Je, dawa za antibiotiki zina madhara gani kwa utumbo wako?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,329
33,138
g

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Miili yetu ina matrilioni ya bakteria ambayo hatuwezi kuishi bila kuwa nayo idadi kubwa ya bakteria hao wakiishi zaidi katika matumbo yetu. Lakini je, tunaharibu kabisa sehemu hii muhimu ya mwili wetu kila wakati tunapotumia dawa za antibiotiki?
"Viini vya bakteria vya utumbo huwa na mchango mkubwa katika afya nzima ya utumbo wa binadamu katika kuuwezesha kuendelea na kazi yake," anasema James Kinross, daktari mshauri wa upasuaji wa utumbo mpana katika Chuo cha Imperial London.
Bakteria hawa wanaoishi katika utumbo wana jukumu kubwa katika kudumisha afya yetu, ikiwa ni pamoja na kudhibiti mfumo wa kinga na kusaidia usagaji chakula. Na wataalam wanasema kwamba antibiotiki ni moja ya tisho kubwa kwa vimelea hawa wnaoishi ndani ya utumbo wetu.
Antibiotiki, ambazo kawaida hutumiwa kwa ajili ya kutibu na kuzuia maambukizi ya bakteria, ni msingi wa dawa za kisasa. Lakini katika mchakato wa kulenga bakteria zinazosababisha maambukizi katika miili yetu, pia zinaweza kufuta bakteria wengine wazuri katika miili yetu bila kukusudia.
Kuna wasiwasi unaoongezeka miongoni mwa wanasayansi kuhusu athari za kiafya za utegemezi wetu unaoongezeka wa dawa za antibiotiki; kati ya 2000 na 2015, maagizo ya kimataifa ya antibiotiki yaliongezeka kwa 65%. Tatizo la kuongezeka kwa matumizi ya antibiotiki ni mara mbili: uharibifu unaosababishwa na vimelea wa utumbo, na kuongezeka kwa upinzani wa bakteria kwa dawa za antibiotics.
h

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Dawa za antibiotiki zimekuwa msingi wa dawa za kisasa, lakini kuna wasiwasi unaoongezeka kuhusu utumiaji kupita kiasi

"Dawa za antibiotiki huvuruga mfumo tata wa ikolojia wa vimelea (bakteria)wazuri katika utumbo na, kwa kufanya hivyo, huweka bakteria waliosalia katika hatari kubwa ya kutoa jeni zao sugu dhidi ya viini vya magonjwa," anasema Gautam Dantas, profesa wa maabara na dawa za jeni katika Shule ya Tiba ya Chuo Kikuu cha Washington kilichopo St Louis nchini Marekani.
Tunajua kuwa kadri bakteria wa utumbo wanavyotofautiana, ndivyo inavyokuwa bora zaidi.
Lakini kila dawa za antibiotics zinavyotumiwa kunakuwa na mvurugano wa idadi hii ya bakteria sababu dawa za kuua bakteria hazilengi vya kutosha kuua tu bakteria wanaosababisha maambukizi tu. Badala yake, wanafuata bakteria zote kwenye matumbo yetu na hivyo kuangamiza pia bakteria wazuri kwa afya zetu.
"Kuna athari ya dhamana," anasema Dantas. "Fikiria msitu ambapo unajaribu kuondoa maambukizi ya magugu; jinsi tunavyotumia dawa za kuua vimelea huwa kunakuwa na kuua bakteria wazuri na wabaya."
Wakati wanasayansi wameangalia tena bakteria za watu ambao wameambukizwa na kufuatiwa na sababu ya antibiotics, wamegundua kuwa utofauti wa vimelea hupona ndani ya miezi michache, Dantas anasema. Lakini katika baadhi ya watu, baadhi ya bakteria nzuri hazijitokezi tena , anaongeza.
Dantas na timu yake ya watafiti wamechunguza sampuli za kinyesi zilizokusanywa kutoka kwa watoto wanaotibiwa katika hospitali ya watoto iliyounganishwa na maabara yake.
Sampuli hizi zilikusanywa mara kwa mara, kabla ya maambukizi yoyote na antibiotics, ambayo iliruhusu timu yake kuona mabadiliko ya watoto wanaopata maambukizi na kupewa antibiotics baadaye.
Dantas ametumia sampuli hizi kulinganisha mabadiliko ya bakteria wazuri wa utumbo baada ya antibiotiki katika makundi mawili ya watoto wachanga - watoto waliozaliwa kabla ya wiki 36, na watoto wachanga, waliozaliwa baada ya wiki 36.

