Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Hivi unataka kumlaumu Nyerere kwa viongozi waliopo huoni hata aibu? Ni mtu mchimvi; juha na mkosefu wa akili ndiye atakayemlaumu Nyerere kwa viongozi hawa tulionao; wa kuwalaumu ni watanzania ambao ndio waamuzi wa mwisho hakuna kiongozi alijiweka madarakani mwenyewe ni kura zetu ndizo zinazowaweka madarakani; Nyerere alitengenezeza mfumo wa demokrasia ya kura ni sisi wapiga ndio tunaopaswa kujilaumu wenyewe; tangu Nyerere aondoke watawala wote walipigiwa kura sasa kama kuna wa kumlaumu basi ni mpiga kura mwenyewe; ni wapi Nyerere alipenda kuabudiwa? Alikuwa ni kiongozi wa kawaida ambaye hakudiriki hata kujijengea Nyumba aliishi kwa mshahara wake hivi hamuoni hata aibu mnapoandika huu uchimvi wenu?? Watanzania wenyewe ndio wanaoruhusu ufisadi sasa hii kumlaumu mtu ambaye hata siku moja hakuwahi kuwa fisadi ni kituko ambacho sijui kinatoka wapi mimi nadhani kosa kubwa alilolifanya Nyerere ni kutoa elimu ya bure wengi wenu humu saa hizi mngekuwa vijijini mnahangaika na jembe!
cc Ng'wamapalala

Huna sababu ya kutumia maneno makali tujadiliane kwa hoja. Nakubaliana kuwa mwalimu alikuwa mwadilifu sana isipokuwa aliamini kuwa hata waliomzunguka kwa maana ya wasaidizi walikuwa kama yeye. Hivyo akaacha kujenga taasisi madhubuti, ukiongea habari ya uchaguzi hapa tz napata wasiwasi kama kweli unaijua nchi hii na mifumo isiyo wazi katika kupatikana kwa viongozi. Mtu anaweza kutangazwa mshindi na kula akupigiwa na wananchi. Hatusemi mwalimu anapaswa kulaumiwa ila aliamini sana katika watu na alikuwa si muumini wa uwazi katika uendeshaji wa serikali akupenda wananchi washiriki katika maamuzi kila ilikuwa kiini macho ndiyo maana ulikuwa unapigia kula mtu na kivuli, watu hawana elimu ya uraia kuna mambo mengi sana mkuu ndiyo mjumuiko wa haya yote tunayoyaona leo.
 
Mkuu chama nimekusoma!.

Hata hivyo huhitaji kujenga hoja zinazobebwa pia na vijembe, matusi na kejeri. Haya maneno kama mchinvi, juha na ukosefu wa akili huhitaji kuyasema kwenye jukwaa la siasa. Hoja ndizo zitajipambanua katika madhaifu yake kwa wasomaji kuhukumu.

Jikite kwenye hoja na ukweli. mipasho waachie watu wa taarabu kwa sababu inaharibu mtitiriko wa hoja mbadala. Tuko hapa kusoma hoja na kujifunza na siyo kusoma vijembe na mipasho. Hili ni jukwaa ya siasa!.

Falsafa, siasa na uchumi alivyoanzisha Mwl. Nyerere pamoja na kubebwa na nguvu zote za kitendaji ambazo ni absolute power lakini zilishindwa kupambana na uhalisia wa mazingira ya ndani na nje ya nchi. Sadly, hakukumbuka hata kuweka safety net kitu ambacho kilipelekea nchi kukaribia kufirisika.

Tutaendelea kumkumbuka kwa kujenga utaifa lakini kwa gharama kubwa ya uchumi nchini.

Tutaendelea kumkumbuka kwa kupigania uhuru wa baadhi ya nchi za Kiafrika lakini kwa gharama kubwa ya uchumi wa nchi.

Tutaendelea kumuenzi kama kiongozi aliyekaa madarakani bila kuwa fisadi.

Tutaendelea kumuenzi kama kiongozi aliyejitoa kupigania kwa moyo wote maendeleo lakini katika njia ambazo hazikuwa sahihi in the long run and he was bold enough to accept his fate.

Mwl. Nyerere ataendelea kuwa polorized figure kwa kizazi hiki na kijacho.
 
khutba haziruhusiwi msikitini kwa wanawake,shangazi FaizaFoxy kaamua kukengeuka na kuja kuleta vioja vyake jf!
 
kwani nyerer ni nani mpaka kila alichokifanya kienziwe, babu mbinafsi mfia dini
 
How many people had access to right information?

Kulikuwa na magazeti mangapi? Yalikuwa yanamilikiwa na nani?

Usiposikia kitu haimaanishi kuwa hakipo, wake up...
nyerere ameshawahi kufungia magazeti? kuna haja gani ya kuwa na magazeti mengi halafu yanaandika kwa mtazamo wa mkurugenzi wa mawasiliano ikulu?
 
Udini hautakupeleka popote wewe dada.
Naomba nikuulize ni kiongozi gani aliyewahi kutokea au aliyopo hapa Tanzania unanayeona amefanya makubwa na mazuri kuliko J.K.NYERERE? kwa fIDA YA tAIFA ZIMA
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.

Chuki zako saa nyigine zinafanya una kurupuka na topic za kipuuzi!. Hakuna kinachoshindikana, na kama Nyerere hakuweka misingi sawa, ina maana hili haliwezi kurekebishwa??? Watawala wote waliofuatia wamefanya nini??

Kumbuka, hakuna kinachoshindikana, na kwa kauli yako una maana Tanzania ndo haitakuja kuwa na misingi imara?? Kwani hili linashindikana?? Mbona kuna nchi nyingi zilikuwa na misingi imara leo hii wanafarakana???

Nadiriki kusema, unajiona unajua kuchambua mada "zinazohusu Nyerere" lakini wewe ni wa kawaida sana kichwani, tatizo chuki zako zikiambatana na UDINI ndo zinakusumbua!
 
Hivi wewe akili yako inafanya kazi? nakupa ushauri kama sembe tumia la Bakhresa tu kwa afya yako hili sembe la kunusa litakutembeza uchi! Wakati Nyarere anatwala alijua wazi utajiri uliopo wa nchi hii na ndio sababu alijitahidi kadri ya uwezo wake kusomesha raia zake ili nchi ijitosheleze na wataalamu hakuwa na haraka ya kutumia rasilimali zetu; pamoja na utajiri wote aliotuachia bado unataka kumalumu Nyerere wewe kweli utakuwa hayawani usie na mfano!

haTA Matajiri wa kiafrica huachia wAToto wao mali ila huwa hawaaachii mbinu/taratibu za kuziendeleza. nyerere hakuaaNdaa/hakuruhusu free thinkers na ndo maana HAdi leo ccm wanasema BAdo tupo kwenye ujamaa na azimio LINAFANYA KAzi .

a
a
 
Huna sababu ya kutumia maneno makali tujadiliane kwa hoja. Nakubaliana kuwa mwalimu alikuwa mwadilifu sana isipokuwa aliamini kuwa hata waliomzunguka kwa maana ya wasaidizi walikuwa kama yeye. Hivyo akaacha kujenga taasisi madhubuti, ukiongea habari ya uchaguzi hapa tz napata wasiwasi kama kweli unaijua nchi hii na mifumo isiyo wazi katika kupatikana kwa viongozi. Mtu anaweza kutangazwa mshindi na kula akupigiwa na wananchi. Hatusemi mwalimu anapaswa kulaumiwa ila aliamini sana katika watu na alikuwa si muumini wa uwazi katika uendeshaji wa serikali akupenda wananchi washiriki katika maamuzi kila ilikuwa kiini macho ndiyo maana ulikuwa unapigia kula mtu na kivuli, watu hawana elimu ya uraia kuna mambo mengi sana mkuu ndiyo mjumuiko wa haya yote tunayoyaona leo.

Hapo hakuna maneno makali huo ndio ukweli wenyewe; unaongelea kuamini wasaidizi wake nadhani upeo wako bado ni mdogo sana au ni maneno ya kusikializa kwenye vilinge vya kahawa; Nyerere alikuwa mtawala wa kidemokrasia na ndio maana aliwapa nafasi wasaidizi wake kutekeleza majukumu ya kujenga nchi hii na kwasababu alikuwa mtu mwadilifu kwenye utawala wake hatukuwa na utitiri wa watu wanaojiingiza kwenye siasa kutafuta utajiri; suala la ETHICS halina mahusiano yoyote na Nyerere ni suala binafsi ukimkuta mtoto wa padri kawa shoga utalaumu baba yake? Huo ni utashi binafsi. Nyerere alijenga mfumo adilifu na yeye mwenyewe alikuwa ni mfano; kama kweli Nyerere alikosea basi itakuwa alifanya makosa mazuri maana hata wapinzani wanamtumia Nyerere kujivunia wananchama; hali kadhalika CCM wananmuenzi Nyerere ili kulinda na kujenga imani yao kwa watanzania!
 
[/COLOR]

haTA Matajiri wa kiafrica huachia wAToto wao mali ila huwa hawaaachii mbinu/taratibu za kuziendeleza. nyerere hakuaaNdaa/hakuruhusu free thinkers na ndo maana HAdi leo ccm wanasema BAdo tupo kwenye ujamaa na azimio LINAFANYA KAzi .

a
a

Bado akili yako changa; na nina uhakika hujasoma rasimalia alizoziacha Nyerere ni nyingi sana aliaziacha kwa maana ya watanzania wanufaike nazo hao free thinkers ndio hawa wenye akili kama zako?
 
Mkuu Ng'wamapalala
Chama sioni tabu wala siogopi juha kumwita juha; nina uhakika kama sio Nyerere leo hii wewe ungekuwa ni mchunga ng'ombe Bariadi; Nyerere ndiye kiongozi anayeing'arisha Tanzania nje ya nchi; kama suala ni theory za uchumi nilishakuambia siku nyingi hakuna mfumo ulio sahihi; hata ubepari una mapungufu mengi na ndiyo hayo yaliyosababisha uchumi wa dunia kuanguka; ninaposema ni juha na mchimvi ndiye atakayemlaumu Nyerere sababu kubwa ni hii; Nyerere alikiri hakuwa malaika na kuna mambo kama kiongozi alikosea; Nyerere ameacha rasimali nyingi untapped kwa lengo moja la kuwakomboa watanzania kiuchumi; raisi Obama alipoingia madarakani kipindi cha kwanza alimlaumu raisi Bush kwa matatizo ya uchumi yanayoikabili USA wananchi walimkubalia lakini yeye hakuishia hapo alikuja na mbinu mbadala ya kutatua matatizo ya uchumi; baada ya miaka minne pamoja na kwamba uchumi wa Marekani ulikuwa haujasimama sawasawa hakuendelea kumlaumu raisi Bush alitumia muda huo kuendelea na sera zake za uchumi na pale alipokosea alirekebisha; wajerumani baadaya vita kuu ya pili walikabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi hawakutumia muda wao kumlaumu Hitler walitafuta njia mbadala iliwachukua miaka 25 (1945-1970) kuondoa matatizo yao ya kiuchumi leo hii Ujerumani ni economic powerhouse kwenye EU; uchumi wa Argentina ulianguka kati 1999-2002 ilifikia wakati pensioners ilibidi walipwe kabichi na macaron; raisi aliyeingia madarakani alikuja na njia mbadala leo hii uchumi wa umepanda; sasa ninapowaita watu wa kaliba yako wachimvi najua nini ninachoongea; tatizo wengi ni shule ndio maana siku zote mnakuja na lawama lakini hamna njia mbadala sasa unataka kuwaite vipi great thinkers?? mkuu nenda shule ukielemika utajua Tanzania tulibahatika kiasi gani kuwa na mtawala kama Nyerere
 
Last edited by a moderator:

...Mkuu umeniacha kinywa wazi. kumbe una akili kiasi hiki? ...mbona unaongea utafikiri umeshajivua gamba? Heshima kwako mkuu! hoja zako zimetulia sana mkuu.
 
Mwl aliamini kwamba watu wake hawana elimu, na ukweli ulikuwa hivyo, mfano concept ya tv haikuwemo kwa wengi,anapoangalia tv na kuona matukio-ili muelewe anasema ameota kuna vita nchi fulani. kwa upande mwingine waliokuwa na elimu walikuwa na usaliti ndani yao,mfano mzuri ni kuvunjwa kwa azimio la arusha kimya kimya. Hali hii ilimfanya awe na wakati mgumu kuwashirikisha watu moja kwa moja. Pia tukumbuke viongozi wengi aliowakataa ndiyo wana nafasi nyeti za uongozi sasa. Hata kama misingi ikiwepo ni rahisi wao kuivunja.
 
Unaitaji misingi ipi zaidi ya aliyoiweka ya usawa kiuchumi na raslimali za nchi kwa raia wote,Taifa kujitegemea, Elimu na afya kwa wote, Uthamini kwa wanyonge na wanawake,,Nadhani hujui uliongealo ndugu yetu..Misingi nyerere aliweka ila imevurugwa na kuharibiwa na waliomrithi.
 
536934_509997152424579_1567512199_a.jpg
 
Napingana na wewe ......hayati mwl Nyerere alituandalia watanzania kujitawala,aliipigani na kutuachia siasa ya ujamaa na kujitegemea..... nini maana ya ujamaaa?..... ndio maishi tunayoishi watanzania, kusaidia wakati wa shida na raha,

Kujitegemea, alimaanisha tushi kwa rasilimali zetu, bila kutegemea misaada....niambi nini kilifuta baada ya ya yeye kutoka madarakani.... tukauza Asset zote, kama watoto wauza unga tunagombea mali za baba baada ya kufariki, aliwekeza kila sector, madini, kilimo afya, elimu,......yako mengi aliyofanya

Matatizo yalikuwa yanatokea katika utekelezaji wa yale aliyoyaanzisha, walikuwa ni watoto wake, amnbao ndio wanashindwa kuongoza nchi leo? aliwalea, akawasomesha, kama hawakuelewa, sasa wacha dunia iwafunze kwa makosa yao.....hata wewe unaweza kuwa na watoto, unawapeleka shule ambayo unadhani ni nzuri, lakini unakuta bado hailewe...., kuwezi kumuondoa kaka list ya waridhi wako kwa kuwa hana akili, haelewi unachomfundisha

Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.
 
Ng'wamapalala Aksante kwa kumsaidia huyu fanatic, sio kwamba ukweli haujui bali ni upuuzi tu umemjaa kichwani kila akilala akiamka anawaza Nyerere, kama unampenda sana nenda umfuate huko aliko.

Last edited by a moderator:
...Mkuu umeniacha kinywa wazi. kumbe una akili kiasi hiki? ...mbona unaongea utafikiri umeshajivua gamba? Heshima kwako mkuu! hoja zako zimetulia sana mkuu.

mkuu Chintu
Sijawahi kuwa gamba na sitawahi kuwa; mimi ni mtanzania ninayeheshimu utawala wa kisheria; nashangaa sana na hawa watu wanaotumia muda mwingi kumpaka matope Nyerere mtu aliyeachia madaraka zaidi ya miaka 30 iliyopita wakati kuna nchi duniani zilipata matatizo makubwa ya kiuchumi kuliko Tanzania na zilitumia chini ya miaka 20 kutatua matatizo yao; Ng'wamapalala ni mzushi tu ila namshauri ajielemishe ataona ni kiasi gani Nyerere alikuwa lulu kwa watanzania na kama anataka kuthibitisha kauli yangu aende kwenye mkusanyiko kama Kariakoo atoe maneno ya kifedhuli dhidi ya Nyerere aone kama hatapata kipigo cha paka mwizi!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom