Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Ninadhani Jizaledo ameeleza waziwazi
1. Tumieni hoja zenye nguvu badala ya nguvu za matusi kuwa ndio hoja!!!!

2. Jibuni mapigo ya hoja badala ya kuwazulia wanabodi wengine hisia zenu potofu

3. Ni dhahiri mnalumbana hapa kwa nguvu za udini kiasi cha kujisahau na kuanza kukasirika na kucharura wanabodi wengine kibinafsi.

4. Mmezowea kuwaona Waislam wananyamaza na kuwaa watulivu hata pale wanapotendewa mabaya na mnataharuki mnapoona hivyo sivyo kinachotokea hapa.

5. Badala ya dhana Admin, anazo data za kumjuwa mwanabodi anayejileta hapa kwa majina mengi hivyo angemjulisha mkuyuga kuhusu watu anaowadhania kuwa ni mtu mmoja na pia wale ambao wanatumia majina mbalimbali.

6. Hii mada inaendelezwa kwasababu kwa jazba za kidini walizonazo walewale wanaolalamikia hilo wewe ukiwa mmojawapo.

7. Nyerere alikuwa na uzuri wake na pia udhahifu wake. Isingekuwa vema kuendeleza hii mada kufikia kumjadili kiundani hata kuchambuwa sababu za yeye i) kuishi mbalimbali na mkewe, ii) kupenda kutumia lugha ya Kimombasa kuwa "ukionja nyama ya binadamu utaendelea kuila siku zote" iii) mapenzi aliyokuwa nayo kwa Maalim Seif kabla hawajakorofishana, iv) sababu za Idd Amin kutamka tamko la aibu kuhusu Nyerere kwenye interview yake na BBC mwaka 1972 na v) hatima ya kifo chake kwa mkanda wa jeshi.
Jasusi said:
Jizalendo,
What is your point?
Mkandara,
Sema mdogo wangu, sema!
 
Timbwili
unasema Mkurugenzi wa Taifa hakubaguliwa na alipewa nafasi na Mkapa.
nakumbuka alipochaguliwa Mkurugenzi wa Taifa siku hiyo hiyo ilianza mada kwenye Blog ya michuzi kuwa jamaa amemaliza madrasa tu hana akijuacho JK kafanya makosa makubwa, haikushia hapo Jamboforums nayo ikichimba sana na ushahidi ukaletwa kuwa ni kuwadi wake JK kapewa nchi kwa kumkuwadia. LEO UNASEMA NI MSOMI NA Mkapa alimpa vyeo vingi! kumbe ule ulikuwa ni uzushi tu kisa kapewa muislam ndio akawa anazuliwa yote yale? sasa hamuoni chuki za kidini zinaweza kulikosesha Taifa watu wenye vipaji kama cha huyo bwana?

MKANDARA
Nyerere hakumshindwa Mwinyi 1993, kwani mwaka 1995 kule Dodoma katika kutafuta mgombea wa CCM je Nyerere jeuri ile aliipata wapi? kwani rais alikuwa Mwinyi na Mweneykiti wa Chama ni MWINYI ilikuwaje alimpiga kikumbo JK na JM na kutuwekea tumbili?
Nyerere alimnyang'anya hadi kadi ya chama Mzee Jumbe yaani sio kumvua tu urais hadi kadi alimaindi.
Sheikh Kassim bin Juma humjui ndugu yangu mara useme alikuwa mganga wa Nyerere , mara Mzee Bin Juma chewa n.k
mwanae gani ambaye ni rafiki yako? nina evidence kibao ila niweka hapa yatanikuta yaliyomkuta Marehemu Malima.
Nilikuwa karibu na marehemu Malima nikamuuliza utaweza vipi kuushawishi huu umma TZ ukuelewe na kufuata chama chako, akaniambia naenda London mara moja nikirudi na huo mkoba unaouona una dondo ambazo nikizimwaga hakuna hata mmoja atampa Nyerere heshima, wakati naondoka kwake nikapishana na Khalifa Hamis amekuja na njaa yake kwenye kiroba. masikini huo ndio ulikuwa mwisho wake marehemu kwani hakurudi tena mauti yalimchukua London.
lakini alipotoka kwenye chama Nyerere alimwita mara mbili nyumbani kwake na Profesa alikataa kwenda mara zote,naona nisiseme mengi napenda maisha yangu.
 
ManjuMakuti,
Mshikaji wewe kiboko!
Yaani umeandika - ISINGEKUWA VEMA....kisha ukamalizia na yale ambayo hutataka tuyazungumzie!...Ndio umeshamwaga, sema tu unataka kuendeleza barza. Nafikiri ni vizuri tulitumie neno UDINI kwa maana halisi..yaani ubaguzi wa kidini. Sidhani kama kuna mtu hapa anatoa maelezo yenye harufu ya ubaguzi.

Wanabodi,
Mimi nadhani Mswahili sii mdini isipokuwa ni mmoja kati ya wengi waliokuwa brainwashed na magazeti yetu ambayo hayana malengo mazuri zaidi ya kueneza chuki za kidini kwa kupitia viongozi wetu. Na ukisoma vizuri hoja zake amenukuu habari za watu wengine kama hoja kwetu tunapozungumzia mada hii. Sote kuna wakati tuna- copy na ku-paste habari ambazo zinautatanishi kwetu. Ni vizuri kumfahamisha ukweli uliosimama ili afanye homework yake vizuri next time...

He is a good guy! isipokuwa hana data kamili za madai ya hao masheikh na kama hayo waliyosema ni kweli... mtu yeyote lazima ushtuke!... Kwa wale tuliopitia malezi ya Nyerere, tunafahamu kwamba mzee yule alikuwa na mabaya yake lakini sii la Udini.

Aliyomfanyia Malechela, mzee Bomani ambaye kila mtu alifikiri kuwa ndiye angekamata Uwaziri mkuu baada ya Uhuru wetu na wengine wengi sii mchezo mdogo. Nyerere alikuwa kama Chogo Chemba, hana dini wala kabila ukija na vijichenga vyako atakutoa nishai na hatajali wewe dini gani... Kisha baada ya ndinga atakukumbatia na kusema ndio mpira huo! Hujafunga goli kabisa.. hakutupi moja kwa moja.