Tunapoteza utofauti katika matumbo yetu na vijidudu muhimu ambavyo vimetudumisha kwa maelfu ya miaka - James Kinross

Ingawa athari hutofautiana kati ya mtu na mtu, na hutegemea umri wetu, makubaliano kati ya wanasayansi ni kwamba athari za dozi moja ya antibiotiki inaweza kudumu.
"Baadhi ya watu huathirika sana na uharibifu wa vijidudu (bakteria wazuri) kutokana na matumizi ya antibiotiki na ikolojia yao ya viini hivyo itabadilika sana na haitarudi kama ilivyokuwa kabla ya kipimo cha dawa," Kinross anasema.
"Tunapoteza utofauti katika matumbo yetu na vijidudu muhimu ambavyo vimetudumisha kwa mamia ya maelfu ya miaka [vinapotea] kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea."
Lakini wanasayansi bado wanajaribu kusuluhisha matokeo ya kiafya ya muda mrefu ya utumiaji wa antibiotics kwa bakteria wazuri wa utumbo.
w

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Bakteria ya pathojeni inaweza kupata upinzani kutoka kwa bakteria hatari ambao huishi kwa matibabu ya antibiotics

"Tunajua kwamba antibiotiki ina uwezo wa kuathiri kazi ya microbiome ( bakteria wazuri wanaoishi katika utumbo wetu)." Kinross anasema. "Hazipunguzi tu idadi ya bakteria, lakini pia huathiri kazi ya vijidudu kwa njia ngumu, za kibinafsi ambazo hatuelewi vizuri."
Sio tu athari kwa bakteria ya utumbo ambayo inasababisha wasiwasi, lakini pia matokeo ya pili juu ya maendeleo ya mfumo wa kinga, Kinross anaongeza.
Uchunguzi unaonyesha kuwa kuchukua vipimo vya mara kwa mara vya antibiotiki kuna athari nyingi, na athari pia ni kubwa zaidi ikiwa unachukua kipimo cha wigo mpana zaidi. Hii mara nyingi hujulikana kama "hypothesis nyingi".

Bakteria sugu wanaweza kuhama kutoka kwenye utumbo hadi maeneo mengine, kwa hivyo kile kinachotokea kwenye utumbo kina athari kwa mwili wetu wote - Craig MacLean

Matokeo mengine ya matumizi ya muda mrefu ya antibiotics ni hatari ya dawa hizo kushindwa kufanya kazi. Wakati idadi ya bakteria inakabiliwa na antibiotiki, wale ambao hawana jeni za udhibiti wa antibiotics hufariki.
Hili huwa tatizo wakati bakteria ya pathogenic huvuna thawabu za kukabiliana na hali hii.
"Kila wakati tunapotumia antibiotics, tunaongeza hatari ya uwiano wa vimelea wanaoishi katika utumbo kurutubishwa kwa jeni zinazokinzana na dawa, "Dantas anasema.
Na mchakato huu hauko kwenye matumbo yetu pekee, anasema Craig MacLean, profesa wa mageuzi na baiolojia katika Chuo Kikuu cha Oxford. "Bakteria sugu wanaweza kuhama kutoka kwenye utumbo hadi maeneo mengine, hivyo kinachotokea kwenye utumbo kina athari kwa mwili wetu wote," anasema.
f

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Wanasayansi wanasema matumizi ya kiholela ya antibiotiki yanaweza kuwa na athari za muda mrefu kwa afya ya utumbo na mfumo mpana wa kinga

Athari mbaya na za kuokoa maisha za antibiotiki ni moja ya utata mkubwa unaowasumbua wanasayansi kote ulimwenguni.
Ingawa hakuna suluhu moja, kuna mbinu ambazo zinaweza kupunguza madhara ya antibiotics kwa afya zetu.
"antibiotics ni dawa za ajabu ambazo zimeokoa mamilioni ya maisha. Ni rasilimali za thamani sana na zinapaswa kutumiwa, lakini tunahitaji kuelewa jinsi ya kuzilenga kwa usahihi," anasema Kinross.
Wanasayansi sasa wanaangalia antibiotiki zinazolenga zaidi sehemu za mwili, na vile vile zinazolenga bakteria maalum, MacLean anasema, kwa wazo la kuondoa tu bakteria unayotaka kuondoa, na kuacha bakteria yenye faida ndani ya utumbo mzima.
Lakini chombo kikubwa zaidi tulicho nacho kwa sasa, anasema Anthony Buckley, profesa mshiriki katika baiolojia ya utumbo katika Chuo Kikuu cha Leeds, ni mlo wetu. "Lishe ni mojawapo ya vichochezi vikubwa katika kutengeneza mfumo wa bakteria katika binadamu," anasema.
Kikundi cha utafiti wa maambukizo yanayohusiana na afya cha Chuo Kikuu cha Leeds kimekuwa kikijaribu athari za antibiotics kwa bakteria wazuri wa utumbo kwa miongo miwili iliyopita.

Ni bora zaidi kutotegemea antibiotiki - James Kinross

Aina nyingi zaidi za vyakula tunavyokula kawaida huhusishwa na aina nyingi za vijidudu kwenye utumbo, na nyuzinyuzi haswa zinaonekana kuwa na athari chanya, "anasema Ines Moura, mtafiti mwenza katika kitivo cha dawa na afya cha Chuo Kikuu cha Leeds, ambaye kwa sasa anafanyia majaribio ya athari za virutubishi tofauti kwenye mfumo wa bakteria wa utumbo na jinsi unavyoweza kupunguza athari mbaya za antibiotiki.
Nyuzinyuzi za lishe ni muhimu sana kwa sababu vijidudu katika mwili wetu huzimeng'enya na kutoa asidi fupi ya mafuta, ambayo hutoa nishati kwa seli zinazozunguka utumbo, anasema Buckley.
"Unapokuwa na antibiotiki, vijidudu vinavyozalisha asidi ya mafuta ya utumbo mfupi hupungua na kuchukua muda kupona. Nadharia yetu ni kwamba, kwa kumeza nyuzinyuzi za chakula, hutoa utumbo unaweza kuwezesha kutengenezwa kwa bakteria hizo na kuzikuza na kuzalisha asidi ya mafuta, na hivyo kunakuwa na matumaini ya kuweka usawa wa bakteria tena kwenye utumbo, "anasema.
h

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Kula lishe yenye nyuzinyuzi nyingi hufikiriwa kusaidia kuunda mazingira ya utumbo yenye manufaa zaidi kwa bakteria yenye afya

Ajabu inayotokana na utumiaji wa antibiotiki ni kwamba, kwa kila dozi tunayotumia, tunaweza kupunguza uwezo wa miili yetu kupigana na maambukizo, na kwa hivyo kuongeza utegemezi wetu kwa dawa hizo.
"Ni bora zaidi kutotegemea antibiotiki," Kinross anasema, "Na badala yake kuzingatia ustahimilivu wa kibaolojia wa ikolojia yetu ya ndani kwa kula vyakula vyenye virutubisho na vyenye kuleta afya, haswa katika maisha ya mapema ya mtu, kwani wakati huu ndio wakati ambapo antibiotics husababisha uharibifu mkubwa. " chanzo. Dawa za antibiotiki ni hatari? na je zina madhara gani kwa utumbo wako? - BBC News Swahili


THE MOST COMMON REASON FOR DEATH GOOD BACTERIA IS ANTIBIOTIC USE.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom