Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Nyerere: The Man, The Myth and the Legend

Kulikoni: Mama Mwantumu Malale sio VC; yeye ni Chancellor. VC ni profesa fulani jina limenitoka.

Nafikiri hiki chuo sio secular angalau kwa vigezo vya udahiri wa wanafunzi na wafanyakazi. Takwimu zilizopo zinaonesha kuwa katika udahiri wa kwanza chuo kilichukua wanafunzi wote wa kiislamu. Hata utawala, vigogo karibu wote (kama sio wote kabisa) ni waislamu! Naomba unisahihishe katika hili kama si kweli!

Mwanasiasa,
Yes, nlikosea mimi. Mwantumu Malale ni Chancellor, na ni mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya ukuu wa chuo nchini Tanzania.

Kwa nlivyoielewa maana ya secular aliyoitumia Mwl. Mushi, nlidhani kamaanisha courses zinazotolewa na curriculum kwa ujumla. Na kwa taarifa nlizonazo the chuo is secular in that sense.

I have another correction, the courses offered so far are B.A. Education, B.A. Mass Communication and B.A. Islamic Studies (nlikosea mwanzo nliposema ni law).

Kwa kweli sina takwimu rasmi za wanafunzi na wafanyakazi, ila nlimsikia muislamu mwenzangu aliekwenda chuoni hapo akilalamika eti kwa nini chuo cha waislamu kinakuwa na walimu na wanafunzi wa kikristo, na hata mavazi hakuna restrictions zozote... hata mama Malale havai hijabu per se, na hivyo basi, kwa mtazamo wake, sura ya kuwa ni chuo cha waislamu haipo. Tukabishana kiasi mimi nikisema kuwa hiyo ndio sawa kwa mazingira yetu ya Tz, hata kama chuo ni chetu hakuna haja ya kuwatenga wengine. Hii ndio 'source' yangu, kama mwenzangu una takwimu rasmi za udahili zitakuwa na nguvu zaidi kuliko 'source' hii.

'Vigogo' karibu wote kuwa waislamu sitashangaa sana, na nadhani sio kosa. Afterall ni chuo cha waislamu. Au kule Tumaini na kwengineko kuko vipi? Ila kwa kweli ntashangaa ikiwa kuna policy ya hata walimu nao kuwa ni waislamu watupu. Namna hiyo hatufiki.
 
mwanasiasa,kulikoni,
kuna wilaya zimekuja na idea ya kuanzisha vyuo vya ualimu, halafu hapo hapo wanakuwa na shule ya sekondari. ni sawa na kuwa na medical university na teaching hospital. naamini hiyo ni idea nzuri sana na inapaswa kuigwa na maeneo mengine.

pamoja na kuunga mkono kuanzishwa kwa chuo kikuu cha waislamu, binafsi ningewasisitiza kuongeza juhudi ktk kuboresha elimu ya sekondari kwa vijana wao.

shule za sekondari zilizosajiliwa tanzania zinakadiriwa kufikia 500. wakatoliki wana shule za sekondari 120, walutheri wanazo 50. waislamu,waanglikana, na wasabato, wanazo shule ngapi?

Yap, that is a great idea... inabidi kuigwa.

Kwa nnavyofahamu, sababu ya kuwa moja ya vitivo vya kwanza vya chuo hicho kuwa ni EDUCATION, ni ili kuweza kuwaandaa waalimu wa kuboresha shule za sekondari zilizopo .. na possibly zitakazojengwa baadae.

Sina idadi ya shule za waislam, waanglikana na wasabato ... lakini ni wazi kuwa individually hazifikii hizo za wakatoliki. It is something madhehebu haya inabidi nayo yaongeze juhudi.
 
mie sioni tatizo liko wapi

hilo la kambi za jeshi nimeridhika kwa kiasi na maelezo yako

je hilo la kufanya maeneo yote ya pwani kuwa HIFADHI YA TAIFA ndio nini?

niliuliza swali kuwa ni jukumu la nani kupeleka maendeleo kwa wananchi?
 
By the way MKAPA alikuwa mtu miongoni mwa watu na waislam wanamvalue high kuliko huyo Mwinyi na JULIASI

by the way mnajua kwa nini Mwalimu alimpiga vita Malecela?
 
Swali la kwa nini wakati wa Mwinyi wengi wa viongozi waisilamu walijitokeza wakati enzi za Nyerere walikuwa kimya nakubaliana nalo kabisa, Lakini naomba tuliangalie pia katika hii awamu ya nne ya JK, Kuna viongozi wengi sana hapo kati wakati wa BM hawakuwahi jionesha kuwa wao pia ni swala tano, hat misikitini iwe ijumaa au siku yoyote walikuwa hawafiki. Lakini mara baada ya serikali hii ya JK wamegeuka kuwa swala tano, ukifika ofisini utaambiwa boss yupo msikitini saa za kazi. Na hili ukitaka lianyie uchunguzi utajua ninachosema ni nini.. Nenda msikiti mmoja upo pale upanga kila siku saa saba, utakuta magari ya serikali hadi yanakosa parking yamefurika . Secretary na gari lake la ofisi, ofisa naye na gari lake , boss naye na gari lake. Swali linakuja mbona wakati wa BM watu hawa hawa walikuwa kimya!! Hatukuona magari ya umma yakijaa misikitini wala makanisani , !! imekuwaje sasa!!!??? Na ukienda ofisini kwao tuliwakuta bila visingizio.
Jibu linakuja kama mmoja alivyojibu hapo juu, kuwa ni tabia ya viongozi wetu kujipendekeza baada ya kuona kiongozi wa juu ana msimamo gani, hivyo katika kuwinda madaraka inawabidi wabadilike mienendo machoni pa watu, lakini wakiwa mafichoni tabia zinabaki pale pale.
 
sasa hoja yako ni nini?

naona mfano wako n msikiti wa pale Upanga

mona husemi yale yanayojazana pale St Peters au ST Joseph?

mimi sioni kama kuna tatizo kama sheria hazijavunjwa kama zimevunjwa sawa

japo msimamo wangu ni kuwa sipendi dini kwa ujumla lakini usiwabully watu waliona dini zao hali kadhalika wasio na dini nao inabidi waheshimiwe

Mfano Nyimbo yetu ya Taifa imekaa kidini dini sasa wasio na dini haki zao ziko wapi? maana sio kila mtu anaamini Mungu au dini wakai huo huo humu ndani tunaongopeana kuwa serikali haona dini
 
DrWHO,
Hii ya kuyafanya maeneo yote ya pwani kuwa hifadhi ya taifa ndiyo mara ya kwanza naisikia. Kwa hiyo ukipata taarifa zaidi tumwagie hapa.
 
Jasusi.

Nyerere alikuwa mkabila wa kutupwa,
Alimpa warioba uwaziri mkuu huku ni ndugu yake, alimpa Musuguri ukuu wa jeshi sababu ni kabila lake. wako wengi miongoni mwao ni Charles Nyirabu alipewa ugavana mkuu wa BOT.

hadi kina Butiku ni watu wa nyerere, jasusi Musoma iliwekwa mbele na Nyerere.
 
Kulikoni: Mama Mwantumu Malale sio VC; yeye ni Chancellor. VC ni profesa fulani jina limenitoka.

Nafikiri hiki chuo sio secular angalau kwa vigezo vya udahiri wa wanafunzi na wafanyakazi. Takwimu zilizopo zinaonesha kuwa katika udahiri wa kwanza chuo kilichukua wanafunzi wote wa kiislamu. Hata utawala, vigogo karibu wote (kama sio wote kabisa) ni waislamu! Naomba unisahihishe katika hili kama si kweli!

Kama sikosei VC ni Prof. Iddi, alikuwa SUA halafu akateuliwa kuwa mkurugenzi wa Misitu na sasa ndio VC pale.
 
Mfano Nyimbo yetu ya Taifa imekaa kidini dini sasa wasio na dini haki zao ziko wapi? maana sio kila mtu anaamini Mungu au dini wakai huo huo humu ndani tunaongopeana kuwa serikali haona dini
DrWHO, kutokuwa na dini haina maana kuwa huna imani, sitaki kuamini kuwa kuna binadamu wenye akili timamu wasio na imani, kama wapo ni wakuhesabika, kwani saikolojia ya akili ya binadamu inamkwalify moja kwa moja kuwa na imani. Vipi kuhusu kuapisha viongozi, tuache pia? Swala tu la kuimba wimbo wa taifa ukiwa umesimama wima bila kutikisika, achilia mbali content ya wimbo, hiyo ni ibada tosha!hiyo ni imani, kama sio dini🙂
 
Jasusi

uistajaabu ya Musa utashangaa ya Firauni

je ya kuwa Nyerere aliamuru Reli ya Mtwara ingolewe nayo huna habari?




dondola

mimi personally nisingependa mwanangu awe anaimba nyimbo ya tafa inayomwambia Mungu hivi au vile

hii itabidi tuitafutie thread tofauti
 
Mzee IO,

Ume-raise a very interesting issues, kwamba betweeen Mwalimu na viongozi waliofuatia the gap ni pana mno, na the udini kipindi cha Mwinyi. Kwa kweli inasikitisha sana, kwa mfano kwenye uchaguzi wa mgombea Dodoma wa CCM, kulikuwa na theme iliyokuwa ikienezwa na Mtandao, wakiongozwa na Nchimbi, kwamba "......Hiii ni zamu ya Waisilamu..." , Ilikuwa ni aibu kubwa sana tena sana, ndio maana matokeo hayatushangazi tuliojionea kwa macho huu upuuuzi, kigezo cha uongozi kikiwa ni pamoja na dini, matokeo yake ni mikataba ya Richmond!

Mzee Joka Kuu,

Hapo umenena, kwamba hawa viongozi wetu wote ni wasaniii watupu, ndio maana matokeo ya uongozi wao ni usaniiiii tu!

Now with all this said, the great leader Mwalimu, kwa nini hakukuwa other greats karibu yake? Na kwa nini hakuliona hili? Maaana look China, the great leader Mao alikuwa na wafuasi ambao ni greats too, hebu angalia kina Guo-Feng, Deng, Chuo, ukirudi hapa Africa, kina Mandela wameacha hawa kina Mbeki, Zuma, ndugu yangu hawa wafuasi nao ni moto wa kuotea mbali, sasa sisi bongo ilikuwaje?

I mean look at Mwinyi, Mkapa na sasa Muuungwana JK, hili ni balaaa gani hili? Please Mzee Jasusi help me kuelewa? What is this mess? A great man aliwezaje kuzungukwa na hawa wasaniii? Hebu angalia Martin Luther King kule ma-US, akawaacha kina Jesse Jackson, Andrew Young, Al-Sharpton wote wakali, sasa sisi bongo WHY? Ninasema WHY? Akatuachia kina Ditopile?

As a nation tunakwenda wapi? tutajuaje tunakokwenda kama hatujui tulikotoka? Hao kina Sykes Dosi Aziz, walikuwa ni watu baaaaaabu kubwa, hawakujali dini hao ndio maana makaputula Mwalimu alipokuja mjini, waligundua kuwa anazo talent ambazo hawana wakampa nafasi, kina Chimwenye, Kawawa hawa walilkuwa ni watu baaaaabu kubwa, the man hata Obasanjo anamzimia kwa kitendo cha kumshikia power Mwalimu mpaka aporudi tena, na kumrudishia bila ya kum-betray, yaani lets say walikuwa hata na udini, lakini wali-deliver, sasa leo vipi? Watu wanataka udini lakini hakuna anayeweza ku-deliver, WHY?
 
Unajua tatizo kubwa la sisi watanganyika ni kwamba "tunalalamika na kulalama sana"

Nadhani tatizo kubwa ni kwamba historia ya Tanganyika imepindishwa sana na bado inapindishwa aidha kwa makusudi kwa kwa faida za wachache walioko madarakani au wanaotaka kuwa madarakani.

Hivi wangapi wanakumbuka baraza la kwanza la mawaziri lilikuwa na mawaziri wangapi. Sasa mngetaka watu wote wapewe uwaziri au la, pia kumbuka wakati ule hawa watu walikuwa na nafasi kubwa kwenye chama ndiyo maana wakapewa hizo nafasi.
Mimi ni mmojawapo ya watu wanaopinga kuwa mkabila, angekuwa mkabila nadhani leo hii wachaga wangekuwa Kabila la mwisho kabisa kupiga hatua. nadhani mwalimu alizingatia zaidi elimu na uwezo wa mtu kutenda kazi.

Kuna mtu kauliza mbona wakati wa Nyerere hatukusikia maProfesa wa Kiislam. Swali langu ni kwa nini wakati huo pia hatukusikia maprofesa wa Kikristu au madokta kama sasa hivi.
Jibu ni kwamba wakati wa nyerere kipao mbele kilikuwa ni utendaji na siyo kujikwaa kwa elimu au vyeo. soma mojawapo ya hotuba zake "the Intelectual need of the society"

chinga:
Kwa hiyo na JK ni mkabila siyo au.

Haya sasa nyerere kaachia madaraka zaidi ya mika 25 iliyopita, linganisha swala la dini na ukabila wakati wa Nyerere na baada ya Nyerere.
Ukirudi kwenye swala la elimu:kama mwalimu angekuwa mdini kama tunavyoambiwa leo hii, nadhani Tanganyika (Tanzania Bara) tungekuwa tunaongea mengine kabisa. Halafu tukumbuke shule nyingi za kanisa zimejengwa baada ya Nyerere kuondoka madarakani. mfano asilimia 80 ya shule zote mkoani Kilimanjaro zimejengwa wakati wa Mwinyi ( kwa hiyo na Mwinyi alikuwa anawapendelea Wakristu).

Tukubali kutokubaliana. Mabaraza ya Kikristu yana tofauti moja kubwa na ya waislam, nayo ni priority. Kanisa limeweka elimu na afanya namba moja kwenye agenda zake, ndiyo maana hata kabla ya kujenga nyumba ya ibada (kanisa) wanajenga shule na zahanati. wao wanaamini dini peke yake haiwezi kuleta maisha bora bila elimu bora na bila elimu bora huwezi kuwa na afanya njema. Mabaraza mengi ya Kiislam yao yameweka kipao mbele kujenga misikiti na kufundisha dini. Hebu niambie ni shule ngapi Dar na Pwani (mikoa yenye waislam wengi) zinamilikiwa na waislam. haitoshi tu kusema wanaonewa au walionewa angali hatuoni jitihada zao.

Hivi unajua madhehebu ya Kikristu yakiamua kujitoa kwenye huduma ya elimu na afya, Tanganyika itarudi nyuma kijamii, kielimu na hata kiuchumi kwa zaidi ya miaka 50. Jaribu kuangalia uwiano wa shule na taasisi za afya zinazomilikiwa na madhehebu haya na zile za Serikali.

mwisho,
nadhani ni wakati wa kulaumu wafu angali walio hai wameshindwa kufanya cho chote.
 
After Sokoine death the system crumbled kwa sababu waliokuwa wanakula rushwa walianza kushamiri tena. Sokoine was the man lakini hakupewa ulinzi wa kutosha.
 
Chinga,
Naona umerudi ndugu yangu. Na hujabadilika. Warioba ni Muikizu. Nyerere alikuwa Mzanaki. Kule Musoma kuna makabila zaidi ya 20. Usishangae. Kuhusu Musuguri nilishawahi kumjibu Mzee ES kule BSC. Kwa hiyo sina muda wa kurudia. Ukabila na udini umeukumbatia mwenyewe. Nakuombea ukombozi.
 
Mzee Dua,

Lovely, point well said, Sokoine was the man baada yake ndio tukaanza kupata hawa viongozi vilaza ndaza watupu!
 
Siamni kuwa Mwalimu alikuwa mdini, lakini ninamfahamu Mzee Mwakawago na robo tatu ya uliowataja mbona ilikuwa sio rahisi kujua kuwa ni Waisilamu? Mpaka Mwinyi alipoingia? Mimi sikujua kuwa Kaduma ni Muisilamu mpaka ulimpotaja leo? Sikujua kuwa Kitine ni Muisilamu mpaka siku moja majuzi nilipomuona bungeni amevaaa kanzu?

Malima mwenyewe ni mpaka enzi za Mwinyi ndio nilikuja gundua kuwa ni Muisilamu, ni kwa nini walikuwa wakijificha? Halafu kwenye list yako umemuacha Maswanya, siamini kuwa Mwalimu alikuwa mdini, but somebody needs to explain ilikuwaje wasialamu walikuwa wanajificha? Mwakawago hata unitishie bunduki ninakukatalia kuwa haakuwahi hata kuonyesha dalili za Uisilamu, mpaka Mwinyi alipoingia, WHY?

Ingawaje ninaheshimu kujitahidi kwako kutoa data, lovely, na udumu!

Mzee P,

Sidhani kama ninaelewa unachosema, ni yupi anyelalamika hapo juu au wewe ndiye unayelalamika, hebu nisaidie kuelewa?


Wanakijiwe, wiki hii ya mwisho wa semester imenibana kiasi nashindwa kuhudhuria klikao hiki sawa sawa; kwa hiyo kama nitarudia yaliyokweisha zungumzwa niwieni radhi.

Mzee ES

Watu hawa dini zao zilikuwa hazijulikani iyo kuwa walikuwa wanajificha, kwani walikuwa wakihudhuria misikitini kama kawaida. Tuwe wakweli kuwa mtu asingeweza kuficha dini yake dhidi ya serikali ya mchonga. Wakati wa Nyerere dini haikuwa mbele ya utaifa kwa hiyo watu walikuwa wanajitambulisha kwa kwa nafsi zao na uwezo wao kikazi bila kuambatanisha dini zao. Wakati wa Mwinyi ndipo udini ulipoanza na watu hasa waislamu kuanza kujitambulisha kwa dini zao.

Aljazeera,

Umesema bila kuzunguka dondoo.
 
Mzee ES,Dua,
Sokoine, MUNGU amrehemu, sera na mtizamo wake zilikuwa za ajabu sana. Hakuwa mtu mwenye upeo wa kufufua uchumi kwa wakati ule.

Binafsi, siamini kama tatizo la Tanzania ni rushwa peke yake. Tatizo kubwa zaidi ni uongozi usiokuwa na mbinu za kutatua matatizo ya Mtanzania.

Kama Sokoine alikuwa waziri mkuu bora kuliko wote, mbona hali ya uchumi wakati wa uongozi wake ilikuwa mbaya kuliko wakati wowote ule wa historia ya tanzania? maamuzi aliyokuwa akichukua yalikuwa kinyume kabisa na kanuni za msingi kabisa za uendeshaji uchumi.

Mwalimu alimsikiliza na kufuata ushauri wa Sokoine,matokeo yake uchumi uliendelea kuporomoka. Mwisho, Mwalimu aliona mawazo ya watu kama Sokoine hayafai, nchi imemshinda, akaamua kuwaachia wengine wajaribu.
 
Mzee Es,
Point yako nzito sana, haibebeki na mnyonge wa kufikiri..

Uliposema haya majina ya watu kufahamika wakati wa Mwinyi hali watu hawa walikuwepo na digree zao wakati wa Nyerere!...
Simple kabisa kuwa wakati wa mwinyi ndipo watu walianza kutazama watu kwa rangi zao yaani dini.
Katika makuzi yetu sisi hatukuwahi kufikiria dini za viongozi ama wataalam wetu. Haya ya kusema waislaam walikuwa kiasi fulani bungeni sijui baraza la mnawaziri nimekuja yaona hvi majuzi. Tazama hata vitabu vya kina Ali Mazrui na Abraham Babu vinazungumzia mfumo wa siasa, upeo wa Nyerere ktk malengo ya kisiasa ama kiuchumi basi na sio dini yake.
Na ukitaka kutazama kuwa sasa hivi tumefikia pabaya, angalia watu wanavyoanza kuhesabu shule za wakristu against waislaam, na wengine hata kusema waislaam wajitahidi...hapa mshikaji ni rangi tupu kila mtu na kundi lake.
Nitarudfia tena kusema huu ndio udini, nakuhakikishia waislaam wanachukia kila wanapoona wanazidiwa kete! yaani macho yao pia wanahesabu mafanikio ya wakristu. Hao wanaodai kuwa Mkapa kafanya jambo la maana nao hawatazami nje ya kabati hili la udini.
Toka lini kuwepo na mafanikio wakati unawatenganisha watu kwa rangi zao? je, sio hivi alivyofanya mkoloni na tukapiga makelele weee kuutaka UHURU wetu. Hamkumbuki kuwa wahindi walikuwa wakisema lugha hiyo hiyo mnayotumia leo kutunyooshea vidole waafrika kwa kutokuwa na uwezo wa kujenga shule zetu wenyewe. Shule zote nzuri baada ya za wazungu zilikuwa za wahindi na huko ndiko tunakoelekea.
I mean guys, wakristu mlikuwa na mashule kibao ambayo yamejengwa na makanisa kwa kupitia mkono wa mkoloni. Hakuna mwafrika hata mmoja aliyejenga shule hata moja. Mkoloni ndiye alijenga hizo shule kutupumbaza na kama wnavyofanya Barricks leo hiihuko vijijini hali wakiiba mali zetu kwa mabillioni...Tulichoachiwa na mkoloni kipi zaidi ya biblia ambayo tulikuwa nayo katika roho zetu kabla hata Mkoloni mwenyewe hajatinga Afrika.

Nakuombeni, tafadhali yasomeni kwa makini maelezo ya Mzee ES, kuna dawa kubwa sana. udni ulianza wakati wa Mwinyi kwa sisi kuwatambulishwa watu kwa dini zao.,, na sisi tunapokubali kuwatambua kwa dini zao inajenga zaidi Udeini kati yetu. Sasa tumefikia hata kutambulisha shule kwa dini zakeviongozi wakichaguliwa kitu cha kwanza tunasoma jina kutafuta dini yake na kama kuna kitu Dr. kinachotangulia. WHY?...Guys what's going on? Kuna shangazi wetu walikuwa wakifundisha shule ya msingi Forodhani kwa zaidi ya miaka 30, leo hii wameachishwa kazi kwa sababu - color of their faith (waislaam). Tunakwenda wapi?...
 
jokaKuu

Sokoine alikuwa PM 13 Feb 1977 hadi Nov 1980 alipojiuzulu kutokana na afya yake. Alirudi tena kuwa PM 23 Feb 1983 baada ya kutibiwa hadi Feb 1984 alipofariki kwa ajali.

1. Upeo upi ambao unaongelea?

2. Je ni nani aliamuru bidhaa kutoka nje kuingizwa Tanzania na wafanya biashara ambazo zilikuwa hazipatikani Tanzania kwa wakati ule?

3. Ni nani ambaye alikuwa na ubavu pekee kumweleza mwalimu matatizo ya wakati ule?

4. Sikusema Sokoine alikuwa waziri mkuu bora kuliko wote kwa sababu sina data, hayo ni mawazo yako – kwa vile umeliongelea hilo Je unaweza kuweka data hapa za uchumi wa Tanzania tangu tupate uhuru ili tuweze kulinganisha ni waziri mkuu yupi alikuwa bora?

5. Ni waziri gani mkuu aliyefuata kanuni na misingi ya uendeshaji wa uchumi na ametufikisha wapi?

6. Ni wapi ambapo mwalimu aliona mawazo ya sokoine hayafai? Unaweza kufafanua hili?

7. Mwalimu alisema mwaka 1980 ndio angeachia hatamu lakini baada ya vita ya Uganda aliendelea kwa miaka mingine 5 ya mwisho, sasa ni wapi ambapo mwalimu aliona ameshindwa awaachie wengine? Siye huyu mwalimu aliyeweka mapango wa kikomo kwa viongozi?
 
Back
Top Bottom