Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Wazee Yote nimeyasikia, kwa upande wangu yanatosha na hiyo issue! Tujaribu kujifunza kumjadili Mwalimu au kiongozi yoyote bila jazba, ukweli na ubaya wake usemwe bila kuficha, ndio maendeleo yenyewe!
 
Mzee Es,

Katika watu ambao Mwalim aliwashusha madaraka na kutokusiliza mauidha yao pia kuna Chief Fundikira. Halafu kama wanavyodai wengine kuwa uchumi chini ya Mzee ruksa ulikuwa bomu ni kweli basi kuna vitendawili viwili hapa vya kutegua. AIDHA i) Mwalim alikosea kutowasikiza akina Mtei na Fundikira, na Mwinyi naye hakukosea kusikiliza ushauri wa kiuchumi wa Lipumba AU ii) vyama vilivyoanzishwa au kuongozwa na akina, Mtei, Fundikira na Lipumba ni mabomu matupu. Baadhi ya wanachama wa vyama hivi wanamtetea sana Mwalim bila ya kujuwa ukali wa Mwalim unaashiria nini kwa misingi iliyowekwa kwenye vyama wanavyojaribu kuviuza kwetu. Na cha hatari zaidi viwili ya vyama hivi ndivyo vilivyoifuatilia CCM ingawa kwa mabli katika uchaguzi uliopita - CUF (Lipumba), CHADEMA (Mtei na Makani). Duh

Walahi Es haya mambo yanachanganya mno na kukatisha tamaa. Mimi siondoki CCM ng'o na nitawaunga mkono wateule wa CCM, kazi ni kuhakikisha kuwa tunateua wanaofaa bali ndani ya CCM.

Mzee Es said:
Mzee Jasusi,

Yes!, kwa sababu inawezekana ndio maana hakutaka ushauri wa viongozi wenziwe, hebu niambie ushauri wa nani? Mtei?

Mwalimu angemsikiliza marehemu Prof. Rweyemamu?
 
Mzee Es,
Uncle nilikuelewa sanaa na ndio maana majibu yangu yako mbele ya kitendawili chako.

Isipokuwa tu nachelea kusema najua kuna watu watakao kuelewa nje ya swala na kuzua mengine yasiyohusika kwa sababu hawakuelewa unazungumza kitu gani.

Kwa bahati nzuri waliojibu hadi sasa ni vigogo wa mijadala na wanaelewa zaidi upeo wa swali lako. Mkira kakupa jibu safi sana.. Yaani JK na wengine hawakuweza kuonekana kwa sababu dini wasn't an issue at all. lakini walikuwepo madarakani ama shule wakipikwa kwa sponsorship za Nyerere.

Leo hii tunaanza kuona makablia na machief wakijitokeza kwa sababu Ukabila unarudi...Na wasiwasi yangu ni kuwa hata Waislaam sasa hivi wanaanza kujitenga kwa madai kuwa walionewa!

Mzee Fundikira mwenyewe alikuwa tofauti sana na Nyerere. Na sababu zinafahamika kwani Fundikira alisoma na Nyerere high school na hata Makelele na siku zote mzee Fundikira alikuwa akimwona Nyerere kama mtu asiyeweza kuongoza. Ni Fundikira pekee aliyepinga Nyerere kupewa madaraka ya Urais kwa sababu alikuwa akimjua kwa tabia na kitu gani kikubwa kilichokuwa kikimsumbua Nyerere... 1. UKABILA 2. UDINI.

Nyerere alipendekezwa na Abdoul Wahid Sykes baada ya kushinda uchaguzi wa kwanza kwa sababu Nyerere peke yake ndiye alitoka ktk kabila dogo na hakuwa Chief. Wengine wote walikuwa machief na toka makabila makubwa na kungetokea sokomoko ktk uongozi, pia vilevile waliokuwa ktk harakati za kupigania uhuru wetu wengi wao walikuwa waislaam.

Mzee Fundikira aliyaona yote hayo na kuwa Nyerere was going to act against!..

Kama kweli Nyerere alikuwa Mdini imekuwaje 1. Waislaam wengi wali-immigrate toka Zanzibar na Comoro kuja bara ktk utawala wake?..2. More converts kuingia Uislaam wakati wa Nyerere kuliko wakati wowote ule 3. Misikiti mingi kujengwa wakati wake. 4. Waganga wakubwa wa Viongozi wetu ikiwa ni pamoja na yeye walikuwa Masheikh wa kiislaam.

Na Mwisho imekuwaje leo hii viongozi wengi waislaam ndani ya CCM wana digrii ikiwa hawakupata nafasi ya kusoma wakati wa Nyerere?...

Go figure!
 
Wazee kuna watu walikuwa wanawashia moto suala la Nyerere kucontribute kwenye ukombozi wa kusini mwa Africa. Nimekuta hii article kwenye mtandao wa Tanzania wanaoishi Atlanta. Hivi kweli hapakuwa na haja ya kushiriki kuondoa hawa jamaa waliokuwa na fikira potofu namna hii kuhusu Waafrika?

Botha's Speech -1985

THE FOLLOWING is a speech made by former South African President P.W. Botha to his Cabinet. This reprint was written by David G. Mailu for the Sunday Times, a South African newspaper, dated August 18, 1985.

"Pretoria has been made by the White mind for the White man. We are not obliged even the least to try to prove to anybody and to the Blacks that we are superior people. We have demonstrated that to the Blacks in a thousand and one ways. The Republic of South Africa that we know of today has not been created by wishful thinking. We have created it at the expense of intelligence, sweat and blood. Were they Afrikaners who tried to eliminate the Australian Aborigines? Are they Afrikaners who discriminate against Blacks and call them Nigge*rs in the States? Were they Afrikaners who started the slave trade? Where is the Black man appreciated? England discriminates against its Black and their "Sus" law is out to discipline the Blacks. Canada, France, Russia, and Japan all play their discrimination too. Why in the hell then is so much noise made about us? Why are they biased against us? I am simply trying to prove to you all that there is nothing unusual we are doing that the so called civilized worlds are not doing. We are simply an honest people who have come out aloud with a clear philosophy of how we want to live our own White life.

We do not pretend like other Whites that we like Blacks. The fact that, Blacks look like human beings and act like human beings do not necessarily make them sensible human beings. Hedgehogs are not porcupines and lizards are not crocodiles simply because they look alike. If God wanted us to be equal to the Blacks, he would have created us all of a uniform colour and intellect. But he created us differently: Whites, Blacks, Yellow, Rulers and the ruled. Intellectually, we are superior to the Blacks; that has been proven beyond any reasonable doubt over the years. I believe that the Afrikaner is an honest, God fearing person, who has demonstrated practically the right way of being. Nevertheless, it is comforting to know that behind the scenes, Europe, America, Canada, Australia-and all others are behind us in spite of what they say. For diplomatic relations, we all know what language should be used and where. To prove my point, Comrades, does anyone of you know a White country without an investment or interest in South Africa? Who buys our gold? Who buys our diamonds? Who trades with us? Who is helping us develop other nuclear weapon? The very truth is that we are their people and they are our people. It's a big secret. The strength of our economy is backed by America, Britain, Germany. It is our strong conviction, therefore, that the Black is the raw material for the White man. So Brothers and Sisters, let us join hands together to fight against this Black devil. I appeal to all Afrikaners to come out with any creative means of fighting this war. Surely God cannot forsake his own people whom we are. By now every one of us has seen it practically that the Blacks cannot rule themselves. Give them guns and they will kill each other. They are good in nothing else but making noise, dancing, marrying many wives and indulging in sex. Let us all accept that the Black man is the symbol of poverty, mental inferiority, laziness and emotional incompetence. Isn't it plausible? therefore that the White man is created to rule the Black man? Come to think of what would happen one day if you woke up and on the throne sat a Kaff*ir! Can you imagine what would happen to our women? Does anyone of you believe that the Blacks can rule this country?

Hence, we have good reasons to let them all-the Mandelas-rot in prison, and I think we should be commended for having kept them alive in spite of what we have at hand with which to finish them off. I wish to announce a number of new strategies that should be put to use to destroy this Black bug. We should now make use of the chemical weapon. Priority number one, we should not by all means allow any more increases of the Black population lest we be choked very soon. I have exciting news that our scientists have come with an efficient stuff. I am sending out more researchers to the field to identify as many venues as possible where the chemical weapons could be employed to combat any further population increases. The hospital is a very strategic opening, for example and should be fully utilized. The food supply channel should be used. We have developed excellent slow killing poisons and fertility destroyers. Our only fear is in case such stuff came in! ! to their hands as they are bound to start using it against us if you care to think of the many Blacks working for us in our domestic quarters.

However, we are doing the best we can to make sure that the stuff remains strictly in our hands. Secondly, most Blacks are vulnerable to money inducements. I have set aside a special fund to exploit this venue. The old trick of divide and rule is still very valid today. Our experts should work day and night to set the Black man against his fellow man. His inferior sense of morals can be exploited beautifully. And here is a creature that lacks foresight. There is a need for us to combat him in long term projections that he cannot suspect. The average Black does not plan his life beyond a year: that stance, for example,should be exploited. My special department is already working round the clock to come out with a long-term operation blueprint. I am also sending a special request to all Afrikaner mothers to double their birth rate. It may be necessary too to set up a population boom industry by putting up centres where we employ and support fully White
young men and women to produce children for the nation. We are also investigating the merit of uterus rentals as a possible means of speeding up the growth of our population through surrogate mothers.

For the time being, we should also engage a higher gear to make sure that Black men are separated from their women and fines imposed upon married wives who bear illegitimate children.

I have a committee working on finding better methods of inciting Blacks against each other and encouraging murders among themselves. Murder cases among Blacks should bear very little punishment in order to encourage them.

My scientists have come up with a drug that could be smuggled into their brews to effect slow poisoning results and fertility destruction. Working through drinks and manufacturing of soft drinks geared to the Blacks, could promote the channels of reducing their population. Ours is not a war that we can use the atomic bomb to destroy the Blacks, so we must use our intelligence to effect this. The person-to-person encounter can be very effective.

As the records show that the Black man is dying to go to bed with the White woman, here is our unique opportunity. Our Sex Mercenary Squad should go out and camouflage with Apartheid Fighters while doing their operations quietly administering slow killing poison and fertility destroyers to those Blacks they thus befriend.
We are modifying the Sex Mercenary Squad by introducing White men who should go for the militant Black woman and any other vulnerable Black woman. We have received a new supply of prostitutes from Europe and America who are desperate and too keen to take up the appointments.

My latest appeal is that the maternity hospital operations should be intensified. We are not paying those people to help bring Black babies to this world but to eliminate them on the very delivery moment. If this department worked very efficiently, a great deal could be achieved.

My Government has set aside a special fund for erecting more covert hospitals and clinics to promote this programme. Money can do anything for you. So while we have it, we should make the best use of it. In the meantime my beloved White citizens, do not take to heart what the world says, and don't be ashamed of being called racists. I do not mind being called the architect and King of Apartheid. I shall not become a monkey simply because someone has called me a monkey. I will still remain your bright star...His Excellency Botha. "
In spite of all their plans and plots, the black man will continue to amuse the Whiteman because God Almighty is on our side. Out of our poverty we serve God better than them. So we will continue to educate ourselves because the Blackman you see today will not be the Blackman you see tomorrow.
Stay blessed and keep the faith.
 
Bob hakuna mahali tuliposema Mwalimu alikuwa mdini, swali lililoulizwa ni kwamba ni kwa nini enzi zake Waisilamu hawakusikia, kama walivyokuja kusikika baada ya Mwalimu kuachia uongozi tu,

Na mimi binafsi nimeshasema nimerdhika na majibu ya waungwana kabla yako, na nikasema kuwa nia yangu ilikuwa kuufufua huu mjadala wa Mwalimu ambao ulikuwa unaogopwa, sina kitendawili na huu ndio mchongo wangu wa mwisho katika hii issue!
 
mTz,
Hiyo hotuba tuliisikia na kwa bahati nzuri niliwahi kuiona ikirudiwa ktk 60minutes.. miaka mingi iliyopita. na tukumbuke kuwa wazungu wengi wanafikiria hivyo hata kama hawasemi mbele yetu.
Mzee ES,
Imetosha, nami nilikuwa najaribu kujibu hoja ambayo wengi waliiogopa kwa sababu inahusu dini zetu!..
 
quarz said:
Kwa Haraka Tu Nawakumbuka Waislam Hawa Waliwahi Kushika Nafasi Mbalimbali Kama Uwaziri Au Ubalozi Wakati Wa Mwalimu Nikikumbuka Nitakuja Na List Kamili
Rashid Kawawa
Chief Abdalah Fundikila
Thabit Kombo
Titi Mohamed
Amir Habib Jamal
Prof Mohamed Babu
Balozi.ally Mchumo
Ibrahim Kaduma
Makame Hasnu
Ali Hassan Mwinyi
Dk.salim Ahmed Salim
Anna Abdalah
Balozi Hassan Diria


Kati ya hao mbona hakuna listi ya wakristo?
 
Mzee Mkandara, maneno yako ni kweli kabisa tena inazidi kuchangiwa na zile picha za tv zikionyesha watoto waliovimba matumbo na mainzi uso mzima.
 
Mkandara I understand hutaki kuzungumzia udini anymore,before you go please help me on this,

4. Waganga wakubwa wa Viongozi wetu ikiwa ni pamoja na yeye walikuwa Masheikh wa kiislaam..........................waganga gani wa mifugo au binadamu?
 
Mtimanyongo aliowafanyia Waislam-Nyerere.


Tarehe 10/23/2006
SIASA
\MWANANCHI
Waislam: Hatuna cha kujifunza kutoka kwa Wakatoliki

Mohamed Said
IMEBIDI kuandika makala hii kutokana na makala iliyoandikwa na Kaanaeli Kaale yenye kichwa cha habari ‘Kusigana kwa matokeo baina ya shule za Kikatoliki na Kiislamu' (Mwananchi 17 Oktoba 2006). Makala ilikuwa inaeleza yaliyojadiliwa katika mkutano ulioandaliwa na Shirika la Elimu ya Sheria Tanzania (TANLET) katika moja ya harakati za kumuenzi hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Katika mkutano huo, ilielezwa kuwa shule za Kikatoliki ndiyo shule bora zinazoshika nafasi ‘kumi bora' kwa kutoa matokeo mazuri ya mitihani na shule za Kiislam ndiyo ‘zinazoshika mkia' katika kutoa matokeo mabaya.
Ama taarifa hizo za shule za Wakatoliki kufanya vyema katika mitihani si habari mpya ni jambo linalotangazwa na vyombo vya habari kila mwaka kwa hiyo linafahamika. Ila kitu cha kushangaza ni kuwa kimezidi nini hii leo hadi ikawa ni muhimu kujadili ufanisi wa shule za Waislam hadharani kisha tukapewa ushauri kuwa Waislamu tujifunze kutoka kwa Wakatoliki ili nasi shule zetu zifanye vyema kama zao ili huu upogo wa elimu kati ya Waislam na Wakristo utoweke?
Ushauri huu umenitia simanzi kubwa na ndiyo hasa sababu ya kuandika makala hii. Bubu alizungumza kwa uchungu wa mwanaWe ni msemo mashuri. Leo hii sisi Waislam tumekuwa watu wa kusaidiwa na Wakatoliki tuelimike! Waswahili tuna msemo ‘Akutukanae hakuchagulii tusi.'
Laiti hao wanaotushauri wengeijua tarikh (historia) yetu wasingetamka hayo. Wamishionari wameingia nchi hii wamewakuta babu zetu pwani yote ya Afrika Mashariki na bara kulikokuwa na Uislam wakijua kusoma, kuandika na kuhesabu. Lakini haya tuyaache yanahitaji muda kueleza. Turudi kwenye mada husika.
Awali ya yote ni kumkejeli hayati Mwalimu Julius Nyerere kwa kuadhimisha kifo chake kwa mkutano wa kuzungumza kubaki nyuma kwa Waislam katika elimu kwa kuwa, kwa kauli yake mwenyewe alisema kuwa upogo katika elimu baina ya Waislam na Wakristo uliorithiwa na serikali yake kutoka kwa Waingereza yeye ameuondosha katika kipindi cha utawala wake.
 
Kauli hii aliitoa Novemba 5, 1985 katika hotuba aliyoitoa Ukumbi wa Diamond Jubille akiwaaga Wazee wa Dar es Salaam. Kabla hajastaafu urais, Mwalimu Nyerere alikuwa na haya ya kueleza kuhusu suala la elimu ya Waislam:
"Waislam wametupa nafasi kupitia sera yetu ya elimu, kurekebisha upogo. Sasa nipo katika hali ya kufurahia kwa kuwa wakati mwingine sielewi kama mbunge mpya, waziri, au katibu mkuu katika wizara zetu za serikali, ni mwislam au mkristo au hana dini labda pale jina lake la kwanza linapotoa utambulisho. Na hata hivyo hiyo siyo njia ya kuaminika kutoa utambulisho wa dini kwa kuwa tuna wakristo wenye majina ya Kiislam, na waislam wenye majina ya Kikristo. Kuvumiliana huku ndiyo sababu; nilichofanya mimi ni kuzungumzia maadili haya kwa niaba yenu."
Sasa ikiwa Baba wa Taifa keshawanyanyua Waislam katika elimu na kafurahishwa na kazi yake nzuri, hawa wanaokuja leo na kusema kuwa Waislam wako nyuma wanataka kumshika uongo Mwalimu Nyerere?
Wanataka hii leo kumsimamisha Baba wa Taifa kizimbani ajibu tuhuma za kuwakandamiza Waislam katika elimu? Kwa hakika si adabu wala ustaarabu kupinga kauli ya Mwalimu Nyerere kuwa hakusema kweli katika tatizo la elimu ya Waislam.
Je, hawa waliokuja na hoja hii nyeti wanatambua uzito wa kauli zao hasa katika kipindi hiki ambapo Kanisa Katoliki lipo katika mchakato wa kumfanya Mwalimu Nyerere kuwa mtakatifu? Hivi hawasikii nchi nzima inavyomtukuza Mwalimu Nyerere kwa sifa za uadilifu? Majibu wanayo wenyewe. Hili la kwanza.
Waswahili tuna msemo mwingine "Asiekujua hakuthamini.' Historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika ni ushahidi wa juhudi za Waislam katika kujitafutia elimu. Wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika tatizo la elimu ya Waislam ndiyo chanzo cha kuanzishwa chama cha upinzani Tanganyika All Muslim National Union (AMNUT) pale akina Ramadhani Mashado Plantan na wenzake walipotoka TANU mwaka 1958, sababu kuu wakihofu Wakristo waliokuwa na elimu kuja kushika madaraka peke yao katika Tanganyika huru na kuwaweka Waislam pembeni.
Suala hili lilileta mjadala mkubwa katika TANU. Ukipenda unaweza ukarejesha msuguano huu ndani ya TANU nyuma kidogo mwaka huo huo wa 1958 pale Sheikh Suleiman Takadir (aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU Dar es Salaam) alipomkabili Nyerere uso kwa uso na kumtuhumu kwa udini.
Haya yalitokea baada ya Uchaguzi wa Kura Tatu pale TANU ilipoteua Wakristo kusimama kugombea nafasi za Legislative Council na kuwaweka Waislam wana TANU pembeni. Lakini katika hili palikuwa na sababu maalum za msingi. Hapa si mahali pake kuzieleza. Kipande hiki cha historia kinaogopwa sana na kwa ajili hiyo nami sitokiendeleza.
Baada ya uhuru kupatikana mwaka 1961 Waislam kwa pumzi ile ile waliyopigania uhuru wakaingia katika harakati za kutafuta elimu. Hawakusubiri wajengewe shule na serikali. Wazee wetu waliitisha mkutano chini ya taasisi zao - Daawat Islamiyya (Mwito kwa Waislam), Jamiatul Islamiya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika na Muslim Education Union kujadili nini kifanyike ili Waislam wapate elimu waliyodhulumiwa na wakoloni.
Mipango ikatayarishwa ya kujenga shule Tanganyika nzima na mwishowe kujenga Chuo Kikuu cha kwanza kwa Waislam katika Afrika ya Mashariki. Huu ndiyo ukweli wa historia ya Waislam.
Waislam hatuna sifa ya uvivu wala kusubiri misaada kutoka Ulaya. Ufupi wa maneno ni kuwa shule sabini zilijengwa na EAMWS na jiwe la msingi la Chuo Kikuu liliwekwa na Mwalimu Nyerere mwenyewe kwa mkono wake. Sasa la kujiuliza ni kuwa juhudi hizi zote za kutafuta elimu ziliishia wapi na nini sababu yake?
Ufupi wa mambo ni kuwa Mwalimu Nyerere alipiga marufuku jumuia zote za Kiislam mwaka 1968 na akwaundia Waislam Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata). Historia ya TANU na uhusiano wa Mwalimu Nyerere na Waislam ina majibu ya swali hili.
Mzee Rashid Mfaume Kawawa yu hai na ni shahidi wa yote yaliyopita katika kipindi kile. Mzee Kawawa anaweza kutoa majibu ya kitendawili hiki. Hili la pili.
Waswahili tuna msemo mwingine ‘Chokochoko mchokonoe pweza binadamu hutamuweza.' Imekuwa vyema leo hii, hili tatizo la elimu ya Waislam limesemwa na wasiokuwa Waislam maana laiti tungelisema Waislam tungeambiwa ‘siasa kali' tunataka kuvuruga ‘amani na utulivu' kama alivyosakamwa marehemu Profesa Kighoma Abdallah Ali Malima alipoionya serikali kuhusu hujuma dhidi ya Waislam kama alivyoikuta ndani ya Wizara ya Elimu.
Mwaka 1987 Profesa Malima aliteuliwa kuwa Waziri wa Elimu akiwa Muislam wa kwanza kushika nafasi hiyo. Mawaziri wanane waliopita walikuwa Wakristo. Kulikuwa na malalamiko kutoka kwa Waislam kuwa wizara hiyo imegeuzwa jimbo la Wakristo hasa Wakatoliki, maana ilifika hadi padri (Simon Chiwanga) kuteuliwa na Mwalimu Julius Nyerere kuongoza wizara hiyo.
Profesa Malima aliposhika wizara hiyo aliona upo umuhimu wa kufanya marekebisho kadhaa ili kurejesha imani ya Waislam katika wizara hiyo. Kulikuwa na tuhuma kuwa Wizara ya Elimu ilikuwa ikiwabagua vijana wa Kiislam kupata nafasi katika vyuo vya elimu ya juu na ilikuwa ikizuia kupanda vyeo kwa Waislam.
Tatizo hili liliwekwa wazi kwa mara ya kwanza mwaka 1981 na wanafunzi wa Sheikh Malik na ndiyo ikawa sababu ya yeye kufukuzwa nchini.
Profesa Malima alipoona dhulma ile iliyokuwapo katika wizara ile dhidi ya Waislam, aliwateua Waislam wanne kushika nafasi katika kurugenzi mbalimbali. Halikadhalika Profesa Malima alibadili mtindo uliokuwapo wa kutumia majina badala ya namba katika mitihani.
Baada ya mabadiliko yale mwaka ule idadi ya wanafunzi Waislam walifaulu kuingia sekondari ilipanda kwa asilimia 40. Profesa Malima akaandika taarifa ya siri kwa Rais Ali Hassan Mwinyi kumtaarifu udini ulioota mizizi Wizara ya Elimu.
Katika taarifa ile kwa rais Mwinyi, Profesa Malima alieleza kuhusu kudumazwa kwa Waislam kwa makusudi katika mgawo wa elimu. Taarifa hii ilivujishwa kwa vyombo vya habari na kwa Wakristo wengine.
Katika watu walioipata taarifa hii ni Mwalimu Nyerere akiwa mstaafu lakini akiwa Mwenyekiti wa CCM. Hiki kisa ni kirefu inatosha tu kusema kuwa yaliyomkuta Profesa Malima kwa kutaka kutenda haki hakuna asiyeyajua. Alisimamishwa kizimbani mbele ya Kamati Kuu ya CCM kwa udini na akatolewa Wizara ya Elimu.
Lakini kabla hatujatoka katika nukta hii ningependa kueleza kuwa katika moja ya sababu kuu iliyofanya serikali ikifungie kitabu kilichoandikwa na Profesa Hamza Mustafa Njozi Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania ni kule kuanika hadharani mbinu zinazotumika nchini kuwanyima Waislam elimu. Profesa Njozi's aliandika:
"…Arabia (May, 1985) wrote under the heading "A Closed Door to the Corridors of Power": ‘The majority of pupils in Tanzanian primary schools are Muslim (80 percent), a percentage which dwindles to 15-20 percent in secondary schools, sinking to a mere five percent at University level'. Almost fifteen years later, on 2 February, 1999 the Member of Parliament for Kigamboni Hon. Kitwana Kondo told the parliament that out of every 100 students who sat for the standard seven examination in Dar es Salaam in the year 1998, 71 were Muslim and 29 Christian. But out of every 100 students selected to join government secondary schools only 21 were Muslim while 79 were Christian. The MP wanted to know whether Muslim children were inherently dull (An-Nuur, February 5-11, 1999).
Yaliyomfika Mzee Kondo nayo yanafahamika. Yapo mengine mengi yaliyofichuliwa katika kitabu hicho yanayohusu mbinu zinazotumiwa katika kuhakikisha Waislam wanabaki nyuma lakini hapa hii leo si mahali pake. Hili la tatu.
Sasa leo Waislam tunaambiwa tukajifunze mbinu za Wakatoliki ili tuboreshe shule zetu…
 
tukajifunze mbinu gani? Kuhodhi madaraka na nafasi katika Wizara ya Elimu na kujipendelea kwa kuwanyima Wakristo nafasi za elimu ya juu? Hili ni muhali kwa Waislam.
Hata kama tungekuwa na uwezo nalo Uislam unakataza vyote kudhulumu na halikadhalika kukubali kudhulumiwa. Kwa Waislam elimu ni fardh jambo ambalo ni lazima litekelezwa na kwa kushindwa kufanya hivyo mja huandikiwa dhambi. Hatuhitaji kujifunza kwa yeyote yule kuhusu umuhimu wa elimu. Historia ya Waislam wa Tanganyika inapingana na dhana hiyo.
Sasa tuzungumze kuhusu matokeo mabaya ya shule za Waislam. Kwangu mimi kwa uzoefu wangu na yale ambayo nayaelewa kuhusu historia ya Waislam wa Tanganyika hili linahitaji uchunguzi zaidi ili tudhihirishe kuwa kweli shule za Waislam zinashika mkia na za Wakatoliki ndiyo zinazotawala ‘kumi bora' miaka nenda miaka rudi kwa haki au ndiyo hizo hizo mbinu alizotahadharisha marehemu Profesa Malima na Mzee Kondo akahoji katika Bunge na zilizosababisha kitabu cha Profesa Njozi kifungiwe na serikali ya Rais Benjamin William Mkapa?
Katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Wajerumani walikuwa wakiwakamata Wayahudi Poland na kwingineko Ulaya wakawatoa katika nyumba zao nzuri na kuwarundika katika ghetto. Umati mkubwa wa watu waliokuwa na nafasi na heshima zao katika jamii wakajikuta wanaishi katika sehemu finyu, chafu isiyo na mifereji ya maji taka wala maji safi.
Wajerumani wakawa wanatuhumu na kuwakashifu Wayahudi kwa uchafu. Katika hali kama hiyo vipi utategemea mtu awe msafi? Huu ndiyo mfano wetu Waislam hii leo.
Hatuna fursa sawa kama walizonazo Wakristo, shule zetu duni na juu ya hayo bado tunahujumiwa kisha tunalaumiwa kwa kutotoa matokeo mazuri. Hili la nne ambalo ningependa lizingatiwe.
Kwa taarifa kwa wale wasiojua ni kuwa Organisation of Islamic Conference (OIC) walitaka kujenga Chuo Kikuu Dar es Salaam. Watendaji Wakristo katika Wizara ya Elimu walipiga vita mradi huo na mwisho chuo hicho kikajengwa Mbale, Uganda.
Darul Iman ya Saud Arabia ilitaka kujenga shule ya ufundi Kibaha na yale yaliyoikuta OIC na wao yaliwafika sawia. Huu ndiyo ukweli wa nchi yetu. Waswahili tunapokabiliwa na mtu mwingi wa mbinu na ghilba tuna msemo maarufu tunautumia kumweleza mtu huyo. Tunasema ‘Kwa nyakanga hakwishi nyimbo.'
Kichwa kinaniuma kutaka kujua hii agenda ya kudumazwa kwa Waislam katika elimu iliyozuka ghafla bin vuu ni ya nani hasa, yao wenyewe TANLET au wametumwa na mtu? Kama wametumwa, nani huyu kawatuma na kwa maslahi ya nani?
Agenda hii si ndiyo iliyomfanya Profesa Malima aandamwe na hatimaye kufukuzwa Wizara ya Elimu? Agenda hii si ndiyo iliyomfanya Mwalimu Nyerere amfukuze Tanzania Bara Mufti Sheikh Hassan bin Ameir na kumrejesha Zanzibar chini ya ulinzi mkali na kuwaweka kizuizini wafuasi wake?
Agenda hii si ndiyo iliyomfanya Sheikh Hussein Malik afukuzwe nchini na serikali ya Mwalimu Nyerere baada ya wanafunzi wake kupitia taasisi yao ya Waandishi wa Kiislam (Warsha) kuzungumza kuhusu tatizo la elimu ya Waislam? Hii leo kimebadilika nini? Wakati una majibu kwa kila jambo, Waislam tusubiri.
 
Mswahili,
Unajua mwandishi huyu anachekesha sana!..Nina hakika umei-copy sehemu ktk magazeti yao haooo, ma -colored. Yaani bado ana mpango wa kuwa shule ile ilijengwa na muislaam, sijui mwarabu. Huu ni kweli kumtekenya pweza...sielewi kabisa ikiwa waislaam walijenga shule sabini inahusiana nini na Watanzania!. Kama mlijenga ni kwa sababu ya kutoa ELIMU kwa wote kama walivyojenga wakristu sijui mia ngapi.
Ni aibu kubwa kwa mtu kuweka maelezo kama haya kwa sababu kati ya kila waislaam kumi kama sio 100 waliosoma na kupata elimu ni mmoja tu alisoma shule iliyojengwa na muislaam. Huko mikoani atwambie hizo shule anazozungumzia.. shule 70!...What a crap.....
Shule nyingi Tanzania zimejengwa na wanaume kwa hiyo mnataka kusema sii vizuri wanawake wapate ELIMU ama kuwa na kiongozi mwanamke ktk shule hizo?..
Kuzungumzia swala hili ukitazama rangi za dini ni ujinga mkubwa sana ambao hata wewe unaejiita MUISLAAM unakuondoa UISLAAM.
Nini maana ya Muislaam kama sio kujisalimisha kwa Mola wako! na kuepuka kueneza chuki baina ya watu!...wangapi kati yenu kweli wameshika ibada kama sio UISLAAM wenu wa majina..
Wapuuzi sana nyie ma mwinyi msiokuwa na haya zaidi ya kuona rangi zenu. Na ni nyie nyie mnaodai kuwa sii Waafrika ila Wabarush, Islamilia, mara Wa -Yemen. Na sii kazi mkasema shule hizo zimejengwa na waarabu sio Waafrika..
Matatizo yote tunayopata waislaam yanatokana na watu kama nyie ambao midomo inawawasha sana kusema nyumba za wengine hali zenu wenyewe zinaota majani hadi ktk paa. Na hata kama mimi ningekuwa Nyerere ningewafukuza nchini, kwa sababu kama kweli hamkwenda shule mbona mnaweza kuandika yote haya...Na kibaya zaidi nyote mna umri wa zaidi ya miaka 40 na mmefika vyuo vikuu... Mlifika vipi huko ikiwa Nyerere aliwazuia?
 
Lakini yote ni kwa sababu serikali pamoja na wanasiasa waliliingilia sana mambo ya imani za watu

Pili ni kuwa walipokuwa wakiambiwa kuna malalamiko hakuna aliekuwa tayari kukaa nao chini kuwasikiliza.

Sasa serikali gani iliyokuwa perfect duniani? Hakuna lakini at least wange acknowledge kuwa tatizo lipo na kuangalia jinsi gani ya kutafutia ufumbuzi nadhani tusingekuwa na mijadala hii humu ndani

Sasa hata hivyo its never too late kukubali kuwa makosa yalifanyika along the way na wanajaribu kuyatafutia ufumbuzi

N a ufumbuzi hauanzi kwa wanasiana kuwaambia watu waoe wake wangapi au wale iddi lini after all kila mtu na imani yake
 
Dr. Who,

Tutazungumzia swala ambalo ni tatizo leo hii na kulitafutia suluhu na sio kurudisha mambo ya nyuma baada ya mashahidi wenyewe Kuondoka duniani... Ni hawahawa Washirikina waliozua kwamba Kighoma Malima alihamia CUF wakitafuta sifa za udini..yaani wakimaanisha Kighoma Malima kama muislaam karudi nyumbani!..Hii haina picha nzuri kwa CUF isipokuwa kukifanya chama hiki sii cha kisiasa ila ni chama cha kidini.... Kumbe ukweli sivyo!
Kwanza kuhama ama kuongea na CUF ni jambo ambalo halikuwa na ukweli na hata kama Malima angekuwa kafanya hivyo kweli ingesemwa ni ktk siasa. Makosa yapo kwa hawa wanaoeneza chuki na ndio tunatakiwa tuwazungumzie ktk mijadala kama hii.
Yote wanayotuletea ni baada ya Kighoma Malima kufa!...hakuna ushahidi wa kweli isipokuwa wao..mbona msiyaseme haya akiwa hai.!
Na mimi nataka sana kuwauliza wao ilikuwaje huyu Muislaam wenu Mwinyi alipitisha mateso na hata kifo cha Sheikh Kassim Bin Juma?... Msivyokuwa na aibu mnamsingizia waziri wa mambo ya ndani wakati huo Mrema kuwa ndiye aliyemuua sheikh Kassim hali ni kwa ruksa ya rais - mtu kushtakiwa na kuteswa kwa tuhuma za ugaidi.
Je, kuna kati yetu aliyekaa na kuuliza ni kitu gani Sheikh Kassim alikuwa akikipinga ktk utawala wa Mwinyi?... NO hamtaki.. sababu ati Mwinyi ni Muislaam mwenzenu na Sheikh Kassim sijui yeye nani! Angekuwa Nyerere hapo mngeyasema yote na mengine kuongezea!..
Dr . hakuna kabisa mapungufu wakati wa Nyerere kwa waislaam isipokuwa wao wenyewe...
Leo hii pamoja na uhuru waliokuwa nao ni shule ngapi wamejenga?...hata kusimamisha community zao wanashindana wenyewe na kubishana kila siku. Wametusambaratisha waislaam nchini hadi leo hatufahamu siku ipi kweli ni sikukuu ya Idd! yaani dini wameigeuza kuwa biashara. Wajinga tu hawa...
Tazama tena mfano wa hapo juu! kisha tazama nje ya dini...mathlan, Ukitaza nyumba zote za miji yetu zilijengwa na wahindi. Zikataifishwa kwa sababu ya kisiasa na sio kwa sababu ya rangi zao. They can think, claim whatever!
Leo hii hao wahindi wakiweka madai yao ya dharau kama alivyoandika huyo mshirikina hapo juu sijui kama tungekaa hapa na kuona umuhimu wa kujadili swala hili..tena wapo wahindi wanaoamini kuwa bila wao tusingekuwa hapa tulipo.
Unapojenga nyumba, shule, hospitali ama ujenzi wowote ule kwa maendeleo ya Umma jina lako linabaki kama bango tu. Ni vizuri kufikiria Utaifa kwanza kabla ya tofauti za kimakabila, dini, gender na kadhalika kwani hakuna mtu kati yao aliyejenga shule akikusudia sifa ila maendeleo ya watu.
Sasa sisi nani wa kuweka sura mpya ya ujenzi huo hali shule hizo tumezikuta.
ndio hawa hawa wanaoutangaza ubora wa kiongozi kutokana na dini zao, kabila zao wakati kiongozi huyo kaboronga. Na ni hawa hawa wanaodai kuwa Uislaam ni uarabu...they are colored. Kwani hatufahamu wanvyoongea hata kiswahili chao....Slam aleikum ndio imewashika midomoni kuliko - Hamjambo!

Mwinyi.. kafanya nini? kama sii mume aliyekuja rithi mali za Nyerere na kumhemea sana mama yetu Tanzania.
 
Mkandara
Naona huna hoja za msingi,
Kwanza kabisa Malima hajawahi kuwa Cuf acha uongo mzee! Malima alikuwa NRA,
sheikh Kassim Bin Juma alifungwa kwa dhamana ya Nyerere na hata ugomvi wake Kassim bin Juma ni dhidi ya Nyerere fuatilia ripoti yote ya marehemu.

Uonezi wa Nyerere kwa waislam uliwekwa wazi na alipelekewa nyerere na 1995 Mzee Abood Jumbe Mwinyi aliandika kitabu miaka 30 ya dhoruba za Nyerere, 1998- kitatoka kitabu cha Mwembe chai, pia kitatoka kitabu cha Sykes-Abdul- wahid na kuweka wazi yote ya Nyerere akiwa hai huyo Nyerere, hakukanusha madai haya, hivyo basi hoja hizi hazikuja baada ya yeye kufa laa, alipewa akiwa hai.ina maana Mzee Jumbe atamdhuria Nyerere? na aliweka jina lake halisi hakutumia mkandara au mswahili kwa uoga na ukweli wa anayosema.
Mwembachai kimeandikwa na profeesor tena ni head wa department-UDSM na ma dr. wakristu wamechangia na kukubali yaliyomo. kama ni uzushi why serikali ilikizuia bila ya kusema sababu au uandishi uliopo ni wa uongo kwa wanabodi kitabu hiki kinatatika kwenye mtandao hakiruhusiwi kutia mguu TZ.
Mkandara sikiliza mawaidha ya marehemu sheikh Kassimu shutuma zake zote zilikuwa kwa nyerere.
na pia hata Malima aliyemuua ni Nyerere kwani Malima alitiliwa sumu hotelini Nairobi kwenye viatu na hadi anafika london akapata mauti.
Malima alikuwa mfuasi mzuri wa nyerere lakini aliyoyakuta wizara ya elimu akamuona nyerere ni nyoka mkubwa.
 
Mswahili.
Sasa huu ni uzushi kama si upuuzi. Nyerere alifikaje kwenye hoteli ya Malima Nairobi na kumwekea sumu kwenye viatu?
 
Kwa kuhitimisha shutuma zako wewe Mswahili unataka kufanya nini ? Waislam wenzio wanataka kulipa kisasi Mnaendelea kubishana sana na Mkandara kasema badala ya kukaa chini na kujipanga ili mfanye mambo ya maana mtu wa aina yako ama Waislam wa aina yako wanalumbana na watakuta tena wamechelewa karne zijazo mtaanza kulia na Mkapa sijui kwamba hakuwapenda Waislam? Fanyeni kazi maana madai yenu ni ya Uongo. Kama kuna Waislam walizuia kusoma waliopo madarakani Tanzania walisomea Nchi gani ya kiarabu ?
 
duh!
hivi wewe mswahili unamatatizo gani? inaonekana umechelewa kweli ndugu!
hivi kweli wewe hauna hata haya kumtetea kigoma malima, ambaye alikutwa na mambilioni ya pesa kazitorosha nje??
hizo pesa aliibia serikali ya jamuhuri ya muungano wa tanzania na zikawa freezed na serikali fulani ya ulaya ndio kilichomuua kighoma malima,
malima is one of the worse finance mininster we have ever had in this country.
 
Back
Top Bottom