Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

Nini Hatma ya Upinzani Tanzania?

Upinzani haushindi kwa sababu Tanzania hamna upinzani wa kweli. Watanzania wengi wana jiuliza kwa nini mpaka leo hii miaka karibia ishirini tokea uingie mfumo wa vyama vingi bado vyama vya upinzani havifui dafu kwa CCM. Ni kwa sababu ya mazingira ambao yaliambatana na kuanzishwa kwa vyama hivi. Ni vigumu kwa vyama hivi kuondokana na mzigo wa historia ya uanzishwaji wao. Nita fafanua mtazamo wangu.

1. CCM ndiyo kilikua chama pekee Tanzania kwa muda mrefu. Kwa maana hiyo CCM ilikua na muda zaidi wa kujijenga kiuongozi, kirasilimali na kiumaarufu. Watanzania wengi hawana vyanzo vya kuaminika na vya haraka vya kupata habari kama wengi wetu humu JF. Kwa hiyo bado kuna Watanzania wengi (amini usiamini) wanaishi "jana".

2. Kabla ya kuruhusu vyama vya upinzania, CCM, chama kilicho kuwa madarakani kilikua na muda wa kujiandaa. Katiba ya kuruhusu vyama vya upinzani iliandikwa na wao na muda wa kujiandaa na mabadiliko wa mazingira ya kisiasa walikuwa nao.

3. "Personalities" nyingi zilizo unda vyama vya upinzani ni wana CCM wa zamani. Ukimuangalia Mrema Sharif Hamad, Mtei wote ni watu waliokua ndani ya mfumo wa CCM. Hata Ibrahim Lipumba ambae sina uhakika kama alikua CCM au la alikua mshauri wa Mwinyi kipindi fulani. Je hii ina wezaje kuwa tatizo kwa vyama vya upinzani?
a) Baadhi ya viongozi waliongia upinzani ina wezekana walikua mamluki ambao walikua hawana mpango wowote wa upinzani wa kweli.
B) Baadhi ya viongozi walioingia upinzani ni watu ambao walikua hawana future CCM kwa hiyo walihama kwa ajili ya kujaribu bahati yao. Hiyo ni kusema upinzani ilipokea watu ambao hawakua nyota wa kisiasa bali "has beens" wa CCM.
c) Baadhi yao ni watu waliyo ondoka CCM kwa maana hiyo mfumo wa fikira ulikua huo huo. Hauwezi kumshinda mwalimu kwa kumpa mtihani wake mwenyewe.

4. Wengi wa viongozi waliounda vyama vya upinzani kwa sababu moja au nyingine ita kuwa wali fikiria kwamba CCM ita shindika kiurahisi. SI ajabu baadhi yao wakadhani kwamba 1995 wange kiondoa CCM madarakani. Kwa maana hiyo basi vyama hivi vya upinzani vilivyo anzishwa vilikua havina mipango ya muda wa kati au mrefu kwa maumaini kwamba uchaguzi una kuja na wao wata shindda. Mpaka leo hii sioni mipango ya kueleweka ya muda mrefu wa chama chochote cha upinzani.

Kwa hiyo basi kama vyama vya upinzani kweli vina taka kushinda basi ni lazima kuwepo na mabadiliko. Lazima waletwe vijana ambao watakua katika mfumo wa vyama vyao. Lazima walete watu ambao hawaku wahi kuhusika na CCM ili kuleta mawazo na fikira tofauti. Ni lazima waji tazame na wajiunde upya. Kusema ukweli sioni chama cha upinzani kati ya hivi vilivyopo sasa kufanya mabadiliko yoyote ya kisiasa labda vyama vipya vita kapo anzishwa au viongozi wa sasa waliotoka kwenye mfumo ule ule, mawazo yale yale na mafunzo yale yale wakija kuondoka.

Ndugu wana JF tuna muda mrefu bado mpaka upinzani wa kweli Tanzania uibuke. Leo hii hatuna wapinzani bali wasindikizaji. Kwa maana kila kabla ya uchaguzi tayari imesha julikana chama gani kita shinda uraisi na chama gani kita kuwa na wabunge wengi Bungeni. Huo si upinzani.
 
Watanzania bado hawana imani na upinzani..
Ccm bado iko very strong.....
Time haijafika bado..
 
Watanzania walio wengi WAMERIDHIKA na hali yao ya maisha wanayoishi sasa.Period.
Hivyo wanapokosa elimu bora,huduma bora za afya,makazi bora etc kwao ni sawa tu...Wanashindwa kulink huduma hizi mbovu na utawala uliopo madarakani.Sasa inapotokea kuwa wananchi wanapewa khanga,kofia,fulana,pombe ili waichague ccm kwao huwa wanaona kuwa huo ni ukarimu wa ccm...Hence the saying,'akufaaye kwa dhiki...'
 
Ndhani kwa ufupi itachukuwa miaka therathini mbele kupata upinzani wa kweli.... Kama si another nusu karne
 
Mwanafalsafa1
Mbona unakwepa sababu moja muhimu ambayo inafanya upinzani usishinde Tanzania? Tutaikwepa hii sababu mpaka lini? Angalia yaliyotokea Kenya 2007 na sasa wanavyojizatiti kuiondoa sababu hiyo: Tume ya Uchaguzi. As long as tume ya uchaguzi inaundwa na serikali ya CCM, as long as UWT wanaruhusiwa kuingilia zoezi la kuhesabu kura, as long as polisi wote wanakuwa CCM na madiwani kutishiwa kuwa maeneo yao yakipoteza kura wamepoteza kazi upinzani hauwezi kushinda katu. Tusisahau hilo. Unadhani kwa nini Mkwere kawatishia wafanyikazi kwamba he can win without their votes? Kwa sababu anajua kuwa CCM ni hodari ku manufacture kura.
 
Mkuu usemayo ni kweli, lakini je hao wapinzani wenyewe mbona hawana umoja, kila mmoja anacheza kivyake... unategemea nini? Nilitegemea wao wangekuwa wamoja ki harakati katika kuwaelimisha wananchi haswa kule vijijini, lakini nao hawaonekani mpaka karibia na uchaguzi.
 
X-Paster,
Hilo la umoja ni muhimu. Hata Kenya walifanikiwa hatimaye kukiondoa KANU mamlakani kwa umoja. Lakini utaunganaje na mtu kama Mrema?
Ngoja akina Mrema wajitokeze uhalisia wao, wale wapinzani halisi walio na uchungu wa nchi watadhihirika. Bado tuna mwendo mrefu mbele, lakini naamini hatimaye tutafika tu.
 
Lakini mkuu mbona watu kama kina Mrema wanajulikana, hii ngoja ngoja mpaka lini... ni miaka ishirini na zaidi sasa tangia vyama vya upinzani vikubaliwe kikatiba... wanacho subiri ni kitu gani...!?

Waache kuuza sura bana.
 
Mwanafalsafa1
Mbona unakwepa sababu moja muhimu ambayo inafanya upinzani usishinde Tanzania? Tutaikwepa hii sababu mpaka lini? Angalia yaliyotokea Kenya 2007 na sasa wanavyojizatiti kuiondoa sababu hiyo: Tume ya Uchaguzi. As long as tume ya uchaguzi inaundwa na serikali ya CCM, as long as UWT wanaruhusiwa kuingilia zoezi la kuhesabu kura, as long as polisi wote wanakuwa CCM na madiwani kutishiwa kuwa maeneo yao yakipoteza kura wamepoteza kazi upinzani hauwezi kushinda katu. Tusisahau hilo. Unadhani kwa nini Mkwere kawatishia wafanyikazi kwamba he can win without their votes? Kwa sababu anajua kuwa CCM ni hodari ku manufacture kura.

Mkuu ulicho sema ni kweli na ipo kwenye category hii hapa.....naji nukuu

2. Kabla ya kuruhusu vyama vya upinzania, CCM, chama kilicho kuwa madarakani kilikua na muda wa kujiandaa. Katiba ya kuruhusu vyama vya upinzani iliandikwa na wao na muda wa kujiandaa na mabadiliko wa mazingira ya kisiasa walikuwa nao.

Tume hiyo ya uchaguzi ipo chini ya katiba iliyo andikwa na chama hicho hicho. Kwa maana kwamba katiba iliyo andikwa kuruhusu vyama vya upinzani iliandaliwa kuifavor kwa kiasi fulani CCM na tume ya uchaguzi ina fall under hii category kwa sababu mkuu wa tume pamoja na wajumbe wakuu huchaguliwa na raisi ambae kwa wakati huo ailikua wa CCM na mpaka leo CCM ina faidi privilege hiyo.
 
