Mkuu wangu labda nikuulize hivi. Huo mradi wa TAZARA wachina wanao kwa miaka mingapi hadi sasa? na Je, tumepoteza au tungefaidika vipi kama ungekuwa chini ya TRA.. je kama mradi ukiwa wa Bandari, serikali na sisi wananchi tunafaidika vipi kama sio kwa kupitia kodi wanazolipa? hivyo haijalishi kama shirika hili ni la Mchina, bandari au Karamagi kinachoingia ktk mfuko wetu ni kodi wanazotakiwa kulipia..Ukweli ni kwamba tutapoteza zaidi inapokuwa mikononi mwa Bandari maana wezi watupu wamejaa huko.
Halafu nakuomba pia soma barua ya kwanza kabisa ktk mada hii inazungumzia hao MHCI wakiulizia nini maamuzi ya wizara kama bado tuko interested na investment yao ambayo inafuata Public Private Partnership act and Regulation ya mwaka 2011 au tutaendelea kutumia mkopo ule wa benki ya Exim toka China na wale CCCC, kama ndivyo basi ombi lao lichukulie null na void na wamejieleza vizuri kukubali matokeo ya uchaguzi wetu. Chaguo la Nundu inaelekea ni option ya pili ambayo wao wameiweka kujinadi ubora zaidi ya ile ya CCCC..Sasa kama kuna fitna na kumalizana hilo swala jingine.
Tatizo la Nundu tunaweza kusema kwamba alikuwa na mpango na hili shirika la MHCI wakati kuna shirika jingine la CCCC ambalo ndilo limeweka mkataba na hata kupatikana kwa hizo Usd 600 millioni lakini jaribu sana kuzifuatilia hizi barua zote hutaona mahala wamepeleka nakala kwake. Kama vile walikuwa wakimkwepa toka mwanzo. Pili inanishangaza zaidi naposoma kwamba mkopo waliotoa benki unasema Usd 470 kama asilimia 90 hoja ya
Candid Scope #3 wakati barua za serikali zinaonyesha usd 444 kama asilimia 85 hoja ya
n00b #9. Tatu, kuna makadirio ya aina mbili moja ikisema Usd 610 na nyingine 523, sasa ipi nni ipi?
Halafu elewa pia kwamba huo mkataba wa Nundu na HMCI tusingetoa hata cent moja wangegharamia wao kwa kila kitu halafu pia kulikuwa na mpango wa kuiboresha pia bandari ya Tanga. Swala la kujiuliza sisi ni:-
1. Je, hizo gate mbili zinaweza ingiza kiasi gani cha faida kila mwaka baada ya matumizi, na hiyo faida kwa miaka 45 itakuwa kiasi gani tofauti na mkataba huu wa CCCC ambayo inatugharimu millioni 600 na bado hatujaweka gharama za uendeshaji na ukarabati. Bandari kama shirika lingepoteza kiasi gani cha fedha kutokana na mradi wa A au B
2. Je, Kama Bandari yetu inafanya kazi kwa faida imekuwaje wameitumia serikali na shirika la CCCC kukopesha kiasi hicho cha fedha toka benki binafsi ya China na sio Banki ya dunia, Afrika au serikali ya China.