Nyerere alisingiziwa mengi sana

Nyerere alisingiziwa mengi sana

Sasa jibu na hili, mbona unalikwepa swali?

BOT kabla ya Nyerere kung'atuka iliwaka moto na hakuna senti moja iliyobakia, ni nani alichukuwa? ni nani alichunguza?

Kwenye swali lako unasema kuwa BOT "iliwaka moto na hakuna senti moja iliyobakia".

Sasa tutumie mantiki, sawa?

Kama BOT iliwaka moto na hakuna senti moja iliyobakia, je, huoni kwamba kuna uwezekano wa hizo senti zote zilizokuwamo humo BOT kuteketezwa na huo moto?

Ni nani alichukua?

Hapa ndo hueleweki kabisa. Unauliza ni nani alichukua hizo senti ilhali ushasema kuwa hakuna senti moja iliyobakia katika huo moto!

Huo moto haukuzitekeza hizo senti zilizokuwamo humo?

Ni nani alichunguza?

Mi sijui ni nani aliyechunguza.

We unajua?
 
Sio bure,huyu bibi kuna jambo alitendwa na Mwalimu mpaka kumchukia Kias hicho.Ngoja nijaribu kuyaorodhesha:
1.Nyerere kupiga ban kadhi court
2.Nyerere kupinga udini
3.Nyerere kuchukua all the credit kwa upatikanajI wa uhuru wakati ni mkristu
4.Nyerere kuongoza nchi kipindi kirefu huku ni mkristu
5.Nyerere kumkemea mwinyi hadharani kugeuza ikulu pango la walanguzi.
6.Nyerere kumtosa Jk mwaka 1995 na kumpa shavu Mkapa

Mtu anayemfahamu mleta mada kupitia threads zake mbalimbali atakubaliana na mimi kwamba kwa udini wake,hizo facts hapo Juu ni baadhi ya sababu za chuki za huyu bibi dhidi ya mwalimu.

Ongezea sababu nyingine kama unazo
 
Sasa jibu na hili, mbona unalikwepa swali?

BOT kabla ya Nyerere kung'atuka iliwaka moto na hakuna senti moja iliyobakia, ni nani alichukuwa? ni nani alichunguza?

Hili swali lako limekaa kimtego sana. Kama Bank iliungua ni wazi pesa zisingesalimika. Labda kama una ahakika chumba cha kuhifadhia pesa (strong room) hakikuungua na hakuna senti iliyokutwa ndani ya chumba hicho, hapo hata mimi nitajiuliza nani alichukua?
 
Hebu jibu hoja, Uliona wapi Nyerere anajiita DK? Japo kwa IQyake alistahili hata kujiita Prof.aliona haina haja kwani mwenye akili anajulikana tu hata bila hizotitle. Nia yako wewe si nzuri hasa baada ya kupitishwa hili lisheria lenu hili!
Mmemsingizia vingi mwalimu. Eti alizuia TVs ili yeye tu ndioanaonekana ana akili. Haya sasa hivi mna uhuru na mainformation kibao mbona hatuoni mambo ya maana?

Uliona wapi mwengine yeyote anajiita Daktari?
 
Hili swali lako limekaa kimtego sana. Kama Bank iliungua ni wazi pesa zisingesalimika. Labda kama una ahakika chumba cha kuhifadhia pesa (strong room) hakikuungua na hakuna senti iliyokutwa ndani ya chumba hicho, hapo hata mimi nitajiuliza nani alichukua?

Swadakta. Hakuna mtego, ni alichunguza? majibu ya uchunguzi yako wapi? na kama ulivyosema benki kuu ni lazima ina "strong room", vipi nayo iliunguwa pia?

Ch a kushangza zaidi na Wizaa ya mabo ya ndni inayohusika na hayo ya uchunguzi nayo ikaunguwa!
 
Tatizo kubwa nnaloliona ni watu kukosa mantiki, sasa wewe kwanini unanishutumu na hyo mambo "anasingiziwa"?

Tuanze na namba moja, jee hauioni mantiki iliyopo?

Hapo sasa inatakiwa, kwa faida ya wengi uje na historia na utuelezee kuwa hakusingiziwa, alipigania hivi na hivi na hivi.

Si wewe kuja na kuanza kunishambulia mimi niliyetowa fursa ya watu kumfahamu mzee Nyerere.
We ni mdini...na malay..a mkubwa ww.huna hekima kabsa mpuuzi ww.
 
Nadhani anasingziwa pia kuwa alikuwa Rais wa kwanza wa Tanzania.
 
Nina uhakika lugha ya Kiswahili unaijua vizuri kabisa. Ila inaonekana maana pekee ya "kupigania" uliyonayo ni kukunjiana ngumi au kumwagiana risasi. Kama hii ndiyo maana uliyonayo sidhani kama kuna watu ambao wanaweza kusema kweli "walipigania" uhuru wa nchi yetu.



Mbona hili hajasingiziwa. TANU bila Nyerere si TANU. Labda tumtafute Rais wa kwanza TANU tumuulize.



Kwanini alitakiwa kuiipenda Tanganyika? Aliipenda Tanzania zaidi bila ya shaka. Sidhani kama kulikuwa na mzungu aliyekuwa Katiba wake mpaka kufa kwake. Katibu wake hadi mauti yanamkuta alikuwa Mtanzania.



Hilo kweli wanamsingizia; hakuna mahali popote katika Historia Nyerere alitajwa kuwa ni Medical Doctor. Ila kwamba alipata shahada kadhaa za heshima za Udaktari hili mbona halina mjadala.



Hakuna mtu yeyote anayejua historia yetu kama taifa anayeweza kusema hivyo. Ila Nyerere ndiyo anashikilia rekodi ya kuwa Mtanganyika wa kwanza kusoma katika Chuo Kikuu cha Uingereza (University of Edinburg). Lakini pia anashikilia rekodi ya kuwa Mtanganyika wa kwanza kupata shahada ya uzamivu (Masters degree) Hili siyo kumsingizia. Inawezekana wanahistoria wamekosea sasa hivyo ili usahihishe unatakiwa useme Mtanganyika wa kwanza kusoma chuo cha Uingereza alikuwa nani na wa kwanza kupata Masters alikuwa nani. Then mjadala unanoga au historia inasahihishwa.

Hao wote uliorusha majina yao hujatuambia nani alisoma wapi na alihitimu mwaka gani ili tulinganishe. Kurusha majina tu hakufanyi kitu kiwe kweli. Inakuwa kama yule msomi mwingine wa histohisia ambaye historia ilimshinda.


Sasa hicho ndiyo kipimo cha mapenzi. Mbona kuna wazazi wanaopenda na watoto wao wengine wote isipokuwa kichaa mmoja; sasa utasema hawapendwi kwa sababu kichaa mmoja alitaka kuchoma nyumba? What kind of reasoning is this?




Sijui mantiq umesoma wapi mwenzetu; kama nyumba imeungua na kila kitu kikapotea sasa kinachoibwa kinabiwa vipi? kikiwa majivu?




Hadi hapa hakuna lolote ambalo umefanikiwa kuonesha kuwa alisingiziwa. Labda uje na orodha mpya tuione.
Ningeshangaa, atajwe nyerere bila mwanakijiji kujibu hata kama ni majibu ya mradi kujibu tu.
 
Ooh, vyema kabisa, kwa hiyo Nyerere hakusingiziwa Udaktari, ni kweli kabisa ni Daktari na umedhihirisa hilo bila ya shaka yoyote. Ukweli kabisa nimeridhika na data ulizoshusha na Nyerere alipewa u Daktari wa heshima na ndiyo maana ni Dr. Nyerere.

Ajabu ni pale watu wanapokejeli u Daktari wa Kikwete. Hauoni kuwa ni "double standard" wakati wote wametunukiwa u Daktari wa heshima?

Upo hapo ulipo?
nahisi kama umechanganya udr na uprof
 
Anasingiziwa na nani? Kikwete naye siku hizi ni daktari. Je, naye anasingiziwa?



Ushahidi kwamba alishindwa masomo ya sayansi uko wapi? Na kwani wote waitwao madaktari wamesomea masomo ya sayansi? Kikwete naye kasomea masomo ya sayansi?



Sasa kama BOT iliwaka moto na hakuna senti moja iliyobakia, kwa nini unauliza nani alichukuwa? Nani alichukuwa nini kama hakuna senti moja iliyobakia?



Hata mantiki nyepesi tu zinakushinda! Unasema BOT iliwaka moto mpaka kuteketeza kila kitu halafu kwa wakati huo huo unadokeza kwamba huenda Nyerere aliiba. Nyerere ataibaje vitu vyote vilivyoteketezwa na moto? Aliiba majivu?

Nyani Ngabu...salute mkuuu! Kuna watu wanajua yamewafika wanataka pakutokea
 
Last edited by a moderator:
Anasingiziwa na nani? Kikwete naye siku hizi ni daktari. Je, naye anasingiziwa?



Ushahidi kwamba alishindwa masomo ya sayansi uko wapi? Na kwani wote waitwao madaktari wamesomea masomo ya sayansi? Kikwete naye kasomea masomo ya sayansi?



Sasa kama BOT iliwaka moto na hakuna senti moja iliyobakia, kwa nini unauliza nani alichukuwa? Nani alichukuwa nini kama hakuna senti moja iliyobakia?



Hata mantiki nyepesi tu zinakushinda! Unasema BOT iliwaka moto mpaka kuteketeza kila kitu halafu kwa wakati huo huo unadokeza kwamba huenda Nyerere aliiba. Nyerere ataibaje vitu vyote vilivyoteketezwa na moto? Aliiba majivu?

Katika points 7 umejibu mbili tu, ina maana unakubaliana na 5 zingine? au?
 
Naona hauelewi kuwa Nyerere alishapinduliwa na ujumbe ukapelekwa kwa U Thans, aliyekuwa mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati huo. Na aliyeyageuza mpinduzi hayo na aliyemuokoa Nyerere na utawala wake ni kati ya hao wajaa "laana".

Unalijuwa hilo?

Nimefurahi kuwa hujakataa kusingiziwa huko kwa Nyerere.

11151026_672328369561213_7796217978073870866_n.jpg
 
Hivi mtu unapata faida gani kumsimanga marehemu....mtu ambaye hakusikii wala hakuoni...mtu ambaye hataguswa na maneno yako kamwe....kuendelea kumjadili au kumsimanga marehemu...ambaye ni mwanadamu kama sisi...ni kuupoteza muda ambao ungetufanya turekebishe pale ambapo tunahisi alikosea kama mwanadamu na kuyaenzi yale mazuri aliyotuachia....

Nyerere ataongelewa sana kwa miaka mingi ijayo, hilo halizuiliki. Ni Rais wa kwanza wa Tanzania.
 
Nyerere wetu, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika na Rais wa kwanza wa Tanganyika na Tanzania, kasingiziwa mengi sana.


Si kweli, kuwa ni mzalendo. Nyerere hajawahi kumuamini mtu yeyote mwenye asili ya Kiafrika, Nyerere alimuamini mtu mmoja tu katika maisha yake yote, nae ni Mzungu aliyekuwa katibu wake mpaka kufa kwake.


Nikirudi narudi na mengine saba aliyosingiziwa Nyerere.

Duh!
Hilo limenifanya kujiuliza kwanini amuamini huyo Mzungu.

Anyway R>I>P Mama Joan.



[h=3]Obituary: Joan Wicken | News | The Guardian[/h]
Thus did Joan, who has died aged 79, travel the country raising cash from peasants - who would contribute a goat or chicken if they did not have money - and better-off sponsors.
 
Alikuwa mdini

Nchi yenye Makabila 267 na Dini 11... kwanini asiwe Mdini na kuunganisha Watanzania Wote? Ukienda Kaskazi; Kusini; Mashariki na Magharibi nchini Unaongea KISWAHILI...

Jaribu - Kiarabu HUKO YEMEN; KISWAHILI - KENYA...

Amani ndio Muhimu...
 
Sipotezi muda wangu kujadili none-sense kama hizi. Karne hii mtu anakuja na hoja za udini na ubaguzi???

We usimheshim Nyerere, Laana itakuandama. Tuache sisi na Nyerere wetu.
 
Nyerere ataongelewa sana kwa miaka mingi ijayo, hilo halizuiliki. Ni Rais wa kwanza wa Tanzania.

Huwa ninajiuliza sana bila majibu, hivi inakuwaje FaizaFox anamchukia sana Nyerere (founder of CCM) but at the same time anaipenda sana CCM?!

Nini kilichojificha nyuma ya hii HATE AND LOVE ya FaizaFox?!
 
Faiza namba 7,nimecheka mpaka basi.Kama ushahidi wenyewe ndo huo nimethibitisha uelewa wako.Hebu nambie Nyerere ni moto ?Bot imeteketea na wewe unamtuhumu nyerere kaiba kwa nn usiwe mkweli moto uliiba kama pametokea wizi ?
 
Back
Top Bottom