Upinzani haushindi kwa sababu Tanzania hamna upinzani wa kweli. Watanzania wengi wana jiuliza kwa nini mpaka leo hii miaka karibia ishirini tokea uingie mfumo wa vyama vingi bado vyama vya upinzani havifui dafu kwa CCM. Ni kwa sababu ya mazingira ambao yaliambatana na kuanzishwa kwa vyama hivi. Ni vigumu kwa vyama hivi kuondokana na mzigo wa historia ya uanzishwaji wao. Nita fafanua mtazamo wangu.

1. CCM ndiyo kilikua chama pekee Tanzania kwa muda mrefu. Kwa maana hiyo CCM ilikua na muda zaidi wa kujijenga kiuongozi, kirasilimali na kiumaarufu. Watanzania wengi hawana vyanzo vya kuaminika na vya haraka vya kupata habari kama wengi wetu humu JF. Kwa hiyo bado kuna Watanzania wengi (amini usiamini) wanaishi "jana".

2. Kabla ya kuruhusu vyama vya upinzania, CCM, chama kilicho kuwa madarakani kilikua na muda wa kujiandaa. Katiba ya kuruhusu vyama vya upinzani iliandikwa na wao na muda wa kujiandaa na mabadiliko wa mazingira ya kisiasa walikuwa nao.

3. "Personalities" nyingi zilizo unda vyama vya upinzani ni wana CCM wa zamani. Ukimuangalia Mrema Sharif Hamad, Mtei wote ni watu waliokua ndani ya mfumo wa CCM. Hata Ibrahim Lipumba ambae sina uhakika kama alikua CCM au la alikua mshauri wa Mwinyi kipindi fulani. Je hii ina wezaje kuwa tatizo kwa vyama vya upinzani?
a) Baadhi ya viongozi waliongia upinzani ina wezekana walikua mamluki ambao walikua hawana mpango wowote wa upinzani wa kweli.
B) Baadhi ya viongozi walioingia upinzani ni watu ambao walikua hawana future CCM kwa hiyo walihama kwa ajili ya kujaribu bahati yao. Hiyo ni kusema upinzani ilipokea watu ambao hawakua nyota wa kisiasa bali "has beens" wa CCM.
c) Baadhi yao ni watu waliyo ondoka CCM kwa maana hiyo mfumo wa fikira ulikua huo huo. Hauwezi kumshinda mwalimu kwa kumpa mtihani wake mwenyewe.

4. Wengi wa viongozi waliounda vyama vya upinzani kwa sababu moja au nyingine ita kuwa wali fikiria kwamba CCM ita shindika kiurahisi. SI ajabu baadhi yao wakadhani kwamba 1995 wange kiondoa CCM madarakani. Kwa maana hiyo basi vyama hivi vya upinzani vilivyo anzishwa vilikua havina mipango ya muda wa kati au mrefu kwa maumaini kwamba uchaguzi una kuja na wao wata shindda. Mpaka leo hii sioni mipango ya kueleweka ya muda mrefu wa chama chochote cha upinzani.

Kwa hiyo basi kama vyama vya upinzani kweli vina taka kushinda basi ni lazima kuwepo na mabadiliko. Lazima waletwe vijana ambao watakua katika mfumo wa vyama vyao. Lazima walete watu ambao hawaku wahi kuhusika na CCM ili kuleta mawazo na fikira tofauti. Ni lazima waji tazame na wajiunde upya. Kusema ukweli sioni chama cha upinzani kati ya hivi vilivyopo sasa kufanya mabadiliko yoyote ya kisiasa labda vyama vipya vita kapo anzishwa au viongozi wa sasa waliotoka kwenye mfumo ule ule, mawazo yale yale na mafunzo yale yale wakija kuondoka.

Ndugu wana JF tuna muda mrefu bado mpaka upinzani wa kweli Tanzania uibuke. Leo hii hatuna wapinzani bali wasindikizaji. Kwa maana kila kabla ya uchaguzi tayari imesha julikana chama gani kita shinda uraisi na chama gani kita kuwa na wabunge wengi Bungeni. Huo si upinzani.

kitu kikubwa walichokosea ni kutojenga msingi imara wa wanachaama waaminifu,vyama vingi vya upinzani vipo mjini tu,walitakiwa wajikita katika kutafuta wanachama kwanza kabla ya kuaanza ulafi wa madaraka na ubinafsi uluowjaa.

ukiangalia mfano CCJ, kimeanza hivi karibu kinataka kusajiriwa, kinapita mitaani kutafuta wananchama kwa nguvu, hapo lazima upate mamluki wengi na wanachama wasiona sifa thabithi na mawazo chanya ya mabadiliko.
 
Lakini mkuu mbona watu kama kina Mrema wanajulikana, hii ngoja ngoja mpaka lini... ni miaka ishirini na zaidi sasa tangia vyama vya upinzani vikubaliwe kikatiba... wanacho subiri ni kitu gani...!?

Waache kuuza sura bana.
Sababu nyingi zilizotolewa ni kweli lakini kuna jambo lingine. Vijana. Chama chochote au movement yoyote ya kuleta mabadiliko lazima ichochewe (siyo lazima iongozwe) na vijana wa wakati huo. Vijana wa Tanzania hawana tofauti na wazazi wao. Ni vigumu kuwa-animate kwa issue yoyote. Kwao mambo ni "shwari', 'hamna noma', 'fresh' hata kama hana uwezo wa kupata chips dume. Hiyo mindset inawafanya waridhike kwa mambao madogo na kukosa thubutu. Siyo katika siasa tu bali na katika nyanja zingine za kimaisha. Ukitaka mabadiliko lazima ukubali na kuonja joto ya jiwe.
 
kitu kikubwa walichokosea ni kutojenga msingi imara wa wanachaama waaminifu,vyama vingi vya upinzani vipo mjini tu,walitakiwa wajikita katika kutafuta wanachama kwanza kabla ya kuaanza ulafi wa madaraka na ubinafsi uluowjaa.

ukiangalia mfano CCJ, kimeanza hivi karibu kinataka kusajiriwa, kinapita mitaani kutafuta wananchama kwa nguvu, hapo lazima upate mamluki wengi na wanachama wasiona sifa thabithi na mawazo chanya ya mabadiliko.
mkuu tupo pamoja, pamoja na lawama zote tunazo wapa CCM lakini hata huku wapinzani bado kuna kitu tuna miss kuwashawishi wananchi kuwa wapo imara
 
Tujaribuni kuwa wa kweli jamani,tuache hypocrisy...Tatizo ni UDINI na CCM....Tanzanians are fed-up with CCM..ila watu wanaangalia wapi dini yao itapata maslahi kwanza..na hii ni kwa sababu watu wanaendesha maisha yao chini ya vivuli vya dini zao...taasisi za dini ndio source za kuendesha life.
Kila kipindi cha Urais....kuna kundi moja la dini linafurahia wakati lingine linahuzunika..kwa hiyo kuipenda au kutoipenda CCM inategemea na interest ya mtu.

Nina uhakika kwamba wakristo wengi hawapendi CUF kwa sababu ya labda viongozi wake wengi ni muslims ama wafuasi wake wengi ni muslims,the same applies to muslims....hawaikubali sana CHADEMA ama wasingeikubali sana CCJ based on the same reasons.

Angalia CUF zenji,kwa sababu hakuna mgawanyiko wa fikra za dini,utaona CUF kila uchaguzi inashinda,na wengi hulalamika kuwa mkono wa udini wa bara ndio unaowanyima ushindi wao kwa nguvu za dola.Almuhimu ni kuwa vuguvugu la kisiasa Zenji liko makini kuliko bara.

CCM wanajua hii hali,na ndio maana wanaweza kuzinchanga karata zao vizuri,mtaona sasa hivi unafiki utakavyojidhirisha hata kwa hao viongozi wa dini....ni maslahi tu.
 
Sababu nyingi zilizotolewa ni kweli lakini kuna jambo lingine. Vijana. Chama chochote au movement yoyote ya kuleta mabadiliko lazima ichochewe (siyo lazima iongozwe) na vijana wa wakati huo. Vijana wa Tanzania hawana tofauti na wazazi wao. Ni vigumu kuwa-animate kwa issue yoyote. Kwao mambo ni "shwari', 'hamna noma', 'fresh' hata kama hana uwezo wa kupata chips dume. Hiyo mindset inawafanya waridhike kwa mambao madogo na kukosa thubutu. Siyo katika siasa tu bali na katika nyanja zingine za kimaisha. Ukitaka mabadiliko lazima ukubali na kuonja joto ya jiwe.

Bado vyama vya siasa vina jukumu kubwa sana la kuhamasisha jamii ya WATANZANIA, hawawezi kuliepuka ili.
 
Si kweli huo mlolongo ulioandikwa na Mwanafalsafa1 aidha inawezekana ni kuanza harakati za kuchomekea ili ionekane CCM bado ni strong ina nguvu na hili na lile, nasema nikutaka kuwajaza watu kasumba.

