Wamiliki wa maduka ya dawa fuateni utaratibu sahihi wa utoaji wa dawa

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt Seif Shekalage amewataka wamiliki wa maduka ya dawa nchini fuateni utaratibu sahihi wa utoaji dawa kwa wagonjwa kulingana na maelezo ya cheti cha daktari.

Dkt. Shekalaghe ametoa agizo hilo leo Jijini Tanga wakati wakufungua kongamano la mrejesho wa Tafiti za Kukinga na kudhibiti Maambukizi na Usugu wa dawa za Antibiotic katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo.

Dkt. Shekalaghe ameeleza kuwa jambo hilo ni la msingi na Serikali wameweka sheria kali kwa mtu atakayekatwa atachukuliwa hatua lakini sasa wanazungumza wanaofanya kwa njia za siri ambao hawajagundulika wanasababisha tatizo linakuwa kubwa kwa jamii.

“Katika hili napenda kusisitiza wamiliki wa maduka ya dawa nchini wafuate taratibu zilizowekwa na Serikali wasitoe dawa kwa wagonjwa kama hawajakwenda na cheti cha daktari”, amesisitiza Dkt. Shekalaghe

Aidha Dkt. Shekalaghe ametoa wito kwa waandishi wa habari nchini kutumia kalamu zao kuweza kutoa elimu kwa wananchi juu ya uelewa wa athari za dawa bila kufata utaratibu

Vile vile amesema kuwa zipo dawa muhimu zilizowekwa kwenye maduka lakini dawa za antibayotiki wananchi wasitumie tu kufata utaratibu wa kuwa na cheti cha Daktari.

“Kutumia dawa bila cheti cha Daktari au ushauri wa daktari mtu unatengeneza mwili wako kuwa na usugu wa vimelea vya dawa mwilini ambapo ukipata dawa sahihi zitashindwa kufanya kazi”, ameeleza Dkt. Shekalaghe
Awali akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa NIMR, Prof. Said Abood ametoa wito kwa wananchi kutokununua dawa bila bila cheti cha daktari kwani kumekuwa na mazoezi wananchi kwenda kujinunulia dawa bila kujua kama kweli wanahitaji kutumia hizo.

Pia Prof. Abood amesema kuwa wanapoandikiwa dawa za daktari wahakikishe wanatumia dozi kamili na wanatumia kwa mujibu ilivyoandikwa na Daktari husika.

Aidha amewataka wananchi kuhakikisha kwamba wanafata utaratibu na matumizi sahihi ya dawa kulingana na cheti cha daktari na kuachana na mambo ya kujitibu wenyewe wanapopata tatizo la kiafya waende hospitalini waonwa na madaktari wapimwe wapate vipimo vya maabara na vitapaporudi kwa daktari ndio wanaweza kujua wanapaswa kutumia dawa ya aina gani.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, Dkt Naima Yusuf ameeleza kuwa katika utafiti huo walichofanya walichukua sampuli kutoka kwa mama na mtoto aliyezaliwa na kama amezaliwa kwa njia ya kawaida au upasuaji na vifaa vilivyotumika.

“Tupo hapa kwa ajili ya kusisitiza wananchi wasitumie dawa bila kujua wanaumwa na nini kwani kuna tabia unaumwa kidogo unakwenda duka la dawa unachukua dawa mwishowe zile dawa zinaacha kufanya kazi” ameeleza Dkt. Naima
20230725_153530.jpg
 
Back
Top Bottom