KWA HALI ILIPOFIKIA HAKUNA MWANASIASA WA KULIJENGA TAIFA KATIKA MISINGI YAKE TENA .
JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA LINATAJIWA LIOKOE HILI TAIFA .
Kuna uvunjwaji mkubwa sana wa Katiba .
Kuna mgawanyo mbaya sana wa rasilimali za Nchi hasa Tanganyika.
Kuna mgawanyo mbaya sana wa ajira katika wizara zisizo za muungano na hata zile za muungano.
Kuna mgawanyiko mkubwa sana wa kisiasa ndani ya vyama vyote.
Kuna uadui mkubwa sana wa Wazanzibari kwa watanganyika wanaodhaniwa kuwa wanampinga mama . Uadui huo usipoangadhibitiwa utaingia ndani ya vyombo vyaulinzi na usalama .
Kuna mgawanyiko mkubwa sana wa kidini . Hakuna mahali popote duniani penye kuheshimu haki na sheria na usatawi wa nchi ambapo Kiongozi yeyote duniani amewahi kudharau na kupuuza kwa wazi maoni na hoja za Viongozi wa juu wa Kanisa Katoliki na makanisa mengine kwa kutumia vizisho na mauaji na propaganda za kidini na machawa halafu nchi hiyo ikawa salama . Haijawahi kutokea popote .
Idara ya usalama wa taifa na Polisi imekua ndiyo sasa tegemeo la ukiukwaji wa haki na kinga kwa wanasiasa,watawala na mahakama zisizofuata sheria na katiba .
Maendeleo ya nchi yanasuasua sana ukilinganisha na maendeleo na utajiri wa kutisha unaopatikana kwa haraka kwa watawala na wansiasa na machawa na wakwepa kodi na wauza unga.
Siasa imegauka kuwa sehemu ya kupora rasilimali za umma .
Jeshi la polisi limekua ni idara inayotumika kuligawa Taifa na kulinda watawala wasiokubalika badala ya kulinda watu wote kwa haki na kupambana na uhalifu . Uhalifu unaibuka kwa haraka sana .Utapeli wa kimtandao unakithiri kwa sababu Polisi muda wote wanahangaika na wakosoaji wa kisera badala ya wahalifu matokeo yake hakuna usalama kwa wananchi wa kawaida na nguvu kubwa inatumika kulazimisha watawala kurudi madarakani .
Maadili yameporomoka sana. Ushoga ,ndoa zinayumba kwa sababu kuna watu wanajionyesha katika mafanikio ya kujipatia fedha pasipo na biashara zinazoeleweka zaidi ya kutakatisha fedha jambo linalowafanya waishi maisha ya ulaghai na anasa huku wakiwa wanatumia fedha haramu kirubuni Vijana wasio na ajira . Hakuna sheria kali ya kulinda familia, yaani mume ,mke na watoto wapate malezi bora ya wazazi wawili badala yake mashangazi yameongezeka kutokana na mifumo isiyofaa ya kupeana vyeo bila kuangalia historia ya uadilifu kuanzia kwenye familila .
Fedha nyingi za umma zinatumika kwa watawala kijijenga kisiasa. KWA MFANO HIVI MTU MAKONDA ANAFANYA BIASHARA GANI INAYOMPA FAIDA YA MABILIONI YA FEDHA? ANA HISTORIA GANI YA KUFANYA BIASHARA POPOTE NA ANALIPA KODI AU VIPi ?
Lkini sio yeye tu bali umekua ni kama mfumo sasa mtu akiwa mteule wa Rais au chawa anageuka kuwa bilonea ghafla wakati miradi ya serikali ikiwa ianenda tatatibu kwa miaka mingi .
Sterehe na anasa zimekua ni kama kipao mbele cha Wanasiasa na watawala huku wazalendo wa kweli kama wanajeshi wetu wakiwa wanajitafutia maisha kwa kwenda kujitoa muhanga kupigania mataifa mangne kama Kongo ,Sudani nk ili wapate angalau pesa za kujenga nyumba na kuziba mapengo ya mikopo yenye ruba kubwa kwa mishahara midogo isiyojali hatari katika kazi zao .
Watanzania wengi hasa Watanganyika wanakufa Katika hospitali za umma na kufilisika kabisa huku wakiziacha familia zao katika imaskini mkubwa kutokokana na gharama kubwa za matibabu ya magonjwa ya Figo ,presha na kisukari .
Hospitali za umma hazihufumii tena watu kwa ajili ya kuponya bali zimegauka kuwa ni miradi ya kakikundi ka watu wachche na bodi yao huku wananchi wanaolipa kodi wakibaki kuwa ndio mitaji yao.
Taifa halina zena ushindani wa hoja kitaaluma na kiitikadi katika kila sekta.
Elimu imedharaulika badala yake machawa na matapeli wanaonekana wa maana na ndio wanaotumiwa na wanasiasa kuonyesha ufahari wa kupata mali pasipo kufanya kazi kwa ufanisi na kwa juhudi na maarifa .
Watawala wamewekeza mabilioni ya pesa kwenye mambo ya kupumbaza akili na starehe kama vile mpira na Makongamano na matembezi ya kuunga mkono kila kitu bila kujali kuwa kuna makosa .
Bidhaa muhimu za uzalishaji kama pembejeo za kilimo zinauzwa kwa bei kubwa wakati pombe na sigara haziwekewi kodi kubwa ili kupunguza ulevi na statehe .
NI LAZIMA PAWE NA CHOMBO KINGINE NJE YA WANASIASA KITAKACHOLIREJESHA TAIFA KATIKA MISINGI YAKE YA UMOJA ,KAZI ,UTU ,UWAJIBIKAJI ,MIIKO ,MAADILI NA MAENDELEO YA NCHI BADALA YA MAENDELEO YA WATU WACHACHE .