Nzega: Risasi zatumika kumuokoa Mbunge Kigwangalla

Wana Jf nipo nzega nikitoka Mwanza katika ziara ya Ndg ridhwani kikwete.

Usikuu huu nikiwa napata chakula nikasikia Risasi zinalia Mjini nikaamua kufatilia na kupata taarifa kuwa Kuna Mgodi ambao unaitwa Isunga Ngwanda ambao siku Mbili zilizopita Mbunge na Wananchi waliungana Kuufunga.

Leo Kilicholeta Vurugu ni Pale Mbunge wa Nzega alipoenda kuwafata wananchi alioshirikiana nao kuufunga Mgodi na kuwataka kuufungua mgodi na yeye akijiunga na Polisi kuwataka wananchi wale waondoke wamuachie muwekazaji.

Wananchi walipandwa na Hasira na kumvamia mbunge na Kuanza kumpiga na Kuvunja Gari ya Daktari wa Wilaya ambayo aliazima naambiwa akiwa nzega huazima gari ya Daktari wa wilaya na kuitumia.

Wananchi hao wenye hasira waliamua kumpiga mbunge kwa kitendo chake cha kuwasaliti wananchi hao na leo kuungana na polisi na wawekezaji.Polisi ilibidi kutumia silaha za moto kumuokoa na na kuwakamata baadhi ya watu na kuwepeleka polisi jambo lilifanya wananchi kuandamana kwenda kuvamia kituo cha Polisi na matokeo yake Polisi kutumia Risasi kuwatawanya wananchi wao.

Liliwaudhi wananchi nitukio la Mbunge Kigwangala kuwageuka wananchi na kujiunga na wawekezaji na Polisi hivi sasa kunavurugu nzega mjini na Maeneo ya Isunga ktk Mgodi huo.

hyo gari ni ya kwake sema inafanana na ya daktari wa wilaya!
 
Mikoba ya sheikh yahya alikurithisha? Nakumbuka hiyo comment yako juu ya hili.u shld open a practice,lol
mimi sio nabii, but kuna post niliweka hapa kwamba jamaa hakuwa nao............
 
Mikoba ya sheikh yahya alikurithisha? Nakumbuka hiyo comment yako juu ya hili.u shld open a practice,lol
hahahaaaaaaaaaaaa

itakua balaa, sasa na wewe umefuata nini kwenye povu la siasa?
 
Hawa wasomi mnaowatakuza nimesha waona wengi sana wanakaa darasani mwisho wanaodoka na cheti akili wanaacha kule kule walikosemea kupata lile gamba so sishangai leo Kigangala anayo yafanya .
 
Kigwangwala anatafuta publicity kwa nguvu yaani anajipa promo bila ya kutumia akili hana lolote huyo ***** tu.
 
Wana Jf nipo nzega nikitoka Mwanza katika ziara ya Ndg ridhwani kikwete.

Usikuu huu nikiwa napata chakula nikasikia Risasi zinalia Mjini nikaamua kufatilia na kupata taarifa kuwa Kuna Mgodi ambao unaitwa Isunga Ngwanda ambao siku Mbili zilizopita Mbunge na Wananchi waliungana Kuufunga.

Leo Kilicholeta Vurugu ni Pale Mbunge wa Nzega alipoenda kuwafata wananchi alioshirikiana nao kuufunga Mgodi na kuwataka kuufungua mgodi na yeye akijiunga na Polisi kuwataka wananchi wale waondoke wamuachie muwekazaji.

Wananchi walipandwa na Hasira na kumvamia mbunge na Kuanza kumpiga na Kuvunja Gari ya Daktari wa Wilaya ambayo aliazima naambiwa akiwa nzega huazima gari ya Daktari wa wilaya na kuitumia.

Wananchi hao wenye hasira waliamua kumpiga mbunge kwa kitendo chake cha kuwasaliti wananchi hao na leo kuungana na polisi na wawekezaji.Polisi ilibidi kutumia silaha za moto kumuokoa na na kuwakamata baadhi ya watu na kuwepeleka polisi jambo lilifanya wananchi kuandamana kwenda kuvamia kituo cha Polisi na matokeo yake Polisi kutumia Risasi kuwatawanya wananchi wao.

Liliwaudhi wananchi nitukio la Mbunge Kigwangala kuwageuka wananchi na kujiunga na wawekezaji na Polisi hivi sasa kunavurugu nzega mjini na Maeneo ya Isunga ktk Mgodi huo.

Duh ni la Daktari au la Serekali?
Akiwa Nzega? kwani jimbo lake ni lipi? ai ni KITU maalumu? maana hawa hawana JIMBO.
 
​Daa, mbunge kabisa anafanya mipango ya wizi namna hiyo?! Lakini si ajabu sana maana ccm kwa wizi/rushwa ndo wenyewe.

Unashangaa hilo muulize alifukuzwa kwa sababu gani kwenye mgodi huo huo anaoulalamikia kila siku, alishawahi kufanya kazi. Na hiyo chuki very likely ni kutokana na kisasi cha kutimuliwa!!!!!!!!!!! Sasa msubirini atakavyokuja kumwaga pumba kwa hili tukio linalosimuliwa hapa!!
 
na Mustapha Kapalata, Nzega

MBUNGE wa Jimbo la Nzenga, Mkoa wa Tabora, Dk. Hamis Kigwangalla (CCM), jana alinusurika kipigo huku gari lake likivunjwa kioo cha mbele kufuatia vurugu kubwa zilizozuka katika mgodi wa wachimbaji wadogo ulioko kijiji cha Mwabangu, Kata ya Nata dhidi ya wawekezaji wanaomiliki eneo hilo.

Akizungumuza baada ya kutoka katika kikao cha ulinzi na usalama, Dk. Kigwangalla alisema kuwa amefanyiwa vurugu na wawekezaji hao ambao hawana dhamana na mgodi huo wakati akiwapigania wachimbaji wadogo wanaotaka kuporwa eneo lao la machimbo na wawekezaji hao.

Mbunge huyo ambaye ameonekana adui mkubwa wa wawekezaji katika Wilaya ya Nzega, aliwasili kijijini hapo baada ya kupata taarifa kuwa wamiliki hao wapya wana mpango wa kuwafanyia vurugu wachimbaji wadogo ambao wamekuwa wakimiliki eneo hilo kwa muda mrefu.

Hata hivyo, Dk. Kigwangalla aliwatuliza wananchi pamoja na wachimbaji kwa ujumla ili kupata suluhu ya tatizo hilo, juhudi ambazo hazikuzaa matunda hatua iliyoibua machafuko makali baina ya pande hizo na kuanza kurushiana mawe.

Mbunge huyo alipambana vikali na kukoswa koswa na mawe ya wawekezaji hao na kuungana na wachimbaji wadogo mpaka kufikia hatua ya kutuliza vurugu hizo baada ya Jeshi la Polisi kuwasili katika eneo hilo licha ya gari lake lenye namba za usajiri T 357 BMP aina ya Caldin kuvunjwa kioo cha mbele.

Dk. Kigwangalla ambaye ameapa kupambana hadi mwisho, alisema katika vurugu hizo wachimbaji wadogo walimpiga mmoja wa wamiliki wa eneo hilo jiwe la kichwani na kumsababishia jeraha kubwa.

Alimtaja majeruhi huyo kuwa ni Moses Kichambati ambaye amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Nzega na anaendelea na matibabu.

Baadhi ya wachimbaji hao wakizungumuza kwa nyakati tofauti, walisema kuwa chanzo cha mgogoro huo ni wawekezaji kuingilia eneo lao kijijini hapo, huku wakiacha eneo ambalo wamekuwa wakilimiliki kwa muda mrefu.

Walisema kuwa mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu na serikali ya wilaya imeshindwa kuutatua mpaka zilipotokea vurugu hizo ambazo zimesababisha wachimbaji hao kujeruhiwa na uharibifu mkubwa wa mali kutokea kwa pande zote mbili.

Kwa upande wake Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Wilaya, Yusuph Sarungi, alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo majira ya saa sita mchana na kusababisha majeruhi wawili. Polisi inamshikilia mtuhumiwa mmoja na upelelezi unaendelea kubaini chanzo hicho cha vurugu.

Aliongeza kuwa tatizo hilo linapaswa kutatuliwa na wizara husika ili kurejesha mahusiano mema kwa wananchi hao na wawekezaji ambapo kila upande unadai una haki kwa eneo hilo.
 
ni vyema tukasikia pia ya wananchi na wawekezaji

I smell funny stuff hapa.... maana tumesikia kapigwa kwa kuwatetea wawekezaji
 
Wana Jf nipo nzega nikitoka Mwanza katika ziara ya Ndg ridhwani kikwete.

Usikuu huu nikiwa napata chakula nikasikia Risasi zinalia Mjini nikaamua kufatilia na kupata taarifa kuwa Kuna Mgodi ambao unaitwa Isunga Ngwanda ambao siku Mbili zilizopita Mbunge na Wananchi waliungana Kuufunga.

Leo Kilicholeta Vurugu ni Pale Mbunge wa Nzega alipoenda kuwafata wananchi alioshirikiana nao kuufunga Mgodi na kuwataka kuufungua mgodi na yeye akijiunga na Polisi kuwataka wananchi wale waondoke wamuachie muwekazaji.

Wananchi walipandwa na Hasira na kumvamia mbunge na Kuanza kumpiga na Kuvunja Gari ya Daktari wa Wilaya ambayo aliazima naambiwa akiwa nzega huazima gari ya Daktari wa wilaya na kuitumia.

Wananchi hao wenye hasira waliamua kumpiga mbunge kwa kitendo chake cha kuwasaliti wananchi hao na leo kuungana na polisi na wawekezaji.Polisi ilibidi kutumia silaha za moto kumuokoa na na kuwakamata baadhi ya watu na kuwepeleka polisi jambo lilifanya wananchi kuandamana kwenda kuvamia kituo cha Polisi na matokeo yake Polisi kutumia Risasi kuwatawanya wananchi wao.

Liliwaudhi wananchi nitukio la Mbunge Kigwangala kuwageuka wananchi na kujiunga na wawekezaji na Polisi hivi sasa kunavurugu nzega mjini na Maeneo ya Isunga ktk Mgodi huo.
Kwa vile Mhe. Dr. Kigwa ni member humu, naamini atajitokeza kutufafanulia kilichotokea.
 
ni vyema tukasikia pia ya wananchi na wawekezaji

I smell funny stuff hapa.... maana tumesikia kapigwa kwa kuwatetea wawekezaji
If you can't beat them, join them!, hebu na tumsubirie.
 
ah! kama kweli kafanya hivyo bora ajivue gamba tu, CDM wajiongezee majimbo bungeni....
 
kigangwalla ni kigeugeu sana, hana nia ya kuwa na wananchi pamoja ila anataka ku-winn political audience! ukiangalia kipindi cha bunge utajua nani yupo serious na anachosema na nani ni msanii! sisi wananchi tunawajua nani ni nani
 
Jamaa hayupo serious kabisa nadhani anatafuta umaarufu wa kisiasa!
 
Ninawasiwasi na mtoa taarifa kujitahidi kuegemea kwa mbunge. Hivi wawekezaji ni wangapi mpaka waweze kutunishiana msuli na wachimbaji wadogowadogo? hebu semeeni ukweli kwamba mbunge alitaka kuwageuka wananchi na kujiunga na wawekezaji ndipo dhahama ilipomkuta. Kapalata hebe acha kujishushia hadhi yako kwa tamaa ndogondogo
 
ina maana wawekezaji wamefikia hatua ya kupiga wabunge???????????
 
Back
Top Bottom