Kwa ufupi sikubaliani na hayo kwa upande wangu na kwa vile sio lazima kuyakubali najiona nipo huru kuchangia vile nionavyo au nikionacho.

Watu au viongozi wa upinzani kuwa walikuwepo ndani ya Chama Cha CCM ,kwa maana kuhusika au kutohusika na CCM ,sio sababu ya kukosekana viongozi shupavu.Vyama vya siasa vyaa upinzani naamini kabisa vina viongozi na uongozi shupavu tena ulioimara.Na siamini kabisa kuwa CCM inashinda uchaguzi kwa kishindo cha kuzoa kila kitu na kugawia pale kinapotaka.

Vyama vyetu bado vipo katika transit period ambacho kinatumika kuweka misingi mbalimbali itakayowawezesha kuimarisha mfumo wa kuwepo kwa vyama vingi vinavyotumia katiba mpya,kwa maana tatizo moja tulilokuwa nalo ni kukosekana kwa KATIBA inayojitosheleza katika kuongoza nchi yenye vyama vingi.

Vyama hivi vinahitaji muelekeo wa kuibadilisha KATIBA ya NCHI hii na sio kulipua mabomu ya ufisadi kwani yaliolipuliwa yote naona yamedumaa.Imani yangu CCM haijawahi kushinda uchaguzi hata mara moja ,kwa maana ya ngazi tofauti mpaka ya Uraisi kwani matokeo wanayotangaza yana utata na kwa ufupi ni ya uongo ,ni viongozi wangapi wamekosa kura hata moja ,kwa maana hata kura yake mtu haioni ,afu unanambia CCM inashinda uchaguzi.

Dawa ya kushindwa kwa CCM inachemka.WaZanzibari na haswa wa Pemba wanawasubiri WaTanganyika kuamka ili kuweza kula sahani moja na CCM ,hivi mbona CCM imeangushwa kule Pemba ,hapa hamjiulizi iweje Pemba wameweza kuiangusha CCM kwengine kusiwezekane ??????? What is wrong with you ? CCM kwa hapa walipo wanaiogopa Pemba ,wanaogopa iwapo msimamo uliopo Pemba utaenea Tanzania nzima basi itakuwa hatari kubwa sana kwa CCM kubakia madarakani ! Tatizo sio viongozi. CCM wanakwiba tena wanakwiba mchana kweupe ,je ni nani alinde kura ,ni kiongozi wa Chama au ni wananchi waliopiga kura.
 
Mkuu Mwiba. Ngoja nikujibu kipande kwa kipande maana umeandika mengi sana.

Si kweli huo mlolongo ulioandikwa na Mwanafalsafa1 aidha inawezekana ni kuanza harakati za kuchomekea ili ionekane CCM bado ni strong ina nguvu na hili na lile, nasema nikutaka kuwajaza watu kasumba.

Mkuu Mwiba this is uncalled for. Kusema nachochea harakati za CCM au kudanganya watu kwa sababu na pingana na wewe si sahihi. Nime toa mtazamo wangu kwa nionavyo mambo. Wote hatuwezi kuona dunia sawa. Kwa hiyo kutoa shutuma kama hizo ili nionekane nina ulterior motives si sahihi.

Kwa ufupi sikubaliani na hayo kwa upande wangu na kwa vile sio lazima kuyakubali najiona nipo huru kuchangia vile nionavyo au nikionacho.

This is what i cal hypocrisy. Iweje mawazo yangu uone nataka kutisha watu lakini bado vile vile hapa una jifanya wewe ni mtetezi namba moja wa kutoa maoni yako? Anyway umeanza kwa jazba isiyo kuwa na lazima na I'm assuming wewe ni supporter wa upinzani so kama nime kugusa ngoja tuone hoja zako.

Watu au viongozi wa upinzani kuwa walikuwepo ndani ya Chama Cha CCM ,kwa maana kuhusika au kutohusika na CCM ,sio sababu ya kukosekana viongozi shupavu.Vyama vya siasa vyaa upinzani naamini kabisa vina viongozi na uongozi shupavu tena ulioimara.Na siamini kabisa kuwa CCM inashinda uchaguzi kwa kishindo cha kuzoa kila kitu na kugawia pale kinapotaka.

Mkuu kwanza hamna sehemu mimi nilipo sema CCM ina shinda ushindi wa kishindo lakini kama ulivyo sema ni imani yako. Mkuu hakuna ushahidi unao onyesha upinzani una uongozi shupavu wala imara na ngoja nikupe mifano.
a) Tokea vyama vya upinzani vianzishwe viongozi wa chama wakuu ni wale wale na pia wanao gombea uraisi ni wale wale. Hapa ina maanisha kwamba hakuna utaratibu wa kupokezana. Vyama vya upinzani vingine hata terms za viongozi havi julikani na wala chaguzi ni lini hai julikani. je huu ni uongozi bora?

b) Juzi tu hapa tumeona viongozi wa upinzani wakienda kwenye mkutano wa CC ambapo CCM ilipo tambulisha rasmi wageni wake. Hiyo ina leta picha gani? Najua wewe utaona si kosa lakini fikiria mwenyewe ni wape umeona viongozi wakuu wa upinzani wakienda kwenye kikao cha kusimika wagombea wa vyama vingine tena supposedly "mpinzani" wao mkuu. Hiyo ina onyesha ni aidha wana kubaliana na sera na falsafa za CCM au wame kosa utashi kabisa wa kikiasa kwa kuto kujua wame leta picha gani. Na kumbuka wapiga kura siyo wote ni die hard fans wa chama fulani kwa hiyo muonekano ni muhimu katika kuwa vuta kukupigia kura.

c) Vyama vyetu vya upinzani ni reactive siyo proactive. This is a fact. baada ya uchaguzi hausikii upinzani wakisema nini wata fanya badala yake wana subiria CCM ikosee wao wakosoe. Vyama vya upinzani vina shindwa kujua kuwa uchaguzi mmoja ukiisha ndiyo mwanzo wa mwingine wao wana enda kulala for five years.

Vyama vyetu bado vipo katika transit period ambacho kinatumika kuweka misingi mbalimbali itakayowawezesha kuimarisha mfumo wa kuwepo kwa vyama vingi vinavyotumia katiba mpya,kwa maana tatizo moja tulilokuwa nalo ni kukosekana kwa KATIBA inayojitosheleza katika kuongoza nchi yenye vyama vingi.

Mkuu it's been 20 years tokea vyama vya upinzani viingie kwenye siasa za Tanzania. Mpaka lini wata baki kwenye transition period? Kama leo hii baada ya miaka 20 vyama vya upizani kwa pamoja vina wabunge 29 tu sielewi miaka yote wana fanya nini. I'm sorry hapo sielewi kabisa. Na swala la katiba nilisha liorodhesha kwenye post yangu ya kwanza lakini hauja arknowledge hilo na badala yake ume rudia swala hilo hilo nililo litaja mimi kama point yako..

Vyama hivi vinahitaji muelekeo wa kuibadilisha KATIBA ya NCHI hii na sio kulipua mabomu ya ufisadi kwani yaliolipuliwa yote naona yamedumaa.Imani yangu CCM haijawahi kushinda uchaguzi hata mara moja ,kwa maana ya ngazi tofauti mpaka ya Uraisi kwani matokeo wanayotangaza yana utata na kwa ufupi ni ya uongo ,ni viongozi wangapi wamekosa kura hata moja ,kwa maana hata kura yake mtu haioni ,afu unanambia CCM inashinda uchaguzi.

Sina haja ya kukujibu hii maana kwenye post yangu ya kwanza nilisha eleza kwamba katiba ilivyo rekebishwa kuruhusu vyama vya upinzani tayari ilikua inaipa mguu mbele CCM. Mkuu hivi ume soma post yangu yote au kwa jazba ulivyo ona tu baadhi ya mambo usiyo yapenda uka rukia kujibu?
 
Vyama vya upinzani wanajitahidi sana hata kama si vyote, tatizo ni ninyi mnaojua ikweli lakini njaa inawasumbua kiasi kwamba hamwezi kuzungumzia ukweli huo mbele ya umma, zaidi ya kupamba CCM kwa maneno ya ajabu ajabu. Kuna maeneo CCM huiba sana au hutisha watu kwa vitisho vingi lakini hamtaki kuzungumzia hilo. Kwanini kuivumilia CCM? wakati wameboronga katika mambo mengi. Wabunge wa chache wa upinzani mchango wao ni mkubwa kuliko lunduko kubwa la wabunge toka CCM, wafanye nini ili watu waone mchango wao ? Mabadiliko ya kweli hayaletwe na chama au viongozi ila huletwa na wananchi wenyewe waliochoshwa na taabu ya chama tawala.

Kuna vijana wasiotambua nchi inaenda wapi chini ya CCM badala ya kushiriki kuleta mabadiliko wanajihangaisha kumchangia JK aliyedhihirisha kushindwa kuleta maendeleo ndani ya miaka miatano. Nafikiri si muda wa kulaumu vyama vya upinzani, ila ni muda muafaka wakujiuliza nimetoa mchango gani kwa vyama makini ilikuleta mabadiliko. Unafiki tuweke kando, tuchukue hatua ya kuiambia CCM wazi wazi kuwa imeshindwa na tuwaambie viongozi wa vyama vya upinzani kuwa tuko tayari kuungana nao kuleta mabadiliko katika nchi hii.

Binafsi naamini nina nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko katika nchi hii. Akili yangu haijaharibiwa na CCM hata kidogo, niko tayari kutoa maisha yangu kwa kusimamia ukweli. Si muda wa kuiogopa CCM as if it is God,
 
Tujaribuni kuwa wa kweli jamani,tuache hypocrisy...Tatizo ni UDINI na CCM....Tanzanians are fed-up with CCM..ila watu wanaangalia wapi dini yao itapata maslahi kwanza..na hii ni kwa sababu watu wanaendesha maisha yao chini ya vivuli vya dini zao...taasisi za dini ndio source za kuendesha life.
Kila kipindi cha Urais....kuna kundi moja la dini linafurahia wakati lingine linahuzunika..kwa hiyo kuipenda au kutoipenda CCM inategemea na interest ya mtu.

Nina uhakika kwamba wakristo wengi hawapendi CUF kwa sababu ya labda viongozi wake wengi ni muslims ama wafuasi wake wengi ni muslims,the same applies to muslims....hawaikubali sana CHADEMA ama wasingeikubali sana CCJ based on the same reasons.

Angalia CUF zenji,kwa sababu hakuna mgawanyiko wa fikra za dini,utaona CUF kila uchaguzi inashinda,na wengi hulalamika kuwa mkono wa udini wa bara ndio unaowanyima ushindi wao kwa nguvu za dola.Almuhimu ni kuwa vuguvugu la kisiasa Zenji liko makini kuliko bara.

CCM wanajua hii hali,na ndio maana wanaweza kuzinchanga karata zao vizuri,mtaona sasa hivi unafiki utakavyojidhirisha hata kwa hao viongozi wa dini....ni maslahi tu.

Mkuu you make a valid point but I think huja angalia the big picture. Kila kikundi katika jamii ina jaribu kugain influence haswa kupitia siasa iwe kikundi cha walemavu, wanawake, wafanyabiashara, masikini, tajiri nk. Ndiyo maana kuna kitu kinaitwa "interest groups" au katika nchi zingine kuna "lobbyists".

Hata wewe mkuu natumai kabla ya kupiga kura una angalia na kuchunguza kiundani ni chama gani ambacho kina ahidi mambo mengi zaidi ambayo ni kwa manufaa yako. Kwa bahati mbaya siasa ina onekana ni mchezo mchafu kwa sababu your interest lazima ita conflict na interests za mtu mwingine so it's not win win. Hata wewe mkuu sidhani kama uta chagua chama ambacho una dhani kina tetea dini nyingine na kupuuzia ya kwako.

With that said mkuu linapo kuja swala la chama kuonekana ni cha dini fulani hiyo challenge ni ya chama si mpiga kura. Kama chama cha kisiasa kinacho taka kura ya Watanzania walio wengi ni lazima kionekane kuwakilisha idadi kubwa ya Watanzania. Labda ndiyo maana vyama vingine havi fanikiwi maana vina onekana vipo pale kwa ajili ya kikundi fulani cha jamii kwa hiyo kukosa kura za vikundi vingine. Kwa hiyo chama chochote lazima kionekane balanced na kuwa kilisha Watanzania wote. Mfano CCM, ni vigumu kukiita chama cha dini fulani kwa sababu dini zote mbili zime wakilishwa tena vizuri tu.

Kwa hiyo mkuu chama kikionekana kipo kwa ajili ya jamii fulani (iwe kweli ama si kweli) ni lazima kifanye jitihada za kuonyesha kuwakilisha kila mtu. Chama kina omba kura kwa hiyo ukiomba ni lazima ubembeleze maana kura ya mtu hailazimishwi na wala haitolewi maelezo wala sababu. Pindi unapo ona chama chako kina chukuliwa in a negative way lazima ufanye mikakati ya kubadilisha hali hiyo. Usipo fanya hivyo ndiyo utazidi kuonekana na ni chama cha upendeleo hata kama that's not the case. Ndiyo maana kwa wenzetu vyama vina ajiri public relations firms na pindi mtu anapo kuwa mgombea ana kuwa na public relations officer ambae ana hakikisha mgombea wake ana chukuliwa katika mwaga uliyo mzuri. Sasa kwa nyumbani sijui vitengo vya public relations kwenye vyama vyetu vikoje.

So kama nilivyo sema juu mkuu kura huombwa na ikisha tolewa hamna maelekezo wala sababu. Kwa hiyo wapiga kura waki kuona kwa njia fulani hauwezi kusema potelea mbali kwa sababu tu wewe mwenyewe una jua wanavyo dhani sivyo. Haitoshi wewe kudhani ni lazima uwaonyeshe kwamba wewe sivyo ulivyo. Kwenye siasa una enda na mazingira yaliyopo na wala usitegemee kwamba kila mtu ana fikiria kama wewe unavyo fikiria. Mimi nakuelewa fika mkuu sema wengine wana elewa? Kama ni tatizo basi it's something the opposition parties just have to deal with. Tatizo likijitokeza hau lalamiki kwa nini. Una jiuliza kwa nini tatizo lipo na ni njia ipi au zipi zita fanikisha kuli tatua hilo tatizo.
 
Vyama vya upinzani wanajitahidi sana hata kama si vyote, tatizo ni ninyi mnaojua ikweli lakini njaa inawasumbua kiasi kwamba hamwezi kuzungumzia ukweli huo mbele ya umma, zaidi ya kupamba CCM kwa maneno ya ajabu ajabu. Kuna maeneo CCM huiba sana au hutisha watu kwa vitisho vingi lakini hamtaki kuzungumzia hilo. Kwanini kuivumilia CCM? wakati wameboronga katika mambo mengi. Wabunge wa chache wa upinzani mchango wao ni mkubwa kuliko lunduko kubwa la wabunge toka CCM, wafanye nini ili watu waone mchango wao ? Mabadiliko ya kweli hayaletwe na chama au viongozi ila huletwa na wananchi wenyewe waliochoshwa na taabu ya chama tawala.

Kuna vijana wasiotambua nchi inaenda wapi chini ya CCM badala ya kushiriki kuleta mabadiliko wanajihangaisha kumchangia JK aliyedhihirisha kushindwa kuleta maendeleo ndani ya miaka miatano. Nafikiri si muda wa kulaumu vyama vya upinzani, ila ni muda muafaka wakujiuliza nimetoa mchango gani kwa vyama makini ilikuleta mabadiliko. Unafiki tuweke kando, tuchukue hatua ya kuiambia CCM wazi wazi kuwa imeshindwa na tuwaambie viongozi wa vyama vya upinzani kuwa tuko tayari kuungana nao kuleta mabadiliko katika nchi hii.

Binafsi naamini nina nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko katika nchi hii. Akili yangu haijaharibiwa na CCM hata kidogo, niko tayari kutoa maisha yangu kwa kusimamia ukweli. Si muda wa kuiogopa CCM as if it is God,

Kumbuka vyama vya upinzani navyo vina nafasi ya kucheza. Lazima vionyeshe watu kuwa wao ni mbadala. huwezi kumuambia mtu achague upinzani simply because CCM ime borongo. Lazima mtu huyo aelezwe ni kwa nini chama fulani kina bidi kipewe nafasi na hiyo ndiyo kazi kubwa ya vyama vya upinzani.

Pia usiwe na mindset kwamba kila mtu yupo kwenye nafasi ambayo upo wewe. Kuna wananchi kijijini ni masikini wa kutupwa lakini hawaelewi uongozi mbovu una chagia vipi hali yao. Uki waambia CCM ni chanzo cha matatizo yao hawajui. Sasa ni nani wa kutembeza sera za vyama kama si vyama vyenyewe? Au unadhani wapiga kura wapo mijini tu ambapo wana soma magazeti na kuona luninga kila siku?

O.K. tueleze mkuu wewe binafsi ume fanya nini kama mwananchi kuhakikisha ujumbe wa mawazo yako yana fikia wananchi wako? Ume walaumu wananchi wengine kwa kuto kufanya chochote sasa tuambie wewe ume fanya nini mpaka sasa.
 
Back
Top Bottom