Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Mungu yu mwema sana na atakuadhibu kwa kukufuru kwako akili yako itakuwa imekufa!hutaitambua hiyo 2035.
nasema mungu yu mwema na ninayaweza yote kwani ni yeye tu ndiye anitiaye nguvu nakwambia tukutane 2035,nasema nikitumaini mungu hato niangusha
 
Ukiona hivyo ujue Nyerere alikua mwiba mkali kwa hawa wachumia tumbo thats why wana m-diss
R.i.p Nyerere
 
Usimrithishe mtoto mali....

mpe elimu....

hapo chacha ndipo baba alipokosea

Unadiriki kubeza mchango wa Mwalimu katika kuondoa ujinga wa watu wa taifa hili!!! Mtendee haki Mwalimu ndugu yangu.
 
faiza foxy hebu twambie ambapo alikosea mwalimu hadi pakapelekea wengine kushindwa kurekebisha hado sasa.
 
Last edited by a moderator:
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.

Ngoja nikusaidie kidogo.
Nchi haijengwi kwa mwaka mmoja au mika 10 au 20, ujenzi wa nchi ni kitu cha kuendelea.

Maendeleo ya kweli katika nchi yeyote ile ni kwanza kuwajenga/kuwaendeleza watu kisha watu wajiletee au wajenge nchi yao.
Nchi yeyote lazima itafute dira yake ya kuingoza.
Nyerere alipochukua nchi toka mikononi mwa Waingereza nchi ilikuwa maskini, watu wake wengi walikuwa hawana hata elimu ya awali ya lazima. Huduma za Afya zilikuwa mbovu au zilikuwa hazipatikani maeneo mengi vijijini.
Alichokifanya ni kwanza kuboresha elimu ya nchi, kuhakikisha kila raia mwenye umri wa miaka 15 anajua kusoma na kuandika.
Anaanza kuwaunganisha Watz wa Pwani na Bara wawe wamoja ili Mmnakonde asimchukie Mmasai mgeni au Mpare asimshangae Mnyakusa n.k.

Baada ya kuwaungainsha watu badae analeta udhibiti wa amani ya nchi, wale wenye mihemko na jazba za kidini wasijeleta sintofahamu katka nchi yetu, anawakaba Wakristo kwa Waislam wenye siasa kali.

Anajenga vijiji vya ujamaa ili watu wakae pamoja waweze kupata huduma za jamii kwa urahisi.
Anaafanya uchunguzi wa kujua kuna rasilimali zilizokwepo na anazilinda ili Watz wake baada ya kuelimika waje kuzivuna kwa ufasaha.
Analeta siasa ya ujamaa na kujitegemea, kwa kua Ujamaa ni mfumo rahisi kumsadia maskini zaidi ya Upebari unaozidisha gap/tabaka la wenye nacho na wasio nacho.

Anajenga viwanda vingi tokea vya nguo, mbolea zana za kilimo,kusindika vyakula n.k .
Na mengi sana ya kujaribu kuleta amani kwa majirani zake.

Sasa waliofuata baada yake walipaswa kuendeleza tokea hapo kwenda mbele, sasa wao wakaamua kuua viwanda kisha kuviuza, kisha kuuza raslimali kwa wageni sasa mwenye kosa ni yeye au hao waliobadilisha nia yake dhabiti???

Najua miaka ya hivi karibuni wametokea wanasiasa wanaotaka wao wasifiwe zaidi ya Nyerere hivyo wanatafuta namna gani wamchafue Julius Nyerere, lakini wamejaribu sana ila wanaambulia aibu mwisho wa siku.

ANGALIZO.
Usichukie watu kwa sababu ya dini zao au kwa sababu ya uchumi wao. Amini unachoamini na fanya kazi
 
Rasilimali zote hakuzigusa, viwanda vyote kang'atuka vikifanya kz, mashirika ya umma na vyama vya ushirika vikiwa imara, umoja na mshikamano pia. Makosa yapi unayoweza jenga hoja kwa mtu aliyetangulia mbele za haki? na tokea kang'atuka mpaka sasa awamu nne za utawala zimeshindwa kurekebisha makosa hayo pamoja na kukua kwa teknolojia?. Ukiyaona hayo tuungane pamoja kama watanzania kuangusha ccm tuanze upya.
 
he has been died for a long time now, and he has been out of power for even longer. So, hayo makosa yake yanasubiri afufuke ili yarekebishwe?

And why are you so obsessed with someone who has been out of power - and this world - that much? Kwa nini usituambie tujadili yanayofanywa leo na walio madarakani leo hii ambapo kila kukicha ni bora ya jana?

tutumie lugha ya taifa tu mkuu!
 
Nyerere walimwita haambiliki. Jaribu kumshauri uone chamoto. Dikteta nyerere kaimaskinisha nchi hii kwa sera zake zisizotekelezeka.
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.

tumlaumu kwa kutofanya wazazi wako wakasoma matokeo yake wakazaa taahira kama wewe
 
Sasa kumbe ulitaka tufananishe na nani? Nyerere alijua wananchi wake wanataka nini na alijaribu kwa kadri ya uwezo wake hata mwenyewe alikiri yeye sio malaika; lakini alifanya kile ambacho raisi mwenye mapenzi na wananchi wake angekifanya; hakuwa tayari kuona raia zake wanakufa njaa; hawakuwa tayari kuona raia zake wanageuzwa watumwa kwenye nchi yao; hakuwahi hata kujijengea nyumba; hakuwa mbinafsi sasa hebu tuelezeni hicho alichokosea!
nyerere alikuwa kama tajiri wa kiafrica ambaye akifa basi familia inafilisika watoto wanageuka wezi na makahaba. we jiulize kwa nini wachina hadi leo wako kwenye line lakini sisi hatueleweki?.
 
The words you quoted, they are in a present continuous tense stressing the permanent nature of the state of being! Kama hujui uliza!
Wakati mwingine ni vyema kukubali makosa. Hakuna kitu kama hicho: has been died! ...he has been dead (nadhani ndio sahihi).

Soma hapa kidogo: (English forum)
You can write:
My father has been dying for two years. (i.e. He has a fatal disease and is very sick, and the doctors say he has not much time to live.)

You can also write:
My father has died. (He died recently.)

Dying is a one-time event. It cannot happen for two years.
Studying grammar can occur over two years. It takes a long time to learn grammar.

To be dead means not to be alive. Someone can be dead for a very long time.
 
uko sahihi sana faizafoxy....na ile sera yake ya ujamaa na kujitegemea nayo imeiyumbisha tanzania japo kuna watu wanaisifu...hawa bila shaka ni wale wanaokariri vitabu...kuna mzee alinisimulia jinsi walivyokuwa wanalazimika kupanga mistari kupewa unga kilo moja ilhali pesa Wanayo!!! maana kutofanya hivyo ilikuwa ni kujipalia makaa...
TUKIACHANA NA VINARA AMBAO NI URUSI NA UCHINA...KARIBU NCHI ZOTE ZILIZOIGA MFUMO HUU NI NCHI MASIKINI SANA KTK ULIMWENGU WA LEO...NA NDIYO MAANA KENYA WAMETUZIDI KIUCHUMI WAKATI SISI TUNA RASILIMALI NYINGI!!!
 
...kuna mzee alinisimulia jinsi walivyokuwa wanalazimika kupanga mistari kupewa unga kilo moja ilhali pesa Wanayo!!! maana kutofanya hivyo ilikuwa ni kujipalia makaa...
Wewe kweli ni Ponjoro. Ni dhahiri ulikuwa haujazaliwa enzi hizo kwa hiyo ni vigumu kupata picha sahihi! Huo unga watu walikuwa wanapewa au wananunua?
 
Last edited by a moderator:
Nadhani umepoteza dhana halisi ya maisha yako, ya babu na babu wa bibi yako nadhalia asilia ya wapi ulikotoka na maendeleoa kiuchumi nk.

Je babu wa babu na babu yako alikuwa dini gani? uislam au ukristu umekuja hivi karibuni lakini babu zetu zama zile waliishi kwa imani zao na maisha yalienda.

Hebu tuambie kwanini hulalami kwamba

1. walikula matunda mabichi, mizizi na hawakuswali wala kutawaza nani aliweka misingi ya maisha yao? Nyerere?

2. kama walifanya makosa mbona FaizaFoxy umestaarabika na kumgeukia mtume? vipi hujabaki kulalama kwa wale wasiojuwa kutawaza wala kuenda misikitini?

Wewe mwanamke FaizaFoxy nimpumbavu unaendeshwa na kuwashwa na udini! chuki za kijinga
zisizo na base wala misingi yoyote zaidi ya unafiki na ufedhuli kufanya uchochezi watu waanze malumbano yasiyo natija.

Umekosa hoja unaanza viroja.

Sikushangai, kivyako hiyo ndio misingi "mizuri" aliyoiweka marehem Nyerere.
 
Huwezi kulaumiwa kuzaliwa masikini lakini unastahili kulaumiwa kwa kufa masikini. (Bill Gates) Husianisha na mada inayojadiliwa.
 
Mtu mzima akikosea hachapwi kiboko lakin matokeo yake ni majanga tu!mtu yuke alikosea-hatuna haja ya kunyoosheana vidole inabidi tubadirike kifikra-tunajikweza mno ili tunufaike kisiasa
 
Kosa kubwa Nyerere alilofanya ni kutupenda sana watanzania na kutufanyia kila kitu. Alituzoesha vibaya mpaka tukawa wavivu wa kufikiri na kufanya kazi.

Alitumia muda mwingi kutulinda na kulinda rasilimali za nchi zisiibwe na mabwanyenye na mabepari wa ndani, Marekani na Ulaya.

Alitumia muda mwingi pia kupigania uhuru wa Afrika. Alijaribu kuwaunganisha waafrika na rasilimali finyu zilizokuwepo. Kwa hatua hii ya kujitoa na kuwatumikia waafrika alishindwa kwakweli kufanya maendeleo makubwa Tanzania.

Japo yapo mengi ambazo yanaonekana na mengine yasiyoonekana aliyofanya nyerere ambayo ingewachukua miaka 10000 viongozi hawa wa sasa kuyafikia.

Ili tuendele tunahitaji

Unified nation
Adequate resources
Ethical leadership

Hizo mbili za kwanza Nyerere alifanikiwa sana isipokuwa kwenye ya tatu ambayo nayo alijitahidi kwa kiwango kikubwa
 
Back
Top Bottom