Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

All I ca say
- NDIVYO TULIVYO!
Kama sii Nyerere basi lazima itakuwa mkoloni, lakini sio sisi wenyewe!

....ndivyo tulivyo ndio maana mpaka leo bado tunamtukuza marehemu na kumtetea kwa jasho letu na damu yetu yoooote! kushindwa kukubali kwamba Nyerere's leadership ndio chanzo na mwanzo wa uozo huu wote ni prove tosha ya mtindio wetu( @least kwa walio wengi) wa ubongo!....
 
Mtamlaumu Mwalimu (RIP) kwa mambo ambayo yalikuwa nje ya uwezo wake. Watu wengi hawajui yaliyokuwa yanaendelea nyuma ya pazia.

Kwa kifupi tu ni kwamba Mkoloni hakuondoka Tanganyika na Afrika nzima kwa ujumla moja kwa moja. Wazungu waligundua kwamba kuitawala Afrika moja kwa moja ni gharama zaidi. Kwa hiyo wakatupa uhuru wa kisiasa lakini wakaendelea kuitawala Afika kupitia mlango wa uani.

Angalia nchi zote ambazo wazungu walishajiimarisha kiuchumi, hawakuondoka kirahisi, au hawakuondoka kabisa, kama vile Zimbabwe, South Africa, Mozambique na Namibia. Ila kwa nchi hizi zetu ambazo walijua kabisa wanaweza kuondoka na kuendelea kututawala kwa kutunga sera za fedha na uchumi kupitia Word Bank na IMF, waliondoka.

Inasemekana kwamba karibu kila kitu alichokuwa anafanya Mwalimu alikuwa analetewa na Waingereza. Hii ni kuanzia siasa ya ujamaa na kujitegemea na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kumbukeni kipindi kile kulikuwa na vita baridi kati ya Magharibi na Mashariki. Waingereza walikuwa wanafuata mfumo wa kibepari. Hivyo walichofanya ni kuchagua baadhi ya yaliyokuwa makoloni yao yaliyoko Afrika kwa ajili ya kufanyia majaribio ya mfumo wa Ujamaa. Viwanda vingi vilivyojengwa wakati wa Nyerere misaada yake ilitoka Uingereza. Kwa kifupi miaka yote hiyo nchi yetu ilikuwa kama "case study" ya mfumo wa ujamaa kwa Waingereza. Who knew? Pengine Ujamaa ungeweza kufanikiwa na ubepari kufa.

Nchi za Kiafrika ambazo viongozi wake walionekana wana kihere here cha kutaka kuleta maendeleo waliuawa katika mazingira ya kutatanisha. CIA walimuua Lumumba kule Congo na kuweka kibaraka wao Mobutu. Sasa hivi Wamarekani wamejaa huko wanafanya "mineral prospecting". Kwa kifupi Congo ilikuwa imehifadhiwa kwa ajili ya kuwa chanzo cha malighafi na madini kwa ajili ya Wamarekani. Na ndivyo ilivyokuwa kwa nchi nyingi za Kiafrika ikiwemo Tanzania.

Nyerere msimlaumu sana! He was being controlled by the British. Maamuzi mengi yalikuwa nje ya uwezo wake, na pia kuna mambo mengi mazuri yaliyokuwa ndani ya uwezo wake ambayo aliyafanya.
 
Dogo:

Kuna unayoyasema yana ukweli wake na mengine ni CONSPIRACY THEORIES. Na hatutajenga nchi hii ya mababu zetu kwa ku-play victim cards.

Tukitaka kuendelea ni lazima tujifunze kushinda katika michezo yao (beat x, y, z at their own game).

Uhuru wa Tanzania ulikuwa kamili na sio wa bendera na hakuna sababu yoyote ya kusema kuwa waingereza wali-control nchi. Makosa yaliofanyika ni ku-underestimate uwezo wa nchi zilizotutawala.
 
Bin Maryam,
Ndivyo tulivyo kwa sababu kila siku hatukossi kisingizio! ikiwa ni pamoja na mimi hapa.
Na kutokana na fact hii inanilazimu kutaka kuamini maneno ya The truth kuwa pengine yawezekana sisi tuna upungufu wa IQ tofauti na imani yangu ya mwanzo kuwa sisi Wadanganyika tuna mapungufu ktk Elimu kiasi kwamba tumefungwa ktk ujinga na kuwa Wapuuzi (negligence) na wazembe (incompetent).
Lakini napoona mawazo yanayojaribu kumlinda mpuuzi na mzembe kwa visingizio vya wale waliotangulia hali leo hii wakiwa nje ya zizi hilo bado wamefungwa kamba ama minyororo miguuni utadhani mnyama aliyefungwa nyumbani kisha akaachiwa huru porini akashindwa kujitegemea.
Mwanzo sikukubaliana na huyo mshirika kwa sababu moja kubwa kuwa IQ ni uwezo mkubwa wa akili kuweza kufikiria kabla ya kusema, kutunga, kuelekeza ama kutenda yale yenye mwelekeo wenye mafanikio katika mazingira yoyote yale tofauti na yule (sisi)wenye uwezo huo lakini hupuuza mazuri kutokana na uzembe.

Leo hii Nyerere kisha kufa miaka 10 iliyopita, wengine wooote (China, Russia, Vietnam na hata Ethiopia) walimeweza fanikiwa na kuna tofauti kubwa toka waanze kuupokea Utandawazi tena walikuwa na siasa kama yetu iliyotawaliwa na chama kimoja kama sisi lakini wao wameweza kuona mwanga tena basi wakiendelea kutumia chama kimoja tu. Hivi kweli sisi tunashindwa kipi hapa kiasi kwamba leo hii tunamyooshea kidole mwalimu hali hakuna hata moja ya hili tunalolizungumza lilikuwa na baraka zake.

1. Ni Nyerere aliyeanzisha vyama vya upinzani tofauti kabisa na nchi nyingine za Kijamaa.. pengine hilo ni kosa la kwanza naomba ufafanuzi.
2. Ni Nyerere alituasa kuhusu Lowassa na hata Kikwete lakini sisi wenyewe tulitunga ngojera zetu kuwatukuza na hata ndani ya CCM wenyewe wanaelewa wazi kuwa haya yalikuwa mapinduzi baridi ndani ya chama chenyewe CCM..
3. Ni mabadiliko yaliyopingana na Nyerere aliyoyaonyesha Mwinyi ktk awamu yake ya pili ambayo wengi mliyakumbatia bila kufahamu kwamba Kiuchumi fedha zinapokuwa nyingi mitaani hua zinaharibu uchumi wa nchi...Kwa wadanganyika mlisherehekea bila kufahamu hatma ya TZ kiuchumi.
3. Ni mabadiliko yaliyopingana na imani ya mwalimu kuhusu Mkapa kabla ya awamu yake ya Pili, jambo ambalo lili cost maisha yake, yet sisi wote kwa kura zetu tuliendelea kumtukuza na kumpa kura za kumwezesha kuiba. Naikumbuka vizuri hotuba ya mwalimu alipotembelea hapa kutuonyesha wazi kuwa Mkapa hakufaa kushika awamu ya pili na alidiriki hata kuapa kwamba hatutaweza toka ktk umaskini hata kama tutapata mafuta!..
 
Bin Maryam,
NDIVYO TULIVYO!... nakuomba unisikilize kwa makini pamoja na kwamba inauma.

Mkuu binafsi nilikuwa naamini sana Ndivyo Tulivyo ikiwa na maana ya kuwa sisi Wadanganyika tumefungwa ktk lindi la Ujinga ambao kwa nguvu zake tumeweza kuwa taifa la Wapuuzi (negligent) tuliojaa Uzembe (Incompetent) hivyo kushindwa kujikwamua ktk lindi hili la Umaskini. imani yangu siku zote dawa kubwa ya kumkomboa Mdanganyika inabidi kwanza elimu ipewe nafasi kubwa kuliko vitu vingine vyote!.

Lakini ikiwa elimu yenyewe ndio hii, elimu ya kunyooshea vidole watu waliokwisha kufa miaka 10 iliyopita kuwa ndio sababu kubwa ya ezembe huu inanifanya nianze kutaka kuamini maneno ya The truth kuwa labda pengine SIVYO TULIVYO ila tumepungukiwa na kitu kimoja muhimu zaidi ktk bongo zetu - IQ.
Nakuomba unielewe hapa kuwa maelezo yangu hayatokani na maelezo yenu yaliyotangulia, isipokuwa ni uwezo wetu sisi wasomaji kutofikiria nje ya somo hilo mlilolitoa na kuona kwamba hakuna ukweli ktk maneno hayo isipokuwa ni hoja za mzee kajamba anayetafuta wa kumshutumu (kwa makusudi kabisa)- kwa msemo wa kibara tunaita Uswahili...Uswahili ni wale wasiokosea wao ila wengine na kama wameshindwa kitu basi lazima kuna mkono wa mtu.

Kama utakumbuka nimewahi zungumzia hili huko nyuma, nikaonyesha wazi kuwa nchi kama China, Russia, Vietnam na hata Ethiopia leo hii wanapiga hatua Kiuchumi na hakuna ujinga kama huu tena chini ya chama tawala kimoja, inakuwaje sisi tushindwe kuvuta hatua hata moja badala yake tunavuta tenzi na historia mabyo kiutawala imekwisha pitwa na wakati?. Tanznaia inazidi kuwa chini ktk daraja la dunia ktk nchi maskini pamoja na jitihada zote hizi.. why? hivi kweli ni Nyerere ama mkoloni wa kuwashutumu?..

Je, si Nyerere aliyeanzisha vyama vingi nchini nje kabisa ya matakwa ya chama CCM pamoja na kwamba nchi za Kijamaa ziliacha kufuata mfumo hata walipoweza badilisha mwelekeo wa nchi zao kiuchumi kwa sababu unapingana na dira yao ya kitaifa. Je kosa lake ni kuanzisha vyama vingi ama kuanzishwa/kuwepo kwa CCM..
Na Nyerere mwenyewe alituambia kuwa chama pinzani kitatoka CCM, tumejaribu nje ya hapo tumegonga ukuta mara kibao, leo hii tunashindwa nini kujaribu kujikata toka CCM!... hali wengi wanaoandika humu ni wanachama halisi wa CCM, chama wanachokitupia madongo wakisingizia viongozi..
Je, sio Nyerere aliyetuasa kuhusu Lowassa na hata Kikwete lakini kura zetu ndizo zilizowapa uwezo wa kutawala tena kwa sifa kubwa zaidi ya kiongozi yeyote yule maanake Nyerere aliweza pata kura asilimia 80 ama zaidi akishindana na Ukuta!

Je, sii Nyerere aliyetuasa kuhusu Mkapa kabla ya awamu yake ya pili lakini sisi wenyewe tuliendelea kumchagua na matokeo yake ndio hayoo! Nakumbuka vizuri hutuba yake Mwalimu alipotembelea hapa mbali na yale nayoyafahamu mimi kutokana na source zangu. Kumbuka tu kama utataka uhakika fulani wa maelezo yangu ambao siwezi kuuweka hapa nakuomba ujue tu (hint) kuwa unazungumza na Mkerewe.

Sasa wakuu wangu ikiwa kweli mnaamini haya na wengine mnaanza kuvutwa na mtazamo huu inanibidi nianze kuogopa kuwa yawezekana kuwa tunasoma biblia mbili tofauti..na kama Agano la Kale haliwezi kuwa na mabadiliko ama nyongeza kutokana na Agano jipya ili kutuwezesha zaidi kufanya ibada hii ya maendeleo ya kiuchumi basi mkuu tuna tatizo kubwa zaidi...

Kumradhini lakini ndio ukweli usiokubalika!
 
Mtamlaumu Mwalimu (RIP) kwa mambo ambayo yalikuwa nje ya uwezo wake. Watu wengi hawajui yaliyokuwa yanaendelea nyuma ya pazia.

Kwa kifupi tu ni kwamba Mkoloni hakuondoka Tanganyika na Afrika nzima kwa ujumla moja kwa moja. Wazungu waligundua kwamba kuitawala Afrika moja kwa moja ni gharama zaidi. Kwa hiyo wakatupa uhuru wa kisiasa lakini wakaendelea kuitawala Afika kupitia mlango wa uani.
Hii habari ya kusema "waligundua kutawala Afrika moja kwa moja ni gharama zaidi" badala ya kukubali ukweli kuwa wananchi walidai uhuru wao ni sawa na kuwatusi waliojitoa kudai uhuru, Nyerere akiwa mmoja wao. Mkoloni alijua fika kuwatawala Watanganyika wanaodai uhuru(kumbuka walishaonja joto ya Mau Mau Kenya na kupingwa vikali kwenye makoloni yao mengine wakati huo) itakuwa mbinde hivyo hawakuwa na jinsi ila kufunga virago.

Angalia nchi zote ambazo wazungu walishajiimarisha kiuchumi, hawakuondoka kirahisi, au hawakuondoka kabisa, kama vile Zimbabwe, South Africa, Mozambique na Namibia. Ila kwa nchi hizi zetu ambazo walijua kabisa wanaweza kuondoka na kuendelea kututawala kwa kutunga sera za fedha na uchumi kupitia Word Bank na IMF, waliondoka.
Kumbuka Nyerere aliwakoromea na kuwagomea hao IMF, WB (wakati Mtei waziri wa fedha in the 70's) hivyo hii nayo siyo hoja, kudai vinginevyo ni kupotosha ukweli.

Inasemekana kwamba karibu kila kitu alichokuwa anafanya Mwalimu alikuwa analetewa na Waingereza. Hii ni kuanzia siasa ya ujamaa na kujitegemea na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kwa maneno mengine hapa unamaanisha kuwa Nyerere alikuwa kibaraka wa Waingereza, pamoja na kuwa siafikiani na baadhi ya sera zake lakini hapa mkuu you are totally out to lunch, hakuna chembe ya ukweli hapo, hiyo ni pure fiction maana hata sentensi yako imeanza na neno "inasemekana".

Kumbukeni kipindi kile kulikuwa na vita baridi kati ya Magharibi na Mashariki. Waingereza walikuwa wanafuata mfumo wa kibepari. Hivyo walichofanya ni kuchagua baadhi ya yaliyokuwa makoloni yao yaliyoko Afrika kwa ajili ya kufanyia majaribio ya mfumo wa Ujamaa. Viwanda vingi vilivyojengwa wakati wa Nyerere misaada yake ilitoka Uingereza. Kwa kifupi miaka yote hiyo nchi yetu ilikuwa kama "case study" ya mfumo wa ujamaa kwa Waingereza. Who knew? Pengine Ujamaa ungeweza kufanikiwa na ubepari kufa.
Duh! Sasa naona umefikia mahali unatunga hadithi kuchangamsha baraza, yaani Uingereza wanaofuata mfumo wa kibepari leo waamue kufadhili majaribio ya mfumo wa ujamaa? Au mkono uliteleza tu pengine ulitaka kuandika Urusi? Halafu kwa kukusaidia tu, viwanda kama UFI, Urafiki n.k. vilijengwa kwa misaada toka China.

Nchi za Kiafrika ambazo viongozi wake walionekana wana kihere here cha kutaka kuleta maendeleo waliuawa katika mazingira ya kutatanisha. CIA walimuua Lumumba kule Congo na kuweka kibaraka wao Mobutu. Sasa hivi Wamarekani wamejaa huko wanafanya "mineral prospecting". Kwa kifupi Congo ilikuwa imehifadhiwa kwa ajili ya kuwa chanzo cha malighafi na madini kwa ajili ya Wamarekani. Na ndivyo ilivyokuwa kwa nchi nyingi za Kiafrika ikiwemo Tanzania.
Hapa unachanganya ndimu na maembe, viongozi kazi yao ni kuongoza wananchi wawe na maisha bora zaidi na ndio maendeleo hayo, hivyo kila kiongozi ana wajibu huo, hakuna cha kiherehere wala nini, ndio maana wanapoomba kura wanaahidi mambo ya kimaendeleo watakayoyatekeleza. Kauli yako imegubikwa na taswira ya dharau kwa viongozi wanaojitahidi kuwaletea wananchi wao maendeleo. Kuuwawa kwa Lumumba ilikuwa ni kuhusiana na vita baridi vya wakati ule ambapo nchi za magharibi (US na Ulaya Magharibi) na nchi za kikomunisti/kijamaa (Urusi, Uchina, Cuba, Ulaya Mashariki) zilikuwa zinajitahidi kushindana kuvutia nchi zinazoendelea kufuata mifumo yao. Sasa ungekuwa unataka kumtetea vizuri Nyerere basi ungekumbuka kuwa alikuwa kati ya waasisi wa Non Aligned Movement (NAM), yaani Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote. Ndio maana Tanzania tuliweza kuwa na uhusiano mzuri na Urusi, Marekani, Uchina, Uingereza, Cuba n.k bila kulazimika kuegemea upande mmoja tofauti na wenzetu Wakenya, kwa mfano. Kwa hili pia Nyerere alionyesha msimamo tofauti na madai yako.

Nyerere msimlaumu sana! He was being controlled by the British. Maamuzi mengi yalikuwa nje ya uwezo wake, na pia kuna mambo mengi mazuri yaliyokuwa ndani ya uwezo wake ambayo aliyafanya.
Unarudia tena kumdhalilisha Nyerere. Kwa taarifa yako Nyerere hajawahi kuwa kibaraka wa Uingereza hata siku moja, tafuta jingine.
 
Bin Maryam,
NDIVYO TULIVYO!... nakuomba unisikilize kwa makini pamoja na kwamba inauma.

Mkuu binafsi nilikuwa naamini sana Ndivyo Tulivyo ikiwa na maana ya kuwa sisi Wadanganyika tumefungwa ktk lindi la Ujinga ambao kwa nguvu zake tumeweza kuwa taifa la Wapuuzi (negligent) tuliojaa Uzembe (Incompetent) hivyo kushindwa kujikwamua ktk lindi hili la Umaskini. imani yangu siku zote dawa kubwa ya kumkomboa Mdanganyika inabidi kwanza elimu ipewe nafasi kubwa kuliko vitu vingine vyote!.

Lakini ikiwa elimu yenyewe ndio hii, elimu ya kunyooshea vidole watu waliokwisha kufa miaka 10 iliyopita kuwa ndio sababu kubwa ya ezembe huu inanifanya nianze kutaka kuamini maneno ya The truth kuwa labda pengine SIVYO TULIVYO ila tumepungukiwa na kitu kimoja muhimu zaidi ktk bongo zetu - IQ.
Nakuomba unielewe hapa kuwa maelezo yangu hayatokani na maelezo yenu yaliyotangulia, isipokuwa ni uwezo wetu sisi wasomaji kutofikiria nje ya somo hilo mlilolitoa na kuona kwamba hakuna ukweli ktk maneno hayo isipokuwa ni hoja za mzee kajamba anayetafuta wa kumshutumu (kwa makusudi kabisa)- kwa msemo wa kibara tunaita Uswahili...Uswahili ni wale wasiokosea wao ila wengine na kama wameshindwa kitu basi lazima kuna mkono wa mtu.

Kama utakumbuka nimewahi zungumzia hili huko nyuma, nikaonyesha wazi kuwa nchi kama China, Russia, Vietnam na hata Ethiopia leo hii wanapiga hatua Kiuchumi na hakuna ujinga kama huu tena chini ya chama tawala kimoja, inakuwaje sisi tushindwe kuvuta hatua hata moja badala yake tunavuta tenzi na historia mabyo kiutawala imekwisha pitwa na wakati?. Tanznaia inazidi kuwa chini ktk daraja la dunia ktk nchi maskini pamoja na jitihada zote hizi.. why? hivi kweli ni Nyerere ama mkoloni wa kuwashutumu?..

Je, si Nyerere aliyeanzisha vyama vingi nchini nje kabisa ya matakwa ya chama CCM pamoja na kwamba nchi za Kijamaa ziliacha kufuata mfumo hata walipoweza badilisha mwelekeo wa nchi zao kiuchumi kwa sababu unapingana na dira yao ya kitaifa. Je kosa lake ni kuanzisha vyama vingi ama kuanzishwa/kuwepo kwa CCM..
Na Nyerere mwenyewe alituambia kuwa chama pinzani kitatoka CCM, tumejaribu nje ya hapo tumegonga ukuta mara kibao, leo hii tunashindwa nini kujaribu kujikata toka CCM!... hali wengi wanaoandika humu ni wanachama halisi wa CCM, chama wanachokitupia madongo wakisingizia viongozi..
Je, sio Nyerere aliyetuasa kuhusu Lowassa na hata Kikwete lakini kura zetu ndizo zilizowapa uwezo wa kutawala tena kwa sifa kubwa zaidi ya kiongozi yeyote yule maanake Nyerere aliweza pata kura asilimia 80 ama zaidi akishindana na Ukuta!

Je, sii Nyerere aliyetuasa kuhusu Mkapa kabla ya awamu yake ya pili lakini sisi wenyewe tuliendelea kumchagua na matokeo yake ndio hayoo! Nakumbuka vizuri hutuba yake Mwalimu alipotembelea hapa mbali na yale nayoyafahamu mimi kutokana na source zangu. Kumbuka tu kama utataka uhakika fulani wa maelezo yangu ambao siwezi kuuweka hapa nakuomba ujue tu (hint) kuwa unazungumza na Mkerewe.

Sasa wakuu wangu ikiwa kweli mnaamini haya na wengine mnaanza kuvutwa na mtazamo huu inanibidi nianze kuogopa kuwa yawezekana kuwa tunasoma biblia mbili tofauti..na kama Agano la Kale haliwezi kuwa na mabadiliko ama nyongeza kutokana na Agano jipya ili kutuwezesha zaidi kufanya ibada hii ya maendeleo ya kiuchumi basi mkuu tuna tatizo kubwa zaidi...

Kumradhini lakini ndio ukweli usiokubalika!

Mkandara:

Naona kuna posti mbili zilizokuwa addressed kwangu. Naomba kujibu moja tu.

Vitabu vya dini kama Biblia au Koran ni kama bahari na wasomaji ni wavuvi. Mvuvi anapotupa nyavu anakamata vitu vingi na tofauti kama vile wasomaji wa vitabu vya dini. Na kama wasomaji wa vitabu vya dini wangekuwa wanakamata vitu sawa basi dini moja isingekuwa na makundi tofauti ya imani. Hivyo mifano yako ya dini katika siasa haina mpango.

Na nakuomba sana uache kutoa mfano wa kuwa Nyerere alimefariki miaka 10 iliyopita basi tuache kusema. Tutaendelea kusema kwa sababu tukiacha kuna watu watakaoturudisha kwenye Azimio la Arusha na Ukiritimba wa kijamaa.

Pili naomba nikufahamishe kuwa inachukua zaidi ya miaka saba kwa mnazi kuanza kutoa nazi. Hivyo inamchukua mkulima mwenye shamba zaidi ya miaka 15 kuanza kupata faida.

Najua kwenu hamlipi zao lolote la kudumu. Inachukua zaidi ya miaka mitatu kwa mti wa kahawa kuanza kuonekana kwamba unatoa kitu.

Sekta ya utalii Kenya mmejengwa kwa zaidi ya 30 kufikia umaarufu tuonao sasa.

Inachukua zaidi ya miaka 20 kwa mwenye shamba la mkonge kuanza kurudisha faida ya nguvu.

Imewachukua zaidi ya miaka 40 kwa Ethiopia Airways kufikia ilipofika sasa.

Nyerere ameacha urais hakiwa hana sekta yoyote ya kuendeleza nchi. Na nakushangaa sana unapowapigia kelele Mzee Mwinyi na Mkapa. Katika vipindi vyao wameweza kufufua mazao mengi kama Korosho na Kahawa. Na vilevile wameweza kuongeza sekta ya utalii na madini.

Kuna magazeti pale maktaba ya taifa kaombe gazeti la uhuru au Daily News na soma bajeti ya Mwaka 1985, Mzee Msuya akiwa waziri wa fedha. Pato la Tanzania la kigeni lilikuwa chini ya dollar millioni 400 au zaidi kidogo ya hapo.

Sasa hivi sehemu kubwa ya pato la Tanzania linatoka katika sekta mpya zilizoanzishwa katika awamu ya pili na ya tatu bila ya kutumia kitabu chochote cha itikadi.

Katika mabadiliko hayo makubwa kuna matatizo ya ufisadi, rushwa na mengine. Na matatizo hayo ndio watu wanayotakiwa kuyafanyia kazi na sio kurudi kwenye siasa za kuvaa viroba.
 
Kwani kuna wasomi wangapi? Kungekuwa na wasomi Tanzania nchi isingeweza kutaifisha mwekezaji anayelipa 40% na baadaye kumuomba radhi arudi kwa kulipa 10%.

natumaini we ni mtanzania! na kama ndo hivyo je wewe unajiweka kwenye kundi gani la wasomi au wasio wasomi?
 
Bin Maryam,
Mkuu wangu unajua kusema ni rahisi sana lakini inapofikia kuyaweka maelezo hayo ktk ukweli amam niseme hali halisi ndipo tunapotofautiana....
Kwanza umezungumzia swala la dini ukazitaja Kuran na biblia, nadhani hakuna mahala niliposema kuhusu Kuran na Biblia kisha hivi vitu haviwezi kutumika katika mfano nilioutoa hapo awali..Ikiwa sisi sote ni dini tofauti basi mkuu sidhani kama tutakuwa na malengo sawa kitaifa.
Pili umerudi katika swala la upandaji miti na kusema kwamba mnazi huchukua miaka saba kuweza kutoa matunda, nachoshindwa kuelewa hapa ni mnazi gani umesha pandwa hadi sasa hivi?..kwani tatizo siyo itikadi ya Ujamaa na Ubepari hapa ila ni Nyerere ambaye alikuwa mMjamaa na leo hii sisi sio Wajamaa tena ila Mabepari..na kibaya zaidi ni kwamba mnataka Ujamaa usirudi wakati lawama zote za Ufisadi ni matunda ya Ubepari na hutokea nchi zote duniani kwa uzito tofauti.
Sasa nimbie huo mnazi uliopandwa umepandwa lini na wapi maanake umezungumzia swala la sekta mpya sijui ni zipi hizo ambazo hazikuwepo wakati wa Mwalimu. Kama ni madini mkuu hapo unajua mwenyewe jinsi hiyo aslimia 3 inavyonuka.
Halafu umezungumzia swala la pato la taifa mwaka 1985, hivi mkuu wangu unajua hata Marekani yenyewe pato la taifa mwaka 1985 ni dogo mara 100 chini ya pato la nchi hiyo hiyo leo hii?...Hapa hata sielewi unachozungumzia kabisa. Mwaka 1985 watu kama Mobutu aliyekuwa na utajiri chini ya Billioni moja alikuiwa ktk hesabu ya matajiri 10 duniani... It' not the same today.. Dollar Elfu 20 uliweza kununua Mercedes Benzi mpyaaa wenyewe wanasemaa zero mileage- hivyo unapotaja pato la taifa mwaka huo ukajaribu kulinganisha na pato la leo ni mchezo mchafu sana. Kama kuna ongezeko lolote kulingana na mahitaji yetu plus population imekuwaje leo hii tumesimama chini zaidi (ranked) yaani nchi ya 8 kati ya nchi maskini duniani?.
Unapozungumzia sehemu kubwa ya pato la taifa kuwa umetokana na awamu ya pili na tatu hapo mkuu bado kabisa sijakupata. Sehemu kubwa ina maana ya Asilimia kubwa ya pato hilo iwe hata 10, kisha 6 zikitokana na Madini utasema asilimia kubwa (60%) ya pato letu linatokana na madini tofauti na yule anayekusanya 100 na madini yakachangia 20 tutasema madini yamechangia asilimia ndogo yaani 20%.
Lakini in reality hiyo 20% ni kubwa kuliko ile asilimia 60 ya mchango wa yule aliyekusanya 10. Hiki ndicho kichaa kinachotembea Bongo watu wanashindwa kuelewa kuwa asilimia ni lugha inayotumiwa kufafanua mchango wa kitu ktk pato la taifa na haina maana kuongezeka kwake kunaweza kubadilisha hali ya kiuchumi ikiwa pato zima halina uuwiano na ongezeko la mahitaji ya nchi pamoja na population yake.

Mwisho umezungmzia kuhusu Ethiopia Airaline, hata sielewi unachojaribu kusema hapa kwani Ethiopia Airline imewahi kuwa ktk kundi la Airline 10 bora duniani na sii chini ya mara tatu wameshika Airline bora Afrika wakati miaka ya 70 na 80. Sasa sielewi mfano wako unalenga nini haswa kwani hapa hatuzungumzii makuzi ya umri wetu isipokuwa makuzi ya uchumi. Kama vile navyosema kila siku kuwa miaka yetu toka Uhuru ni makuzi yetu kama Taifa kiumri haina maana hata Kiafya basi tutahitaji kuwa wazima na wenye afya bora tukifika miaka 100.
Nchi kama Marekani leo hii zinavuna huo mnazi baada ya kazi ngumu ya kupanda na kuumwagilia maji huo mnazi miaka ileeee lakini sisi kwa Uvivu wetu hatujapanda kitu. Tunachofanya ni kuihsi maisha ya Primitive - uncivilized human being ambao tunategemea zaidi kile Mungu alichotutupa (Maliasili -Madini na Wanyama pori) kama ndio biashara itakayo weza kutuondoa ktk Umaskini. Sasa kweli hapa tuna tofauti gani ya yule Mswana wa Gods must be crazy?..maanake hakuna pato la taifa linalotegemea kitu tulichoweza kuzalisha sisi isipokuwa kile Mwenyezi Mungu alichotujalia yaani tumerudi miaka 50 nyuma kutegemea madini, Wanyama, Mlima Kilimanjaro..na kila siku tunaomba Mungu tupate mafuta tuwe kama Dubai.. Hizi kama sio ndoto za Alinacha mkuu wangu ebu nambie!..
NDIVYO TULIVYO, haikatazi mtu kumzungumzia Nyerere na mabaya yake lakini kusema tyeye ndiye sababu ya Upuuzi huu wa akili na matemdo, Uzembe huu wa akili na matendo ya Wadanganyika mkuu wangu utakuwa umetafuta kajamba nani!..Lakini mashuzi tunayatoa sisi wenyewe kwa kutozingatia kuwa ELIMU na exposure ni silaha kubwa ya Mdanganyika kuondokana na Umaskini.
Kila nchi iliyokuwa na wasomi wengi kulingana na population yake ndivyo nchi hiyo imeweza kuwa ktk rank nzuri zaidi ya kuendelea. Na wenzetu wlisoma ili wapate ufunuo zaidi wa akili zao kuweza kufikia hatua ya KUTOA AJIRA kutokana na Ubunifu wao ili kukidhi supply vitu kutokana na mahitaji (demand). Leo sisi tunasoma tukiwa na lengo la KUTAFUTA AJIRA ndio maana nasema hatujapanda mnazi tunapanda mchicha kutuwezesha mvuto wa tonge la toka kwenye sahani hadi kinywani.
Nyerere amekufa miaka 10 iliyopita na toka mabadiliko yanze ni zaidi ya miaka 25 umri mkubwa kuliko utawala mzima wa Nyerere lakini tunachokiona ni kipi zaidi ya Ufisadi na masiha mabaya zaidi kwa wananchi...China walikuwa na Mao Tse Tung, Russia, Vietnam, Ethiopia wote hawa walikuwa na mtu kama Nyerere tena yawezekana mbaya kuliko Nyerere na mabadiliko ya Kiuchumi tumeyaanza wote pamoja lakini wao wameweza kuondokana na umaskini kirahisi zaidi yetu, wao wansonga mbele tena wakiwa bado wamekumbatia fikra za viongozi hao kuliko sisi tuliochagua Umalaya wa kuiga!.
Uchumi wetu ni sawa na malaya changu doa tunaovizia Mchati, afadhali hata hao Kenya na Botswana ni malaya lakini wanatafuta kina Eliot Spitzer, dau huwa wanalipanga wao....
 
Wazee naheshimu michango yenu makini humu.

Wengi tunasema Nyerere alitu-lostisha na uchumi ulikufa kabisa na mengine mengi ambayo yametugharimu kama taifa bila kusahau siasa za TANU na ujamaa. Lakini wakuu naomba tujiulize kidogo, Nyerere ameondoka two decades plus kwenye usukani wa uchumi wetu. ARE WE ANY BETTER TODAY AS A NATION THAN DURING MWALIMU`S ERA?

Yes, Mkapa Mwinyi na JK wote wameleta wawekezaji na ni ukweli fedha za kigeni zimekuwa nyingi sana..just name it, but has a common man on the street I mean rank and file amefaidika vipi? hizo investments zime-translate vipi katika maisha ya mtanzania wa kawaida? Ni % ngapi ya watanzania leo wanaishi below poverty line? Mi nadhani tuache nadharia, anachoongea muungwana Mkandara hapa kina mantiki kubwa sana.

Hatuwezi kuendelea kumlaumu Mwalimu wakati tatizo tunalijua mfano Nyerere ana uhusiano gani na mtu kama Karamagi anayesaini mkataba wa mamilioni hotelini London wa kupora mali za watanzania? Balali, EPAs, Tanesco, TRA and on and on..hizi idara zote kama zingeongozwa kwa makini ndo injini ya uchumi na maendeleo ya mtanzania. Period. watu wanaliibia taifa, rushwa its all time high..what has mwalimu got to do with that?

Swala la umaskini wetu Tanzania ni sisi wenyewe wa kujilaumu. Nyerere aliweka misingi ambayo kama tungeitumia vyema tungekuwa tunaipumulia kooni Malaysia au Korea ya Kusini! Hiyo misingi kila mtu anaielewa.

Ni kweli Nyerere had his own failure too. But it will be grossly unfair and unreasonable kuendelea kulia na siasa za 1970s za kula unga wa yanga na kupanga foleni za sabuni. The old man did it but with good intentions and now we can all proudly see what he did. ni %% ngapi ya watanzania walipata elimu kipindi chake, health care na emngineyo? Lets get real!

Bila kuwa na viongozi wawajibikaji maendeleo ni ndoto kwa Tanzania na Africa yote. Na kama wengine walivyosema, vongozi wetu ni reflection yetu wapiga kura. We have no excuse waafrika tuna matatizo ya IQ kama alivyosema Dr. Watson!

Ulishawahi kusikia nchi kama Germany inamlaumu Hitler kwa majanga ya karne iliyopita? France inawalaumu watawala wake wa enzi hizo? Japani na nk? They know it and they are confronting the future with optimism and hardwork. Only Africans are blaming their past for their failure to reach Mt. Sinai..hata USA its the black race which is complaining! tALK OF dR. WATSON! HE SAID WHAT MOST OF PEOPLE ARE AFRAID TO SAY IN PUBLIC! BUT ITS TRUE!
 
Nyerere alikuwa anajikusanyia fedha nyingi za walala hoi lakini ujanja wake ulinasa kwenye tundu bovu ,feza yote akimpa Jamal amhifazie Uswiss kwa jina la Jamal ,sasa Jamal alipofariki ,Nyerere akamwendea mkewe Jamal na kumuuliza habari ya feza ,mke wa Jamal akaruka na kusema Bana hakuniambia kama wewe naweka feza zako kwake ,hata akauti zake sioni jina lako ,tafadhali hakuna feza hapa ,Nyerere kusikia hayo hakuwa na la kufanya na kupata ugonjwa ghafla na kufariki.Hiki ndio sababu iliyomuua baba wa Taifa.
 
This is so funny!!!
 
Masanja,
Shukran mkuu afadhali umenielewa vizuri na pengine itasaidia Wadanganyika wengine kama mimi kuanza kujitazama vizuri..
Hili neno NDIVYO TULIVYO kusema kweli nimelipenda sana na namshukuru sana Nyani Ngabu kwa kuliibua tena nadhani itabidi sasa aombe riba juu ya matumizi yake.

Ukitazama neno hili kisha ukauweka msemo ule usemao kuwa Vingozi ni reflection yetu!.. basi bila shaka jibu la matatizo yetu tunayo sisi wenyewe tatizo ni kwamba kama manyani hatuoni makalio yetu.

Leo hii pamoja na uhuru wote viongozi wetu wamefikia kutuita sisi wananchi WAJINGA, yaani pamoja na ujinga huo ni pamoja na kuendelea kuwachagua, kuwatetea na hata kuona kila hoja ni negative kwa sababu tu inamgusa kiongozi ambaye kwa mtazamo wa wengi hana makosa ya kuchusha isipokuwa kuna kitu kilichomtangulia. Ndio yale wakati wa Nyerere tuliwasema sana wakoloni, wakatuachia nchi tujitawale wenyewe sasa baada ya miaka karibu 50, maendeleo hakuna na kilichobakia ni kuzua vioja!.. kajamba nani?
Hii inatokana na sisi wenyewe kuwa na tabia hizohizo (reflection) kwa hiyo haiwezekani hata kidogo tukaweza yaona mabaya isipokuwa yale yasiyofanana nasi - Watu kama kina Nyerere.

Ebu mkubwa tazama nchi nzima tunahitaji sana usafiri, barabara zetu mbovu haya tuseme uwezo hatuna, lakini kwa sababu tunahitaji sana usafiri kwa nini baiskeli zisitengenezwe nchini na hao wawekeshaji?..China na Malesia ndiko walikoanzia ama sio?..Pili Tanzania nzima joto kama kiyama kwa nini hao wawekeshaji wasiwekeshe ktk vitu kama Air condition ama Humidfiers ambazo hazina utaalam mkubwa isipokuwa watu tunashindana kuagiza vitu toka nje. Basi hata sindano na uzi wa kushonea viraka vyetu bado tunaagiza nje jamani?....

Wawekeshaji hao toka nje kama sii wote wamekuja nunua mali za Umma zile ambazo tulikuwa nazo na pengine muhimu zaidi kiuchumi kwetu zikiwa kama Commanding height ambazo kwa mujibu wa IMF ilikuwa ni lazima tuziuze ili tupate mikopo yao.
Hivyo bado sio mawazo ama mapendekezo ya viongozi waliotangulia na wala hayakuwa mawazo ya wananchi isipokuwa ni importation ya policies ambazo tulifikiria zinaweza kutusaidia zaidi, kumbe ktk vision ya viongozi wetu ambao kama sisi wenyewe walifikiria kwanza ULAJI! -Je, upo, ndio maana NBC IPTL, TCCL na makampuni mengine kibao yaliuzwa kwa bei ya kutupa. Dhahabu yetu imetolewa buree na hiyo gas kama tukipata mahesabu yake tunaweza jichimbia kaburini..

Haya yote yametokea mbele ya macho yetu na tunachokifanya leo ni kulaumu sana lakini ndani ya nyoyo zetu tunaamini kabisa kuwa Mkapa na pengine JK ni viongozi wazuri na bora kuliko Nyerere hivyo ni bora kwenda na hili zimwi tulijualo kuliko kufikiria nje ya kioo kilichopo machoni petu...
NDIVYO TULIVYO = Viongozi ni reflection yetu.. sisi wote ni Wapuuza (Gross Negligence) na Wazembe (Incompetant) kwa hiyo ni lazima tutavuna Mafisadi.
Tunahitaji kubadilika na mabadiliko hayawezi kuja kama sisi wenyewe hatutakubali kuwa tuna tatizo hili kubwa..
Mgonjwa yeyote anaye kana kuumwa mara nyingi hukataa kutibiwa!
 
Nyerere alikuwa anajikusanyia fedha nyingi za walala hoi lakini ujanja wake ulinasa kwenye tundu bovu ,feza yote akimpa Jamal amhifazie Uswiss kwa jina la Jamal ,sasa Jamal alipofariki ,Nyerere akamwendea mkewe Jamal na kumuuliza habari ya feza ,mke wa Jamal akaruka na kusema Bana hakuniambia kama wewe naweka feza zako kwake ,hata akauti zake sioni jina lako ,tafadhali hakuna feza hapa ,Nyerere kusikia hayo hakuwa na la kufanya na kupata ugonjwa ghafla na kufariki.Hiki ndio sababu iliyomuua baba wa Taifa.
[COLOR="Green"STORY YA KIFO CHA WAZIRI WA ZAMANI WA FEDHA ALIYEJILIMBIKIZIA MAPESA IMEGEUZWA KUWA YA JK.........! (wanaharakati)[/COLOR]hii kali....!
 
Nimechelewa kufatilia majadiliano haya lakini kwa ufupi kama kuna uwezekano wa kuchagua kwa kuzingatia maslahi ya walio wengi na ya Taifa hili basi bila kusita ningemchagua Mwalimu na sera zake kwani kwa vyovyote alikuwa na moyo wa kuipenda nchi hii ukilinganisha na waliokuja baadaye - kosa kubwa la Mwalimu kwa mtazamo wangu hakuwa mwanademokrasia na hiyo ni wakati akiwa madarakani - jee alipowaachia wengine warekebishe pale alipokuwa yeye kakosea wamefanya nini? .... nafikiri jibu linajulikana.
 
Waislamu wengi ni wabaguzi sana,kwa wasio waislamu,na ukifuatilia fujo nyingi tz source ni waislamu,wakidhani wakristo hawawezi kufanya noma-noma na nginja-ngija kila kona ya dunia,tuna wajoki tuuu,ila siku ya siku lazima tuwapeleke shule panapo.

Hafu kuna wengine ni malimbukeni sana,hasa huku mamtoni,wakimwona mwarabu wanachanganyikiwa sana,sijui wanapewa nini?yaani wanakudelete kabisa mtz kama hawakujui,hafu utakuta wanachongachonga na waarabu,na kujipendekeza pendekeza kusikokwisha.mmmmhh hataro kwelikweli.

Mwalimu alifanya kazi kubwa kutuweka pamoja,na hakum-bagua mtu kwa itikado za dini yake.Ndo maana wakati wa uongozi wake hakukuwa na movement za fujofujo zenye misingi ya kidini.

I love Nyerere,til kifo.Hakushindwa kitu,matatizo tuliyonayo ni watendaji walofuata wamecheza foul.

MUNGU ilaze roho ya Nyerere mahali pema,amen.
 
Yamekuwa haya tena! Maneno ya kibaguzi na kichochezi utoe wewe kwa kisingizio cha kumsifia Nyerere halafu hapohapo uwalaumu Waislam kwa kuwa wabaguzi na wapenda shari, kama siyo unafiki uliopita kikomo!

Hivi kweli na akili yako unaona kuwa chanzo cha matatizo Tanzania ni Waislam? Mfano tu, umeme kupanda hivi utawasingizia Waislam? Sakata la mafisadi, Ukosefu wa madawa mahospitalini, upungufu wa madaktari, walimu, madawati, janga la ukimwi na mengine mengi tu, je, yote haya chanzo chake Waislam?

Acha udini ndugu yangu na wala usiwababaikie waarabu hivyo na wewe ukiwaona ruksa "kuchonga" nao tatizo liko wapi?
 
Back
Top Bottom