Nini kitatokea dawa ikimdhuru mtu aliyeinunua pharmacy bila cheti cha daktari? Majibu haya hapa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Mfamasia Neema J. Nagu kutoka Wizara ya Afya anasema kuna dawa za aina mbili zinazouzwa kwenye Duka la Dawa, zipo ambazo hazitolewi bila cheti kama Panadol na zile za mafua na nyinginezo.

Anasema “Dawa nyingine zinatakiwa kutolewa na cheti mfano dawa zote za Antibiotic hizo lazima anayehitaji awe na cheti cha Daktari.

“Inapotokea mtu kauziwa Antibiotic bila cheti ni kosa na mgonjwa akipata madhara basi mwenye muuzaji anatakiwa kuwajibika, ndio maana katika taratibu za usajili wa Duka la Dawa lazima awepo mtaalam wa Famasia ambaye amesomea na kuna ukaguzi unafanyika kuhakikisha hilo mara kwa mara.
pharmacy.jpg
“Ikitokea mtu kauziwa dawa ambayo alitakiwa kuipata akiwa nc cheti cha Daktari kisha mgonjwa akapata madhara na Mamlaka ikijiridhisha juu ya hilo, hatua ya kwanza Duka litafugwa, yule mtu wa Famasi ambaye cheti chake kimetumika naye atawajibika.

"Kuchukua hatua za kinidhamu kwa Professionals, kuipeleka case Mahakamani kama italazimika na kuendelea kutoa Elimu stahiki ili tatizo lisije jirudia tena."

Ameeleza kuwa uwepo wa Pharmacy Council (Baraza la Famasi) ambacho ni chombo cha kisheria chini ya Sheria ya Famasi sura ya 311 kinadhibiti mazoezi ya wataalamu wa maduka ya Dawa na masuala yanayohusika nayo.

Baraza hilo linahusika na Professional Conduct kwa wataalam (pharmaceutical assistants, Pharmaceutical Technicians na Pharmacists).

Kuhusu matukio ya matukio ya wagonjwa kulazimisha kupewa dawa wanapikuwa sehemu hizo anasema mhusika anatakiwa kuwa na msimamo na kuzingatia maadili ya kazi yake.

Pia soma
- Atakayeuza Antibiotic bila cheti cha Daktari kupelekwa Mahakamani
 
Back
Top Bottom