Mkuu unaamini jeshi likishika nchi mambo yatakuwa mazuri zaidi hapa sio?
Umefafanua vizuri Mkuu Ok General gani wakijeshi au jeshi lipi sasa la kushika nchi na kufanya hayo uliyo yafafanua?
Jeshi hua ndicho chombo kinachoinusuru nchi isiingie kwenye machafuko ya kisiasa ,kijamii na hata kiuchumi.
Vita vya kikabila ,kidini na kisiasa hua zinasababishwa na serikali kupitia vyombo vya dola.
Mafano : Kongo wakati wa mabutu Jeshi lilikua na nafasi nzuri ya kumtoa Mabutu na kunusuru nchi na wengi wakapona kuliko kumlinda mtu mmoja .
Mnaweza mkaacha mtu mmoja mkidhani ni kiongozi kumbe ameshachanganyikiwa au amepaniki kutkana na akili yake kufubaa. Watawala Wengene wanatumia sana vilevi na kuingia ofisni wakiwa na hang over.
Wengine wa hasira ya kukosolewa sio hasira ya kupambana na ufisadi kama tuliye naye Tanzania.Sasa watu kama hao ni rahisi kutoa mwanya kwa wapambe wake kutumia risasi kuwaua wanaompinga ili kumfurahisha matokeo yake damu zinaibua hasira za watu kidogo kidogo.
Jeshi likiwahi linaokoa hali ya mkwamo wa kisiasa na kunusuru nchi kuingia kwenye machafuko.
Mfano tu Tanzania kwa sasa ni wazi kabisa kuwa Samia anatumia nguvu kubwa sana kuutaka urais na hatuekewi anataka kulinda maslahi ya nani hasa maana maslahi ya nchi hayalindi ,usalama wa watu halindi yeye zaidi watu wanapotezwa na watu ambao hata yeye hawajui ikiwa na maana ameshindwa kutoa maelekezo ya kukomesha mauaji na utekaji .
Lakini pia ni wazi kuwa Samia anaona wazi kuwa kuna mpasuko unajitokeza wa kidini lakini yeye kama vile anauchochea ili kupandisha hasira upande mmoja na kufurahisha upande wa pili .
Yaani ni kama vile anaandaa upande mmoja wa dini kupambana na upande ule unaompinga .
Yaani kwa hali ya kisiasa ilivyokaa ni kichekesho na kucheza na amani ya nchi kwa Rais kuita viongozi wote wa dini moja nchi nzima na kutumia jukwaa hilo kutoa matamko ya kulaani dini nyingine au kutumia jukwaa hilo kujibu matamko ya kisiasa.
Yaani Samia alitakiwa kama mkuu wa nchi ajitenge kabisa na masuala ya kidini kwa kuitisha kama Rais .
Ndio maana ukifuatilia mitandaoni utagundua kuwa kuna dini moja inajiandaa kumlinda rais kuliko hata vyombo vya dola .
Sasa hii ni hatari sana.
Mfano Makanisa yamefungwa na mapadri wanapigwa na wachungaji wanatekwa lakini hayafungwi kwa sababu ya kuukashifu au kuutukana Uislam bali kwa sababu ya kukeme utekaji na mauaji yanahusishwa na siasa . Sasa cha ajabu wanaojitokeza kuwatukana kwa wazi na kuwatisha hao viongozi wa makanisa ni Mashehe na baadhi ya waumini wa Kiislam. Tena kwa hisia kkoli kuwa amani itapotea mkiendelea kukosoa na kukemea wizi wa kura,ufisadi na mauaji . Na Sasa kwa hali hiyo unaona wazi kuwa nyuma yao kuna watu wakubwa inawatumia kujinufaisha.
Haki haina dini wala kabila lakini kwa sasa haki imekua ni jambo la kidini kwa babu tu serikali haitaki litumike wakati huu wa uchaguzi cha ajabu kuna dini inaunga mkono kuwa haki iwepo na doni nyingine kupinga suala la haki kwa sababu tu ya kuwa tayari kupambana na yeyote asiyemuunga mkono rais.
Sasa kwa hali kama hiyo bila Jeshi kuingilia kati na kushika dola kwa Muda nchi itaingia kwenye machafuko au mauaji makubwa yanayofanywa na dola ikishirikiana na wapambe ,machawa na wale wanaofadhiliwa kupambania serikali ndani ya dini.
Kule zimbabwe Mugabe alipumzishwa kwa manufaa ya nchi maana alikua hajui hata anachofanya .
Kusubiri eti uchaguzi ufanyike ni kuliangamiza taifa. Uchaguzi gani wa rushwa , uongo , lakni ukiojaa hisia za kidini tena kwa wazi kabisa .