Mswahili,
Hapa umechanganya madawa...unaposema Nyerere hakumshindwa Mwinyi na umetoa mfano wa Uchaguzi wa 1995.

Swala hapa sii Uchaguzi, hata Mkapa kazidiwa karata na Mwinyi, Kingunge na mtando ambao hawakuwa wenyekiti. Nyerere alimshindwa hata Mkapa na kama angekuwa hai uchaguzi wa 2000 sidhani kama Mkapa angechukua..Na sintaona ajabu kama alipigwa kipapai kabla ya Uchaguzi ili Mkapa apate kutawala tena.

Jumbe mjinga yule, mbegu mbaya sana na mdini. Acha Nyerere, mimi binafsi ningemtoa nishai kwa sababu ktk kipindi chake Wapemba walikuja juu sana na kuanzisha matabaka upya. Na ndio maana Komadoo mzee Salmin alipokuja akafagia uchafu wote. Kiongozi yeyote aneyechukua mkondo wa udini ama ukabila hatufai na hata hiyo kadi kunyang'anywa size yake..Alifanya nini Jumbe zaidi ya kuwa kibaraka cha waarabu..

Kuhusu Sheikh Kassim sidhani kama nimesema namjua yeye binafsi!. Kumjua mtu neno zito ndugu yangu.
Nimesema alikuwa mganga wa Nyerere na huko Bagamoyo Nyerere alikuwa akimwona Mzee Chewa.. sijui kigumu kipi hapa. Na mwanae mkubwa ndiye swahiba wangu na hivi navyoandika yupo hapa!... sasa wasemaje?... nimekwambia ULIZA watu watakufahamisha zaidi kuhusu mimi.

Kighoma Malima kukusanya data za Nyerere alikuwa na lengo gani? yaani watu wamchukie Nyerere?... basi hakuwa na maana kwani Watanzania tunataka kiongozi sio kujenga majungu. Mbona hamzungumzi kuwa Mwinyi alimuondoa (dismissed) Kighoma Malima ktk Uwaziri wa fedha baada ya kushauriwa na donors achukue measures dhidi ya Malima kwa sababu za corruption. Je, unajua ya kwamba ni Kighoma Malima aliyetoa sheria ya kusamehe kodi wawekeshaji ktk madini jambo ambalo lilitukosesha Tanzania sii chini ya 50/m per year... miaka hiyooo!..
Huyu mchumi tena sii mchezo kasoma chuo kikubwa sanaa kinachoheshimika Marekani yote lakini katulaza milango wazi....Na bado Mwinyi akampachika sehemu nyingine...viwanda! Je, utakubaliana na wakristu wakisema huo ulikuwa Udini?..Acha ndugu yangu hawa jamaa wanakuzingua kutafuta KULA yao basi. Nafahamu fika kuwa wewe sii mdini isipokuwa nukuu hizi za magazeti zimekujaza jazba na machungu hali ukweli ni mdogo sana.

Mwanasiasa,
Nimekusikia baba, lakini hiyo ya Chadema vipi?.. umesha jiunga mwenzetu!.....mbona hatushtuani?... KULA yangu ipo?
 
Aluuuuuuuuuu mimi wa kunyumba , Bombii hii nyumbi hii nasema Boooob Mkandara nakupa mke wa jirani bure na mke wangu nakaa naye mwenyewe ndiyo ukarimu wa huku kwetu songea kwa mtu mchapa kazi na mtenda haki . Nasema Mkandara you have done it well and never get tired Bob . You are real na mimi nakupa thumbs up.Huu ndiyo ukweli and these guys need to research before they storm in internet cafes. Okoa mawazo hafifu waelekeze waijue Tanzania na wajue Mwalimu hakuwa wa kawaida . Leo kuna watu wanataja watoto wa Malecela wako Marekani nk , kesho tutasema watoto wa JK wanao someshwa na wazungu baada ya baba yao kulamba dume lakini Watoto wa Mwalimu wanalima Butiama na wako Kijijini kama sisi wananchi wengine wa Kawaida . Mwalimu believed in equal rights and aliishi hivyo hadi anakufa .

Mwalimu wakati anakufa kule London alisema maneno haya . Nakufa , Watanzania wangu nimewa wachia manyangáu watateseka sana .Hakusema watoto wangu wala wakristo wangu .

Jamani muogopeni Mungu na turudi kwenye issue tuache kejeli .
 
Je na haya ya kutaifishwa mali za taasisi za Kiislam alizozivunja Nyerere nayo yalikuwa na nia gani.

Sheikh Yahya alipua bomu

2006-10-27 19:24:51
Na Mwandishi Wetu, Jijini


Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bwana Jakaya Kikwete kuipa changamoto BAKWATA juu ya mali kadhaa za Waislamu kupotea mikononi mwao, Sheikh maarufu nchini, Yahya Hussein, ameibuka na kulipua bomu zito.

Sheikh Yahya ametaja majumba kibao yaliyoko Jijini baadhi yakiwa yanatumiwa na viongozi wa juu wa Serikali ambayo amedai yote yalikuwa mali ya Waislam.

Madai hayo ya Sheikh Yahya yamekuja baada ya changamoto ya Rais Kikwete aliyoitoa wakati akizungumza kwenye Baraza la Iddi el Fitr juzi Jijini Arusha.

Katika taarifa yake, Sheikh Yahya ameambatanisha vielelezo kadhaa vya kuthibitisha maelezo yake juu ya upotevu wa mali hizo za Waislamu.

Amesema kwa kuwa aliwahikuwa msimamizi wa mali za Waislamu kupitia BAKWATA miaka '96 hadi '98, anafahamu na anavyo vielelezo vya kutosha kuonyesha kile anachokisema.

Akasema Sheikh Yahya katika taarifa yake kuwa hapo kabla, Waislamu kupitia Jumuiya zao za Tanzania Muslim Welfare Society na East African Muslim Welfare Society walikuwa na mali zao kadhaa ambazo baadaye, wakati wa Serikali ya awamu ya kwanza, mali hizo ziliamuriwa kwenda mikononi mwa BAKWATA ambao nao walitakiwa wazifuatilie na kuzichukua.

Baada ya hapo, anasema Sheikh Yahya kuwa BAKWATA ilijikuta ikipoteza mali hizo nyingi, huku majumba mengine yakitwaliwa na Shirika la Nyumba NHC na mengine yakichukuliwa na watu binafsi.

Akasema Sheikh Yahya kuwa kwa sababu hiyo, anaungana na nasaha za Rais juu ya BAKWATA kusimamia vyema mali za Waislamu na kuhakikisha kuwa inajijenga upya ili kurejesha imani kwa Waislamu.
 
Jizaledo,
Binafsi namheshimu sana Sheikh Yahya Hussein kwa sababu ambazo ni nje ya dini. Anaweza kuwa na point isipokuwa hakuziweka kiutaalam kwani Utaifishaji halikuwa swala la kidini.

Mali za watu wengi na hasa biashara zilitaifishwa na ndio maana ya kutaifisha...

Mara nyingi tunashindwa kuelewa mifumo ya serikali na malengo yake.. na wakati mwingi huwa tunashindwa pia kuelewa hotuba za viongozi wetu kabisa...toka JKN na sasa msanii JK ndio anatutoa nje kabisaaa.

JK alipo hutubia waislaam siku ya Idd haina maana kajitenga na ukweli wa Kitaifa na kunyoosha kidole chake kuwashutumu wasiokuwa waislaam. Tunapoambiwa waislaam tujitahidi tupate kufanikisha kitu haina maana kwamba JK karudi nyumbani na atawafunga kamba wengine ili sisi tupate urahisi wa safari yenu....

Mimi nimeukubali Uislaam na hasa Sunni kwa sababu moja tu kubwa sana. Nayo ni - Hakuna binadamu yeyote kati yangu na Mungu! yaani hakuna mbora kwa Mungu kati yetu isipokuwa yule mwenye kufanya ibada. Huyo Sheikh ama Mufti ni binadamu kama mimi, anaomba kama mimi na haifahamu hukumu yake. I can challenge him/her. Hana ukaribu na Mungu isipokuwa kwa ibada yake kwa usawa wa chances niliyopewa mimi pia. Naweza kuwa na daraja kubwa kwa Mungu kuliko yeye...

Lakini imani hii pia imekuja na madhara yake. Moja kubwa ni la hapa duniani! Sunni hatuna kiongozi wa kidini ktk maisha ya kila siku zaidi ya kuwasikiliza walimu, graduates ama wenye elimu ya juu ya dunia kwa ushauri wao. Nje ya kitabu (quran na hadith) We can choose to listen or not! - Kila mtu na mzigo wake duniani na akhera!... Hii kkt maisha ya kuviziana kama mafisi ni hatari kubwa sana.

Mbaya zaidi basi yaani sisi Sunni hata kujenga msikiti shurti tunakamatana mashati tofauti na wenzetu Ismilia ama Shia. Mara nyingi tunategemea tajiri (akina Bakhresa) fulani aweze kusimamisha kitu kama sadak, hatuna jumuiya nje ya msikitini tunaposali. Till today bob sunni hatuna mwongozo zaidi ya sheikh fulani wa msikiti fulani, nje ya msikiti Sheikh hana sauti. Hii ndio sababu tumepewa chombo cha Bakwata kuweza kutusimamia kama tulivyokuwa tukisimamiwa na TMWS. Lakini bado waislaam tuliona kama ni propaganda za Nyerere kuwa na chama ambacho kinatambulika na serikali...

Pia hii ndiyo ilikuwa hotuba ya JK kutufahamisha majukumu yetu na chombo kama Bakwata tukitumie kwa manufaa yetu... lakini wapi! tunarudi nyumaa na kuanza kudai nyumba za Tanzania Muslim Welfare Society na East African Muslim Welfare Society, hali jumuiya za Kibaniani, Masingasinga, wazungu (wakristu) wa madhehebu tofauti wote walitaifishwa majumba.

Upanga, downtown na O'bay kote hapakuwepo na mali ya mswahili yeyote...

Kosa kubwa tunalolifanya Waislaam ni ile kuweka rangi yetu mbele tunapoweka madai ambayo yamewahusu watu wote!.. Inaonyesha kama sisi tulitengwa na kuonewa hali kila dini ili-athirika na mfumo huo wa Ujamaa. Inabidi tujifunze mbinu za kuandaa malalamishi yetu.
 
Mkandara maneno mazito mzee chagua mji nikupe maana kama waislam wenzio hawawez kupata elimu hii ya bure hawataelewa maishani .wao na viji gazeti vya chuki na kumkomalia mwalimu kila mara hawautaki ukweli na wanadhani walio newa na hata wanayaka kuonewa.
 
Nimekuelewa Mkandara.

Yahaya Hussein hajasema kuwa utaifishaji lilikuwa jambo la udini, yeye amenung'unikia vile BAKWATA ilivyozorota au kuzoroteshwa kusimamia mali za taasisi za Kiislamu zilizovunjwa. Na hili linakufanya mtu ujiulize kama kweli BAKWATA ilikuwa na haki na mgongo wa kuzuwia mali hizo zisisambaratishwe kama anavyodai yeye.

Sasa hapa kuna mambo machache ya kutafakari: i) Kujiuliza kama BAKWATA nayo ilikuwa ni chombo kilichoidhinishwa kumiliki mali zilizotaifishwa tukichukuliwa msimamo wako kuwa mali zote zilitaifishwa kwa dhamiri moja tu ya kutaifisha bila kujali mali hiyo ni ya nani. Wakati ule majumba yaliyotaifishwa ni yale ambayo thamani yake ilizidi Shillingi laki moja. Kwa hili nadhani pia ingekuwa vizuri na wewe nawe utowe hoja kama hizo za Yahya Hussein pamoja na kutokukaa vizuri (uonavyo wewe) zakuonyesha kuwa taasisi za Kikristo nazo pia zilivunjwa wakati ule na ikaundwa taasisi moja ya Kikristo ya kukabidhiwa mali taasisi hizo. Madai ya Yahya Hussein hapa ni kuwa baada ya kukabidhiwa BAKWATA mwisho majumba hayo yaliishia kwa watu binafsi serkalini na NHC!! Mwenzetu wewe unaweza ukawa na data za kutufumbuwa macho kuhusu majumba na mali za taasisi za Kikristo zilizotaifishwa kwani sisi tulichoona kuendelezwa ni kuimarishwa juhudi za mashule za makanisa na makanisa kupewa unafuu hata wa kuingiza magari na vifaa bila kulipa ushuru.

ii) Kwa misingi ya imani ya Sunni uliyojitamba nayo BAKWATA haiwezi kikawa ni chombo cha kusimamia na kuwaongoza Waislam. Imani ya Sunni kwa Mungu mmoja kamwe haiondowi uongozi unaotakiwa kusimamia maslahi ya Waislam ndio maana baada ya Mtume (SAW) kufariki akina AbuBakari waliongoza na wakaongoza vizuri tu sio kwa kupachikwa na Manaswara uongozi huo bali kwa nafasi waliyokuwa nayo kwa ukaribu wao kwa Mtume, kuelewa mambo yanayomuhusu Muislamu na kukubalika mbele ya Waislam wengine. Kwa manthari hiyo BAKWATA iliyoshinikizwa kwetu na makafiri akina Nyerere si taasisi halali ya kusimamia mambo ya Uislamu na kuchukuliwa mali za taasisi za Kiislam kupewa BAKWATA ilikuwa ni dhuluma na njama ya kujificha ya kuvunjavunja kila jema zilizoanzishwa na taasisi hizo. Kama BAKWATA ilikuwa na mali hivyo hili la BAKWATA hiyo hiyo kuwa nyakati nyingine inafadhiliwa na pesa za Kanisa Katoliki na akina Mengi hadi kufikia kuwatunuku nishani akina Mengi lingetokea wapi.

Kama hoja yako ya kuwa mali hizo zilitaifishwa kama vile zilivyotaifisha za watu wengine ina uzito, itabidi kwanza utafute hoja za kukanusha madai ya Yahya Hussein kuwa hizo nyumba zilizopokorwa taasisi za Kiislamu hazikukabidhiwa BAKWATA kwani BAKWATA haikuwa taasisi iliyoundwa kupokea mali zilizotaifishwa ziwe za vyama vya Waislam au za mtu yeyote mwengine. Kulikoni basi ikakabidhiwa mali hizo badala ya kukabidhiwa Msajili wa Majumba na NHC?

Mkandara said:
Jizaledo,
Binafsi namheshimu sana Sheikh Yahya Hussein kwa sababu ambazo ni nje ya dini. Anaweza kuwa na point isipokuwa hakuziweka kiutaalam kwani Utaifishaji halikuwa swala la kidini.
Mali za watu wengi na hasa biashara zilitaifishwa na ndio maana ya kutaifisha...
Mimi nimeukubali Uislaam na hasa Sunni kwa sababu moja tu kubwa sana. Nayo ni - Hakuna binadamu yeyote kati yangu na Mungu! yaani hakuna mbora kwa Mungu kati yetu isipokuwa yule mwenye kufanya ibada.
Lakini imani hii pia imekuja na madhara yake. Moja kubwa ni la hapa duniani! Sunni hatuna kiongozi wa kidini ktk maisha ya kila siku zaidi ya kuwasikiliza walimu, graduates ama wenye elimu ya juu ya dunia kwa ushauri wao. Nje ya kitabu (quran na hadith) We can choose to listen or not! - Kila mtu na mzigo wake duniani na akhera!... Hii kkt maisha ya kuviziana kama mafisi ni hatari kubwa sana.

Till today bob sunni hatuna mwongozo zaidi ya sheikh fulani wa msikiti fulani, nje ya msikiti Sheikh hana sauti. Hii ndio sababu tumepewa chombo cha Bakwata kuweza kutusimamia kama tulivyokuwa tukisimamiwa na TMWS.

Pia hii ndiyo ilikuwa hotuba ya JK kutufahamisha majukumu yetu na chombo kama Bakwata tukitumie kwa manufaa yetu... lakini wapi! tunarudi nyumaa na kuanza kudai nyumba za Tanzania Muslim Welfare Society na East African Muslim Welfare Society, hali jumuiya za Kibaniani, Masingasinga, wazungu (wakristu) wa madhehebu tofauti wote walitaifishwa majumba.
Upanga, downtown na O'bay kote hapakuwepo na mali ya mswahili yeyote...
 
Mkandara
Mzee Jumbe sio mpemba na wala hawawivi na seif Sharif Hamad kama unajua mambo Jumbe alimpa uwaziri wa elimu-Seif ikawa wapemba ndio wanapendelewa sawa na Mzee Jumbe akamuuliza Seif mbona unataka kuwagawa wananchi kwa upemba na uunguja? na sera za Comando zilikuwa ni muendelezo wa marehemu Karume na Jumbe. lini uliona Jumbe anakwenda Pemba hata nyumba zake ziko Kigamboni na Unguja na hana hata mke mpemba.

Kuna mwanabodi anasema Nyerere alimuomba Gadaf ajenge msikiti Butiama jee msikiti huo una faida gani? wakati kazuia maendeleo mengi tu ya waislam? kazuia ujenzi wa vyuo vikuu na mashule. alipoona anaumwa na anaogopa historia hii tunayoiandika ndio akataka kujikosha na huo msikiti na huku kitita kingine kanywa!

Mzee Jumbe ameanzisha na kutafuta wafadhili wa chuo kikuu cha Zanzibar leo unasema hajafanya kitu? chuo hiki kinasaidia nchi na hadi watu toka malawi,uganda na kenya hadi Zambia wako pale.

sasa unaweza kulinganisha na msikiti wa Nyerere? pia hatuhitaji misikiti mbona hakujenga shule kama kweli alikuwa na nia ya kuwaendeleza waislam? msikiti wa butiama unamsaidia nini mtu wa Kigoma? lakini Znz University inabeba watu nchi nzima na zimepatika ajira, uchumi umekuwa na mengi sana.

Mzee Jumbe alipoona mambo ya Nyerere ni kigeugeu alimuandika waraka maalum kumueleza kasoro mbali mbali na mapungufu yake, matokeo yake mzee Jumbe ni kuitwa Dodoma na kuvuliwa kila kitu na kunyang'anywa hadi kadi. badala ya kujibu hoja kavuliwa kila kitu.

Malima hakuwa mla rushwa naomba uthibitisho? na amekufa masikini fuatilia hata maisha ya wanawe wanaishi kwa taabu sana hawatofautiani na watoto wa sokoine, kama Malima mla rushwa jee Msuya na Sumaye ni nani? pia shirika gani lilolishinikiza Malima atolewe uwaziri? Malima alimchukia Nyerere kwa ubaguzi wake wa kidini kwanini raia wengine wawe second class citizen?

UDINI NA uKABILA WA Nyerere
ukienda jeshi utajua kazi ya nyerere wote akina chacha,wambura,kiaro,mwita,musuguri n.k kifupi wamejazwa watu wa musoma tu ndio maana hata ule msemo maarufu mtu ukimuona afande unasema (haroooh afande au liafande mwita) Nyerere hakuona aibu kuwapa vyeo homeboy zake David musuguri ambaye ni darasa la nne alipewa ukuu wa jeshi na Nyerere kisa ukabila, Warioba ambaye ni binamu yake alimpa uwaziri mkuu, Charles Nyirabu alipewa ugavana huku hana sifa ila ni home boy, sasa anayesema hakuwa mkabila labda ni mkurya,mjita au mzanaki.

Udini ndio hatusemi waulize akina Titi Mohamed,Takadir,Tewa Said n.k

mfano mzuri baraza la mitihani kulikuwa na MR. MBIKU ambaye hadi juzi tu alikuwa ana act kama director huyu jamaa ni mwalimu wa kawaida hana sifa yeyote zaidi ya ukatoliki, huyo ndio anahakikisha akina Maua seminary wako kwenye kumi bora.

pia ana kaka yake Father Mbiku ambaye yuko chuo kikuu cha Dsm naye huyu anaingia hadi kwenye selection ya wanafunzi wakati ni padree tu, sasa mbona hakuna sheikh huko? mfano mzuri kuna mtoto alikuwa na division three (nahifadhi jina lake) na ilikuwa huwezi kuingia Udsm kwa alama hizo lakini Father Mbiku alimpenyeza. yapo mengi ya uchungu nakupa nyingine kuna sheikh anaitwa Bosha alikuwa anahubiri Arusha ikatokea wamasai wengi wakawa wanaingia uislam na ni mwaka juzi tu. Sumaye akampa deportation ya 24 hours na aliisimamia mwenyewe Sumaye.

jamani acheni kutania watu nyie mmekula neema za kanisa hamjui dhiki zetu.
 
Mkandara,

Ninakutahadharisha tu kuwa ulimi hauna mfupa na hata siku moja simba awezi akawa tembo na tembo akawa simba kwani ulimi wake utamkosowa. Haya machache tu niliyoyanukuhu kutoka kwenye maandishi yako yanaonyesha wazi kuwa wewe si sunni wala muislam kwani ndani ya haya mna lack basic knowledge kuhusu Uislam na mengine ni maneno ya kufuru.
Mkandara said:
Jizaledo,
Tunapoambiwa waislaam tujitahidi tupate kufanikisha kitu haina maana kwamba JK karudi nyumbani na atawafunga kamba wengine ili sisi tupate urahisi wa safari yenu....
Mimi nimeukubali Uislaam na hasa Sunni kwa sababu moja tu kubwa sana. Nayo ni - Hakuna binadamu yeyote kati yangu na Mungu! yaani hakuna mbora kwa Mungu kati yetu isipokuwa yule mwenye kufanya ibada. Huyo Sheikh I can challenge him/her. Lakini imani hii pia imekuja na madhara yake. Hii kkt maisha ya kuviziana kama mafisi ni hatari kubwa sana.
Till today bob sunni hatuna mwongozo Hii ndio sababu tumepewa chombo cha Bakwata kuweza kutusimamia kama tulivyokuwa tukisimamiwa na TMWS.
 
Ehhhhhhh! Jizaledo, Mswahili, DRWho, by the way what Jesus, or --- (I cannot write I am afraid); got to do with our present era. They died 2000 years ago, we are blaming and also sometimes killing each other today (especially in the third world of Africa, Middle east and Asia). Who is of priority to you? Imagine if your father was a christian or a muslim what would you say when yourself 're from a different religion? We have such families worldwide. I think sometimes religion is a virus, it enters our organs and to cure a virus needs to eliminate an organ (the host).

Are we talking about Nyerere favouring christians or about power struggle? Je hizo data zenu mlizipata kutoka kwa Jumbe au kwa walalahoi? Mie nafikiri masimulizi yenu katika hili ni power struggle.

Swahiba Mkandara welldone kwa uvumilivu wako, ni wachache sana wawe wakristo au waIslam ambao wanaonyesha upeo wa uelewo katika dini zao. It comes from your heart, I can see it. Kufikia upeo kama huo kwa majority yetu tunahitaji watu kama wewe.
 
""lini uliona Jumbe anakwenda Pemba hata nyumba zake ziko Kigamboni na Unguja na hana hata mke mpemba"".
Du very entertaining, that thinking only makes me not even try again to participate in such forums, unless I know what was your meaning!
 
IO,

Sintachoka kuwafafanulia ndugu zangu hawa ambao wamekuwa brainwashed na baadhi ya wakerereketwa wa kidini. Hii nio kazi yetu kubwa kuwa na mijadala ambayo kesho itaweza kuwaamsha wananchi ktk kuzitaza taasisi mbali mbali za kijamii.

Mswahili,

1. Sikusema Mzee Jumbe alikuwa Mpemba isipokuwa alikuwa Kibaraka wa Waarabu (Wapemba). Rudia tena kusoma maelezo yangu. Sababu kubwa iliyowashtua Waunguja kuhusu Jumbe ilikuwa elimu. Seif Sharrif alipokuwa waziri wa elimu aliwatenga Waunguja nao wakiwa Waislaam. Sehemu kubwa za biashara Unguja zilichukuliwa na Wapemba na hata kuwa na nguvu kuliko Waunguja wenyewe. Ni baraza la Mapinduzi lililomshtakia Nyerere kuhusu Uongozi wa Jumbe na kuwa Jumbe alikuwa akirudisha Utengano. Sasa nambie hao baraza la Mapinduzi sio Waislaam?.. au nao ni vibaraka wa katoliki!...

Je, sio baraza la Mapinduzi lilopendekeza jina la Mwinyi badala ya Salim ktk kushika nafasi uteuzi wa rais... kabla ya vyama vingi kupitishwa na Nyerere akafanya kama alivyoaagizwa!. Wewe hujiulizi huyu Mwinyi katokea wapi hadi kushika madaraka makubwa ghafla kiasi hicho!..

2. Sikusema Malima alikuwa akila rushwa yeye isipokuwa ktk uongozi wake kama wizara ya fedha kulikuwepo na RUSHWA wizarani kiasi kwamba Donors walimshauri Mwinyi amwondoe Malima ktk wizara hiyo. Ukitaka ushahidi wasiliana na LEAT watakupa kesi nzima... SIKUTUNGA swala hili. Wala hakuna sehemu nimesema Sumaye na Msuya sio wala rushwa. U missed my point brother!

3. Enzi za Nyerere hakuna mbongo aliyetaka kuwa Mwanajeshi!... wote sisi tuliingia mitini tukihofia maswala ya vita Msumbiji, Angola na kwingineko. Kuingia jeshi ni HIARI ya mtu itakuwaje leo tumshushie Nyerere hali haikuwa uteuzi?..Makabila hayo ni Warriors by nature, jeshi ndio mapenzi yao kama walivyo Wachagga na biashara. Je, Nyerere pia aliwapendelea Wachagga kuwa wafanya biashara?..

4. Akina Bibi Titi walitaka kupindua serikali ya Nyerere sasa sijui wewe ungefanya nini... na bahati msivyokuwa na shukrani Nyerere aliwasamehe woteee!..Kiongozi gani Afrika anaweza kufanya hayo!

Jizaledo,
Hakuna kufuru yoyote ktk maelezo yangu kwa sababu KUFURU ni kumshirikisha MUngu kwa njia yeyote ile. Labda wewe ndio hufahamu maana ya kufuru na tofauti ya Sunni na madhehebu mengine. Mfano niliposema:- Hakuna binadamu yeyote kati yangu na Mungu. sikuwa na maana zaidi ya kuwa Sunni hatuna MUNGU MTU. Mtu ambaye anaaminika kuwa karibu na Mungu na anaweza kukufutia madhambi ama kukuombea msamaha kwa Mungu. Ama kuuthamini kidini ukoo wa mtume na kuwafanya wawe saints ama mamlaka ktk dini...Mungu pekee ndiye anayemfahamu saint ni nani.

Najua wewe umevuka mpaka na kujiuliza kuhusu Mitume, je sio watu kati yako na Mungu?... nasema kuwa Mitume ni mwongozo wao ktk Quran na hadithi nje ya hapo hawa ni binadamu kama mimi na tunawaombea pepo vilevile.
Nimemaliza!...

Hatuna Mwongozo, haina maana nje ya kuwepo na mwongozi ktk maisha yetu ya kila siku nje ya dini..i.e POLITICS...

Kiongozi wetu ni Quran na hadithi sio binadamu.
Kabish!
 
Mkandara,

1. Soma dini tena kama wewe kweli ni Muislam ili uielewe na ili ujuwe kuwa wapo waliopewa madaraka kuwaongoza Waislamu hapa duniani na kuna mfumo wa kudhihirisha madaraka hayo katika Mwongozo wa waislam wote na kwenda kinyume na Mwongozo huo ni kuudhalilisha, kuukana na hivyo kutokuuamini huo pamoja na kutokumuamini Mwenyezi Mungu aliyeuleta. Kutokuwa na imani ni kufuru ya wazi na apukika tu kwa kuwa within zile arkanu l'imaan ambazo ni sitatu.

2. Kwa taarifa yako kukufuru kuna njia mbalimbali likianzia na outright denial ya kuwepo Mwenyezi Mungu kwa kutokuzingatia hizo nguzo sita za imani. Sasa wewe ni wazi huelewi maana ya kumshirikisha mwenyezi Mungu uliyoitaja hapa. Mimi siko hapa kukupa darasa hili ambalo ni very basic kwa muislam yeyote anayewajibikiwa na faradhi za dini yake. Labda nikushauri tu uelewe kuwa kuna kufuru nyingine watu huzifanya bila kujuwa inapokuwa hawauelewi uislam na misemo ya watu hao ndiyo inayowadhihirisha kuwa wanajifanya waislam kwa kusikia eti kuna sunni na shia na kutumia kivuli cha kujifanya kwao huko washambulie haki na kupigiana makofi wao kwa wao katika kushamiria batwili. Nikudokeza kitu kimoja tu tuone kama kweli wewe unajuwa kukufuru ni nini? Hivi unajuwa wewe kuwa unapokwenda kwa mganga wa kienyezi (muite umuitavyo - sangoma, sheikh n.k) ili akunyooshee mambo yako uwe na kazi nzuri, upate ubunge n.k basi wewe umekwisha kufuru. Sasa hujaona waislamu wanaofanya hivyo au mashekh wanaowafanyia watu hivyo

3. Kwa taarifa yako nyingine ni kuwa Quran si "kiongozi", bali kiongozi wa uma wa karne hizi ni Muhammad na wewe fanya ufanyavyo huwezi ukaufikia ukaribu alio nao kwa Mwenyezi Mungu na ndio ile siku ya malipo yeye atakuwa nayo fursa ya kuwaombea msamaha wale wanaostahili ambao matendo yao hapa duniani yalistahili msamaha huo. Sasa hili la kuwa hakuna binadamu yeyote mwengine kati ya wewe na Mungu nalo ni kutoelewa philosophy ya dini hii ya kuwa wewe uko accountable moja kwa moja kwa Mwenyezi Mungu na wala si kwa mtu yeyote. Kuwa accountable kwako moja kwa moja kwa Mwenyezi Mungu hakumuondolei seniority aliyonayo Mtume mbele ya Mwenyezi Mungu dhidi ya sisi akina yakhe. Huu ni umma wa Nabii Muhammad naye ndiye Kiongozi Mkuu wa umma huu na uongozi huo uliamia kwa makhalifa yeye alipoaga dunia na mfumo huo unaendelea hadi leo. Bakwata ya Nyerere haitaki kufuata mfumo huo ndio maana tunakuwa kichekesho tunapoendelea kufunga Ramadhan baada ya siku thelathini kupita kinyume ya taratibu za dini na kinyume ya maelekezo ya viongozi waliokabidhika alama dhahiri za uongozi huo ambazo unafika wakati zinawasuta waislam wanaoongozwa na BAKWATA ya Nyerere wanapokwenda kuhiji kwani ni lazima wafuate kauli za viongozi wa Kiislam kwenye hili swala la hijja, watake wasitake.

3. Umesema Sunni hatuna mwongozo. Kwa taarifa yako mwongozo tunao na sina haja yakuendeleza kufafanuwa hili. Kuenda kinyume na mwongozo huo kunamuelekeza mja kubaya na asipotaharuki kabla ya wakati si ajabu akafa hali yumo katika kufuru yaani akafa kafiri (Mwenyezi Mungu atuepushe Waislam na hili). Na tahadhari hii ninaitowa kuongelea swala tu la kwenda kinyume na mwongozo. Hivyo ninataka kusisitiza kuwa kudai hakuna au kuukana mwongozo huo kwa kusema hakuna is more serious kuliko kule kwendesha maisha yako kinyume chake. Huku kuukana, kusema haupo ni outright kufru.

Labda ndugu yangu wewe kiswahili hakipandi vizuri, bali nia haiko hivyo bali uelewe katika swala la kukufuru sababu za upungufu wa lugha hazikubaliki kwani Mwenyezi Mungu ametupa maarifa na akasisitiza tuwe tunajielimisha, na usipofanya hivyo ni wazi unaweza ukakufuru bila ya wewe mwenyewe kujuwa. Daima sisi huwa tunamuomba Mwenyezi Mungu atuepushe na kufuru inayoweza kutokea kwa njia hii ya tatu ambazo sina haja ya kukuelezea hapa kwani wewe huonekani kutaka kujifunza bali kushamiria adhima zako uzijuwazo mwenyewe. Kama wewe kweli ni muislamu basi ni wazi una kazi kubwa ya kufanya ili uijuwe dini hii vema ufuate mafundisho yaliyomo katika mwongozo wake, uelewe viongozi wako ni wapi, na inshaAllah ukifanya hivyo kwa nia njema tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu atakuongoza kwenye swirat-ul mustakiyma kama vile tunavyomuomba awaongoze hivyo waislam wote wake kwa waume. La kama unajifanya Muislam ili ushamiriwe kashfa zako kwa waislamu ili upigiwe makofi na mashabiki basi mimi sina la kuongeza kwani Mwenyezi Mungu na Mtumewe ndio wajuwao.

4. Ninakukumbusha kuwa nilikuomba utuletee list ya taasisi za kikristo zilizotaifishiwa mali zao na chombo walichoundiwa kama ilivyoundwa BAKWATA kwa ajili ya waislam na sheria iliyovipa nguvu vyombo kama hivi vipewe mali za taasisi za dini zilizovunjwa, badala ya mali za "kutaifishwa" huko kukabidhiwa vyombo rasmi vya ROB na NHC vilivyoundwa kwa ajili ya kumiliki mali zilizotaifishwa. Vipi mbona umeingia mitini hapa na wala hukuligusa hilo wakati hilo lilikuwa ndilo lilikufanya uchangie mada hii, sasa mambo haya vipi sheikh, eh?

Mkandara said:
Jizaledo,
Hakuna kufuru yoyote ktk maelezo yangu kwa sababu KUFURU ni kumshirikisha MUngu kwa njia yeyote ile. Labda wewe ndio hufahamu maana ya kufuru na tofauti ya Sunni na madhehebu mengine. Mfano niliposema:- Hakuna binadamu yeyote kati yangu na Mungu. sikuwa na maana zaidi ya kuwa Sunni hatuna MUNGU MTU. Mtu ambaye anaaminika kuwa karibu na Mungu na anaweza kukufutia madhambi ama kukuombea msamaha kwa Mungu. Ama kuuthamini kidini ukoo wa mtume na kuwafanya wawe saints ama mamlaka ktk dini...Mungu pekee ndiye anayemfahamu saint ni nani.
Najua wewe umevuka mpaka na kujiuliza kuhusu Mitume, je sio watu kati yako na Mungu?... nasema kuwa Mitume ni mwongozo wao ktk Quran na hadithi nje ya hapo hawa ni binadamu kama mimi na tunawaombea pepo vilevile.
Nimemaliza!...
Hatuna Mwongozo, haina maana nje ya kuwepo na mwongozi ktk maisha yetu ya kila siku nje ya dini..i.e POLITICS...
Kiongozi wetu ni Quran na hadithi sio binadamu.
Kabish!
 
jamani ebu tuacheni haya mambo ya kufikiri ndani ya box tu kila wakati, unajua utambulisho(identity) ya mtu ni utamaduni wake na sio dini yake, hili nimeliona mimi baada ya kuishi ulaya kwa mda mrefu sana, mimi ninarafiki zangu hapa watanzania na ni waislam na mimi ni mkristu.

na tunajiona sisi tupo karibuzaidi na ni marafiki zaidi kwa kujiona sisi ni watanzania na tunazungumza kiswahili na unajua watanzania tukiwa huku nje tunakuwa ni ndugu kabisa, tofatui zingine zote za dini tunaziweka pembeni,
sasa hapa kuna waarabu ambao ni waislam na pia wapo wazungu ambao ni wakristu, sasa kama identity ya mtu ingekuwa ni dini inamaana mimi marafiki zangu wa karibu wangekuwa ni wazungu ambao ni wakristu na hawa rafiki zangu rafiki zao wa karibu wangekuwa ni waarabu ambao ni waislam, lakini hapana, hao wote wanatubagua sisi kama weusi regardless ya dini yake.

mimi nafikiri hili ni somo kubwa sana, mtu unaweza ukawa na dini yako tu kama kawaida lakini wakati huohuo hiyo dini yako isije ikakufanya wewe umkatae ndugu yako utakuwa ni mjinga, sisi watanzania awe mkristu,mwislamu au dini nyingine sisi ni ndugu.

badala ya kukaa chini na kuanza kujadili mambo muhimu yanayolikabili taifa hili,tunaanza kunyosheana vidole vya dini, kama wewe ndugu jizaledo au mswahili manaona nyerere aliwaonea, mnaweza kwenda kufungua kesi mahakani na mpeleke na ushahidi huko,hapa kwa sasa tunaomba mtuanche tujadili SIASA.
 
Chuki chuki chuki na chuki na hdithi na majazba ni ujinga na upuuzi sana . Ndiyo maana Wapalestina wanaumia kwa kuwa ya imai yao na madai ambayo hayasikilizwi mana yanakuja na chuki na wanaacha kujua kwamba Dunia imeendelea na watumie njia zingine za kuwakabili waisraeli. Jizalendo na nduguzo Tanzania ni ya wote na Mwalimu did well na hakuna wa kukataa hilo .Hubirini watoto wenu wasome na si chuki maana mkichelewa na wao watasoma hadithi kama hizi na wakashindwa kufanya mambo ya maana . Mwalimu alikuwa mwisho wa matatizo kila Muislam mwenye akili timamu knows .
 
Mkandara
nimekuuliza kuhusu waraka wa jumbe kwa nyerere naomba jibu lake?

Jumbe hawivi na wapemba uliza hadi sasa jinsi wanavyomchukia kisa wanadai ni Mngoni. hivyo madai yako kuwa alikuwa mtu wa kuwafagilia wapemba sio kweli.

Mzee Shughuli
Waislam hawaenezi chuki na ni watu wa upendo kwa binadamu yeyote ndio maana hata ukienda kuomba maji nyumba ya muislam hunyimwi.

chukulia mfano mwepesi Nyerere alikuja na kaptula na waislam hawakuona kinyaa kukaa nae na wakamfundisha hadi kuvaa suruali.

waislam hawakumbagua kuwa katoka bara na pia mkristu laa!! waliishi nae na kumfadhili mambo mengi tu hatuna haja kuyasema kwa marefu. sasa kama chuki angechukiwa yeye na hata hawakuona taabu kumpa nafasi ya urais kwani ilikuwa mali ya Abdul wahid sykes. jiulize kwenye zile harakati za uhuru alikuwa na wakristu wangapi? na waislam wangapi? utaona mchango wa waislam bila kinyongo wala chuki na hata sasa, anaweza kuja mkristu anaenda kwa mganga muislam basi atasaidiwa matatizo yake kama alivyokuwa anafanyiwa Nyerere na Mzee Ramia na kuna siku alifunga swaumu ikawa kali hiyo ilikuwa dua maalum ya kumtoa Governor Twinning na mbuzi akachinjwa magomeni ili kuzima nguvu za Twinning. jee kanisa gani liliwahi kufanya misa kuomba wakoloni waondoke tena kumfanyia muislam? huo ni upendo wa waislam. kama utakumbuka miaka yake ya mwanzo ya uhuru alikuwa akivaa kibagharashia(kofia) na bakora akiona fahari kujifananisha na wastaarabu(waislam). huko mbali hata ukienda mpira utasikia beki mkristu(beki mwenye roho ).

Mzee Shughuli nimelazimika kukuweka sawa ingawa sasa mnatuona sisi waswahili (hatujaendelea)
imagine Mzee una nyumba yako jee unaweza kumpangisha muislam? lakini tizama nyumba za waislam zinapangisha watu wa dini zote fanya utafiti uone waislam walivyo rahimu na hawana chuki unazodai.
JK amekuwa kipenzi kwa wananchi sababu ana hulka za kiislam, ndio maana anahangaika kuwapeleka akina shughuli bwana gurdoto ili waweze kujua jinsi ya kuishi na kuwahudumia watu(mijitu miprofessor lakini hawajui jinsi yakuongea na watu) maarifa haya kwa waislam unayapata mtaani tu.

pia jifunzeni wanapokuja marais waislam basi wananchi wote wanawapenda mafano kwa ruksa na sasa JK ambapo mtu kumwita mwanaye JK ni jambo la kila siku,

nani anaweza kumwita mwanaye Mkapa? yote ni hulka na silka ya kujua kuishi na watu? au mzee shughuli unaweza kumwita mwanao Magufuri? narudia tena nimeyasema haya kukusaidia Shughuli bwana na wenzako muuonao uislam ni kikundi cha chuki.
 
Quarz,

Kwa hiyo uliowaona wanajibishana kwenye mada hii ni Jizaledo na Mswahili tu. Kweli wewe kubwa yao.

Hivi ni wapi niliposema kuwa Nyerere alinionea. Hapa tunajadili ukweli kuhusu Nyerere hatulalamiki kuonewa mtu bali tunajadili hitilafu na ufanisi wa mfumo wa uendeshwaji wa taifa chini ya Nyerere hili hadi kutufikisha hapa tulipo ili tubuni njia za kuboresha mambo ili taifa hili likwamuke. Kwa taarifa yako, ikiwa Nyerere alionea watu basi wapo ambao asingeweza kuwaonea hata kama angetaka kwani angefanya hivyo angejianika kweupeeeee. Mimi taifa lilinipangia scholarship ya kusomea taaluma adimu nje kutokana na matokeo ya Cambridge O-levels peke yake na nilifanya A-levels ili kukamilisha taratibu za kuingia chuo kikuu Uingereza tu na wala si kwa ajili ya kutunukiwa schlarship na taifa. Na baada ya A-levels nilighorodheshwa tena kwenda Nairobi university, yaani nilipewa double allocation kabla ya kutagharuki kuwa walikwisha nipangia kwenda nje ya nchi. Kabla hujapata mawazo ya ajabu ajabu inabidi nikutaarifu kuwa mimi si wala sijawa shushushu. Sasa ningesema vipi kuwa mimi binafsi nilionewa. Hatuongelei mambo ya ubinafsi hapa.

quarz said:
kama wewe ndugu jizaledo au mswahili manaona nyerere aliwaonea, mnaweza kwenda kufungua kesi mahakani na mpeleke na ushahidi huko,hapa kwa sasa tunaomba mtuanche tujadili SIASA.
 
Back
Top Bottom