naipongeza serikali kwa juhudu kubwa na bila kumwonea mtu haya sakata la vyeti fake. Hilo Mh Rais ameonesha dhamira ya dhati kabisa.

List nimeikagua mwanzo mwisho, sijafanikiwa kuona jina la mtu yeyote ninayemfahamu.

Lingine, sijaelewa baadhi ya waajiri au vituo vya kazi kuhusiana na hao watumishi hewa. Kuna mahali nimekuta tu MANZESE, UTAALAM, MAKAO MAKUU nk. Sikuelewa vzr,au labda typing error.

Mwenzangu umeona mtu unayemfahamu kwenye hiyo list? Dsm imeonekana kuwa na fake wengi sana.

View attachment 502849View attachment 502850View attachment 502851View attachment 502852View attachment 502853View attachment 502854View attachment 502855View attachment 502856View attachment 502857
Namfahamu D.A BASHITE dah afadhali sijamwona, hayumo ktk listi,yaani ingeniuma sana kama angekwepo ktk hii listi,kwa kweli niseme uhakiki umezingatia vigezo vyote
 
Back
Top Bottom