Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

BinMaryam,
Unajua wakati mwingie mifano yako huwa nashindwa kuifahamu vizuri!.. Hizo kazi za Kujitegemea ndio kazi gani hizo? ama ulikuwa na maana ku volunteer?... Mbona hata hapa kwetu wapo wanafunzi wanaokwenda volunteer baada ya masomo ku gain kutengeneza CV zao?.
Pili unaposema shida haiwezi kukupa ujanja ni msemo wa Kidanganyika, usemi wa kivivu na unaojengwa na imani kuwa fedha zinaweza kuondoa umaskini yaani ujanja ni kupata. Ndio maana vijana wengi wanavamia bwimbwi.
Mkuu huwezi kupata bila kutoka jasho ama kuumia kwani maendeleo ya nchi za Ulaya zote umekuja kwa cost kubwa sana. Leo hii wanakula wakiwa kivulini na mswahili unataka uruke ugumu wote uwe kama Marekani kwa kupitia mgongo wa mtu...Taabu kweli kweli.
 
tunalo liona hapa ni mgongano wa kimawazo ambao upo imbalanced kwelikweli. There is a tendency now developing of blaming mwalimu for today's misfortunes by showing mwl ndo aliyapika na haya ni matokeo yake. This is especially in the economy and these are popular beliefs of western models of economic development which do not serve social needs. The common saying of "Ujamaa ulifeli, na ndio chanzo cha umasikini wetu" is wholly untrue. Tatizo kubwa na watu kutosoma hotuba za mwl wakati ni kiongozi na pia kutoangalia focus za uongozi wake. Hebu tujaribu ku analyse.

UCHUMI; Focus ya mwalimu haikuwa kuwa na pato kubwa la taifa (national income) while majority of the people remained in abject poverty. if it were so angeisha gawa madini, mbuga na viwanda kama walivyofanya waliotangulia. Mwalimua ali understand, western models of economic development do not provide holistic development of the population but rather segmented upliftment. Kwa mfano, leo hii tuna viwanda, wanachimba madini, ubinafshishwaji, pato la taifa linakuwa (they say so) lakini hospitali ni mbovu, shule hazitoshi, huduma za jamii ni nzuri mijini tu etc. Kwa a prudent thinking individual it is not difficult to understand social needs are not addressed in such model of economic development. Serikali inajitoa kwenye huduma muhimu za jamii kwa kisingizio haina pesa. Wakati wa mwalimu serikali ilikuwa at the forefront in providing huduma za jamii. Ingekuwa ni mwalimu ndo yupo madarakani, wale wanafunzi waliokwama Ukraine wasingerudi nyumbani.

A point to note, haya mashirika yote tunayowagawia wazungu, tuliwezaje kuyaanzisha kipindi kile? yaliwezaje ku survive for this long? mbona tuliowapa hawajaleta mitaji mipya ila wametumia waliyoikuta!!! Ni kweli tumeshindwa kuyaendeleza? leo hii tunaleta wataalam toka nje, hawa ma professor na wasomi wanafanya nini kwenye vyuo vikuu vya serikali? we have to comprehend the fact kuna wanasiasa wanatumia jina la mwalimu for political advantage kama vile India baadhi wanaotumia jina la Gandhi for vote bank politics. Mwalimu hakutaka masanamu yajengwe, the same as Castro because of the effect of personification or idolatry. We cannot blame mwalimu the fact they are constructed today when he is absent!

Also, liberation of other African countries was not done for the purpose of capturing their economic resources for this would defeat the sole purpose of liberation. We wanted to free our African brothers from colonialism, not just politically, but socially and economicall. it was a self-sacrifice on our part for they would have done the same had we been in their shoes. The whole concept of economic benefit ndo wanachofanya Wamarekani Iraq, South Korea, japan etc. its immoral and dehumanizing.

So game theory it is unfair to blame mwalimu for the mistakes his successors have committed. This is not to suggest Mwalimu never had his own shortcomings, but he was true to his course and his course was genuine and on top of that directed towards development of the country. Ndo maana watu walisoma bure, walitibiwa bure, walikuwa na uhakika wa kazi, mashirika ya serikali yalifanya kazi, kilimo kilistawi.
 
Elimu ya kujitegemea na Volunteer ni vitu viwili tofauti. Elimu ya kujitegemea ilikuwa ni lazima na kila shule ilikuwa na miradi ambayo kwa kiwango kikubwa ilikuwa ni CHILD ABUSE. Mwanafunzi alitumia muda wa masaa manane darasani na baadaye alitumia masaa mawili mpaka manne katika kazi za elimu ya kujitegemea.

Kazi za elimu ya kujitegemea ndio shida nilizosema ambazo hazikumpa mwanafunzi ujanja wowote. Niambie elimu ya kujitegemea ilisaidia nini taifa zaidi ya kudumaza kiwango cha elimu?

Kupata bila jasho kupo kama unatumia akili. Na kutumia akili pekee yake kunaweza kuwaondoa watu kwenye kundi la SISI NDIVYO TULIVYO.
 
tunalo liona hapa ni mgongano wa kimawazo ambao upo imbalanced kwelikweli. There is a tendency now developing of blaming mwalimu for today's misfortunes by showing mwl ndo aliyapika na haya ni matokeo yake. This is especially in the economy and these are popular beliefs of western models of economic development which do not serve social needs. The common saying of "Ujamaa ulifeli, na ndio chanzo cha umasikini wetu" is wholly untrue. Tatizo kubwa na watu kutosoma hotuba za mwl wakati ni kiongozi na pia kutoangalia focus za uongozi wake. Hebu tujaribu ku analyse.

UCHUMI; Focus ya mwalimu haikuwa kuwa na pato kubwa la taifa (national income) while majority of the people remained in abject poverty. if it were so angeisha gawa madini, mbuga na viwanda kama walivyofanya waliotangulia. Mwalimua ali understand, western models of economic development do not provide holistic development of the population but rather segmented upliftment. Kwa mfano, leo hii tuna viwanda, wanachimba madini, ubinafshishwaji, pato la taifa linakuwa (they say so) lakini hospitali ni mbovu, shule hazitoshi, huduma za jamii ni nzuri mijini tu etc. Kwa a prudent thinking individual it is not difficult to understand social needs are not addressed in such model of economic development. Serikali inajitoa kwenye huduma muhimu za jamii kwa kisingizio haina pesa. Wakati wa mwalimu serikali ilikuwa at the forefront in providing huduma za jamii. Ingekuwa ni mwalimu ndo yupo madarakani, wale wanafunzi waliokwama Ukraine wasingerudi nyumbani.

A point to note, haya mashirika yote tunayowagawia wazungu, tuliwezaje kuyaanzisha kipindi kile? yaliwezaje ku survive for this long? mbona tuliowapa hawajaleta mitaji mipya ila wametumia waliyoikuta!!! Ni kweli tumeshindwa kuyaendeleza? leo hii tunaleta wataalam toka nje, hawa ma professor na wasomi wanafanya nini kwenye vyuo vikuu vya serikali? we have to comprehend the fact kuna wanasiasa wanatumia jina la mwalimu for political advantage kama vile India baadhi wanaotumia jina la Gandhi for vote bank politics. Mwalimu hakutaka masanamu yajengwe, the same as Castro because of the effect of personification or idolatry. We cannot blame mwalimu the fact they are constructed today when he is absent!

Also, liberation of other African countries was not done for the purpose of capturing their economic resources for this would defeat the sole purpose of liberation. We wanted to free our African brothers from colonialism, not just politically, but socially and economicall. it was a self-sacrifice on our part for they would have done the same had we been in their shoes. The whole concept of economic benefit ndo wanachofanya Wamarekani Iraq, South Korea, japan etc. its immoral and dehumanizing.

So game theory it is unfair to blame mwalimu for the mistakes his successors have committed. This is not to suggest Mwalimu never had his own shortcomings, but he was true to his course and his course was genuine and on top of that directed towards development of the country. Ndo maana watu walisoma bure, walitibiwa bure, walikuwa na uhakika wa kazi, mashirika ya serikali yalifanya kazi, kilimo kilistawi.

Tusidanganyane hapa mwalimu hakuelewa western model of Economy. Ni nani alikwambia Western Model hai-serve social needs? Kama ingekuwa hivyo misaada mikubwa ya uchumi isingetoka katika nchi za West.

Mwalimu alikuwa Pioneer na kabla yake kulikuwa hakuna mifano ya mweusi kuongoza nchi. Hivyo kufanya kwake makosa ni kitu cha kueleweka na tunachotakiwa ni kuelewa makosa yaliofanyika na ku-move on.

Kinachofanyika sasa ni Tanzania kuwa kichwa cha mwendawazimu. Kila mtu ana-pile makosa yake.
 
Bin Maryam,

Mkuu wangu taratibu ili nipate kukuelewa vizuri taratibu
Elimu ya kujitegemea unasema iliweza vipi kutusaidia na umeiita ni Abuse!.. mkuu wangu lazima uwe mtu unayetazama mazingira ya mtu kwanza kabla hujalinganisha na Ulaya.
Tanzania na Afrika nzima watoto huenda kulima mashamba ya nyumbani kwao wakiwa wadogo. Ni utamaduni wetu ambao kutokana na Umaskini wetu ulikuwa muhimu zaidi kudumishwa kuhakikisha kuwa watoto wanaenda pata elimu wakiwa na matumbo yaliyojaa. Wazazi wetu walikuwa hawana uwezo nje ya jembe yaani kilimo ndicho kilikuwa uti wa mgongo wa maisha ya mwafrika karne na karne. Hivyo kuongezeka kwa elimu ktk tamaduni zetu hakuwezi kuondoa umuhimu wa chakula ama jembe.
Halafu basi, mbona vijana wengi humu JF ni matunda ya Mwalimu! na tena naweza kukupa changamoto ujaribu kutafiti wasomi wanaojitokeza humu ni matunda ya nani. Wengineo wote wameikimbia nchi na wamepata elimu zao nje tena wakati wa Mwinyi ama Mkapa. Waliobaki ni vijana walio soma ama wanasoma UDSM, na Please mkuu wana matatizo mengi sana kielimu, vifaa na njaa zikiwa ni sababu kubwa sana za kudorora kiwango cha elimu nchini. Wanasoma vyuo vikuu ili wapate ajira kesho, badala ya kusoma ili kesho wawe waajiri hii ni karne ya 20 mkubwa hayo ni mawazo ya miaka 100 iliyopita kama bado unataka kulinganisha na Ulaya.
Tatizo lako mkuu unataka kufananisha Marekani hii ya leo na Tanzania hasa baada ya kuletewa hili neno Child abuse wakati wenzetu wamewahi pitia maisha hayo hayo. Ukisoma historia za matajiri wengi na hasa Wayahudi utaona waliokotokea mkuu.
 
..kuna mashirika ambayo hatukuanzisha bali TULITAIFISHA. kitu cha kusikitisha mashirika hayo yamekufa. hiyo ni aibu kubwa.

..wengi hapa wanadai tulianzisha viwanda. hapana tulikopa, ama tulipata msaada, kuanzisha viwanda.

..huduma za elimu na matibabu tulizokuwa tunapata "bure" zilitokana na kodi za mazao, mikopo, na misaada toka nchi wahisani/wafadhili.

..kulitokea uhaba mkubwa sana wa bidhaa na vilevile huduma za jamii kama elimu, afya, na maji zilidorora kwa kiasi kikubwa.

..kama viwanda na mashirika yetu yalikuwa yanafanya kazi kwa tija na ufanisi, ni kwanini basi kukawa na uhaba wa bidhaa?

..hata kampuni ya kutengeneza majembe ktk nchi ambayo 80% ni wakulima ilikufa. what were we doing wrong?

..swali la kujiuliza ni makosa gani yalitokea wakati wa utawala wa Mwalimu mpaka tukashindwa kuendesha viwanda na mashirika yetu?

..kwa uelewa wangu makosa ya Mwalimu hayakuwa ktk nia au lengo lake. Makosa yake yalikuwa ktk mbinu na mikakati aliyotumia kuelekea ktk malengo yake ya kiuchumi na kijamii.

Bin Maryam,

..you are 100% right kuhusu udhaifu wa elimu ya kujitegemea. wanafunzi walikuwa wakifanyishwa kazi za mitulinga na kulima baada ya masomo.

..lengo la Mwalimu lilikuwa ni kujenga taifa la viwanda[industrialized nation]. sasa nashangaa kwanini watoto[taifa la kesho] wakawa wanalazimishwa kulima, tena kwa jembe la mkono?

..hivi kwanini tusingewapeleka watoto wale kwenye workshop na karakana za ufundi na teknolojia? lengo si lilikuwa kuelekea ktk nchi yenye viwanda?

..pia kuna dhana potofu ati Mwalimu aliahirisha kuchimba madini mpaka tuwe na wataalamu wetu wenyewe.

..hatukuwa na wataalamu wa viwanda wa kutosha lakini tulianzisha viwanda. nchi kama saudia arabia hazikuwa na wataalamu wa kuchimba mafuta lakini walichimba. botswana nao utasema nini? wameingia hasara gani?

..wakati tukijua kwamba tunayo madini, lakini hatuna utaalamu wa kuyachimba, hakuna juhudi zozote zilizofanyika kuanzisha mafunzo ktk sekta hiyo. vyuo vyote vya ufundi vilivyoanzishwa wakati wa Mwalimu havikuwa na Idara ya Mining Engineering.

..Taifa lilikuwa na uhaba wa wataalamu wa kilimo, lakini tulipoanzisha vyuo kikuu, tukaanza na kitivo cha sheria!! we never had our priorities right.
 
Bin Maryam,

Mkuu wangu taratibu ili nipate kukuelewa vizuri taratibu
Elimu ya kujitegemea unasema iliweza vipi kutusaidia na umeiita ni Abuse!.. mkuu wangu lazima uwe mtu unayetazama mazingira ya mtu kwanza kabla hujalinganisha na Ulaya.
Tanzania na Afrika nzima watoto huenda kulima mashamba ya nyumbani kwao wakiwa wadogo. Ni utamaduni wetu ambao kutokana na Umaskini wetu ulikuwa muhimu zaidi kudumishwa kuhakikisha kuwa watoto wanaenda pata elimu wakiwa na matumbo yaliyojaa. Wazazi wetu walikuwa hawana uwezo nje ya jembe yaani kilimo ndicho kilikuwa uti wa mgongo wa maisha ya mwafrika karne na karne. Hivyo kuongezeka kwa elimu ktk tamaduni zetu hakuwezi kuondoa umuhimu wa chakula ama jembe.
Halafu basi, mbona vijana wengi humu JF ni matunda ya Mwalimu! na tena naweza kukupa changamoto ujaribu kutafiti wasomi wanaojitokeza humu ni matunda ya nani. Wengineo wote wameikimbia nchi na wamepata elimu zao nje tena wakati wa Mwinyi ama Mkapa. Waliobaki ni vijana walio soma ama wanasoma UDSM, na Please mkuu wana matatizo mengi sana kielimu, vifaa na njaa zikiwa ni sababu kubwa sana za kudorora kiwango cha elimu nchini. Wanasoma vyuo vikuu ili wapate ajira kesho, badala ya kusoma ili kesho wawe waajiri hii ni karne ya 20 mkubwa hayo ni mawazo ya miaka 100 iliyopita kama bado unataka kulinganisha na Ulaya.
Tatizo lako mkuu unataka kufananisha Marekani hii ya leo na Tanzania hasa baada ya kuletewa hili neno Child abuse wakati wenzetu wamewahi pitia maisha hayo hayo. Ukisoma historia za matajiri wengi na hasa Wayahudi utaona waliokotokea mkuu.

Elimu ya kujitegemea ni CHILD ABUSE (Period). Unakosea unaposema kuwa wengi ni matunda ya Mwalimu. Kwani wakoloni nao waliacha shule na wengi waliopata digrii au kusoma kipindi cha Nyerere alipitia shule za mkoloni na hivyo tunaweza kusema kuwa SHULE NA ELIMU ya darasani ni MATUNDA YA MKOLONI. Ni mkoloni aliyemfanya Nyerere ajue kusoma na kuandika. Na bila ya infrastructure ya mkoloni Nyerere asingefanya kitu.

Matatizo yako Mkandara ukada umekuzidi na unaacha kuangalia facts. Watanzania hawakuzaliwa na majembe mkononi. Hivyo kabla ya ugunduzi wa jembe zana zingine zilitumika. Na walipogundua kuwa jembe la mkono litaleta ufanisi zaidi, instantly waliachana na matumizi ya zana zilizo inferior kwa jembe.

Na mwanafunzi wa shule alikuwa anapata nafasi za kuelewa jumuia zingine zilizoachana na matumizi ya jembe na kuongeza uzalishaji wao. Na mtu yoyote anayefahamu kuwa kuna zana bora zaidi, hatakubali mafundisho yanayoendeleza matumizi ya zilizo duni.

Jiografia ya darasa ya sita ili-expose mwanafunzi wa shule ya msingi na uzalishaji wa nchi mbalimbali. Na bado mwanafunzi huyo akienda sekondari anatakiwa aende na panga na jembe. Mtaji huu ni sawa na kukubali mafundisho ya elimu ya magharibi lakini kukataa matumizi yake.
 
Sina Tatizo Kuhusu Mwalimu,ila Nasikitika Kwa Unafiki Na Tamaa Kubwa Aliyowafanyia Watanzania Ndugu Wiliam Benjamini Mkapa,mungu Atamlaani!!!
 
Nasikitishwa na mtizamo wako finyu wa kimawazo, pia pole sana kwa kutozijua nyakati,hayo ndiyo unayoyajua juu ya mwalimu,lakini usisahau sana kwani tanzania baada ya uhuru nguvu kazi ya taifa ilikuwa haina elimu ya kutosha, pia mwalimu alijitahidi kulinda maslahi ya kizazi kijacho.
Mbona unasahau kuwa viongozi wengi wa kiafrica walishindwa ni mfumo gani wa uongozi waufuate kwa kipindi kile, kenya walifuata capitalism na sasa unayaona yanayowafika, lakini kwake mwalimu alidhani kuwa kama hoja yake ya ujamaa ingeugwa mkono na viongozi wenzake Tanzania tungepiga hatua, ila wakamsaliti mwalimu akabaki boya,kwa kuthibitisha hayo ndiyo maana tunaona yeye aliendelea kuwa maskini hadi hapo Mungu alipomtwaa, angeweza kuwa kama Kenyatta au Mabutu seseko ila yeye hakufanya hivyo.
Huu siyo wakati wa kumlaumu mwalimu Nyerere na kumuita Mungu mtu,ila kwa sasa tujipange upya, kwani Tanzania hii ni yetu sote, tuijenge japo kuna vidudu watu wanaiuhujumu nchi yetu,kwa kuingia mikataba mibovu,kujimilikisha maliza umma,kama nyumba na vinginevyo.
Ndugu zangu watanzania tusiumize vichwa kwa yaliyopita kwani tunapoteza muda, kwa sasa tufikiri juu ya upandaji ya gharama za maisha,na pia ni wakati muafaka kujadili kuhusu Katiba yetu, ili tuweze kujikomboa na hayo yatakayojili hapo mbele
 
Isaya Mwita:

Utaifa kwanza. Hayo mambo ya viongozi na nchi zingine za kiAfrika walishindwa hayana mpango wa kueleza ni kwanini tunaboronga.

Ukitaka maendeleo unahitaji vitu vinne:
  1. Watu
  2. Ardhi
  3. Siasa Safi
  4. Na uongozi Bora

Vipengere hivyo hapo juu, havikuwekwa na wananchi. Ni viongozi wenyewe wamevisema wakati wakiwa na uhakika wa kufanikiwa na siasa zao. Na wanaposhindwa hakuna sababu ya kutafuta visingizio vingine wanachotakiwa ni kurudia vipengere hivyo juu na kuacha longolongo.

Hivyo, kiongozi anaposhindwa kuleta maendeleo kwa watu wake basi ubovu utakuwa katika siasa zake au kuna uwalakini katika uongozi wake na hakuna sababu ya kutaja nchi zingine za kiAfrika au kusema viongozi wengine hawakusimamia maagizo yake.
 
eti elimu ya kujitegemea ilikuwa ni child abuse? kweli hii ni shukrani ya punda manake kama elimu ingekuwa ilivyokuwa nchi za magharibi sijui wasomi wangekuwa wangapi bongo..!
 
Kwani kuna wasomi wangapi? Kungekuwa na wasomi Tanzania nchi isingeweza kutaifisha mwekezaji anayelipa 40% na baadaye kumuomba radhi arudi kwa kulipa 10%.
 
.....shoot 'em down, one by one!! Good job, Bin Maryam.....

mpaka siku watakayokubali kwamba Nyerer ndio kisa cha matatizo yetu, basi watanzania tuta/watakabaki kama walivyo.
 
Hivi aliyeanza kulea viongozi wanaoboronga na kuwahamisha toka sehemu moja hadi nyingine wakaboronge zaidi alikuwa nani vile?
 
alikuwa ni yeye aliyeanzisha ccm. Kama ccm ikiendelea kuwa madarakani basi nchi hii itaoza na kufia kaburini kama Nyerere aliye kaburini kwa miaka karibu 10.
 
All I ca say
- NDIVYO TULIVYO!
Kama sii Nyerere basi lazima itakuwa mkoloni, lakini sio sisi wenyewe!
 
All I can say is:-
NDIVYO TULIVYO!
Kama sii Nyerere basi bila shaka itakuwa ni mkoloni lakini sii sisi wenyewe.
 
Vipi Mkandara,
mbona unajichanganya? Unasema "ndivyo tulivyo" hapohapo tena unasema "sii sisi wenyewe", which is which mkuu?
 
alikuwa ni yeye aliyeanzisha ccm. Kama ccm ikiendelea kuwa madarakani basi nchi hii itaoza na kufia kaburini kama Nyerere aliye kaburini kwa miaka karibu 10.
Halafu siku zote nilikuwa nafikiri CCM ilianza baada ya TANU na ASP kuungana kumbe zote hizo fiksi, ukweli ni kwamba Nyerere mwenyewe ndiye aliyeanzisha CCM. Uzuri wa JF unajifunza jambo jipya kila siku.
 
ukimlaumu nyerere kwa sera zake, utamlaumu pia kwa kuanzisha ccm au sio mkuu. Nadhani nimepata sababu nyingine ya kuwa mpinzani wa ccm, kumbe ilianzishwa na nyerere (the guy who is dead almost 10 years now)? inaonekana hata hii sisiemu itaisha karibuni
 
Back
Top Bottom