Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,154
- 128,811
Mkuu Kimbunga, mambo mengine wee acha tuu!.Mkuu Pasco una maana beneficiaries walishachukua chao mapema hivyo PIGA GAUZA CCCC lazima wapewe na ili waweze kurejesha pesa walizotoa. Hata hizo za Mfutakamba ni sehemu ya hizo pesa. Watu wanachukua upfront Mkuu. Unaambiwa chetu mapema kabisaaa sasa Nundu anapoingia kuzuia ndipo yanapomkuta hayo yanayomkuta! Anapigwa dana dana, anabezwa na kushambuliwa toka kila upande!
Jana nilivyomuangalia kwenye TV nikaona ana siri kubwa moyoni hakutaka tu kutaja ila Naibu wake ametaja. Ustaarabu tu wa kikazi na kutawalana mahala pa kazi; hata kama Naibu Waziri anapata ruhusa toka kwa Waziri Mkuu lakini si inabidi umuage Waziri wako? Utaondokaje bila Waziri wako kufahamu? Mfutakamba alitumwa?
Nimeuliza nani anaejua hao CCCC wamepatikanaje?, hakujatolewa tangazo lolote hata la EOI tuu achilia mbali tender!.
Laiti watu wangelimjua who is behind Mfutakamba, mtagundua Nundu ni mtu wa kuhurumiwa tuu!.
Nchi hii inajengwa na wenye moyo kama Nundu na inaliwa na wenye meno kama Mfutakamba!.
Last edited by a moderator: