Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Nyerere Alifanya Makosa Makubwa...

Kajifunze kuandika Kiingereza ndio uje nikuelewe una maanisha nini.

Huo ndio msingi uliowekwa na Nyerere. Hujuwi Kiingereza na nna uhakika hata Kiswahili hukijui.
Naungana na wewe kabisa misingi aliyoacha nyerere ndiyo inatusumbua hadi leo, alijenga jamii ya wanafiki na kutufanya tushabikie akila jambo hata kama hauliamini kwa moyo wa dhati badala ya kujenga jamii wa watu wanajua nakufuatilia mali asili kwa kuwahoji viongozi yeye alikuwa anataka watu kupiga makofi. Aliwafanya watanzania wasijue nchi inaendeshwaje ili viongozi mafisadi waibe na wasiulizwe amejenga msingi mbovu uliozaa hawa mafisadi wote hivyo hawezi kukwepa lawama za kuharibu nchi hii kwa misingi mibovu na ya ukandamizaji
 
Wakati mwingine ni vyema kukubali makosa. Hakuna kitu kama hicho: has been died! ...he has been dead (nadhani ndio sahihi).

Soma hapa kidogo: (English forum)
You can write:
My father has been dying for two years. (i.e. He has a fatal disease and is very sick, and the doctors say he has not much time to live.)

You can also write:
My father has died. (He died recently.)

Dying is a one-time event. It cannot happen for two years.
Studying grammar can occur over two years. It takes a long time to learn grammar.

To be dead means not to be alive. Someone can be dead for a very long time.

Agreed about accepting mistakes - which anyone can - and indeed - do. Kuna kitu kinaitwa "typo", kitu hicho (i.e. typo) huwa hakibadili logic ya kitu kinachoongelewa (kwa mtu mwelewa wa vyote, yaani kinachoongelewa na kuwepo possibility ya typo yenyewe). Kushindwa kuelewa kuwa hapo kuna "typo" kunaashiria one and only thing: uwezo mdogo wa mhusika kuhusu jambo husika!
 
Inaonekana wewe ni mgumu kuelewa, licha ya kukubali makosa yako!
 
Inaonekana wewe ni mgumu kuelewa, licha ya kukubali makosa yako!

Ni mtazamo wako - na una uhuru na haki ya kuamini unachotaka kuamini. Proof: Kuna watu wengi sana wameisoma post yangu - na HAIWEZEKANI KUWA wote hawajui Kiingereza - and am sure wengi wameliona kosa langu na wametoa maoni yao kuhusu LOGIC ya kile nilichokisema japo wameiona typo iliyopo kwenye hiyo post. Haiwezekani wote walio soma post yangu wamebuni, the post was crystal clear. Typo or no typo.
 
The words you quoted, they are in a present continuous tense stressing the permanent nature of the state of being! Kama hujui uliza!
Is this what you meant by "typo"? Anyway, I leave it at that! Tuyamalize kiutu uzima.
 
ni kiongozi mjinga anaejaribu kuachieve a national dream katika utawala wake. alitakiwa kujua kwamba umoja wa africa hauwezekani wakati nchi ndo inapata uhuru. alitakiwa kujua kuna watu grreedy kama IMPLA, UNITA , UNITA NA RENAMO. hakuwa na maono

Ni kweli unatakiwa kuelewa kila mtu ana ujinga wake! Na pia kila mtu anajaribu katika maisha na katika kazi anayofanya kufikia malengo fulani yeye yake ni kuunganisha Afrika kwa kuonesha mfano wa Tanzania ambapo pia akifanikiwa sera ya uchumi iwe ujamaa na kujitegemea kuwafanya waafrika kitu kimoja katika kiuchumi na kijamii.Pengine alifanikiwa na pia Pengine alishindwa lakini bora alijitahidi kujituma kuliko kutokufanya kitu kabisa au kuharibu rasilimali ovyo kama viongozi wengine kama kina Mobutu na Bokasa. Changamoto kubwa ni kuyafanyia kazi yale aliyoshindwa ambayo kizazi cha leo tunaona kama angeyafanya tungekuwa kama South Africa au zaidi.

Pia nilichoona hapo kwako ni kuhusu national dream; kwa hapo nachangia kwa kusema kwamba pengine ilikuwa ni vizuri kwake kuweka dira ya taifa ambayo itakuwa inaenda na wakati na sio kutegemea majira yaleyale kama ya mwanzo mfano ni Azimio la Arusha. Tuliona jinsi gani ambavyo azimio hili jinsi miaka ya 80 inavyoingia lilizidi kushidwa kuwa na mashiko kiuchumi na kijamii lakini Nyerere hakuwa tayari kwa mabadiliko. Naitetea hoja hii kwa kuiangalia China ambayo Mwisho mwa Miaka ya 70 na na miaka ya 80 ilifanya mabadiliko makubwa ya kimfumo ikiwa pamoja na kuruhusu baadhi ya vipengele vya kibepari ambavyo viliifanya China ya kijamaa kuwa na kasi ya ukuaji wa uchumi na hadi leo ina mfumo wa uchumi ambao unaitwa Market Socialism. Kwani na sisi tungejifunza na kutengeneza ya kwetu kama tulivyofanya kwa Azimio la Arusha tungeshindwa?
 
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.

Wewe kweli ni Mtanzania au Mnyarwanda, mbona kama hauna akili timamu, kaa kumya kama hauna la kuongea
 
He has been died for a long time now, and he has been out of power for even longer. So, hayo makosa yake yanasubiri afufuke ili yarekebishwe?

And why are you so obsessed with someone who has been out of power - and this world - that much? Kwa nini usituambie tujadili yanayofanywa leo na walio madarakani leo hii ambapo kila kukicha ni bora ya jana?

safi sana mkuu!! nimependa arguement yako!!

but kwann rep power yako ni 0 wakati naona umo humu muda mrefu?
 
nyerere alikuwa kama tajiri wa kiafrica ambaye akifa basi familia inafilisika watoto wanageuka wezi na makahaba. we jiulize kwa nini wachina hadi leo wako kwenye line lakini sisi hatueleweki?.

Hivi wewe akili yako inafanya kazi? nakupa ushauri kama sembe tumia la Bakhresa tu kwa afya yako hili sembe la kunusa litakutembeza uchi! Wakati Nyarere anatwala alijua wazi utajiri uliopo wa nchi hii na ndio sababu alijitahidi kadri ya uwezo wake kusomesha raia zake ili nchi ijitosheleze na wataalamu hakuwa na haraka ya kutumia rasilimali zetu; pamoja na utajiri wote aliotuachia bado unataka kumalumu Nyerere wewe kweli utakuwa hayawani usie na mfano!
 
Unachosema ni kweli alilinda maliasili na akapeleka watu kusoma, tatizo kubwa alijenga mfumo mbovu wa kiutawala uliojaa usiri mkubwa kwa watawala na kujengea wananchi hofu ya kutohoji namna watawala wanaovyoendesha nchi. Matokeo yake ni kuleta kizazi cha viongozi mafisadi. Labda nikuulize unajua baada ya kutoka tu madarakani akiwa hai aliona namna uongozi aliouachia madaraka ulivyoshambulia mali ya umma, rushwa ikashamiri. Tatizo alishindwa kujenga mfumo bora wa kidemokrasia wenye kufanya viongozi wawajibike kwa wanachi akajenga mfumo uliowafanya viongozi kuwa kama miungu huku wakifanya mambo kwa usiri mkubwa na wote walikuwa wanasubiri atoke ili waibe. Ndiyo maana hata hizo mali alizoacha kwa mfumo huu hazijatusaidia zinawasaidia viongozi. Ni sawa na baba una mali watoto hawazijui ukifa wajanja watazitapanya watoto watakuwa wanaambiwa ile ilikuwa ya baba yenu aanajiuliza kwa nini alipokuwa hai akutuambia namna ya kuitunza? Mzee alikuwa anapenda sana kuabudiwa ndiye chanzo cha haya yote tunayoshuhudia kwa kweli ameliacha taifa njia panda.
 
Mtu mzima akikosea hachapwi kiboko lakin matokeo yake ni majanga tu!mtu yuke alikosea-hatuna haja ya kunyoosheana vidole inabidi tubadirike kifikra.

Ni kweli mkuu! Tena never blame a dead man!

CC: FaizaFoxy
 
Last edited by a moderator:
Nchi hii ilikosa misingi ya kuifikisha ipasapo ilipokabidhiwa madaraka ya kujiendesha yenyewe. Kumbuka, hatukupewa Uhuru, kwani mwaka 1961 tulikuwa hatutawaliwi.

Aliyeshindwa kuweka hiyo misingi imara ni Julius Kmabarage Nyerere. Jee, tumlaumu kwa kuwa alikuwa hana uzoefu wa kuongoza? au tumlaumu kwa kuwa alikuwa akiendeshwa na waliomuweka madarakani?

Nyerere alishindwa kuweka misingi imara na ndio maana kila alichokifanya nchini kikashindwa au alikuwa hajui kuwa kila alifanyalo ni kosa mbeleni? alikuwa hana muono?

Tujadili.

Sijui wewe ni mfuasi wa dini/dhehebu gani? Maana natatizwa na kuanzisha topics za watu walioenda mbele ya haki,na kwa Hakimu wa wote,The lord,Allah,Nkosi,Mungu,Mola, etc. Kama mema au mabaya aliyotenda,hukumu yake keshaipata,kubwa,katutoa mimi na wewe kwenye ukoloni na kutupa haki ya mtu ni utu.
 
Unapotaka kufananisha mtu aliyekaa madarakani miaka 23 na aliyekaa miaka 8 unaonyesha ukosefu wa upeo, lakini hata utakapoamua kufanya hivyo kwa kutumia vitu vinavyopimika utaona aibu mwenyewe.

Mwalimu hayupo, lakini maadui zake bado wameendelea kumshambulia. Sasa hivi maadui wa Mwalimu wanataka kuleta serikali tatu ili kuangusha nguzo ya mwisho ya legacy yake. Sijui watu hawa wananufaika vipi na chuki waliyo nayo kwa Mwalimu!

Hapa naomba tupishane, kwanza nyerere siyo Mungu hivyo mfumo wa serikali mbili yalikuwa ni maono yake ambayo leo hii mfumo huu umeonyesha kushindwa kutatua matatizo ya Watanzania. Sasa hatuwezi kufika mahali tukashindwa kutafuta mfumo ambao tunaona utakidhi mahitaji yetu kisa itaonekana hatumuenzi nyerere tutakuwa wapumbavu. Mfumo unaweza kukidhi matakwa kwa wakati fulani lakini inaweza kufika mahali ukawa hauwezi tena tunabadilisha siyo dhambi kwa hiyo tunaotaka serikali tatu siyo maadui wa mwalimu ila tuna maono yetu na sababu zetu za msingi kabisa kwa wakati huu wa sasa na si kosa hivyo lazima kuheshimu mawazo ya wengine pia ndiyo demokrasia ya kweli
 
nyerere hakuwahi kuuza tembo au twiga ha, hakuchimba madini.hakuwahi kuwa fisadi hakufanya biashara ya sembe.na watoto wake walibaki wakiiheshimu ikulu na nchi kiujumla si sasa hata mtoto wa katibu kata anaweza kukutisha.nchi ilianza kuoza mikononi pa mwinyi na ndipo tulipoona wake za marais wakichanua kuliko waume zao.kife chama cha mapinduzi.
 
Ukweli ni kwamba uyu nyerere kosa lake kubwa ni kutoshaurika,sio tu tunapigishwa kelele eti alikua kiongozi bora!..msiache tukataja ufisadi wake alioufanya ktk nchi hii enzi za uhai wake
 
Hapa naomba tupishane, kwanza nyerere siyo Mungu hivyo mfumo wa serikali mbili yalikuwa ni maono yake ambayo leo hii mfumo huu umeonyesha kushindwa kutatua matatizo ya Watanzania. Sasa hatuwezi kufika mahali tukashindwa kutafuta mfumo ambao tunaona utakidhi mahitaji yetu kisa itaonekana hatumuenzi nyerere tutakuwa wapumbavu. Mfumo unaweza kukidhi matakwa kwa wakati fulani lakini inaweza kufika mahali ukawa hauwezi tena tunabadilisha siyo dhambi kwa hiyo tunaotaka serikali tatu siyo maadui wa mwalimu ila tuna maono yetu na sababu zetu za msingi kabisa kwa wakati huu wa sasa na si kosa hivyo lazima kuheshimu mawazo ya wengine pia ndiyo demokrasia ya kweli

Je, unataka kusema kwamba Nyerere Upeo wake ulishindwa kwenda beyond 2015? Je, kwanini haja ya serikali tatu haikuonekana wakati Mwalimu akiwa kwenye system?
 
Je, unataka kusema kwamba Nyerere Upeo wake ulishindwa kwenda beyond 2015? Je, kwanini haja ya serikali tatu haikuonekana wakati Mwalimu akiwa kwenye system?

Naamini unajua mambo mengi ya nchi hii kipindi cha mwalimu majadiliano ya mamabo mengi ambayo yalionekana ni kinyume na mtizamo wake hayakupewa nafasi. Nadhani unakumbuka habari ya G55 kuhusu muundo wa muungano na namna mwalimu alivyoizima. Si kwamba halikuwa hana mtizamo wa 2015 aliamini kuwa wale aliokuwa nao watatenda kama yeye huku akiacha kujenga mifumo madhubuti na badala yake akawaamini watu sasa wote aliofikiri watatenda kwa kadiri ya mtizamo wake wamegeuka lakini angejenga mifumo madhubuti ingesimamia yale aliyoyaamini. Hata leo tukisema mwalimu alisema ili ni baya viongozi wanafanya wakijua akuunda vyombo madhubuti kuyasimamia mambo yake. Ni sawa unakuwa mpiganaji kutafuta maisha unapata mali kisha uziwekei ulinzi unasema wote wanaonizunguka ni waaminifu ukienda kulala wanaiba kwa nini usiweke ulinzi kwa kuwa silika ya mwanadamu ni kubadilika na Mungu aliyemuumba anajua.
 
Njaa Mbaya Hivi unataka kumlaumu Nyerere kwa viongozi waliopo huoni hata aibu? Ni mtu mchimvi; juha na mkosefu wa akili ndiye atakayemlaumu Nyerere kwa viongozi hawa tulionao; wa kuwalaumu ni watanzania ambao ndio waamuzi wa mwisho hakuna kiongozi alijiweka madarakani mwenyewe ni kura zetu ndizo zinazowaweka madarakani; Nyerere alitengenezeza mfumo wa demokrasia ya kura ni sisi wapiga ndio tunaopaswa kujilaumu wenyewe; tangu Nyerere aondoke watawala wote walipigiwa kura sasa kama kuna wa kumlaumu basi ni mpiga kura mwenyewe; ni wapi Nyerere alipenda kuabudiwa? Alikuwa ni kiongozi wa kawaida ambaye hakudiriki hata kujijengea Nyumba aliishi kwa mshahara wake hivi hamuoni hata aibu mnapoandika huu uchimvi wenu?? Watanzania wenyewe ndio wanaoruhusu ufisadi sasa hii kumlaumu mtu ambaye hata siku moja hakuwahi kuwa fisadi ni kituko ambacho sijui kinatoka wapi mimi nadhani kosa kubwa alilolifanya Nyerere ni kutoa elimu ya bure wengi wenu humu saa hizi mngekuwa vijijini mnahangaika na jembe!
cc Ng'wamapalala
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom