NYARAKA: Omar Nundu ni msafi...

NYARAKA: Omar Nundu ni msafi...

Jaman invisible kauliza swali,sasa ni jukumu letu kusoma na kutoa mawazo yetu..kwa hili swala na kulingana na doc huyu jamaa siyo msafi hata nukta..yan kitendo cha kutoa bandari kwa 45yrs ni ujinga uliokithiri,em tuwe wachumi kidogo..
 
I wish I had power to execute him immediately without delay.
WANACHEZA NA MAISHA YA WATANZANIA.
 
Mkuu umeandika mengi lakini hatutuelezea Public Procurement Act, 2011 inaemaje kwenye maswala ya manunuzi? Ni kampuni gani kati hizo mbili ime comply with the respective act to the letter? Ya Mh.Nundu naona inataka kukwepa kufuata utaratibu wa jinsi sheria yetu ya manunuzi inavyotaka. Na kama unaona huo ndio uzalendo basi kuna tatizo. Mh.Zitto juzi alisema kamati yake inapendekeza eyes on hands off. Tuache wahusika wa Procurement Management Unit wakiongozwa na katibu mkuu wafanye kazi na mawaziri kazi yake iwe ni kuwa watch dogs ili mambo yasonge mbele. La sivyo tutabaki kuwaonea huruma wanaotoa machozi ya kinyonga
Mkuu wangu pengine mimi sikusoma vizuri lakini sioni hata hiyo ya kwanza imefuata kitu gani..nakuomba soma hoja namba 10 ya n00b kuna mahala imeeleza wazi kwamba ni CCCC walioonyesha interest ya kujenga mradi huo mwaka 2009, haikuonyesha ufuatiliaji wa Public procuament za wakati ule.

Halafu, binafsi yangu mimi sintopoenda kabisa kurudia ya kina Lowassa na Richmond ambapo inafanyika tender na anachukuliwa yule anayetoa 10% kama unataka generators nenda kanunue GE kuliko kuweka tender kwa walanguzi, haya maswala ya kuweka tender wakati nchi yetu maskini, hayo mashirika makubwa huwa hayajitokezi mara kwa mara kama vile mkazi wa Manzese akitaka kujenga nyumba si rahisi contractor wakubwa kujihusisha na tender hiyo, wewe mwenye kutaka kujenga ndio unafanya utafiti lakini kama linajengwa jumba la PPF Samora hapo utayasikia mashirika yote makubwa yakijitokeza, Kidunia Tanzania yetu ni kama Manzese, inabidi sisi ndio tuwatafute wajenzi bora. Hii ndio reality lazima tuikubali maana tutaingizwa mjini kama Richmond, IPTL, Citywater na kadhalika haya yote tumefungashiwa kutokana na haya maswala ya tender.

Hivyo sioni kosa kubwa la Nondo maadam hili shirika la MHCI ndilo kubwa China na hata ukisoma report yake Bofya inatisha maana ni kazi yao na wameifanya kwa miaka. Na yaonyesha wazi tunge serve kiais kikubwa cha fedha ukilinganisha na makubaliano ya kwanza.. Kula tunaliwa maana JK kesha sema tusipokubali kuliwa hatuli, ndio sera ya CCM. Jambo linalosikitisha tu kwangu ni kwamba tunajaribu sana kuboresha bandari ya Dar ambayo ktk ukurasa huo huo ukisoma sababu za ujenzi wa gate hizi utashindwa kuelewa kwa nini tunatumia mabillioni kupanua bandari ambayo uwezo wake ni mdogo mdogo sana kwa sababu gate zinazoongeza zitasaidia tu kupunguza msongamano lakini kwa jinsi biashara inavyozidi kukua kila mwaka ilitakiwa bandari za Tanga na Mtwara ziimarishwe kwa kutazama mahitaji yetu ya mbele zaidi na sii uwezo wa bandari ya Dar.

Mwisho, muafaka wa wizara ya kampuni hii ya MHCI na Nondo hauna maana yoyote ikiwa haukupitishwa bali proposal yao kwa wizara na hata kwa wanaofahamu wataelewa ndivyo shirika hili hufanya kazi zake. Lina invest lenyewe na kuendesha Bandari kwa miaka kadhaa serikali ikila kodi yake tu baada ya hapo wanawakabidhi mzigo wenu, iwe ujenzi wa barabara (toll) daraja au bandari, hivyo kulingana na sisi wababaishaji ingesaidia sana ufanisi na kuondoa ubabaishaji..Binafsi yangu bora miradi mikubwa kama hii tuwape wanaoweza kuiendesha maana sii madini kama dhahabu..
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kwanza tunasubiri doccuments na nondo za utetezi wa mambo anayoyafanya Nundu, ikiwa ni pamoja na kujiumbua kwa waandishi wa habari na kitendo cha yeye kushindwa kusema na kuwasilisha docs kwenye kamati. Lakini pili, hakuna kibaraka humu na pengine usiwe kama huyo waziri wewe ni mtu unayeheshimika sana katika jamii, usihukumu watu, humu watu wanataka data na doccuments ambazo tunasubiri za kujibu hizi zilizopo si maneno tu, ambayo yeyote anaweza kuyasema. Maneno kama "nani alimpa ruhusa kwenda kuhongwa" yanahitaji kubebwa na ushahidi wa kutosha maana ni tuhuma nzito kutolewa na Waziri dhidi ya Waziri mwenzake. Kama Mfutakamba amehongwa anastahili kushitakiwa na Nundu asaidie Takukuru (japo haina meno) kumshitaki Naibu wake na Naibu naye kama ana data (hajawahi kusema) naye asaidie dola kumshughulikia Nundu. Hapa hakuna anayebebwa katika mawaziri wala watendaji wako wa serikalini na mashirika yao yanayomeza fedha za umma kila kukicha.

Jambo linalonifurahisha ni kauli yako kwamba kuna mkono wa RA na kwamba Serukamba amewekwa madareakani na RA.... Ukweli ni kwamba kama ni mkono basi si wa RA bali ni EL ambaye ndiye mtu wa Serukamba na nimefurahi pia kusikia kutoka kwako kwamba hii kashfa ya bandari ni zaidi ya Richmond!! Kumbe Richmond ilikuwa kashfa? Kumbe EL na RA hawakuonewa kuwa ni magamba? Naona hapa tuko pamoja, na kwa kweli kama Mfutakamba na yeyote awe Nundu ama nani, wakihusika na ulaji, hakuna wa kubaki wote waondoke. Pia tusaidie kutuambia, taratibu zinasemaje Naibu Waziri ama Waziri akisafiri anamuaga nani? baada ya hapo ndio tuangalie kama kweli alikosea ama la?

Pia, nadhani Nundu asikwepe kama anataka atuambie pia na Dk. Kawambwa naye amekula fedha ili list iwe ndefu na Mkulo naye amekula kwenye hili la Bandari, hakuna kuuma maneno na wote kama wanahusika waache "wafu wazike wafu wenzao" tusimtetee mtu hapa, lakini pia tusifanye ukasuku, tumwage data na ushahidi, wa wazi. Nundu alete hapa hiyo LAPTOP yake aliyoingia nayo katika kamati akasema hana Doccuments. Tuache kushambuliana binafsi tujenge HOJA kwa HOJA, wezi wang'oke tu.

Asante sana Mkuu Halisi.........halafu Pasco ni "Mwanasheria".......hizi lugha anazotumia sijui tumueleweje.........
 
SIKU ZOTE Usikubali kuwarushia mawe wenzako wakati wewe unaishi kwenye nyumba ya vioo! Huyu Nundu kwa kweli alipaswa kujiuzuru mara moja bila hata pressure ya bunge maana alichoongea jana HAKINA HADHI YA UWAZIRI.
 
Mkuu big up kwa kutupa ushahidi wa rushwa ya hili kampuni. Kuna articles fulani nilisoma mwaka jana (I believe in "The Economist") kuhusu madudu yao hawa na Sinopec (kampuni yao ya mafuta) kuhusiana na rushwa katika uchimbaji wa mafuta huko Angola. Sijafanikiwa kuzipata online.

Nimeshauliza hapa, kama hawa watu wanajulikana kabisa kwa rushwa mpaka wamekuwa listed hivyo na World Bank, kwa nini tufikiri Tanzania hawakutembeza rushwa? Kulikuwa na open tender? Kuna transparency kiasi gani katika process yote?
mkuu tupo pamoja....nimeshtuka sana baada ya kugundua hii ndo kampuni inayopigiwa kelele hapa.....hawa jamaa wa CCCC ltd wamepigwa marufuku kule Ufilipino kwenye miradi yoyote inayofadhiliwa na world bank kwasababu ya fraud waliyofanya kule.....yaani wamepigwa marufuku mpaka 2017......kwa sababu ya hongo/rushwa/ufisadi waliofanya kule.....kwenye miradi ya WB....kwa hiyo hapa TZ sitashangaa wakifanya hivyo hivyo.....haswa ukizingatia mkataba walioingia na TZ kwa 45 years....hapa kuna rushwa ndugu yangu... si bure...i can bet on this......ndo sababu hawa mawaziri wanatupiana mipira....hapa kuna richmond nyingine ndugu yangu.....Infact kumsafirisha bure waziri Mfutakamba kwenda china na kurudi bure tayari ni hongo.......hili liko wazi kabisa......hawa jamaa wamewahonga serikali ya TZ kupitia kwa hawa mawaziri vihiyo ili tupigike kwa miaka 45.....
 
According to the Chinese country’s criminal law….it is an offence for Chinese companies and Chinese nationals to bribe foreign government officials. The law applies to companies organized under Chinese law and would include Chinese companies overseas and wholly foreign-owned enterprises in China. This is according to a World Bank statement issued in Washington in July 29[SUP]th[/SUP]/ 2011…when the WB announced the debarment of China Communications Construction Company (CCCC) Limited, and all its subsidiaries, for fraudulent practices under the Phase 1 of the Philippines National Roads Improvement and Management Project.

Under the sanction, CCCC is ineligible to engage in any road and bridge projects financed by the World Bank Group until January 12, 2017. This action was based on recent changes in the World Bank sanctions system to clarify that successor organizations- through purchase or reorganization –will be subject to the same sanctions applied to the original firm.

My take:
This is the same company involved here in TZ and already under this very suspicious deal….involving the current transport ministers from the TZ government. I will take the said paid for trip to China involving Minister Mfutakamba as bribery offered by the CCCC Ltd for the port’s deal……no wonder minister Nundu is trying to isolate himself from this fiasco……something is very fishy here…..we could be in for another Richmond….or Buzwagi or Kiwira here…..very sad that this is again happening under JK's government……these guys seem not to learn from their past mistakes……kweli sikio la kufa halisikii dawa…….

Source: Read about this from here: http://www.worldbank.org/en/news/20...imited-for-fraud-in-philippines-roads-project

Asante sana Mkuu Nderingosha
 
Alafu nimeshangaa kwenye hiyo barua moja hapo juu jamaa wanamwalika eti waziri Nundu aende SHENZEN (baada ya kusoma na kui study draft ya MOU) ili akasaini MOU akiwa SHENZEN.......ina maana kumbe hata MOU ilisainiwa china na si TZ ambako ndiko project inapofanyikia!!!!!!!.....jamani hii si Buzwagi nyingine hii!!!!!!!kama kweli Nundu alisaini MOU akiwa SHENZEN basi hapa kuna shida kubwa saana......
 
Where is Pasco with the flip side of the coin?... Mwaga vitu mkuu.
 
mkuu tupo pamoja....nimeshtuka sana baada ya kugundua hii ndo kampuni inayopigiwa kelele hapa.....hawa jamaa wa CCCC ltd wamepigwa marufuku kule Ufilipino kwenye miradi yoyote inayofadhiliwa na world bank kwasababu ya fraud waliyofanya kule.....yaani wamepigwa marufuku mpaka 2017......kwa sababu ya hongo/rushwa/ufisadi waliofanya kule.....kwenye miradi ya WB....kwa hiyo hapa TZ sitashangaa wakifanya hivyo hivyo.....haswa ukizingatia mkataba walioingia na TZ kwa 45 years....hapa kuna rushwa ndugu yangu... si bure...i can bet on this......ndo sababu hawa mawaziri wanatupiana mipira....hapa kuna richmond nyingine ndugu yangu.....Infact kumsafirisha bure waziri Mfutakamba kwenda china na kurudi bure tayari ni hongo.......hili liko wazi kabisa......hawa jamaa wamewahonga serikali ya TZ kupitia kwa hawa mawaziri vihiyo ili tupigike kwa miaka 45.....

Mkuu Nderingosha.....kwa sasa......kuna makubaliano kati ya MFIs kama WB, IMF, AfDB, AsDB, EU, DfID, etc etc kuwa endapo kuna individual au kampuni itaoneka imejiingiza katika vitendo vya rushwa and the likes.....basi hao wasiruhusiwe kupata kazi inayofadhiliwa na MFIs hizo..............serikali yetu pia is in support of this......na ndio maana watu kama Norconsult AS walipigwa chini TZ.........halafu leo tunataka kuwabeba CCCC......hivi hawa Exim are they for real kweli?........Damn!
 
Naona Mkuu data zenu ni nzuri sana kuhusu uchafu wa CCCC lakini hapa kuna tatizo, ambalo sijui kama mumeilewa vyema hoja husika na kampuni gani imeingia mkataba wa aina gani.

Kwanza naona munachanganya kati ya CCCC na hiyo Chinese Mecharnt, maana munazungumzia mkataba wa miaka 45 wa CCCC wakati MoU ya miaka 45 ni wa Nundu na Chinese Merchant ambao yeye anakiri kushuhudia lakini anasema aliyesaini ni Katibu Mkuu wake. Lakini pia kuna kutoelewa tatizo lilipo. Tatizo ni hoja kwamba Waziri kama ameona kuna tatizo, asingekimbilia kutafuta wawekezaji (si kazi ya Waziri) bali angeshauri kuvunjwa kwa mkataba ama kusitishwa kwa mchakato wa mradi husika kama alivyofanya kwa mradi wa ujenzi wa hifadhi ya magari (ambako nako ni kashfa, tunadaiwa USD 10m).

Baada ya kusitisha ama kuvunja mkataba, angesaidia vyombo husika kuchukua hatua kwa wahusika bila kujali nyadhifa zao, akiwamo Waziri aliyemtangulia, Dk. Kawambwa, Katibu Mkuu wake Chambo, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulu, Bodi ya Mamlaka ya Bandari na Menejimenti ya Bandari, kabla ya yeye kuanza mchakato wa kutafuta mwekezaji mpya. Huo mchezo wa kusema amepata mwekezaji wa bei rahisi (USD 300m), ametumia vigezo gani, ambavyo ni tofauti na wenzake waliopata mwekezaji wa bei kubwa (USD 600m)? Hivi kama kweli yeye alikuwa ama yuko sahihi, atatekelezaje kazi zake ikiwa hana mahusiano mazuri na uongozi wote wa wizara, Bodi na menejimenti yas TPA, Wizara ya Fedha, Waziri Mkuu, Ikulu, Wabunge wa Kamati ya kisekta!!! Angeiomba mamlaka husika imsaidie ama kuchukus hatua ama kumbadili na aweke rekodi sawa na si kusema tu na kufanya ubabe. Inakuaje aidharau kamati ya kisekta hata kama anaona haina uwezo?

Ni hatari sana tena sana na anazidi kukosea kuonyesha udhaifu wake. Anajua kwamba amekuwa akijinasibu kuwa na mahusiano na wakubwa, jambo ambalo halihalalishi jambo lolote, zaidi ya kujiharibia yeye binafsi na hao wakubwa wenyewe na ndio maana analalamika kuwa Naibu wake alimzunguka na kuomba kibali cha safari kwa PM.....

Mawaziri na Manaibu wakisafiri wanamuaga na kupata kibali kwa PM na si kwingineko..... narudia tena, Nundu ama wapenda nchi watupe data za safari za Mfutakamba kama aliufadhiliwa na Wachina na Naibu naye atupe data za Nundu kufadhiliwa na Wachina.... ili wamalizane wenyewe kama walivyoanza sasa na hilo halimsaidii yeyote kati yao, bali watamsaidia zaidi Rais kufanya mabadiliko badala ya kuumiza kichwa amuondoe nani.....

Waache wafu wazikane.....
 
hizi barua hazimsafishi nundu bali zinaonyesha kuwa alikuwa ana kaurafiki haramu na hii kampuni ya china merchants holdings nje ya njia zinazokubalika yaani kiofisi maana hawa wanaonekana hawafuati njia sahihi zinazotakiwa kufuatwa na kampuni bali wanatumia kiongozi mla rushwa/mlafi kama omar nundu kuipiga bao kampuni ya china communications construction ltd ambayo tayari proposal yake imekubalika na imeshapata fedha toka exim bank china!

Sasa sijui ni punda gani anaweza kuacha mradi ulioiva namna hiyo wa china cummunications construction ltd akaenda kwa huu wa china merchants holdings ambao haujasema ni kiasi gani ita-finance huo mradi na kwa riba kiasi gani! Hapa simply hii barua inaonyesha jinsi mawaziri wetu vilaza walivyo tayari ku-take risky decisions na ku-subotage miradi mikubwa ya maendeleo ili mradi tu wamehakikishiwa kushibishwa matumbo yao na miradi fake inayokosa transparency bali kupitia kwa vimemo viinavyoweza kui-cost nchi kama mikataba ya umeme ta tanesco!

Omar nundu lazma ajiuzulu manina.....!
hahahahaha.......soma nundu ame kuwa accused na kitu ??? Yeye kama umefatilia kosa lake ni kuchelewesha kuruhusu kampuni hii ya china kupata tenda hiii , yeye ametaka iitwe tenda ili kampuni ilio bora ipewe kazi hio, hili likachukuliwa na kamati ya bunge kwamba waziri nundu ana kampuni yake anataka kuipendelea..... Na pia amesababisha kuchelewa kuanza kazi hii ya upanuzi ambapo ilitolewa mfano wenzetu mombasa wameanza kupanua bandari yao...

Waziri nundu kwa kutaa amefanya kazi kubwa sana ..juu utaona hawa china merchants walikua wajenge bandari na wai endeshe wao kwa miaka 45 !!! Lakini ukiangalia barua ya juu hapo goverment wao ndio kama wakopaji ( borrower) hivyo serikali ingelipa deni hili dollari 550 million....na wakati huo huo china merchants wangelipwa na mkopo huu kujenga port hii na at the same time wataiendesha wao kwa miaka 45...sasa hapa kama nundu alitia ngumu hili lisifanyike basi huytu ni shujaa.....na kweli atakua adui wa watu wengi.
 
Naona Mkuu data zenu ni nzuri sana kuhusu uchafu wa CCCC lakini hapa kuna tatizo, ambalo sijui kama mumeilewa vyema hoja husika na kampuni gani imeingia mkataba wa aina gani.

Kwanza naona munachanganya kati ya CCCC na hiyo Chinese Mecharnt, maana munazungumzia mkataba wa miaka 45 wa CCCC wakati MoU ya miaka 45 ni wa Nundu na Chinese Merchant ambao yeye anakiri kushuhudia lakini anasema aliyesaini ni Katibu Mkuu wake. Lakini pia kuna kutoelewa tatizo lilipo. Tatizo ni hoja kwamba Waziri kama ameona kuna tatizo, asingekimbilia kutafuta wawekezaji (si kazi ya Waziri) bali angeshauri kuvunjwa kwa mkataba ama kusitishwa kwa mchakato wa mradi husika kama alivyofanya kwa mradi wa ujenzi wa hifadhi ya magari (ambako nako ni kashfa, tunadaiwa USD 10m).

Baada ya kusitisha ama kuvunja mkataba, angesaidia vyombo husika kuchukua hatua kwa wahusika bila kujali nyadhifa zao, akiwamo Waziri aliyemtangulia, Dk. Kawambwa, Katibu Mkuu wake Chambo, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulu, Bodi ya Mamlaka ya Bandari na Menejimenti ya Bandari, kabla ya yeye kuanza mchakato wa kutafuta mwekezaji mpya. Huo mchezo wa kusema amepata mwekezaji wa bei rahisi (USD 300m), ametumia vigezo gani, ambavyo ni tofauti na wenzake waliopata mwekezaji wa bei kubwa (USD 600m)? Hivi kama kweli yeye alikuwa ama yuko sahihi, atatekelezaje kazi zake ikiwa hana mahusiano mazuri na uongozi wote wa wizara, Bodi na menejimenti yas TPA, Wizara ya Fedha, Waziri Mkuu, Ikulu, Wabunge wa Kamati ya kisekta!!! Angeiomba mamlaka husika imsaidie ama kuchukus hatua ama kumbadili na aweke rekodi sawa na si kusema tu na kufanya ubabe. Inakuaje aidharau kamati ya kisekta hata kama anaona haina uwezo?

Ni hatari sana tena sana na anazidi kukosea kuonyesha udhaifu wake. Anajua kwamba amekuwa akijinasibu kuwa na mahusiano na wakubwa, jambo ambalo halihalalishi jambo lolote, zaidi ya kujiharibia yeye binafsi na hao wakubwa wenyewe na ndio maana analalamika kuwa Naibu wake alimzunguka na kuomba kibali cha safari kwa PM.....

Mawaziri na Manaibu wakisafiri wanamuaga na kupata kibali kwa PM na si kwingineko..... narudia tena, Nundu ama wapenda nchi watupe data za safari za Mfutakamba kama aliufadhiliwa na Wachina na Naibu naye atupe data za Nundu kufadhiliwa na Wachina.... ili wamalizane wenyewe kama walivyoanza sasa na hilo halimsaidii yeyote kati yao, bali watamsaidia zaidi Rais kufanya mabadiliko badala ya kuumiza kichwa amuondoe nani.....

Waache wafu wazikane.....

ndugu Halisi.....ukifatilia kwa makini hizo nyaraka/barua tangu mwanzo utagundua kuwa hawa CCCC Ltd ndio wana mkataba/contract na TPA......on EPC basis.....na hata huo mkopo TZ inaomba toka EXIM bank-china ili kufanikisha project waliyoingia kati ya TPA(TZ) na CCCC Ltd...Ukifatilia hiyo barua ya Chinese Merchant Holdings hapo juu utaona kuwa kuna misunderstanding waliyonayo na imewafanya wamwandikie Nundu barua kutafta clarity juu ya nini kinaendelea kwani wao nao wanataka kuingia mkataba na TZ on PPP basis........

Nimejaribu kuangalia kama hawa Merchant Holdings ni subsidiary ya CCCC Ltd lakini nimegundua hizi ni kampuni mbili zinazojitegemea......That said....inaonekana hapa kuna mgongano wa kimaslahi kwa upande wa hawa mawaziri wa TZ......kwamba tayari kuna maktaba kati ya TPA(TZ) na CCCC Ltd na pia kuna hawa Merchant Holdings ambao wanaonekana kuwa very desperate kupata hii lucrative deal.......

Sasa sijui hawa mawaziri wametoa conclusion gani kuhusu hili jambo....only time will tell........
 
You got it right Mkuu!! Mkataba hapo ni CCCC na TPA na hawa CMH wamepewa matumaini na Nundu na sasa wanashangaa mbona wamepata taarifa za Mkulo kuendelea na mawasiliano na Exim on CCCC!!! sasa hapa ndio nasema Nundu alipaswa kutafuta njia ya kuvunja mkataba kwanza na hawa CCCC ndipo aendeleze dili na CMH... sina ugomvi na hilo, ugomvi wangu ni kwamba serikali moja haiwezi kuwa na kampuni mbili tofauti kwa mradi mmoja kwa wakati mmoja.

Ndio maana pamoja na udhaifu na kuingizia hasara serikali, Nundu alikuwa sawa na bodi ilikubaliana naye kuvunja mkataba wa ujenzi wa maegesho ya magari kama nyaraka hii inavyoonyesha hapa;

attachment.php
 
Attachments

  • Magesho-Nundu-2.jpg
    Magesho-Nundu-2.jpg
    36.7 KB · Views: 201
You people are confusing us ujue which which then an who is right above all? Hivi mnaeleweka kweli kwa mtanzania wa kawaida kabisa wa kule kwa bibi na babu au mnacheza tu na akili za wachache?
 
You people are confusing us ujue which which then an who is right above all? Hivi mnaeleweka kweli kwa mtanzania wa kawaida kabisa wa kule kwa bibi na babu au mnacheza tu na akili za wachache?

Ndio maana ya "The Home of Great Thinkers", tuchambuane hapa, then kikieleweka (kama EPA/Richmond etc) ndio kina Slaa wetu wanapeleka kwa umma uamue..... Walipinga watu wakasema "Ya kuokoteza kwenye mtandao"!!! Pole pole tu tutafika.... Kitaeleweka tu!!! Watabana, weeee!! mwisho kitaeleweka tu!!! Ukweli ndio njia pekee, bila ubishi!!
 
Nchi imeoza.

Pande zote 2 kuna tatizo. Kwanza ni kwa nini hiyo kazi isitangazwe wazi kampuni zishindane kama taratibu zinavyotaka.

Inakuwaje wizara 1 inakua na makundi mawili kila moja linakimbiza dili kivyake hii pia ni dalili kuwa kuna harufu mbaya kwenye dili nzima.

Lakini huyu Nunda ndio ametia fora hata aibu hana. Yuko tayari kukabidhi mradi pekee unaozalisha kwa wageni kwa miaka 45 kwa pesa ambazo naamini mradi ukikamilika gharama za ujenzi zinaweza kupatikana ndani ya mika 10.

Kichekesho zaidi ni jinsi ujinga huu ulivyo wazi lakini mamlaka husika zimeshindwa kuwawajibisha wahusika.

Kwa ushahidi huu naelewa sasa kwa nini hata magogoni wanajikanyaga.

Kwa sasa hatima ya nchi hii ipo kwa Watanzania wenyewe. Hakuna tena uongozi jahazi la nchi linazama.
 
Ndio maana ya "The Home of Great Thinkers", tuchambuane hapa, then kikieleweka (kama EPA/Richmond etc) ndio kina Slaa wetu wanapeleka kwa umma uamue..... Walipinga watu wakasema "Ya kuokoteza kwenye mtandao"!!! Pole pole tu tutafika.... Kitaeleweka tu!!! Watabana, weeee!! mwisho kitaeleweka tu!!! Ukweli ndio njia pekee, bila ubishi!!

Kuna mambo mengi bado hayajawekwa wazi na hapa nataka pia mwenyekiti wa kamati ya bunge ya miundo mbinu - Peter Serukamba ahojiwe ambaye amekuwa mbele kusema CCCC ipewe kazi mara moja. Je, TPA wanafahamu nini kuhusu hiyo CCCC? Wameichunguza hiyo CCCC na kuridhika kuwa wana record nzuri na sio wala rushwa? Pia gharama walizotoa CCCC hata kama ni mkopo ndio gharama halisi za kujega gati? Na nani aliwaambia CCCC au China Merchants kuwa Tanzania wanataka kukarabati gati? TPA walitangaza tender?
 
Mkuu Nderingosha.....kwa sasa......kuna makubaliano kati ya MFIs kama WB, IMF, AfDB, AsDB, EU, DfID, etc etc kuwa endapo kuna individual au kampuni itaoneka imejiingiza katika vitendo vya rushwa and the likes.....basi hao wasiruhusiwe kupata kazi inayofadhiliwa na MFIs hizo..............serikali yetu pia is in support of this......na ndio maana watu kama Norconsult AS walipigwa chini TZ.........halafu leo tunataka kuwabeba CCCC......hivi hawa Exim are they for real kweli?........Damn!
Ogah you are right.....TZ ni muumini wa maridhiano mengi sana duniani lakini ndie mvunjaji namba moja wa maridhiano haya.....chukua tu mfano mdogo.....

Leo hii JK anatoka Brazil kuudhuria mkutano wa uwazi na uwajibikaji serikalini....wakati serikali yake mwenyewe sasa hivi mawaziri wake wanatuhumiwa kwa kukosa uwajibikaji.....what a paradox eh!!na pia hamna uwazi kwenye serikali yake...ukichukulia suala la hii mikataba.....Ukija kwa upande wa hizi nchi kama china...wao wana criminal law yenye kusema kuwa bribery(rushwa)itolewayo na makampuni yao/watu wao nje ya nchi ni offense.....na kwa maana hiyo ungetegemea kampuni hii ya CCCC Ltd iliyopigwa marufuku na WB kule Ufilipino kwa sababu za fraud ingechukuliwa hatua na jamhuri ya china lakina hilo halikufanyika...

...hapa unapata picha moja tu kuwa hawa jamaa wanalindwa na serikali yao wawapo nje.....tofauti na ambapo haya yangefanywa na kampuni za nje zilizopo china (wangeadhibiwa na china).....no wonder utazikuta kampuni za china hata kwenye rogue countries kama iran, libya, syria etc etc ambako wana operate kwa kuwahonga watawala.........
 
Back
Top Bottom