Bin Maryam
JF-Expert Member
- Oct 22, 2007
- 685
- 14
Bin Maryam,
Mkuu wangu unajua kusema ni rahisi sana lakini inapofikia kuyaweka maelezo hayo ktk ukweli amam niseme hali halisi ndipo tunapotofautiana....
Kwanza umezungumzia swala la dini ukazitaja Kuran na biblia, nadhani hakuna mahala niliposema kuhusu Kuran na Biblia kisha hivi vitu haviwezi kutumika katika mfano nilioutoa hapo awali..Ikiwa sisi sote ni dini tofauti basi mkuu sidhani kama tutakuwa na malengo sawa kitaifa.
Pili umerudi katika swala la upandaji miti na kusema kwamba mnazi huchukua miaka saba kuweza kutoa matunda, nachoshindwa kuelewa hapa ni mnazi gani umesha pandwa hadi sasa hivi?..kwani tatizo siyo itikadi ya Ujamaa na Ubepari hapa ila ni Nyerere ambaye alikuwa mMjamaa na leo hii sisi sio Wajamaa tena ila Mabepari..na kibaya zaidi ni kwamba mnataka Ujamaa usirudi wakati lawama zote za Ufisadi ni matunda ya Ubepari na hutokea nchi zote duniani kwa uzito tofauti.
Sasa nimbie huo mnazi uliopandwa umepandwa lini na wapi maanake umezungumzia swala la sekta mpya sijui ni zipi hizo ambazo hazikuwepo wakati wa Mwalimu. Kama ni madini mkuu hapo unajua mwenyewe jinsi hiyo aslimia 3 inavyonuka.
Halafu umezungumzia swala la pato la taifa mwaka 1985, hivi mkuu wangu unajua hata Marekani yenyewe pato la taifa mwaka 1985 ni dogo mara 100 chini ya pato la nchi hiyo hiyo leo hii?...Hapa hata sielewi unachozungumzia kabisa. Mwaka 1985 watu kama Mobutu aliyekuwa na utajiri chini ya Billioni moja alikuiwa ktk hesabu ya matajiri 10 duniani... It' not the same today.. Dollar Elfu 20 uliweza kununua Mercedes Benzi mpyaaa wenyewe wanasemaa zero mileage- hivyo unapotaja pato la taifa mwaka huo ukajaribu kulinganisha na pato la leo ni mchezo mchafu sana. Kama kuna ongezeko lolote kulingana na mahitaji yetu plus population imekuwaje leo hii tumesimama chini zaidi (ranked) yaani nchi ya 8 kati ya nchi maskini duniani?.
Unapozungumzia sehemu kubwa ya pato la taifa kuwa umetokana na awamu ya pili na tatu hapo mkuu bado kabisa sijakupata. Sehemu kubwa ina maana ya Asilimia kubwa ya pato hilo iwe hata 10, kisha 6 zikitokana na Madini utasema asilimia kubwa (60%) ya pato letu linatokana na madini tofauti na yule anayekusanya 100 na madini yakachangia 20 tutasema madini yamechangia asilimia ndogo yaani 20%.
Lakini in reality hiyo 20% ni kubwa kuliko ile asilimia 60 ya mchango wa yule aliyekusanya 10. Hiki ndicho kichaa kinachotembea Bongo watu wanashindwa kuelewa kuwa asilimia ni lugha inayotumiwa kufafanua mchango wa kitu ktk pato la taifa na haina maana kuongezeka kwake kunaweza kubadilisha hali ya kiuchumi ikiwa pato zima halina uuwiano na ongezeko la mahitaji ya nchi pamoja na population yake.
Mwisho umezungmzia kuhusu Ethiopia Airaline, hata sielewi unachojaribu kusema hapa kwani Ethiopia Airline imewahi kuwa ktk kundi la Airline 10 bora duniani na sii chini ya mara tatu wameshika Airline bora Afrika wakati miaka ya 70 na 80. Sasa sielewi mfano wako unalenga nini haswa kwani hapa hatuzungumzii makuzi ya umri wetu isipokuwa makuzi ya uchumi. Kama vile navyosema kila siku kuwa miaka yetu toka Uhuru ni makuzi yetu kama Taifa kiumri haina maana hata Kiafya basi tutahitaji kuwa wazima na wenye afya bora tukifika miaka 100.
Nchi kama Marekani leo hii zinavuna huo mnazi baada ya kazi ngumu ya kupanda na kuumwagilia maji huo mnazi miaka ileeee lakini sisi kwa Uvivu wetu hatujapanda kitu. Tunachofanya ni kuihsi maisha ya Primitive - uncivilized human being ambao tunategemea zaidi kile Mungu alichotutupa (Maliasili -Madini na Wanyama pori) kama ndio biashara itakayo weza kutuondoa ktk Umaskini. Sasa kweli hapa tuna tofauti gani ya yule Mswana wa Gods must be crazy?..maanake hakuna pato la taifa linalotegemea kitu tulichoweza kuzalisha sisi isipokuwa kile Mwenyezi Mungu alichotujalia yaani tumerudi miaka 50 nyuma kutegemea madini, Wanyama, Mlima Kilimanjaro..na kila siku tunaomba Mungu tupate mafuta tuwe kama Dubai.. Hizi kama sio ndoto za Alinacha mkuu wangu ebu nambie!..
NDIVYO TULIVYO, haikatazi mtu kumzungumzia Nyerere na mabaya yake lakini kusema tyeye ndiye sababu ya Upuuzi huu wa akili na matemdo, Uzembe huu wa akili na matendo ya Wadanganyika mkuu wangu utakuwa umetafuta kajamba nani!..Lakini mashuzi tunayatoa sisi wenyewe kwa kutozingatia kuwa ELIMU na exposure ni silaha kubwa ya Mdanganyika kuondokana na Umaskini.
Kila nchi iliyokuwa na wasomi wengi kulingana na population yake ndivyo nchi hiyo imeweza kuwa ktk rank nzuri zaidi ya kuendelea. Na wenzetu wlisoma ili wapate ufunuo zaidi wa akili zao kuweza kufikia hatua ya KUTOA AJIRA kutokana na Ubunifu wao ili kukidhi supply vitu kutokana na mahitaji (demand). Leo sisi tunasoma tukiwa na lengo la KUTAFUTA AJIRA ndio maana nasema hatujapanda mnazi tunapanda mchicha kutuwezesha mvuto wa tonge la toka kwenye sahani hadi kinywani.
Nyerere amekufa miaka 10 iliyopita na toka mabadiliko yanze ni zaidi ya miaka 25 umri mkubwa kuliko utawala mzima wa Nyerere lakini tunachokiona ni kipi zaidi ya Ufisadi na masiha mabaya zaidi kwa wananchi...China walikuwa na Mao Tse Tung, Russia, Vietnam, Ethiopia wote hawa walikuwa na mtu kama Nyerere tena yawezekana mbaya kuliko Nyerere na mabadiliko ya Kiuchumi tumeyaanza wote pamoja lakini wao wameweza kuondokana na umaskini kirahisi zaidi yetu, wao wansonga mbele tena wakiwa bado wamekumbatia fikra za viongozi hao kuliko sisi tuliochagua Umalaya wa kuiga!.
Uchumi wetu ni sawa na malaya changu doa tunaovizia Mchati, afadhali hata hao Kenya na Botswana ni malaya lakini wanatafuta kina Eliot Spitzer, dau huwa wanalipanga wao....
Mkandara:
Kweli soma kwako gumu kupanda. Mifano yote niliyotoa nilionyesha kuwa vitu vyote unavyoviona vinawapa watu faida ni matokeo ya muda mrefu. Ukichukua minazi, mikahawa, shirika la ndege la Ethiopia, mafanikio China, you name them.
Nyerere alikuwa na mapinduzi ya muda mfupi. Alitaka sera yenye kuanza leo na kesho kutoa matunda na matokeo yake ni hapa tulipo.
Na hizo lawama sio pekee yake, kuna mtu anaitwa Kaunda wa Zambia naye alikwenda kwa spidi za Nyerere na matokeo tupo kwenye kundi moja.
Hivyo kabla ya kujilinganisha na nchi zingine angalia historia yao na kama una uwezo jenga ya kwako na sio kukurupuka.
Mambo mengine naona una-spin kama kawaida yako.