Nyani Ngabu Kafa!!!!

Status
Not open for further replies.
Kama mwanachama mwingine ameenda nyumbani kwake.. na kukuta jamaa ka log in na yeeye akaamua kupost tu badala ya kusubiri kujiandikisha itakuwaje? Miye niko open minded... na ninafuatilia lakini sasa hivi sipuuzii jambo lolote kwani wanadamu tunauwezo wa mambo mengi sana.

Kweli kabisa Mwanakijiji!! Watu wanadhani haiwezekani mtu mwingine ku post kwa kutumia jina la mwingine. Binamu yangu Nyani ni mtu ambaye alikuwa anapenda convinience. Kwake mambo ya ku log in and out kila alipotaka kubandika alikuwa hayapendi. Kwa hiyo mara zote yeye alikuwa ame log in.

Halafu sielewi kwa nini watu wanatilia mashaka habari hii ya kuhuzunisha. Sishangazwi sana kwa sababu kuna ambao wanaamini kuwa Balali kafa na kuna wanaoamini kuwa Balali yu hai.
 
Watu wanakufa kila siku , we wacha tu, ila hawa walioko hai tusiwape nafasi ,alafu CCM wananunua muda kwa visa vya kuuwana ,huwezi kujua.
 
Nyani what are you up to bro? Au ushakwapua mahali na wewe na unataka ujipoteze kwa kujifanyia ballalization? Basi malizia kabisa tangazo lako kuwa mazishi yatakuwa ni kwa 'ndugu wa karibu' tu.
 
Ndugu yangu usipuuzie hata kidogo habari hizi......Mimi ni ndugu yake wa karibu sana...


Sasa wewe mkuu umepata vipi password yake?
Maanake hata ku-share password ni kosa hapa JF. anyway,ngoja nichelee kusema R.I.P

Plz usijekuta unafanya masihara ya weekend lakini
 
Wee binamu yaani umefiwa bado unapata muda kukaa hapa badala ya kulia sana kama wasukuma wote walivyo!..
 
Habari zinazoingia sasa hivi ni kwamba Bwana Nyani Ngabu alikuwa kwenye starehe na rafiki zake watatu wa kike ktk eneo la Camp Creek Market Place, ukatokea ugomvi kati ya mmoja wa madada aliokuwa nao na mtu ambaye identity yake haijatambulika. Kama ilivyo kawaida ya ndugu yetu Nyani Ngabu, hakuweza kuvumilia na akaingilia kati ugomvi huo........

Mkuu so far reports zilizoko ni ile shoot out iliyotokea Game Room 1326 Moreland Avenue.
 
Hii haipendezi hata kidogo,kwa Mtindo huu tutakuwa tunakaribisha Mambo yasiyo ya kistaarabu katika Uwanja huu,Forum hii ni kubwa na inasomwa na wengi kuliko tunavyofikiri,sasa kidogo tujaribu kuwa serious,na kutoa Ripoti zenye ukweli.Hata kama habari hii ina ukweli,lakini mtindo wa kuiripoti umekaa vibaya.Wakuu tufanye masahihisho kwa hili,kama kuna chochote kimemtokea ndugu yetu tupewe Taarifa iliyokamilika.....

Ndugu wa Karibu wa Nyani kama sio Nyani mwenyewe,liweke sawa hili,vinginevyo tutakuja kuwa tunapuuza mambo yanayotaka attention ya haraka.Wanachama mliopo humu lifuatilieni hili kwa ukaribu..
 
Jamani mwee hivi bado hamjamshitukia huyu jamaa Nyani Ngabu?..
anachotaka kudhihirisha hapa ni kile kila siku anachosema...NDIVYO TULIVYO..na moja ya definition ya huu msemo ni kuwa - Believe this, you will believe anything!..
 
R.I.P Nyani ngabu, I hope kabla hajafa alifanikiwa pia kuchagua nchi ya kuzikiwa !!!
 
Naona hapa ni kutaka kuwekana sawa kwa zilizokwisha tokea ,GO ON NYANI NGABU ila ulichokosea waliokufa hawasemi kungefanya kama binamu kweli kujisajili na jina jingine au ungetafuta mweneza propaganda mwanachama humu.

Binamu pole kwa msiba mzito kwa kweli ameacha pengo kubwa hapa JF na amekufa akiwa mtu huru.
 
Wee binamu yaani umefiwa bado unapata muda kukaa hapa badala ya kulia sana kama wasukuma wote walivyo!..

Sasa mimi binamu yake nikianza kulia lia hakuna la maana litakalofanyika. Katika huu muda mgumu ni muhimu kwa mimi kugangamala kama mwanamume wa shoka...
 
makubwa marehemu ndo kapost?mimi sielewi kitu hapa!au kauliwa akiwa online?ndo wauaji wamepost.
 
Mwenye kutaka kuamini na aamini na asiyetaka kuamini na yeye asiamini ila sisi ndugu zake wa karibu tunaendelea kuomboleza. Mnaochukulia hili jambo kwa masihara hiyo ni juu yenu na uamuzi wenu kama manavyofanya kuhusu Balali!
 
Sasa mimi binamu yake nikianza kulia lia hakuna la maana litakalofanyika. Katika huu muda mgumu ni muhimu kwa mimi kugangamala kama mwanamume wa shoka...

Mkuu jaribu kupiga hii number 770-306-3001
Alafu mwili uko hospitali gani? natumaini Grady.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom